Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

sawa tu, kwani zenji hakuna wakristo? Au mmeshauwa wote?

Kama wapo, tunapata katiba mpya ya wananchi, tunampata rais aliyetokea Zanzibar ambaye ni mkristo.Taifa linasonga mbele!

Tutaangalia uwezo na sio din yake.but akiwa muislam itapendeza zaid.tusubirin kidogo.usilete ukabila mkuu.kwan akiongiza muislam ww utapungukiwa na damu?
 
nimeamini kuna watanzania wapumbavu, yaani baadhi ya comment ni za kidini halafu watu bila haya wanalike. kuna haja ya kuwa na mkono wa cuma ili watu namna hii wasiishi juu ya uso wa Tanzania.
Mkuu dunia ya sasa maoni ya watu yanaruhusiwa kabisa almradi hauvunji sheria ya nchi!

Dunia ya sasa ya kisiasa ni ya kuvumiliana tu mkuu!La sivyo tutajingiza kwenye udikteta na kuvunja haki za binadamu!

Cha msingi ni sisi kuchambua mchele na pumba, na kubakiza mchele pumba tupa huko!

Ukiwa una mind kihivi, basi utashangazwa sisi wachagga tunavumiliaje kutukanwa kila siku na watu kulike hizo comment?

Kiukweli kwenye hii thread ni kauli mbili tatu tu za maudhi kutoka kwa baadhi ya member.Lakini ujumbe ni wa muhimu kiasi kwamba ni sawasawa tu kuwaignore.Ikiwa kuna comment umeiona kuwa offensive, basi bonyeza kitufe cha kureport abuse..

Other than that ni vyema tukajadili bila hisia, mihemko na kwa utulivu!
 
Hata Kijana, kuanzia jina ni Christian name, mama ni Christian, Mke ni Christian, watoto ni Christian, na kanisani ataingia!. Uislamu wake ni kwa Baba tuu kama alivyo Baraka Hussein!. He is fit in every aspects!.
Pasco

Jogoo hajawika mara tatu ushamkana Lowasa, kweli we mfia tumbo kama Mwakyembe.
 
Heshma mbele mkuu! Long time not see you mkubwa!

Mkuu tuko pamoja kabisa! Nashangaa sana wanaoipinga rasimu ya katiba mpya iliyopatikana kutoka kwa wananchi na kuwakilishwa na mh jaji Warioba.

Ninaweza kuzungumzia hilo, lakini ni ukweli wa wazi kuwa serikali mbili ni kizungumkuti.

Kabla ya hapo, bado tulikuwa tukielekea upande huo huo ninaouzungumzia hapa.

Kumbuka Mwinyi alipokuwa akizungumziwa kuwa ni jiwe moja ndege wawili? Kwamba alikuwa muislam na kwa asili katokea Zanzibar?

Hadi usawa, hatuna utaratibu tena wa kupokezana madaraka kati ya nchi ya Zanzibar na Ile ya Tanganyika! Ndo maana baada ya Mwinyi, hakunanrais wa Zanzibar aliyetokea kuwa wa muungano! Maana kwanza hawana shida kubwa kuhusiana na maamuzi wanayotaka kufanya.Wana hadi wimbo wa wa Taifa nk.

Ni vyema tukaweza kutofautisha mambo ya muungano na hili ninalolizungumzia hapa,, ambapo wengi wetu wanaongozwa na hisia pamoja na nidhamu ya woga wa mazoea, wakidhani kuwa amani tuliyonayo ipo kwa bahati mbaya tu!

Hilo la kipimo ama kikomo cha uongozi, ni Issue ya kikatiba kama ilivyo ile ya muungano.

Sasa umekubali kuhusiana na hayo ya kina Mwinyi, hayo yalikuwa ya kikatiba lakini bado unalalamika kiwa hakuwa mzanzibari, kesho utaacha kulalamika kwanini hakuwa muislam? Sasa hapo nani atakuwa mdini?

