Uchaguzi 2020 Polepole aongea na Waandishi wa Habari kuhusu mazingatio kwa wagombea wa CCM, aweka wazi ratiba ya uchukuaji fomu ya Wabunge na Madiwani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,924
141,891
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM komredi Polepole ataongea na waandishi wa habari kuanzia saa 10.00 jioni.

Kikubwa ni nidhamu ya kuzingatiwa kwa watia nia ya kugombea Ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama tawala yaani chama dume CCM. Baba Lao.

Mkutano unafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Updates;

Maendeleo hayana vyama!
===



Mh. Polepole ameanza kwa kueleza mafanikio waliyoyapata katika kutafuta Wagombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Polepole amewashukuru Wanadodoma kwa kuwapokea vyema katika mji huo na Wajumbe wote waliofika katika mji huo kuwa na wakati mzuri sana na kuwafanya kumaliza mkutano wao kwa amani na mshikamano mkubwa.

Sambamba na hilo, Polepole amewashukuru Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kumpa dhamana Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kugombea kwa kipindi kingine ili akaikamilishe kazi aliyoianza katika muhula wa kwanza.

Zaidi ya hayo, Polepole amewashukuru wasimamizi wa Uchaguzi kuanzia kwenye Halmashauri kuu kwa kazi waliyoifanya kuanzia kwenye mchakato wa kumpata Mgombea urais Zanzibar na Wasimamizi wa uchaguzi waliowezesha kumpata Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Aidha, Polepole ameeleza kuwa kutokana na kuwapo kwa maswali mbalimbali yapo mambo mbalimbali ambayo chama kingependa kutoa ufafanuzi baada ya Uchaguzi wa Wagombea nafasi za Urais kukamilika.

Moja, Polepole amesema kuwa kumekuwepo na maswli mengi kuhusu gharama za fomu ya Wagombea wa Ubunge na Udiwani katika Chama cha Mapinduzi. Katika hili Polepole amesema kuwa "Chama cha Mapinduzi kinazuia michango holela kwakuwa chama hicho kinaongozwa kwa mujibu wa katiba na kanuni ambazo wamejiwekea. Hivyo, michango yote katika ngazi zote ni lazima kwanza ijadiliwe na ipitishwe na kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya eneo husika".

Polepole ameongeza kuwa "licha ya kwamba kamati za siasa zina mamlaka ya kuweka mapendekezo ya michango hii, michango yoyote kwa Wanachama inabaki wakati wote kuwa ni michango ya hiari, ni marufuku Mwanaccm kulazimishwa kuchanga mchnango kwenye chama chetu. Mwanaccm anayeamini ana mchango anapenda kujitoa kwenye chama chetu afanye hivyo kwa hiari yake mwenyewe".

Polepole amesisitiza kuwa "kamwe, katu na asilani mchango usiwe kigezo cha kumpa au kumyima Mgombea fomu, Wagombea Wapewe fomu sawasawa na viwango vilivyoainishwa katika kanuni. Na mtu akishapewa fomu yake mnaweza kumweleza Chama kimepitisha harambee. kwahiyo wanachama wote wanakaribishwa kuchangia. Sasa iwe hiari yake kuchangia au kutokuchangia, ndani ya vikao tutajua huyu amejitoa kwenye chama na huyu hajitoi lakini kamwe isitumike kumkubalia mtu kupata fomu au kumkatalia."

Aidha akifafanua kuhusu viwango vya kuchukua fomu mbalimbali, Polepole ameeleza fomu ya udiwani kwa ngazi ya kata ni Shilingi elfu kumi tu (10,000/=), fomu ya Ubunge au Uwakilishi kwa Zanzibar ni Shilingi laki moja tu (100,000/=) lakini hii haizuii kamati ya siasa kuweka michango lakini si lazima.

Kwa upande wa fomu za Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi ni shilingi laki tano tu (500,000/=) wakati fomu za Urais ni shilingi milioni moja (1,000,000/=)

Pili, Polepole ameeleza jambo lingine lililofanyiwa mabadiliko katika katiba hiyo ni kupanua wigo wa demokrasia. Katika hili ameeleza kuwa Mkutano mkuu wa kata ambao awali ulijumuisha watu wachache kwa sasa utajumuisha pia Wajumbe wapya wanaoingia katika kikao hicho ambao pia ni Wenyeviti wa mashina yote katika kata husika ambao wanajulikana pia Mabalozi na wana dhamana ya kupiga kura za maoni.

