Uchaguzi 2020 Dkt. John Magufuli amerudisha fomu ya maombi ya kugombea Urais Makao Makuu ya CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
31,627
2,000
Dkt. Magufuli ambaye ndiye Rais wa Tanzania leo atarudisha fomu ya maombi ya kugombea urais kupitia CCM kwenye makao makuu ya chama jijini Dodoma.
===
Updates:
Rais Magufuli anarudisha fomu ya maombi ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Makao Makuu ya chama, Dodoma. Hadi sasa ni Mwanachama pekee wa CCM aliyechukua fomu hiyo.

Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally anasema "Hii ni hafla yako wewe mwenyewe (Rais Magufuli) kukabidhi fomu kwa mujibu wa kanuni. Nikupe taarifa fupi tu, wiki iliyopita tulikuwa na semina ya mashauriano na Wenyeviti wote wa CCM Mikoa yote 32 wakiongozana na wenyekiti wa jumuiya ya chama"

Aidha Dkt Bashiru ameeleza ulipochukua fomu walikuwa katika wakati mgumu sana kwa sababu wanachama wote katika Mikoa yao walitaka kukudhamini, kwahiyo wameratibu zoezi hilo. Mimi nimefanya kazi ya kubeba masanduku ya fomu na nyingine ziko nje haziwezi kuenea humu ndani.

Jumla ya wanachama 44, 415 wa Mkoa wa Dodoma wamemdhamini Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli kuwania Urais kupitia CCM.

Pia, jumla ya wanachama 71,491 kutoka Mkoa wa Dar es salaam wamemdhamini katika fomu za kuwania Urais wa Tanzania.

Katika Mkoa wa Mjini watu 2,394 pekee waliruhusiwa kumdhamini Rais Magufuli.

Kwa Geita, jumla ya wanachama 89,595 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kuomba kuwania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia chama hicho.

Mkoani Mara wanachama 87,550 wamejitokeza kumdhamini Rais Magufuli huku Morogoro wakijitokeza wanachama 117,450

Mpaka sasa, Wenyekiti CCM wa mikoa mbalimbali wanaendelea kuzungumza na kueleza idadi ya Watu waliomdhamini Rais Magufuli katika mikoa yao.

Mkoa wa Morogoro jumla ya Wanachama 117,450 wamejitokeza kwa ajili ya kumdhamini Rais Magufuli.

Mkoa wa Mtwara jumla ya Wanachama 7,596 wamejitokeza kumdhamini Rais Magufuli.

Mkoa wa Njombe jumla ya wanachama 17,810 wa CCM wamejitokeza kumdhamini Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Pwani jumla ya Wanachama 20,603 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea tena Urais.

Mkoa wa Rukwa jumla ya Wanachama 5,600 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Ruvuma jumla ya Wanachama 56,350 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Shinyanga jumla ya Wanachama 12,000 wa CCM wamedhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Singida jumla ya Wanachama 13,452 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Simiyu jumla ya Wanachama 3,693 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Songwe jumla ya Wanachama 11,744 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Tabora jumla ya Wanachama 29,486 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Mkoa wa Tanga jumla ya Wanachama 62,839 wa CCM wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais.

Aidha, kwa upande wa jumuiya ya Wanawake (UWT) jumla ya wanawake 66,633 Tanzania wamemdhamini Rais Magufuli kugombea Urais. Katika idadi hiyo mikoa iliyoongoza ni Dodoma ambapo wamejitokeza Wanawake 11,241 Tanga Wanawake 10171 na Kigoma Wanawake 6,083.

Hivyo, katika udhamini huo jumla ya Wanachama 646,956 katika mikoa yote 32 na jumuiya zake wamejitokeza kumdhamini Rais Magufuli kugombea Urais kwa awamu ya pili.

Katibu Mkuu wa Chama, Dkt Bashiru ameeleza kuwa katika zoezi zima la kutafuta Wadhamini jumla ya Wadhamini wote milioni moja na elfu ishirini na tatu laki moja na kumi na moja.

Baada ya zoezi la kutaja idadi ya wadhamini waliohusika katika zoezi hilo, zoezi linalofuata ni Rais Magufuli kukabidhi fomu kwa ajili ya kuzisaini.

Hotuba ya Rais Magufuli
Amewashukuru Viongozi wote waliojitokeza katika tukio hili sambamba na kuwashukuru Wanachama wote waliojitokeza na kumdhamini Tanzania bara na Visiwani.