Twende taratibu mkuu...Ushaanza kulalamika Mwinyi hakuwa mzanzibari.Unadhani ungeacha kulalamika endapo asingekuwa muislam!?

Unafiki unatusumbuwa watanzania! Tusijadili kwa hisia, tutulizane tutumie fahamu zetu ipasavyo bila bias!

Kamanda mie nipo namshukuru mola niko hai,

Unajua mkuu amani tuliyo nayo it is not amani bali woga na ni kwasababu watanzania hawajaamka kujua haki zao na jukumu la watu wanaopewa uongozi. Ukweli wa mambo ikipotea hii nidhamu ya woga na watu wakawa na courage ya kudai haki zao amani unayoiona itapotea kama siagi inayowekwa katika jua.

Turudi katika mada Swala la uzanzibari ni la msingi sana hasa wakati huu ambapo muungano upo kitanzini. Rasimu ya warioba imeamsha mwamko na hamasa ya uzalendo na utaifa wa kila upande. Upande mmoja ukitetea maslahi ya wazanzibari na kudai mamlaka yao kamili na upande wa pili wakidai uwepo wa Tanganyika na kudai kujitenga na Zanzibar. Kiufupi Taifa la Tanzania liko mashakani kupotea na kuzaliwa tena upya kwa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar.

Hoja ya Rais Mzanzibari ina mashiko zaidi kuliko mkristo kwani kwanza itasaidia kurudisha umoja wa Kitanzania ambao umedumu miaka 50 sasa. Pili sio umoja tu hata amani kwani mihemko hii ya uzanzibari na utanganyika sio yote inaishia mwisho mwema. Hivyo ni vema tukauenzi utanzania wetu na kumuenzi baba wa Taifa na jitihada alizozifanya kuleta umoja na mshikamano nchini.

Pili hoja ya Rais mkristo haina mashiko kwasababu badala ya kuleta amani itachochea mpasuko zaidi. Kwanza elewa hata kama walikuwa marais waislamu kwa kipindi cha miaka 10 lakini Serikalini na kwengineko bado wakristo ni wengi sana kulinganisha na waislamu. Kwa kuanzia asilimia 75 ya cabinet members ni wakristo ambapo waislamu ni asilimia 20 na 5 dini nyenginezo kama wapagani. Sasa ratio hii haiko sawa na hili limeleta manunguniko mengi miongoni mwa waislamu hadi kupelekea kudai kuna MFUMO KRISTO Tanzania.

Vile vile hata ukienda katika taasisi zenginezo kama mahakama na kwengineko ratio ya wakristo dhidi ya waislamu ni kubwa sana mfano mahakama tu.

Sasa pamoja kansa hii bado tunapiga debe tunataka Rais ajaye awe mkristo je tutafika?

Mwisho kabisa matatizo yetu watanzania sio dini bali ufisadi na kama tutapata Rais mwadilifu na mchapakazi awe mkristo, mwislamu na pagani huyo ndio anafaa kuwa kiongozi na sio kulazimisha awe mkristo hilo ni kupoteza mwelekeo ndugu.
 
Na awe mpagani ili asimuonee mtu haya kwa kigezo kuwa huyu ni wa dini yangu na hivyo wenzangu watanishangaa.......
 
Tutaangalia uwezo na sio din yake.but akiwa muislam itapendeza zaid.tuiliubirin kidogo.usilete ukabila mkuu.kwan akiongiza muislam ww utapungukiwa na damu?
Mkuu hii thread ina kurasa 7 tu hadi usawa huu sioni ni kwanini umepata uvivu wa kupitia posti zote?

Dini si uwezo wa uongozi mkuu! Nimeshairudia hii kauli mara nyingi tu na hata kwenye bandiko la kwanza ipo!

Pia unaonyesha kuchanganya madawa kabisa! Unasema ninaleta ukabila kwa kukataa muislam asiwe rais ajaye, wapi nimeongea hayo?

Wewe unaweza kusema kwanini unataka aendelee kuwa wa dini moja?Ama kwasababu tu imekupendeza kama ulivyosema kuwa "itapendeza zaidi akiwa muislam"?!