Kwa upande wa ngazi ya Jimbo au Uwakilishi, Wataanza na Mkutano Mkuu wa jimbo ambapo katika Mkutano huo Wagombea wote wataingia na wataeleza kwanini wanataka kupewa dhamana ya Ugombea kupitia CCM kisha kamati za siasa za ngazi mbalimbali zitafuata utaratibu kwa kuweka mapendekezo mpaka kufikia Halmashauri Kuu ya taifa ambalo ndiyo itaamua jina moja.

Polepole ameeleza wamejifunza kutoka katika mchakato wa kupata Ugombea wa Urais walioufanya hivi karibuni. Kutokana na kujifunza huko ameeleza kuwa mchakato wa upigaji kura katika chama hicho utakuwa wa wazi ili kuepusha masononeko. Hivyo, wanataka uchaguzi ndani ya chama hicho kuwa huru na haki.

Sambamba na hilo, Polepole ameeleza utaratibu wa mawasiliano ndani ya chama na kubainisha kuwa hivi karibuni wataeleza sehemu ambapo taarifa za uchaguzi zitapatikana

Akisoma kipengele cha kanuni ya uongozi wa maadili ya chama kwa upande wa haki za Wanachama ukurasa wa (18) Polepole amesema Mwanachama atakuwa na haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi endapo kugombea nafasi nyingi kuitasababisha kuzorota kwa uhai wa Chama hatateuliwa.

Aidha, Polepole ametahadharisha Wagombea na watia nia kufanya vitendo ambavyo vinakatazwa na Chama ikiwemo kuweka mabango na kutumia vipeperushi na kupost kutia nia kuwa haviruhusiwi kwani ni sawa na kuanza kampeni kabla ya wakati wake.

Aidha, Polepole ameeleza ratiba ya Uchukuaji, urejeshaji fomu pamoja na mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hicho kama ifuatavyo:

1594727103673.png
1594727122020.png
1594727150027.png
1594727160940.png


 
Huu ni woga wa CCM Mpya. Zoezi la kutia nia ubunge na udiwani limepooa kupitia CCM Mpya, linafanywa kwa kificho gizani na kutojiamini kisa na sababu mazingatio yanayotolewa Dodoma kuwa wanaogopa makundi.

13 Julai 2020
Dodoma, Tanzania

Polepole : Mabango au Vipeperushi viwe vya ktk nguzo au mtandaoni haviruhusiwi na CCM Mpya

Watia nia ktk kutaka kuteuliwa kugombea uongozi wa nafasi vyombo vya dola kupitia CCM Mpya wasomewa makatazo ikiwemo vipeperushi ktk mitandao ya kijamii
 
Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM komredi Polepole ataongea na waandishi wa habari kuanzia saa 10.00 jioni.

Kikubwa ni nidhamu ya kuzingatiwa kwa watia nia ya kugombea Ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama tawala yaani chama dume CCM. Baba Lao.

Mkutano unafanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Up dates;

Maendeleo hayana vyama!

Yuko live TBC
 
Humphrey Polepole huku Songwe wanaCCM wanalalamika sana siasa za ndani ya CCM Mkoa wa Songwe toka 2017

Mapema leo humu ndani nimeona thread inayosema kuwa (Mkakati wa Zambi na Mulugo kupinga mabadiliko ya Katiba ya CCM [mtu mmoja,cheo kimoja] wafichuka
Wadau, amani iwe kwenu.)

Ndani ya huo uzi kuna watu wametajwa kwa majina na nafasi zao pamoja na nia ya mwandishi aliyowabebesha hao viongozi bila ya wao kusema.

Mfano mzuri tu kuwa Mheshimiwa Zambi kupitia kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Julai 2016 muda wa saa 2 usiku VETA HOTEL katika chakula cha pamoja na wajumbe wa Mkutano huo toka Mbeya na Songwe aliwaaga na kuwathibitishia kuwa hatogombea tena nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa iwe Mbeya au Songwe.

