Polisi wafanya unyama mpya mgodini Nyamongo

Wanaokaa nje ya mgodi wengi wao ni wenyeji wa palepale yaani wamezaliwa palepale.Lakini wawekezaji na viongozi wa mgodi waliotoka nje ya Nyamongo hawakai mitaani.


Kwahiyo unataka kuniambia kwamba barrick pamoja na macontractors wake wameajiri wafanyakazi wengi wazawa wa nyamongo sio? you must be joking...
Katika akili ya kawaida ingekusaidia kufahamu kwamba hata migodi ya GGM, Buly na Buzwagi ambapo tunaweza kusema hakuna vurugu kama hizi za nyamongo bado wawekezaji na viongozi wa migodi hawakai nje ya migodi kwenye vijumba vya wenyeji bali wana maeneo yao maalum wanayoishi. Bahati nzuri nimefika migodi ya buly na buzwagi kwahiyo ninafahamu ni kwa kiwango gani wafanyakazi wao wanaishi ndani ya migodi na wanaoishi nje ya migodi.
 
Tatizo wewe ni mwanasiasa.Ukweli unaujua kuhusu watu wa Nyamongo lakini hutaki kuusema.

Tatizo lako bado umefunikwa na ukungu wa siasa za ccm wanaogeuza nyeusi kuwa nyeupe. Mimi huko ni kwetu kwahiyo ninakigfahamu hiki ninachokiandika kuliko ninyi mnaokwenda kule na kusimuliwa na wawekezaji kwakuwa wamewapatia viujira sasa mkitoka huko mnajifanya kuwa ma-advocates wa devils kwakuwa tu mnajipatia rizki zenu huko.
 
Mwita ndugu yangu, mimi sijasema ABG wanataka kufunga mgodi, soma tena.. nimesema wanataka kuuza kwa wachina na sababu moja wapo ni hasara wanazopata.Kingine kama umesoma vizuri nimesema intruders ndio wanaosumbua pale, si wananchi wote wa Nyamongo, lakini wanapokuja kuvamia hawa jamaa muda mwingine hufika hata watu 200 -300, lakini siwezi kusema ni watu wote wa Nyamongo. Kwa kifupi Nyamongo kuna tatizo na haswa hao intruders, wewe unataka tu kukataa ukweli na kile wanachofanya intruders sio kitendo cha kuachiwa tu. Mzee unajua mimi kuna workmate wangu walimchinja? Acha kutetea uhuni bwana.
Barrick hawajawahi kutangaza kupata faida katika mgodi wowote, si north mara, buzwagi, bulyanhulu ama tulawaka. Na walipotangaza kuuza migodi yao hawakusema kwamba wanauza north mara na kuacha buly na buzwagi, kwahiyo north mara huwezi kuutumia kujustify sababu za barrick kuuza migodi yake hapa nchini.btw kwahiyo unakubaliana na vitendo vya polisi kuua raia kila siku kwa kisingizio kuwa ni intruders? kwanini kila siku wanawapiga risasi za vichwani na vifuani, kwanini wasiwapige miguuni kama kanuni za kipolisi zinavyowataka na kuwaelekeza? wanawaua ili kuficha nini? unafahamu biashara wanayofanya askari polisi kwa kushirikiana na hao intruders?
 
Polisi kuna wakati inabidi atumie silaha za moto si kwa kutaka ila pia kujilinda naye ili asiuwawe.Maana wale watu wa Nyamongo hata ukipiga mabomu ya machozi wao wanakuwa na silaha za jadi utamwona bado anakufuata tu na wewe kama askari ili unusuru uhai wako inabidi utumie risasi za moto ili kujilinda.Utumiaji wa silaha za moto unakuwa mbaya tu pale askari anapolenga/anapozitumia kwa mtu ambaye hana silaha kwa ajili ya kumdhuru askari.
nia yangu si kukupinga, lakini uniambie umekwisha shuhudia lini askari wa kutuliza ghasia uingereza au marekani wakiwa na silaha za moto. sababu ukizingatia utu na haki ya kuishi, si tofauti za kiuchumi na demokrasia.
 
nia yangu si kukupinga, lakini uniambie umekwisha shuhudia lini askari wa kutuliza ghasia uingereza au marekani wakiwa na silaha za moto. sababu ukizingatia utu na haki ya kuishi, si tofauti za kiuchumi na demokrasia.
Umeshasema Uingereza au Marekani.Unaonyesha ulivyo na upeo mdogo,utalinganishaje nchi tajiri na masikini,nchi za dunia ya kwanza na ya tatu.
 
Heshima yetu ilipungua sana....! Lazima tuchukue hatua kama polisi hasa inapofika wakati raia hawatak kutii sheria bila shuruti
 
Umeshasema Uingereza au Marekani.Unaonyesha ulivyo na upeo mdogo,utalinganishaje nchi tajiri na masikini,nchi za dunia ya kwanza na ya tatu.

Hakuna nchi maskini wala nchi tajiri. Zungumzia watu maskini na watu matajiri. Watu maskini katika nchi zilizoendelea na watu matajiri katika nchi zinazoendelea
 
Mkuu Mwita Maranya, hayo yote nakubaliana na wewe. Tunachojadili leo ni issue iliyoletwa na mwenzetu kiribo kuwa polisi wamevamia barabara na kuanza kupiga wananchi. Tunachojiuliza ni nini kimesababisha polisi wakafanya hivyo. Mimi sababu iliyopelekea polisi kutumia nguvu, nimeisema na wewe sema yako. Usiwe na dhana kwamba wewe pekee ndo unajua mengi kuhusu nyamongo. Hayo ni madogo, tunafahamu makubwa zaidi ya hayo ya polisi. Mind your tongue
even for you polisi mind your speech and your statements si mara 1 polisi wanablock barabara kule wakiwa wanafukuzana na wana intruders na wanapiga watu ovyo mpaka watoto kuna siku walimpiga mpaka mwkt wa kijiji akadondosha bastola yake chini kutaka kuiokota wakasema anawatishia silaha wakampiga zaidi ikabidi waingilie kati mi nachoshangaa ni pale polisi wanapoua tarime inahalalishwa kumbe huko trm sio viumbe hai tena maana kama ni viumbe basi hawathaminiki bora hata mbu
 
Mtu ambaye hajawahi kufika Nyamongo ni vigumu kufahamu picha halisi ya ubabe wa watu wanaovamia mgodi kwa ajili ya kujipatia dhahabu. Polisi wenyewe wanawagwaya kwa sababu mabali na wavamizi kutumia silaha za jadi wanazo pia silaha za moto ambazo hutumika kufanya uhalifu kwenye maeneo mengine kanda ya ziwa kwa kuiba mifugo kuvamia pia na kupora mali na pesa sehemu yoyote wanapohisi kuna kitu cha kupora. Sio watu wa kuchezea hawa.
masaburi on work
 
Kwa habari yeyote ile ihusuyo nyamongo niulizeni mimi,manake nyie mnataka wakuu watembelee tu waone basi mimi naishi hapa hapa bila shaka anayepinga ukatili huu sina budi kusema thank you for telling us nothing.
 
Umeshasema Uingereza au Marekani.Unaonyesha ulivyo na upeo mdogo,utalinganishaje nchi tajiri na masikini,nchi za dunia ya kwanza na ya tatu.

nchi zote duniani ziko sawa, hakuna iliyo juu ya nyingine. Soma public international law utaelewa. Kwanini tusilinganishe, kwani sisi miili yetu imeumbwa kwa chuma?.
 
Back
Top Bottom