Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

Rais ajaye ni lazima awe mkristo?

jmushi1

Platinum Member
Joined
Nov 2, 2007
Posts
26,390
Reaction score
25,510
Naona watu wanajadili kutokana na kwamba wagombea urais waliokuwa wamejiandaa sasa wanajitokeza! Makamba naona yuko kwa kasi sana na ana watetezi wengi ndani ya chama especially wale wa gia ya "rais kijana"

Si lengo la thread hii kusema kuwa dini flani ndo kigezo cha urais kama vile wale wa kigezo cha ujana wanavyofanya.

Lengo halisi hapa ni kutafakari na kuchukua maamuzi ya busara zaidi.Tunafahamu taifa letu mbali na kugawanywa kwa misingi ya chuki za kikabila na kidini zilizochochewa kwasababu tu ya ulafi wa madaraka na wagombea wa chama tawala esp. Uchaguzi uliopita, bado tuna nafasi ya kuuenzi umoja wetu na mshikamano uliopeleka amani tuliyonayo!

Mbali na hayo, chini ya taratibu zetu ndani ya awamu nne, hatujawahi kuwa na marais wawili mfululizo wenye imani moja!

Kwa utaratibu huo, ni wazi kuwa sasa ni muhimu tukapata kiongozi mwenye imani ya tofauti, inaweza ikawa hata mpagani!

Tusipofanya hivyo, tunaweza tukapata matatizo yatakayopelekea kudumaa kwa shughuli za kimaendeleo hususan jitihada zetu za kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini kwa kutumia nguvu kazi, maarifa pamoja na rasilimali zetu ikiwemo watu.

Pia haina maana kuwa hatuna haki ya kuendelea kuwajadili wale wenye imani sawa na rais anayemalizia muda wake, ie Membe na Makamba, bali ni muhimu kutilia mkazo umoja wetu na mshikamano wetu, vitu ambavyo vimetusaidia kudumisha amani miongoni mwetu!

Nina amini kuwa rais anayekwenda kumaliza muda wake, aliweza kupata madaraka hayo kwasababu watanzania waliudumisha utamaduni ule wa kuhakikisha hatupati watawala wenye kutoka kwenye imani moja awamu mbili mfululizo.

Unless tuwe na viongozi wenye qualifications ambazo zinawazidi wengine wote kwa kiasi kwamba kuuvunja utamaduni wa kubadilisha watawala kwa kuzingatia imani kukawa justified!

Utamaduni huu upo taka tusitake, nafahamu kuna watakaosema kiwa huo ni utaratibu wa ccm, well! Ccm ndo wanatupatia watawala, na hilo la dini za watawala wetu limekuwa ni mjadala nchini mwetu na hata humu jukwaani sote tunafahamu hilo.

Kwa maoni yangu, hypothetically, si vyema kureplace malalamishi ya mfumo wa imani moja kwa kuupachika mfumo wa imani nyengine.
 
Katiba ya zamani haijaandika kubadilishana wala hatutapitisha hata kwenye rasimu haipo. Mwaka 2015 sio wa hija za kikirsto hata tutake rais mkristo.

Haya ni maoni ya kutaka upendeleo wa namna fulani ndo umetufikisha hapa. Mara Nyerere alipendelea wakristo, mara Kikwete anapendelea waislamu. Kwetu muhimu ni kiongozi atakayeongoza kwa msingi wa katiba na utaratibu. Wakiongozana waislam kumi wasio mafisadi na wenye kujali mahitaji ya wananchi bila kujali imani zao itakuwa vyema, hivyo hivyo hata kwa wakristo. Hizi kelele ni ombwe la usawa ndo maana wadini hufikiri akija wa namna yao watapata ahueni kwa kuwapendelea.

Na utu uzima wangu huu sijaona rais bora kwa mkristo wala muislam. Tupanuke kifikra nje ya macho ya upendeleo, utu wEema, uadilifu ni haiba ambazo wanazo hata wasioingia makanisani na msikitini wakiwa heri kuliko mashekh na makasisi wanaotusalisha.
 
