Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Basi kwa vile tunataka kufanya mambo yetu business as usual (yaani kibongobongo hasa hasa ki-fleva), Rais ajaye awe na sifa zifuatazo kwa msingi wa ZAMU:

1. Mzanzibara
2. Kijana
3. Mdada
4. Mkristo
 
Mkuu unadhani kwanini wengi huwa wanasema zitto anachukiwa chadema kwasababu ni muislam? Na ingetokea marais wote waliopita wakawa wakristo bafo tungekuwa na amani?

Anayekwepa maswalini nani? Ama huyaoni?
Swala la Zitto limesemwa hivyo kwa sababu watu wanaamini Udini upo, kama vile wewe ukiamini kwamba ile ndege ya Malaysia ilipotea kwa mazingira ya uchawi basi lazima kila sababu zako zitafuatia mazingira ya Uchawi kuwa ndio somo. Lakini haina maana kila mttu anaamini hivyo!

Pili, Ni kweli kabisa kuna watu wanaomchukia na kumkataa Zitto kuwa kiongozi kwa sababu ya dini yake isipokuwa chama kilimchukia kwa sababu ya Ushindani wake ambao uliwanyima raha walopenda madaraka. Ndani ya vyama vyote vya siasa kila mtu anataka ULAJI apewe yeye nafasi ya KULA na hutumia dini ama sababu zozote ili mradi kuhakikisha nafasi yake haopokonywi. Tazama vyama vyote wakubwa wameendelea kuwa wakubwa kwa miaka zaidi ya 30 wasikubali mawazo mapya bila kupitia kwao.

Nakumbuka miaka ya 1980 hadi 90s wasomi wengi walokuwa wakirudi nyumbani toka nje masomini walitishia sana nafasi za ajira (kazi) za maofisa wa mashirika ya serikali na wizara zake ikafikia kiasi kwamba Watu walikuwa hawapeani maji maofisini. Kama unayoyaona Bungeni leo wakiviziana kwa sababu Ulaji ndivyo ulikuwa ktk maofisi ya watumishi wa Umma miaka hiyo. Na ndivyo ilivyo kwa vyama hivi vya wenyewe iwe Chadema, CUF , NCCR, TLP - kote huko kila mtu anatafuta upenyo wa nafasi yake ili kukaa ktk meza kubwa ili naye apate kula kwa Umma na kisu na sio kukaa janvi la mkeka huko kwa kina wanachama. Wako tayari kuitoa roho yako ili wao wasimame ulipo na watakutafutia kila fitna usikubalike, sijaona chuki ndani ya chama kimoja isipokuwa Tanzania.

Udini, Ukabila na kadhalika vyote vitatumika ili kuwaondoa waliopo ama kuwaweka tunaowataka lakini wote wanashindwa kujenga hoja ya maana kwa nini tunamhitaji Zitto badala ya Mbowe ama kwa nini Mbowe asiendelee kuwa Mwenyekiti. hapo ndipo utayakuta ya Uislaam/Ukristu, Uchagga, ukoona kadhalika kwa sababu hawana (Jawabu) hoja ya msingi. Ukweli ni kwamba UMASKINI wetu ndio adui wa umoja wetu kila mmoja wetu atatumia kila hila apate kuingia ktk madaraka hivyo hata kama hana sifa za Uongozi basi dini, Kabila, rangi au jinsi vinaweza kutumiwa kuwapa nafasi kama tulivyoona ktk viti maalum vya bunge, wakubwa huwachagua vimada vyao vya kujirusha inapohitajika.
 
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuw dini flani ndo kigezo cha urais kama vike wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amani kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.

the Red line, propaganda za raisi kijana zina hila ndani na ndio maana umeona utitiri wa surport of Makamba
 
Swala la Zitto limesemwa hivyo kwa sababu watu wanaamini Udini upo, kama vile wewe ukiamini kwamba ile ndege ya Malaysia ilipotea kwa mazingira ya uchawi basi lazima kila sababu zako zitafuatia mazingira ya Uchawi kuwa ndio somo. Lakini haina maana kila mttu anaamini hivyo!

Pili, Ni kweli kabisa kuna watu wanaomchukia na kumkataa Zitto kuwa kiongozi kwa sababu ya dini yake isipokuwa chama kilimchukia kwa sababu ya Ushindani wake ambao uliwanyima raha walopenda madaraka. Ndani ya vyama vyote vya siasa kila mtu anataka ULAJI apewe yeye nafasi ya KULA na hutumia dini ama sababu zozote ili mradi kuhakikisha nafasi yake haopokonywi. Tazama vyama vyote wakubwa wameendelea kuwa wakubwa kwa miaka zaidi ya 30 wasikubali mawazo mapya bila kupitia kwao.

