Polisi wafanya unyama mpya mgodini Nyamongo

ni sheria ipi unayoifahamu inaruhusu kupiga, kujeruhi na kuua raia under whatever circumstance??siku zote nakukumbusha subiri yakupate wewe au ndugu yako auawe then you will regain your sense and think twice when it come to the question of tanzanian police!!

sheria ya mwenendo wa makaosa ya jinai inaruhusu kutumia nguvu ya ziada lakini isizidi nguvu anayotumia adui yako. Iko hivyo.

Tatizo la kazi ya uasikari, si kwamba hawajui wanachokifanya, bali ni wabunge wa ccm waliotufikisha hapa tulipo. Askari wanakuwa ni wahanga tu wa maamuzi mabaya ya wabunge wa ccm.

Siku zote mimi naamini katika uzuiaji wa matukio, ambapo jitihada zote lazima zifanywe awali kuhakikisha kila kitu kinakuwa safi. Sasa watengeneza mazingira wanaposhindwa kuandaa mazingira mazuri kwa watendaji, watendaji wataonekana ndio waovu wakati wako katika kutekeleza sheria iliyoandaliwa na watu wengine kabisa.

Take care, maisha bila ccm yanawezerkana
 
Kuna swali halijajibiwa hapa. Polisi walianzaje kupiga watu? Hata kama ni sababu za kijinga tuzijue.
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

Wewe jamaa ni kada haswa, unabishana mpaka na ukweli?
 
Kwa kauli hizi za zomba,radhia&co naona uhusiano wa moja kwa moja wa mauaji haya ya polisi ccm,its not by coincidence washabiki wote wa mauaji wawe ni wa chama fulani tu!!
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

Mkuu mimi nimewahi kutembelea hayo maeneo. Kusema kweli huko. Nyamongo kila siku ni vita na risasi. Wananchi huwa wanavamia kwenea kutafuta mabaki ya madini wakiwa katika makundi na silaha za jadi.

Hapo sasa ndipo polisi hupiga risasi kuwatawanya. Kuna siku nilikuwa mgodini nikasikia risasi zinaunguruma basi nikajiweka tayari nikidhani mgodi umevamiwa na watu ili kujitwalia vipande vya dhahabu.

Jamaa wakaniambia hakuna shida ni huko nje polisi wanapambana na raia wavamizi. Magari ya polisi huko Nyamongo yamepondwa mawe na yana wire mess utadhani yote ni FFU. Hali ni tete kila kukicha afadhali ya jana. Raia wanauawa na polisi halikadhalika
 
Siungi mkono matumizi ya risasi lakini kwa Nyamongo pale huwa ni timing; polisi akicheza anakuwa chakula cha mto tigite. Hali ya usalama pale ni mbaya sana. Hamkumbuki kuna wakati wananchi waliishusha helkopta kwa kombeo? Chezea wanyamongo na wanyabasi wewe.
 
Ukweli nakuheshimu sana mzee mwanakijiji,kwa nini kwanza tusiwafundishe raia kutii mamalaka na kuacha vurugu? haiingii akilini eti polisi aje nyumbani kwa mtu ampige pasi na sababu! hebu tuache ushabiki!

Kule Iringa polisi walipiga mabomu ya machozi kwenye ofisi za Chadema ambazo zilikuwa zimefungwa !!. Ilibidi wabomoe mlango na madirisha ili waweze kupiga mabomu ndani. (Kwako wewe hili linaingia akilini ??)

Kule Iringa polisi walimtesa na kumuua mwandishi wahabari asiyekuwa na hatia yoyote ile. (Kwako wewe hili linaingia akilini ??).
CCM, Polisi, wewe na wengine wote wanaoshabikia mauaji kama haya,

Damu mnayoimwaga inawalilia kwa uchungu mkubwa sana. Damu hii itawafuata ninyi wote pamija na vizazi vyenu vyote mpaka mwisho wamaisha yenu.
Atawalaye kwa upanga, kakika atakufa kwa upanga.
 
pamoja na wanaharakati, wasomi, na wanahabari, wanasiasa na wanajamii kuingiwa na wasiwasi na kujitahidi kulaani unyama uliofanywa na polisi kule IRINGA kwa kuua mwandishi wa habari wakituo cha television chahanel 10 leo kama kwaida yao wameonesha ubabe mkubwa kwa kuvamia barabara na kuanza kupiga wananchi huko TARIME mara kwenye makazi yaliyo karibu na mgodi wa north mara hatimaye wakarusha risasi na mabomu yaliyojeruhi akina mama wawili na watoto watatu, kwenye mji wa mzee ngewa ikumbukwe kuwa tarehe 29 walikuwa wameua watu watatu jamani tunaenda wapi

Unapata faida gani unapoandika uongo? Kwamba POLISI WAMEVAMIA BARABARA NA KUANZA KUPIGA WATU! Historia ya mgodi wa nyamongo imeshaandikwa sana. Mahusiano kati ya wananchi wanaozunguka mgodi na mgodi wa nyamongo imeshazungumzwa sana. Ujeuri wa watu wa Tarime unafahamika fika
Wananchi wa Tarime huwa wanadai ile ni mali na wana haki ya kuingia mgodini na kuchukua dhahabu. Je warusiwe waingie? Only a fool can agree. Kilichotokea wiki iliyopita ni hiki hiki cha kutaka kuingia mgodini wakiwa na mapanga, sime marungu n.k. Jamani jaribuni kufika Tarime au Rorya muone jinsi watu wa huko walivyowakatili. Polisi wamefanya kazi nzuri sana kurejesha hali ya usalama katika mkoa wa Mara.
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

mbona humtetei mzazi wako wa kike anapopewa kichapo na mzazi wako wa kiume pindi am-baniapo paja,wakati haki sawa,unatetea policethithiem wanaendelea kukatisha uhai wa walala hoi.
 