Hata Kijana, kuanzia jina ni Christian name, mama ni Christian, Mke ni Christian, watoto ni Christian, na kanisani ataingia!. Uislamu wake ni kwa Baba tuu kama alivyo Baraka Hussein!. He is fit in every aspects!.
Pasco
 
mzee mbona umebadilika ghafla?
jengo lenu la kampeni linakamika kule kati mkuu usibadili mwelekeo plz yl ni mzee wetu Pasco
 
Last edited by a moderator:
Ilikuwa Kijana sasa linakuja suala la dini. Rais atachaguliwa kwa mujibu wa katiba, full stop. Vigezo havitaangalia, ujana, uzee, dini, jinsi na mambo kama hayo.

Rais fisadi hata awe wa dini gani au mpagani, hanufaishi watu wa dini yake. Ufisadi unaadhiri watu wote bila kujali dini, jinsi au umri wao. Mimi mkristo lakini bora aje Rais muislamu muadilifu kuliko mkristo fisadi!
 
Katiba ya zamani haijaandika kubadilishana wala hatutapitisha hata kwenye rasimu haipo. Mwaka 2015 sio wa hija za kikirsto hata tutake rais mkristo.
Haya ni maoni ya kutaka upendeleo wa namna fulani ndo umetufikisha hapa. Mara Nyerere alipendelea wakristo, mara Kikwete anapendelea waislamu. Kwetu muhimu ni kiongozi atakayeongoza kwa msingi wa katiba na utaratibu. Wakiongozana waislam kumi wasio mafisadi na wenye kujali mahitaji ya wananchi bila kujali imani zao itakuwa vyema, hivyo hivyo hata kwa wakristo. Hizi kelele ni ombwe la usawa ndo maana wadini hufikiri akija wa namna yao watapata ahueni kwa kuwapendelea.
Na utu uzima wangu huu sijaona rais bora kwa mkristo wala muislam. Tupanuke kifikra nje ya macho ya upendeleo, utu wEema, uadilifu ni haiba ambazo wanazo hata wasioingia makanisani na msikitini wakiwa heri kuliko mashekh na makasisi wanaotusalisha.
Mkuu umeandika maneno ya maana sana, lakini unfortunately, hali halisi haiko hivyo!

Labda kama unadhani tumepata marais wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya?

Hilo hatuwezi kulikwepa mkuu!

It is an unwritten rule! Akija rais muislam awamu ijayo lazima kutakuwa na maneno!
 
Hata Kijana, kuanzia jina ni Christian name, mama ni Christian, Mke ni Christian, watoto ni Christian, na kanisani ataingia!. Uislamu wake ni kwa Baba tuu kama alivyo Baraka Hussein!. He is fit in every aspects!.
Pasco
Nani huyo mkuu? Makamba? Au Membe!?
 
Mkuu umeandika maneno ya maana sana, lakini unfortunately, hali halisi haiko hivyo!

Labda kama unadhani tumepata marais wa dini za tofauti kila awamu kwa bahati mbaya?

Hilo hatuwezi kulikwepa mkuu!

It is an unwritten rule! Akija rais muislam awamu ijayo lazima kutakuwa na maneno!

In RED, you mean unwritten constitution bila shaka!
 
Katiba ya zamani haijaandika kubadilishana wala hatutapitisha hata kwenye rasimu haipo. Mwaka 2015 sio wa hija za kikirsto hata tutake rais mkristo.
Haya ni maoni ya kutaka upendeleo wa namna fulani ndo umetufikisha hapa. Mara Nyerere alipendelea wakristo, mara Kikwete anapendelea waislamu. Kwetu muhimu ni kiongozi atakayeongoza kwa msingi wa katiba na utaratibu. Wakiongozana waislam kumi wasio mafisadi na wenye kujali mahitaji ya wananchi bila kujali imani zao itakuwa vyema, hivyo hivyo hata kwa wakristo. Hizi kelele ni ombwe la usawa ndo maana wadini hufikiri akija wa namna yao watapata ahueni kwa kuwapendelea.
Na utu uzima wangu huu sijaona rais bora kwa mkristo wala muislam. Tupanuke kifikra nje ya macho ya upendeleo, utu wEema, uadilifu ni haiba ambazo wanazo hata wasioingia makanisani na msikitini wakiwa heri kuliko mashekh na makasisi wanaotusalisha.

Thank you for a useful post...ubarikiwe
 
Back
Top Bottom