Uchaguzi 2020 Polepole: Watia nia wanaotoa rushwa kote Mikoani chama kina taarifa zao, hawatapata Uongozi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM komredi Polepole amesema chama kinapokea taarifa za watia nia wanaotoa rushwa kutoka kote mikoani kila siku.

Polepole amesisitiza kuwa watu hao ambao majina yao yapo makao makuu hawatapewa fursa ya kugombea uongozi kamwe.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Rushwa ni jinai bwashee, ni kwa nini wasichukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria kama taarifa mnazo? Kamati kuu ya ccm imekuwa ndio mahakama?

Au ndio mnaandaa mkakati wa kuwakata watu kwa hila kwa kisingizio cha rushwa?
 
Hata Kanisa Katoliki na Bakwata wana mahakama zao bwashee!
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM komredi Polepole amesema chama kinapokea taarifa za watia nia wanaotoa rushwa kutoka kote mikoani kila siku.

Polepole amesisitiza kuwa watu hao ambao majina yao yapo makao makuu hawatapewa fursa ya kugombea uongozi kamwe.

Chanzo: Channel ten.

Maendeleo hayana vyama!
Kwenye hiyo list Tulia yupo?
 
Siamini kama wataweza, robo Tatu ya wabunge Wa sasa Wa ccm mpaka sasa wamegawa rushwa za kutosha, akiwemo waitara na lusinde. .
 
Rushwa ibaki chadema

Hapo ulipo unaona aibu kinoma. Jinsi wanaccm walivyokuwa wanamchora rais kuwa kaidhibiti rushwa, na hiki kinachoendelea ni vitu viwili tofauti. Na ukitaka kujua rais alikuwa hapambani na rushwa, bali alikuwa alikuwa anawakomoa asiowapenda kwa kichaka cha kupambana na rushwa, hutaona hatua zozote za maana za wanaccm kupelekwa mahakamani. Simply ni kwakuwa hata yeye anategemea rushwa kuendelea kubaki madarakani.
 
Zama zimebadirika CCM mpya Chini ya Mhe.Dr. Magufuli haina urafiki na rushwa, wote watafyekwa.

Wanafyekwa badala ya kupelekwa mahakamani na kufungwa? Mnapambana na rushwa au mnaleta siasa uchwara? Mtu msafi anayepambana na rushwa hawezi kuwa adui wa vyombo vya habari. Hao wanaccm wenzake si ndio walikuwa wanamvika kilemba cha ukoka kuwa kadhibiti rushwa, yako wapi? Nasema hivi Magufuli na chama chake hawapambani na rushwa, bali mapambano ya rushwa yanatumika kukomoa wasio upande wa rais.
 
Hii ni CCM mpya, haikubali rushwa na ubadhilifu. Wataisoma namba.

Naona MATAGA wote mnakimbia huu uzi. Wale wahuni wa takukuru mliowatuma kufanya siasa chafu ofisi za cdm, wako wapi kuwapeleka hawa wanaccm wanaogawa rushwa kama njugu mahakamani? Zile sifa mlizokuwa mnapamba nazo Magufuli kuwa kadhibiti rushwa, mbona chama kinachopambana na rushwa ndio kinachafua picha? Hivi mtaweka wapi sura zenu baada ya kuhadaa umma kuwa mnapambana na rushwa, huku mnafanya vituko mbele ya hao wahuni wanaojiita takukuru, na hakuna mwanaccm yoyote kapelekwa mahakamani?
 
SAME magharibi zinagawiwa Rushwa za Magari.
Polepole jitokeze ukemee mambo haya, yule mbunge mtoro David Mathayo kwenye orodha ya wabunge watoro bunge la 11 anahonga magari sasa na pesa ili achaguliwe tena.
 
Back
Top Bottom