Wewe binafsi unaweza usione ubaya, lakini ndo mambo tunayotakiwa kuyaheshimu kama utaratibu wetu Ili kuilinda na kuidumisha amani yetu!
 
Kama tumefikia hatua hii basi hatuna taiga.Yaani watu wanazungumzia udini kwenye kumpata raids!!!hii no hatari Kwa taifa
 
naona waifia dini at work. kla la heri.

Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuw dini flani ndo kigezo cha urais kama vike wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amani kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.
 
Kamanda mie nipo namshukuru mola niko hai,

Unajua mkuu amani tuliyo nayo it is not amani bali woga na ni kwasababu watanzania hawajaamka kujua haki zao na jukumu la watu wanaopewa uongozi. Ukweli wa mambo ikipotea hii nidhamu ya woga na watu wakawa na courage ya kudai haki zao amani unayoiona itapotea kama siagi inayowekwa katika jua.

Turudi katika mada Swala la uzanzibari ni la msingi sana hasa wakati huu ambapo muungano upo kitanzini. Rasimu ya warioba imeamsha mwamko na hamasa ya uzalendo na utaifa wa kila upande. Upande mmoja ukitetea maslahi ya wazanzibari na kudai mamlaka yao kamili na upande wa pili wakidai uwepo wa Tanganyika na kudai kujitenga na Zanzibar. Kiufupi Taifa la Tanzania liko mashakani kupotea na kuzaliwa tena upya kwa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar.

Hoja ya Rais Mzanzibari ina mashiko zaidi kuliko mkristo kwani kwanza itasaidia kurudisha umoja wa Kitanzania ambao umedumu miaka 50 sasa. Pili sio umoja tu hata amani kwani mihemko hii ya uzanzibari na utanganyika sio yote inaishia mwisho mwema. Hivyo ni vema tukauenzi utanzania wetu na kumuenzi baba wa Taifa na jitihada alizozifanya kuleta umoja na mshikamano nchini.

Pili hoja ya Rais mkristo haina mashiko kwasababu badala ya kuleta amani itachochea mpasuko zaidi. Kwanza elewa hata kama walikuwa marais waislamu kwa kipindi cha miaka 10 lakini Serikalini na kwengineko bado wakristo ni wengi sana kulinganisha na waislamu. Kwa kuanzia asilimia 75 ya cabinet members ni wakristo ambapo waislamu ni asilimia 20 na 5 dini nyenginezo kama wapagani. Sasa ratio hii haiko sawa na hili limeleta manunguniko mengi miongoni mwa waislamu hadi kupelekea kudai kuna MFUMO KRISTO Tanzania.

Vile vile hata ukienda katika taasisi zenginezo kama mahakama na kwengineko ratio ya wakristo dhidi ya waislamu ni kubwa sana mfano mahakama tu.

Sasa pamoja kansa hii bado tunapiga debe tunataka Rais ajaye awe mkristo je tutafika?

Mwisho kabisa matatizo yetu watanzania sio dini bali ufisadi na kama tutapata Rais mwadilifu na mchapakazi awe mkristo, mwislamu na pagani huyo ndio anafaa kuwa kiongozi na sio kulazimisha awe mkristo hilo ni kupoteza mwelekeo ndugu.
Mkuu uhusiano wetu na Zanzibar utaamulika kikatiba na si vinginevyo mkuu!

Huu utamaduni unaweza ukanusirika kwa serikali 3 endapo tutapata katiba mpya.Zanzibar ni nchi nyingine mkuu.Serikali 3 zitatusaidia sana kuendeleza umoja wetu na udugu.
 
Kama tumefikia hatua hii basi hatuna taiga.Yaani watu wanazungumzia udini kwenye kumpata raids!!!hii no hatari Kwa taifa
Mkuu ujana ndo ubaguzi, ni heri tuudumishe utamaduni wetu tuliokuwa nao kuliko hoja ya kibaguzi kabisa ya ujana! Unamtetea Makamba?