Pia wakati wa ziara zake za kukutana na Halmashauri Kuu za CCM kwenye wilaya zote aliwaambia wajumbe kuwa hatogombea tena na atampisha mwana CCM mwingine kwani anataka kutumia muda mwingi wa kumsaidia Mheshimiwa Rais Magufuli kama Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Lakini pia alisema kwa sasa hawazi na kufikiri kugombea ubunge Jimbo la Mbozi 2020.

HIVYO MHESHIMIWA GODFREY ZAMBI HAGOMBEI TENA UENYEKITI WA CCM MKOA MBEYA AU SONGWE.

Kuhusiana na Mheshimiwa Philipo Mulugo ambaye ni Mbunge wa Songwe naye hakuna sehemu ambayo amewahi kutangaza kugombea nafasi ya uongozi katika Mkoa Mpya wa Songwe hasa katika nafasi hiyo ya mtoa uzi aliyoandika ya Uenyekiti wa Mkoa.
Mulugo ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM(Mnec) na alikuwepo kwenye kikao kilichopita cha NEC kule Ikulu na walikubaliana kwa pamoja kukubali mapendekezo hayo.

Leo hii hawezi kuwa sehemu ya usaliti maana anakifahamu chama na kujua utaratibu wake.

Yeye kwa sasa yupo busy na wapiga kura wake ambao ndio waajiri wake.
NA HANA MPANGO WA KUGOMBEA UENYEKITI WA CCM MKOA WA SONGWE.

Ndugu wana JF kwenye andiko la huyo ndugu ambaye ni majeruhi wa Siasa za uchaguzi 2015, amemzungumzia pia Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ileje ndugu Kibona, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbozi ndugu Aloyce Mdalavuma na Katibu wa CCM Wilaya ya Mbozi ndugu Doris Kimambo kuwa nao ni sehemu ya mkakati huo kwa kutumia group la Whatsapp.
Mfano mdogo ni huyo Mwenyekiti wa CCM Ileje yeye hanaga makuu zaidi ya ujenzi na uimarishaji wa Chama wilayani kwake na hata masuala ya Whatsapp sio muumini sana wa magroup na kuchagia.

Kuhusiana na Mdalavuma na Doris Kimambo hawa wamekuwa sehemu ya hasira za majeruhi wa siasa za 2015 huko Mbozi na amewaandika kwa hila zake zilizo na chuki binafsi.

Miaka yote Mkutano Mkuu wa CCM unaenda kupokea na kubariki mapendekezo ya vikao vya NEC ambavyo navyo vinatangukiwa na CCM.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu eana kazi moja tu ya kupitisha.

Alafu majeruhi huyo anakwambia Wajumbe wa Mbozi ambao ni 10 pekee wasafiri kwa gari ya Chama Wilaya ambayo ameitaja kwa aina na namba ya usajili, kitu cha kuchekesha ni kuwa watu 10 wa Mbozi wawe sehemu ya kuhamasisha Wilaya nyingine Tanzania sembuse Mbeya na Songwe tu?

HAPA INAHITAJI AKILI NYEPESI KUELEWA KAMA HUU NI UZUSHI.

Mwisho, ndugu wana JF tambueni kuwa CCM Mpya yenye kuanikisha TANZANIA Mpya inakuja kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa kupitisha mapendekezo ya Katiba ya CCM Toleo la 2012, Kanuni za Uchaguzi pamoja na Kanuni za Jumuiya zake ambazo tayari mabaraza ya kupitisha yamekaa huko Dodoma.

Nawaonya tu majeruhi hao wa Siasa za Mkoa wa Songwe kwenye uchaguzi wa 2015 kule Mbozi na Songwe kwa majina yao George Mwenisongole na Noel Nkana acheni upuuzi na uzushi wa kuandika uongo huu kwenye mitandao ya kijamii.
TUMESHAWAFAHAMU

Source : Mkakati wa Zambi na Mulugo kupinga mabadiliko ya Katiba ya CCM (mtu mmoja, cheo kimoja) wafichuka
 
Back
Top Bottom