Siungi mkono matumizi ya risasi lakini kwa Nyamongo pale huwa ni timing; polisi akicheza anakuwa chakula cha mto tigite. Hali ya usalama pale ni mbaya sana. Hamkumbuki kuna wakati wananchi waliishusha helkopta kwa kombeo? Chezea wanyamongo na wanyabasi wewe.

Mtu ambaye hajawahi kufika Nyamongo ni vigumu kufahamu picha halisi ya ubabe wa watu wanaovamia mgodi kwa ajili ya kujipatia dhahabu. Polisi wenyewe wanawagwaya kwa sababu mabali na wavamizi kutumia silaha za jadi wanazo pia silaha za moto ambazo hutumika kufanya uhalifu kwenye maeneo mengine kanda ya ziwa kwa kuiba mifugo kuvamia pia na kupora mali na pesa sehemu yoyote wanapohisi kuna kitu cha kupora. Sio watu wa kuchezea hawa.
 
Polisi hutumia nguvu pale tu watu wanapofanya ukaidi wa kutokutii amri za mwanzo. Usijifanye hilo hulijui.

Mwandisi Daudi Mwangosi aliuawa na polisi kwa kutotii amri gani ya mwanzo ??
Yaani polisi zaidi ya saba wenye silaha za moto walimzingira mwandishi !!! Wakamtesa sana na kumuua !!
Eleza katika tukio hili Mwandishi alikaidi amri gani ya kwanza ??
Eleza hili kwanza kabla ya kutetea mauaji, maana kwa kutetea mauaji haya, wewe mwenyewe unashiriki dhambi hii ya mauaji.
Atawalaye kwa upanga, hakika atakufa kwa upanga.
 
Hao wananchi walipigwa tu bila sababu za msingi? Kama walivamia eneo la mgodi, sidhani kama kulikuwa na makosa upande wa askari. Askari walikuwa wakitimiza wajibu wao wa kazi kama kawaida.

wewe huwa unawashwa muda wote kuropoka usiyoyajua aeee!
 
Ukweli nakuheshimu sana mzee mwanakijiji,kwa nini kwanza tusiwafundishe raia kutii mamalaka na kuacha vurugu? haiingii akilini eti polisi aje nyumbani kwa mtu ampige pasi na sababu! hebu tuache ushabiki!

Kwani polisi wao hawawajibiki kutii sheria? sheria gani inayowaruhusu kuua raia kiholela? Wananchi wangapi wameuwawa na polisi wakiwa mikononi mwao achilia mbali kuwavamia majummbani mwao.
Kama kichwa chako ni kizito itakuingiaje akilini polisi kuvamia nyumba ya mtu na kuua bila sababu ya msingi.
 
Mkuu huwezi kupata jibu. Watabaki kubwabwaja tu. Askari HAWAWEZI kuanza kutembeza mkong'oto bila sababu

Marehemu Ally Zona (Morogoro) akiwa kwenye kibanda chake cha magazeti aliuwawa kwa kushindwa kutii amri gani ya polisi?

Marehemu Daudi Mwangosi (Iringa) akiwa katika kutekeleza majukumu yake aliuwawa na polisi kwa kulipuliwa na bomu kwa kushindwa kutii amri gani ya polisi?

Ukiwa na kichwa cha kuku huwezi kuuona huu ufirauni wa polisi, utaishia kuwashabikia tu hadi hapo ndugu yako ama wewe mwenyewe litakapokukuta ndipo utapata akili.
 
Polisi tu,kila siku nyie na wananchi wa kawaida tena waungaji hata mlo wao,vp wezi wakubwa wa taifa hili mmewafanya nn?tembo anaibwa,msafara wa yule wa magogoni mafuta yaliyochakachuliwa ndiyo anajaziwa,feza ya msafara watu wanajiongeza.nyie kimya embu jitambueni sasa.
 
Siungi mkono matumizi ya risasi lakini kwa Nyamongo pale huwa ni timing; polisi akicheza anakuwa chakula cha mto tigite. Hali ya usalama pale ni mbaya sana. Hamkumbuki kuna wakati wananchi waliishusha helkopta kwa kombeo? Chezea wanyamongo na wanyabasi wewe.

Punguza pumba mkuu wewe si wa kiwango hicho. Kujustfy mauaji ya raia wasio na hatia kwa kisingizio cha polisi kuuwawa na kutupwa mto tigite ni akili ya kuku. Lete ushahidi hapa wa askari polisi waliouwawa na kutupwa mto tigite.

Sheria gani ya nchi inayowataka polisi kuua kila mtu anayesemekana kutenda kosa mgodini nyamongo ama maeneo ya kuzunguka mgodi? Watu wanaaoshabikia mauaji haya ya kiholela yanayofanywa na polisi wanahitaji kupimwa akili zao kama ziko vizuri.
 
Binafsi nimefanya reserarch tatu maeneo ya Nyamongo, lisemwalo ni kweli kuna unyama mkubwa sana wanaofanyiwa wananchi na polisi, mbaya zaidi vitisho kutoka kwa mkuu wa wilaya. kwa ufupi eneo hilo halina amani. Imefikia wakati mtu anayetoa sauti yake hufuatwa na kupewa vitisho, na wengine hubambikiziwa kesi bila sababu ya msingi
 
Back
Top Bottom