Cc@Selemani
 
Kwa wakristo Hata Wakiongoza Waislamu 200,Haina shida ILA KWA WENZETU "MFUMO KRISTO"Utawaka MOTO NA PATACHIMBIKA.....
mkuu mimi sijawahi kuona waislam wakiongoza nchi hii. wewe unawafahamu hao waislam waliowahi kuongoza nchi hii?
 
Ndugu Mushi

tazama hii link hapa. Ni text kwenye PDF. Ukiweza kuishikiza kama kielelezo kwenye huu uzi itasaidia sana kupanua huu mjadala.

http://www.juliusnyerere.info/images/uploads/farewell_speech_diamond_jubilee_1985.pdf

Natumia teknolojia ya hayati Steve Jobs hapa, inashindikana kuiambatanisha.
Mkuu, wenye kusema vijana ndo wabaguzi.Sasa niambie kosa langu liko wapi? Ama kwasababu kwenye hoja watu wana mitazamo kutegemea na mtu wanayemsapoti for presidency?

Hizi ni jus two cents of mine, kwasababu nimezingatia hali halisi ya siasa za nchini mwetu, couple with the fact that siamini kuwa it was a coicidence tukawa na maraisi wenye imani tofauti kila awamu.

Nimefanya uchunguzi wangu tu na kugunduwa kuwa ni unwritten rule yetu Iliyoplay a tremedous role on the peace we enjoy in our country today!

Huo ni ukweli usiopingika tuache unafiki mkuu!
 
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuw dini flani ndo kigezo cha urais kama vike wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.

Kwenye mada yangu [h=3]Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote [/h]
niliwahi kusema hivi

Wanabodi,

Kumewahi kuwepo kwa dhana ya urais ni kupokezana kati ya Bara na Visiwani na kati ya Rais Mkristo na rais Muislamu.
Jee hizi ni dhana tuu, ama kiukweli, zina karata ya turufu. katika mustakabali wa taasisi ya urais wa JMT?!.

Kama ilivyotokea kwa mwanzo, watu kudhani marais kupokezana kati bara ya visiwani kwa Nyerere kutoka bara, then akaja Mwinyi kutoka Zanzibar, then Mkapa kutoka bara, aliyemfuatia Mkapa, hakupaswa kutoka Zanzibar?!. Kitendo cha rais kutoka bara, akafuatiwa na rais kutoka bara, kume break the circle ya coincidence ya kupokezana, na huu ni uthibitisho kuwa kwenye urais wa JMT, kupokezana ilikuwa ni dhana tuu!, hakuna kupokezana, rais ajaye, anaweza kabisa kutoka tena bara, na ajaye kutoka bara na anayefuatia na anaye fuatia hadi uwezekano wa rais wa JMT asitoke tena Zanzibar!.

Au rais ajaye, pia anaweza kutoka Zanzibar, akafuatiwa na Mzanzibari, akafuatiwa na Mzanzibari tena na tena tena na hata kuna uwezekano rais asitoke tena bara, kwa sababu hatuna utaratibu wa kupokezana!.

Vivyo hivyo kwenye hili la udini, Tanzania ni secular state, serikali haina dini, ila watu wake wana dini zao!. Rais nchi hachaguliwi na serikali isodini, bali huchaguliwa na watu wenye dini zao!. Jee kuna uwezekano, wa dini ya mgombea urais kuwa ni moja ya vigezo, vitakavyomfanya achaguliwe?!.

Japo haijaandikwa popote kuwa urais unapatikana kwa kupokezana kwa zamu, kati ya Wakristu na Waislamu, ila ni ukweli halisi kuwa by coincidence tuu Nyerere alikuwa Mkristo, akafuatiwa na Mwinyi, Muislamu, then Ben, Mkiristo, akaja JK Muislamu, hivyo 2015 coincidence inapaswa ku play in favour ya ni zamu ya Mkristo? If we don't break it!.