Nakumbuka miaka ya 1980 hadi 90s wasomi wengi walokuwa wakirudi nyumbani toka nje masomini walitishia sana nafasi za ajira (kazi) za maofisa wa mashirika ya serikali na wizara zake ikafikia kiasi kwamba Watu walikuwa hawapeani maji maofisini. Kama unayoyaona Bungeni leo wakiviziana kwa sababu Ulaji ndivyo ulikuwa ktk maofisi ya watumishi wa Umma miaka hiyo. Na ndivyo ilivyo kwa vyama hivi vya wenyewe iwe Chadema, CUF , NCCR, TLP - kote huko kila mtu anatafuta upenyo wa nafasi yake ili kukaa ktk meza kubwa ili naye apate kula kwa Umma na kisu na sio kukaa janvi la mkeka huko kwa kina wanachama. Wako tayari kuitoa roho yako ili wao wasimame ulipo na watakutafutia kila fitna usikubalike, sijaona chuki ndani ya chama kimoja isipokuwa Tanzania.

Udini, Ukabila na kadhalika vyote vitatumika ili kuwaondoa waliopo ama kuwaweka tunaowataka lakini wote wanashindwa kujenga hoja ya maana kwa nini tunamhitaji Zitto badala ya Mbowe ama kwa nini Mbowe asiendelee kuwa Mwenyekiti. hapo ndipo utayakuta ya Uislaam/Ukristu, Uchagga, ukoona kadhalika kwa sababu hawana (Jawabu) hoja ya msingi. Ukweli ni kwamba UMASKINI wetu ndio adui wa umoja wetu kila mmoja wetu atatumia kila hila apate kuingia ktk madaraka hivyo hata kama hana sifa za Uongozi basi dini, Kabila, rangi au jinsi vinaweza kutumiwa kuwapa nafasi kama tulivyoona ktk viti maalum vya bunge wakubwa huwawachagua vimada vyao vya kujirusha inapohitajika.

Utakuwa ni ujinga tukikubali kuingiza udini na ukabila kama mnavyofanya, why divide and rule, mkuu ni raisi kubomoa lakini si raisi kujenga kama unavyodhani

CCM waliingia madarakani kwa propaganda ya udini na siku kikwete anatangazwa neno la kwanza akasema "waandishi wa habari tusaidianeni kuondoa swala la udini"ambalo akulikiri kabla bali alitambua lipo baada ya kutangazwa kushinda.
 
Mkuu usibase kwenye negativity!Hao watu wa aina hiyo wapo, wenye kukashfiana imani zao ama kubezana! Hao tusiwape nafasi hata kidogo.

Ni kama utamaduni huu umeleta kuheshimiana! Ebu Imagine marais wote waliopita wangekuwa wakristo, kungekuwa na amani?

Amani tuliyonayo haijajileta yenyewe mkuu! Ni matunda na matokeo ya mshikamano na tamaduni zetu Iimesaidia kudumisha amani na pia kuwafunga mdomo maextremist wa pande zote, hususan wenye kuweza kuzungungumzia kuhusu mifumo nk.

Sasahivi watu wanasema dini si issue na kumekuwepo na malalmiko kuhusiana na dini za viongozi wakuu?

Ama unadhani imetokea bahati mbaya tukawa na marais wa imani tofauti kila muhula? Think again!

Mkuu,

Mushi negativity pia imo katika kudai trivial stuff tukaacha more relevant matters. Kuna msemo unasema small minds discuss people while large minds discuss issues. Sisi badala ya kudiscuss more relevant issues kama ufisadi, ukuaji wa uchumi tunaanza kudiscuss watu huyu dini gani yule dini gani. Huu kwa jina la mtaani unaitwa uduwanzi.

Na binafsi naona swala la dini ya mtu sio la msingi ila la mwanamke ni la msingi kwa vyama vya siasa kwasababu kama zifuatazo:-
Mosi kuwepo katika jamii kundi kubwa la wapiga kura na ni wanawake hivyo kuteua mwanamke kuna msingi muhimu sana.

Pili kuteaua waarabu na wahindi ni kundi la watu ambao hawakuwamo serikali kwa muda mrefu. Watu hao pia sehemu ya jamii na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta binafsi. Hivyo uzeofu wao unaweza kusaidia katika kukuza uchumi wa nchi.
 
Wewe hujalijua Kanisa.Hakuna kinachoshindikana kwake.Kampeni zilipigwa Misikitini kuwahadaa waislamu kwamba Wamchague Mwislamu mwenzao ili waweze kumshinda Dr.Slaa.Ukweli ni kwamba Waislamu walitekwa akili.Ukitaka kujua Mziki wa Kanisa CCM imependekeze Muislamu 2015.

Farudume,

Acha kuweka mkwala mimi ninajua tena kwa uhakika mwaka 2010 Kanisa lilikuwa linataka Dr Slaa ashinde. Tena alikuwa akipigiwa kampeni hadi makanisani na waumini kutengwa kwasababu walikuwa hawakubaliani na kanisa kuhusu mtazamo wa kulazimishana kuwa Mteule wenu Dr Slaa ashinde urais. Sasa mbona alishindwa? Usitake kutisha watu nakupa tahadhari ndugu hiki ni kizazi cha dot com achana nacho kabisa. Jaribuni tena 2015 muone tena aibu itakayowakumba tena.
 
Ataapa kwa kitabu kipi cha maandiko matakatifu?Hatutaki matambiko ikulu!!
Kwani Kingunge huwa anaapa kwa kitabu kipi cha maandiko matakatifu? Hata kama yuko peke yake Tanzania nzima ni zamu yake!!
 
Acheni udini pumbafu nyie, tunataka rais mzalendo wa kweli bila kujali ni dini gani.
 
Mkuu,

Mushi negativity pia imo katika kudai trivial stuff tukaacha more relevant matters. Kuna msemo unasema small minds discuss people while large minds discuss issues. Sisi badala ya kudiscuss more relevant issues kama ufisadi, ukuaji wa uchumi tunaanza kudiscuss watu huyu dini gani yule dini gani. Huu kwa jina la mtaani unaitwa uduwanzi.

Na binafsi naona swala la dini ya mtu sio la msingi ila la mwanamke ni la msingi kwa vyama vya siasa kwasababu kama zifuatazo:-
Mosi kuwepo katika jamii kundi kubwa la wapiga kura na ni wanawake hivyo kuteua mwanamke kuna msingi muhimu sana.

Pili kuteaua waarabu na wahindi ni kundi la watu ambao hawakuwamo serikali kwa muda mrefu. Watu hao pia sehemu ya jamii na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika sekta binafsi. Hivyo uzeofu wao unaweza kusaidia katika kukuza uchumi wa nchi.
Mkuu soma tena heading ambayo ina alama ya kuuliza, pamoja na content ya ujumbe uone kama haya ni madai.Yani mkuu umeanza kusema ni udini, nimekuelewesha, lakiji sasa eti unasema nimedai?nimedai trivial stuff?!

Kwani wewe unaamini Imetokea coicidentaly kualternate?
 
Acheni udini pumbafu nyie, tunataka rais mzalendo wa kweli bila kujali ni dini gani.
Nani amesema anataka rais wa dini flani? Heading ni swali na content ni hoja.Kama huna jibu wala hoja piga kimya tu mkuu kuliko kuandika kama umetoka kula kushabu na kiroba?

Huyo rais mzalendo bila kujali dini anapatikana through wenye dini, na hata huyo mzalendo anaweza akawa ana dini ama asiwe nayo, hiyo siyo ujumbe wangu hapa!

Wakati unataka kupachika mgombea wako huoni udini, wenzako wakipachika unauona! Daah! Ndo bias yenyewe hiyo toka mwanzo nimesema tuwe makini!
 
Farudume,

Acha kuweka mkwala mimi ninajua tena kwa uhakika mwaka 2010 Kanisa lilikuwa linaidaka Dr Slaa ashinde. Tena alikuwa akipigiwa kampeni hadi makanisani na waumini kutengwa kwasababu walikuwa hawakubaliani na kanisa kuhusu mtazamo wa kulazimishana kuwa Mteule wenu Dr Slaa ashinde urais. Sasa mbona alishindwa? Usitake kutisha watu nakupa tahadhari ndugu hiki ni kizazi cha dot com achana nacho kabisa. Jaribuni tena 2015 muone tena aibu itakayowakumba tena.
Hizo zaweza kuwa porojo tu mkuu! Kura ni siri ya mtu bana!

Sidhani kama makanisa yalikuwa na program za kupigia kampeni wagombea urais kwa kutumia watu/waumini wake hadi useme walitengwa baada ya kukataa!

Hizo ni porojo na propaganda tu za wale wenye ushindani wa kidini.Ambapo kama si utamaduni huu tulionao wa ku alternate, basi kamwe tusingekuwa na amani hata kidogo!

Hayo makanisa yalijuaje waumini wamempigia nani kura hadi waweze kuwatenga! Huwezi ona hizo ni porojo tu mkuu?
 
Mushi,

Sawa wewe zione porojo lakini ndio ukweli. Na come 2015 zitaendelea kuwa porojo na ndio maana namtahadharisha achana na kizazi cha dot com kabisa utapata tabu. Na kuhusu kampeni Mushi usijifanye hukuwa unayaona yanayoendelea kuanzia waraka, vijembe vya maaskofu makanisani hadi wakafikia kusema asiangaliwe mtu kwa anayoyafanya bali tupinde kidogo kuangalia utendaji wake, hadi ikafika hali wale waliokuwa wakipingana na maaskofu walikuwa wakitengwa kanisani. Mushi ukweli usiopingika kuwa kanisa liliamua kuungana kumpigia kampeni Slaa na mipango ikakwama sasa Tunasubiri hiyo 2015....
 
Rudia kusoma badiko la kwanza vyema, ikishindikana kaongeze lensi ya magogo yako uweze kuuona udini through magnification!

Pole sana!
Sio nadiko la kwanza tu, bali post zingine nyingi nimezisoma... ni kwamba hujiamini kutetea hisia zako na badala yako unatengeneza excuses nyingi. UKishaleta hoja kwamba provided Rais wa sasa NI Mwislamu basi anayefuata awe Mkristo(ingawaje umejifanya ku-include hadi wapagani wakati unafahamu probablity ya hao watu kuwepo kwenye circle ni ndogo), huo tayari ni UDINI na mengine yote ni blah blah tu!
 
Sio nadiko la kwanza tu, bali post zingine ngi nimezisoma... ni kwamba hujiamini kutetea hisia zako na badala yako unatengeneza excuses nyingi. UKishaleta hoja kwamba provided Rais wa sasa NI Mwislamu basi anayefuata awe Mkristo(ingawaje umejifanya ku-include hadi wapagani wakati unafahamu probablity ya hao watu kuwepo kwenye circle ni ndogo), huo tayari ni UDINI na mengine yote ni blah blah tu!
Twende pound for pound unionyeshe huo udini, unatapatapa tu na wakati huna proof zaidi ya kujidai unajuwa watu.You don't know me like dat man! And if you think you do, weka hayo mabandiko niliyoonyesha udini badala ya unafiki unaounyesha hapa!

Wewe ndo wale ambao kama rais angekuwa mkristo awamu zote pengine ungejilipuwa wewe!

Acha hisia za kipuuzi baki kwenye mjadala usianze kujadili watu, as If hujawahi kuona matusi humu kuhusu mifumo na imani za viongozi wasio waislam kama wewe?

Watu wengine bana! Ukitaka za uso utapata mkuu! Lakini hakuna anayetaka kuweka ladha mbaya kwenye mahusiano yanayogusa maslahi ya Taifa.Mimi ni mtanzania kwanza kabla hata ya dini yangu, wewe je?

Kwani nani asiyejuwa udini wako? Sasa ndo unataka kuona kila mtu ni kama wewe!?

Acha chuki wewe!
 
Mushi,

Sawa wewe zione porojo lakini ndio ukweli. Na come 2015 zitaendelea kuwa porojo na ndio maana namtahadharisha achana na kizazi cha dot com kabisa utapata tabu. Na kuhusu kampeni Mushi usijifanye hukuwa unayaona yanayoendelea kuanzia waraka, vijembe vya maaskofu makanisani hadi wakafikia kusema asiangaliwe mtu kwa anayoyafanya bali tupinde kidogo kuangalia utendaji wake, hadi ikafika hali wale waliokuwa wakipingana na maaskofu walikuwa wakitengwa kanisani. Mushi ukweli usiopingika kuwa kanisa liliamua kuungana kumpigia kampeni Slaa na mipango ikakwama sasa Tunasubiri hiyo 2015....
Ni viongozi gani wakristo ambao unaona hawafai kuongoza taifa come 2015?

We sema tu bila kujali vyama.Maana mkuu si tunafahamu wewe pia ni muislam mwenye msimamo kabisa? Haya sasa, madhali unafahamu nimesema kwangu mimi hata akiwa mpagani sijali, wewe naona una prefer tuendelee kuwa na marais waislam bila ku alternate kama ilivyo utamaduni wetu?Maana sioni hoja yako hapa mkuu!

Ama kuna mahali umeona nimesema kuwa ninataka wakristo ndo watawale? Ama nyama ya binadamu ishakunogea mkuu?
 
Kuna watu naona wanataka tuwe natawala za imani moja tu, wanakuja na kujificha kwa kusema hoja yangu ni ya kidini, simply kwasababu wanataka waendelee kupata mgombea mwenye imani kama za kwao indefinetly!wanadai eti si wadini, si afadhali ninayesema tubadili kama ilivyo kwa utamaduni wetu na ikishindikana hata kama ikiwa mpagani?

Shame on them!
 
Kamanda mie nipo namshukuru mola niko hai,

Unajua mkuu amani tuliyo nayo it is not amani bali woga na ni kwasababu watanzania hawajaamka kujua haki zao na jukumu la watu wanaopewa uongozi. Ukweli wa mambo ikipotea hii nidhamu ya woga na watu wakawa na courage ya kudai haki zao amani unayoiona itapotea kama siagi inayowekwa katika jua.

Turudi katika mada Swala la uzanzibari ni la msingi sana hasa wakati huu ambapo muungano upo kitanzini. Rasimu ya warioba imeamsha mwamko na hamasa ya uzalendo na utaifa wa kila upande. Upande mmoja ukitetea maslahi ya wazanzibari na kudai mamlaka yao kamili na upande wa pili wakidai uwepo wa Tanganyika na kudai kujitenga na Zanzibar. Kiufupi Taifa la Tanzania liko mashakani kupotea na kuzaliwa tena upya kwa mataifa mawili ya Tanganyika na Zanzibar.

Hoja ya Rais Mzanzibari ina mashiko zaidi kuliko mkristo kwani kwanza itasaidia kurudisha umoja wa Kitanzania ambao umedumu miaka 50 sasa. Pili sio umoja tu hata amani kwani mihemko hii ya uzanzibari na utanganyika sio yote inaishia mwisho mwema. Hivyo ni vema tukauenzi utanzania wetu na kumuenzi baba wa Taifa na jitihada alizozifanya kuleta umoja na mshikamano nchini.

Pili hoja ya Rais mkristo haina mashiko kwasababu badala ya kuleta amani itachochea mpasuko zaidi. Kwanza elewa hata kama walikuwa marais waislamu kwa kipindi cha miaka 10 lakini Serikalini na kwengineko bado wakristo ni wengi sana kulinganisha na waislamu. Kwa kuanzia asilimia 75 ya cabinet members ni wakristo ambapo waislamu ni asilimia 20 na 5 dini nyenginezo kama wapagani. Sasa ratio hii haiko sawa na hili limeleta manunguniko mengi miongoni mwa waislamu hadi kupelekea kudai kuna MFUMO KRISTO Tanzania.

Vile vile hata ukienda katika taasisi zenginezo kama mahakama na kwengineko ratio ya wakristo dhidi ya waislamu ni kubwa sana mfano mahakama tu.

Sasa pamoja kansa hii bado tunapiga debe tunataka Rais ajaye awe mkristo je tutafika?

Mwisho kabisa matatizo yetu watanzania sio dini bali ufisadi na kama tutapata Rais mwadilifu na mchapakazi awe mkristo, mwislamu na pagani huyo ndio anafaa kuwa kiongozi na sio kulazimisha awe mkristo hilo ni kupoteza mwelekeo ndugu.

Mushi,
Pitia bandiko hili langu la 150. Mie kigezo cha msingi ni awe msafi na mchapakazi. Dini nimesema ni cancer na italipeleka pabaya taifa let u. Kwasababu tukimchagua mtu kwa misingi ya dini tuna hatari ya kupata kiongozi mbovu sana. Pia tutalipasua taifa kwani tayari hakuna fair distribution kwenye utendaji Kuanzia cabinet hadi katika mataasisi ya serikali yetu. Wakristo wako wengi ukilinganisha na waislam na wataalamu Wapo but shida ni nepotism.
 
Back
Top Bottom