Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Ebu kaa na soma maandishi yako mwenyewe halafu nambie una discuss au una argue?..
Na rudi kunisoma miye halafu unambie kama na discuss ama nina argue maana mimi nakueleza hadi chimbuko mla kila hoja na nakupa mifano wewe umekazania kuwalaumu waislaam. Ni wapi mimi nimewalaumu wakristu kama sio wewe mdini?.

Mkuu hata hayo ya waislaam kujiandikisha kupigana ni fikra zako kwa sababu huwezi kunielezqa sababu gani Watanzania walikwenda kupigana vita ya South Afrika, Angola, Msumbiji na kadhalika kama ilikuwa Uafrika ama kuutaka Uhuru wao. Kwani hao hayo Mataifa mengine hawaendi kupigana vita nje? Juzi tu wamekufa Wamarekani wawili ktk vita ya Gaza na waliandikishwa wengi kupigana vita ya Bosnia.

Na ajabu ni kwamba huhesabu Waamerika na mataifa makubwa wanaokwenda nchi ya wengine iwe Iraq, Misri, Syria au Libya kwamba ni wadini kujiandikisha kupigana huko ila wale wanaojiandikisha kuwalinda wenyeji wa nchi hizo. wakenya na Ethipia wameingia vipi Somalia nchi isokuwa yao kupigana vita kama sio ushenzi halafu mashambulizi upande toka wa pili ni Ugaidi.
Mimi ni natinalist, napingana na Wazanzibar na napingana na utawala huu wa CCM bila kujali rais ni Kikwete au Mkapa. That's me!
Mkuu umeenda kwenye argument kwa kuniita mdini kwasababu tu nimesema utamaduni tulio nao ambao wengine mnauita bahati mbaya na mimi nasema ni mzuri?

Pia si nimesema huwezi kusema kuwa wewe si mdini kwasababu tu unaishi kwenye nchi ya magharibi?
 
Mkuu umeenda kwenye argument kwa kuniita mdini kwasababu tu nimesema utamaduni tulio nao ambao wengine mnauita bahati mbaya na mimi nasema ni mzuri?

Pia si nimesema huwezi kusema kuwa wewe si mdini kwasababu tu unaishi kwenye nchi ya magharibi?
Nop, wala sii kweli ati uliposema ni utamaduni wetu nilikuita Mdini kwani nimekwambia kwanza kuna utamaduni mbaya usitakiwa na tuufukie, Nikazungumzia hadi ya kupokezana iwe kwa Utanganyika au Uzanzibar maana haitakiwi vitu hivyo hii leo, lakini wewe umeenda mbali zaidi hadi kueleza kwani nini wewe huwakubali Waislaam na ukaitoa mifano kibao hii kuonyesha what was the reason behind. Siku zote motive huwaongoza watu ktk hoja ama actions zao nawe ukaiweka wazi ndio maana nikakuita Mdini.
 
Rais wa taifa letu awe na sifa hizi:"Mwenye haki,Mcha Mungu,Mwadilifu,Mstahivu,awezaye kutawala roho yake na mwili wake!
 
Si lengo la thread hii kusema kuwa dini flani ndo kigezo cha urais kama vile wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita, bado tuna nafasi ya kuuenzi umoja wetu na mshikamano uliopeleka amani tuliyonayo!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Nina amini kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.
Mkuu jmushi1, natumaini sasa roho kwatu!, hii pattern na utamaduni huu unaendelea!. This game is on again!.

Hongera.

Pasco
 
Back
Top Bottom