Aidha, Rais Magufuli ameeleza kuwa ameirudisha fomu hii kwa kutambua kwamba yeye ni Mtumishi wa Watanzania na ameirudisha akiwa anaamini kwamba bado wanamhitaji atumike.

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli amebainisha kuwa bado kuna changamoto nyingi katika taifa letu, katika kipindi cha miaka mitano walijiwekea mipango mbalimbali ambayo mingi katika hiyo waliitekeleza lakini wamegundua kuna mipango mingi inatakiwa itekelezwe na kuna ambayo imetekelzwa lakini haijakamilika.

Vilevile, Rais Magufuli amesisitiza kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya mipango waliianzisha ndiko kulichomsukuma Rais kuchukua fomu tena kwani anaamini kuwa walioianzisha mipango hiyo ndio wanaoweza kutekeleza.

Pia amesisitiza kuwa watu wataotokeza kugo wafanye kazi kistaarabu na watangulize maslahi ya Tanzania. Hivyo kipindi hiki cha uchaguzi Wagombea wasikitumie katika kukibomoa Chama cha Mapinduzi.

Katika kufafanua suala hili la kukibomoa Chama Rais Magufuli amesema "Nimeshaanza kuiona dalili hii Zanzibar Wagombea wameshafika 33, wengine wanatumia mitandao wanamsema mwenzao, wengine kwenye magazeti lakini atakayechaguliwa ni mmoja tu na Mungu wetu wa Mbinguni anamfahamu sisi tulikuwa 42."

Hivyo, Rais Magufuli amesisitiza Wagombea wa Urais Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi wakawe waangalifu katika kunadi sera zao wasiumizane kwani watawapa nafasi Washindani wao.

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli amewasisitiza wagombea kutoka ngazi mbalimbali wa Chama hicho kuwa wavumilivu na kutokugombana. Ikitokea akapota yopyote kutoka kwa wengi waliotia nia wote wamuunge mkono.

Katika hili Rais Magufuli amesema "Tukigombana wakati wa kampeni tutapoteza Direction. Atakayechaguliwa wakati wa kampeni tumbebe. Nafasi zipo nyingi za kuteua na hata sasa zipo kama 4 sijateua. Najiuliza nimteue nani? Muhimu ni tushike Dola kwanza."

Sambamba na hilo, Rais Magufuli ametoa rai kuwa vijana na Wanawake pia wanatakiwa kupewa nafasi katika kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka huu.

Akiongelea kuhusu harakati za maendeleo mbalimbali zilizotekelezwa na awamu ya tano, Rais magufuli amesema kuwa Nchi hii ni tajiri isipokuwa ufisadi ulikuwa unakwamisha nchi kwenda mbele, kilichokuwa kinapatikana hakikuenda kwa walengwa ndio maana katika utawala wake miradi mbalimbali ikiwamo ujenzi wa ndege imewezekana.

Rais magufuli amesema "tunataka kila Mtanzania wa kila mahali afaidike na matunda na Rasilimali tulizopewa na Mungu"

Rais Magufufuli amesema kuwa Tanzania ni nchi ya 10 kwa Afrika kwa kuwa na uchumi mkubwa lakini pia ni miongoni mwa nchi tano Afrika ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Zaidi ya hayo, Rais Magufuli amesisitiza Wanaccm na Watanzania kumuunga mkono katika kujenga taifa la Tanzania.

Mwisho, Rais Magufuli amepiga picha za kumbukumbu na Wanachama mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria tukio hilo.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
950
1,000
Dr Magufuli ambaye ndiye Rais wa Tanzania leo atarudisha fomu ya maombi ya kugombea urais kupitia CCM kwenye makao makuu ya chama chake jijini Dodoma.

Up dates;
Unapokuwa na rais Kama huyu yaani unaomba uchaguzi uwe kesho insha Allah umchague tena....

Unapokuwa na waziri wa mambo ya nje kama mh. Membe ambaye anaamini katika tume ya uchaguzi iliyomchagua rais wake mh.Kikwete halafu miaka michache baadae HAAMINI UHALALI WA TUME ileile iliyomuingiza aliyekuwa WAZIRI MWENZAKE basi HARAKA unaomba kumuona mgombea wa CCM akiirudisha ile fomu.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
950
1,000
Kuna kila dalili hata NEC fomu zake wakishapokea za CCM basi ofisi inafungwa na kila anayerudisha fomu mkurugenzi wa NEC hatakuwepo ofisini
Mh. Mbowe aliibadilisha GIA angani,mh.Lowassa akawa mgombea wa chadema....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom