Uchaguzi 2020 TAKUKURU walitishwa na CCM kuwajibishwa endapo hawatawachukulia hatua watia nia wanaojihusisha na vitendo vya rushwa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Wakuu kama mnavyojua kuwa watia nia wengi majimboni wamekuwa wakikumbana na rungu la Takukuru kwa tuhuma za kutoa rushwa ili kuweka mazingira ya kupitishwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi mkuu 2020.

Pia soma> Uchaguzi 2020 - Polepole: Watia nia wanaotoa rushwa kote Mikoani chama kina taarifa zao, hawatapata Uongozi

Sasa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole leo baada ya kikao kilichomchagua Dkt. Mwinyi kuwania Urais Zanzibar, akijibu swali la mwandishi kuhusu wanaccm kukamatwa kwa rushwa amesema haya...

Chama cha Mapinduzi kilielekeza kwa Takukuru kwamba kama chama, Kamati ya Maadili na Usalama na Kitengo chake cha Udhibiti wa Nidhamu hasa ya viongozi yenye dhumuni la kuthibiti masuala ya rushwa na masuala ya maadili, iwapo sisi tutawakamata wala rushwa eneo husika na Kakukuru hawajafanya hivyo, basi tutakapokuwa tumeshika dhamana basi tutachukua hatua kwa viongozi hao wa Takukuru.

Tumekuwa na mazungumzo marefu na mazuri mno na uongozi wa Takukuru na tunaelewana vizuri. Tumeweza kuonesha mfano, tunaposema rushwa ni adui wa haki ni jambo la kimsingi na kiitikadi kwa Chama cha Mapinduzi, Hivyo mwanaCCM na asiye mwanaCCM

Takukuru wana jukumu, kama ambavyo tuliruhusu wafuatilie mchakato wetu wa ndani na kama kuna wala rushwa na wavurugaji wachukuliwe hatua, wakamatwe, washtakiwe na kwa kweli wafungwe. Vivo hivyo Takukuru inatakiwa kufanya hivyo kwenye vyama vingine.

Ifike wakati chama cha mapinduzi kinasema Rushwa katika nchi ni basi. Hii inaonesha kiwango CCM imejitazama na kujikosoa yenyewe na kuwa kinara wa kuichukia kwa namna zote rushwa. Kwetu sisi rushwa ni jambo la kiitikadi, haitakiwi na haipatikani kwenye chama chetu.

Rushwa tunaamini ni adui wa haki na inanyanyasa zaidi wanyonge, na uongozi wa CCM hautakiwi kuupata kwa kupatikana na rushwa. Uongozi wa CCM unapewa yule tunayeona anastahili. Uongozi wa CCM haulaliwi mlango wazi kama ambavyo wanafanya kwenye vyama vingine. Jambo la rushwa hili moto wake hautaisha sasa, tutaendelea muhula wa pili na kuhakikisha wale masalia wachache wala rushwa tunamalizana nao.


Muhula wa pili mwanzoni tutahakikisha nchi hii ni Corruption free zone kama ambavyo corona haina nafasi
 
Wamefanya vizuri. Na imependeza zaidi aliposema kuwa Takukuru wanatakiwa wafanye hivyo hivyo kwa vyama vingine. Vyama vingine haviwezi kudai vinaonewa kwa sababu Takukuru wameishaonyesha kuwa wao hawaangalii sura.

Amandla...
 
Wamefanya vizuri. Na imependeza zaidi aliposema kuwa Takukuru wanatakiwa wafanye hivyo hivyo kwa vyama vingine. Vyama vingine haviwezi kudai vinaonewa kwa sababu Takukuru wameishaonyesha kuwa wao hawaangalii sura.

Amandla...
Kwani hao waliokamatwa wamepelekwa wapi mpaka sasa
 
Pamoja na majigambo ya Rais Magufuli kuwa amekomesha rushwa awamu hii uhalisia uko kinyume chake!

TAKUKURU mpaka sasa wanapambana na rushwa ndani ya CCM yenyewe. Tumeona kilichotokea Dodoma kwene NEC na Mkutano Mkuu wa CCM. RUSHWA IKO NJENJE!

Lakini tunapoelekea kwenye Uteuzi wa Wagombea wa Ubunge na Udiwani kwa CCM hali itakuwa mbaya zaidi.

Dawa ya RUSHWA ni kuitosa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu- 2020.
 
Back
Top Bottom