Vivyo hivyo hata kama imetokea rais wa kwanza akawa ni Mkristu, akafuatiwa na Muislamu, then akaja Mkristu, na sasa aliyepo ni Muislamu, kwa vile hakuna utaratibu rasmi wa kupokezana, ili kuundoa mfuatano huo wa coincidence tuu, mnaonaje kama rais ajaye awe Muislamu tena, na tena this time atoke Zanzibar, ili kupunguza marais wa kutoka bara tuu ndio wafuatane, yaani Mkapa alitoka bara, JK ametoka bara, na 2015 mnataka kutuletea tena rais wa kutoka bara?!, huu utangua kweli ni muungano wenye usawa?!.

Tukikubali to break the circle, ya urais hakuna kupokezana, wala hakuna zamu, pia tunaweza ku break kale ka secret code kuwa amkiwa Mkristo basi ni lazima awe wa dhehebu fulani!, yaani tujiaminishe kuwa kuwa rais alipokuwa Juliasi, it just happened kuwa pia alikuwa ni Mkatoliki, na alipokuja Bunyamini, pia it just happened alikuwa Mkatoliki, hivyo hata akija Membe ambaye ni Mkatoliki, it will be "just happened!", can't we break the "just happened!", kwa kuhakikisha wengine wenye uwezo nao pia wanakuwepo kwa kuthamiria to break the circles za just happened?!.

Yaani Tanzania tuendelee kuchagua rais kwamere coincidence kuwa it just "happened" au tudhamirie kumchagua kwa sababu?!.

Namalizia kuuliza, jee suala la zamu, kupokezana kati ya bara na visiwani, na kupokezana Wakristo na Waislamu, zina turufu yoyote katika siasa za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?!.Do they just happened by a mere coincidence, na sisi tnaziacha hizo mere coincidences zi play part katika nafasi ya urais, or its about time to break the circle kwa kumchagua rais mpagani asiyetoka bara, wala visiwani?!.

Pasco
 
Kweli utumwa hautaisha especially tanzania baada ya kujadili mambo ya msingi mnaanza kujadili vipara na dini ,hii nchi ina wajinga wengi sana ndio maana umaskini hautaisha huwezi kuona nchi yoyote africa ikijadili raisi kwa criteria za vipara na dini
 
ni lazima awe mkristu aliyelelewa na familia tiifu ya kikristu na si kama kina membe ambao huku muislamu na kule mkristu.hatuna njia nyingine tunataka mkristu.kwishney
 
ni lazima awe mkristu aliyelelewa na familia tiifu ya kikristu na si kama kina membe ambao huku muislamu na kule mkristu.hatuna njia nyingine tunataka mkristu.kwishney
Toa mfano kama nani ambae unamuona ni mkirsto safi ajachanganya na uislam.
 
Ilikuwa Kijana sasa linakuja suala la dini. Rais atachaguliwa kwa mujibu wa katiba, full stop. Vigezo havitaangalia, ujana, uzee, dini, jinsi na mambo kama hayo.

Rais fisadi hata awe wa dini gani au mpagani, hanufaishi watu wa dini yake. Ufisadi unaadhiri watu wote bila kujali dini, jinsi au umri wao. Mimi mkristo lakini bora aje Rais muislamu muadilifu kuliko mkristo fisadi!

Sasa kuna asiye fisadi, wewe tu mwenyewe wakikupa urais kitu utacho anzanacho ni ufisadi, rais ajaye awe fisadi, awe nini lakin awe tu mkristo, wenzetu watoto wa mamdo mme prove fairure ktk uongozi. Hihihihiiiiiiiiiiiiiikwiiiiiiiiiiiii!
 
Kati ya Makosa makubwa watakayoyafanya CCM ni kumpitisha MWISLAMU kugombea Urais,Wakristo wataungana waziwazi kumpinga.Hawatakubali Mapadre na Wachungaji waendelee kuuwawa kwa miaka mingine Kumi.

ukweli ndio huo mkuu, japo wengi wata ubeza
 
Sidhani kama mapadri ni wajinga kiasi hiko ila ni chuki na udini unakusumbua
 
Back
Top Bottom