Humphrey Polepole adaiwa na Mwana-CCM kushiriki kuhujumu Katiba ili Samia asiwe Rais

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Hii ni kwamujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya Chama kwamba ndugu yetu mzee wa darasa la uongozi na genge lake walijaribu kuzuia mafuriko kwa mikono, waliratibu mbinu zote ili Samia asiwe Rais lakini wakashindwa,

kwa hali hii natamka rasmi kwamba sisi vijana wa CCM hatumtaki Polepole kwenye chama kwanzia leo

-----

Haji Jumaa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa toka Mkoa wa Pwani amesema haya

Tumwambie ndugu Humphrey Polepole kuwa wengi walipita kwenye nafasi ya Uenezi CCM Taifa, hivyo asione kuwa nafasi ile ilikuwa mahususi kwa ajili yake. Sisi tunajua nia yake iliyo nyuma za ajenda anazojaribu kuziibua kupitia kipindi chake cha Darasa la Uongozi.

Kama Humphrey Polepole anafahamu kuna watu wanaendesha nchi yetu kwa utaratibu anaosema wa parallel state au Parallel party ni vizuri akawa muwazi kwa kuwataja majina ili aisadie nchi.

Kuhusiana na hoja ya kikundi kidogo kinaongoza nchi, tumwambie tu Humphrey Polepole kuwa, duniani kote iwe dhairi au sirini, Serikali itaendeshwa na wachache kwa niaba ya wengi. Hakuna Serikali inaendeshwa na kila mtu.

Utaratibu wa wachache kuongoza kwa niaba ya wengi unakubalika, kuliko mtu mmoja kuongoza pekee yake kwa niaba ya wengi. Arejee maamuzi ya chama wakati wake Humphrey Polepole akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi

Humphrey Polepole awambie Watanzania kwanini alikuwa anamchongea aliyekuwa Katibu Mkuu wake kwa Mwenyekiti mpaka kupelekea kutenguliwa kwa Ukatibu Mkuu wa CCM

Kumekuwa na tuhuma nyingi za rushwa na unyanyasaji wa kingono wakati wa uongozi wa Humphrey Polepole, hata pale maelekezo ya kutochangisha pesa za michango kwa wafadhili kwaajili ya kampeni ndugu Polepole alifanya hivyo. Zipo taarifa za michango hiyo kuishia njiani

Kama Humphrey Polepole ana nia safi ya kutoa elimu, CCM inamalizia Chuo Cha Uongozi ni vyema akaomba kufundisha huko kwa nia safi badala ya ilivyo sasa kutumia kipindi chake cha Darasa la Uongozi kuisema Serikali iliyopo madarakani

Ndugu Humphrey Polepole na kikundi chako ambacho hakiamini nguvu ya mwanamke katika kuongoza tuwaambie mtashindwa kama mlivyoshindwa mwanzo katika zoezi la kuzia katiba ya nchi yetu isifuatwe ili kukidhi imani yenu ya kuwa nchi hii haiwezi kuongozwa na mwanamke

Tumsihi ndugu Humphrey Polepole aache kupenda vyeo na ukubwa, nchi yetu ni kubwa kuliko yeye. Anapokosa nafasi kubwa kubwa atulie tu na anyamaze, kwani hata alipofikia sasa ni pazuri,ni vyema akalinda heshima yeke
 
Hili taifa bhana, kila anayepewa sehemu nyeti hasikilizi waliochini, akiondoka kwenye hako kanafasi, anaanza kuyaona maumivu ya waliochini na anaumia kwa ajili yao

Huyo mneki naye kwa sasa bila shaka atakuwa kwenye kanafasi ka ulaji, akiondolewa na yeye atakuwa kama polepole

Siasa ni upuuzi sana
 
Hii ni kwamujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya Chama kwamba ndugu yetu mzee wa darasa la uongozi na genge lake walijaribu kuzuia mafuriko kwa mikono, waliratibu mbinu zote ili Samia asiwe Rais lakini wakashindwa,

kwa hali hii natamka rasmi kwamba sisi vijana wa CCM hatumtaki Polepole kwenye chama kwanzia leo
View attachment 1948517View attachment 1948518View attachment 1948519
Aliyeleta hili ni anapenda maneno ya wambiea tena anafanana na maraya malaya polepole


Ni nyundo sio hao anaitwa chaka
Shoka sijui shaka


Polepole ni kiongozi ni mtu hatari sana

Tena ni kiongozi anayetoa mawazo
 
Kama ilivyo kawaida msikose shule yetu ya uongozi🤣
20210922_172616.jpg
 
Pole Pole kachanganyikiwa . Hapa mnazidi mpa kiki tu.
Achaneni nae.
 
Acha uongo polepole angewezaje kuzuia utekelezaji wa katiba. Ndio mlizua kumtia mashaka samia kwa watu wema. Kazi kujipendekeza tu wakati hata itikadi ya ccm hamjui mnajua kusaka vyeo tu
 
Polepole anwezaje kushiriki wakati hakuwa bungeni na sheria zinabadilishwa bungeni?
Inawezekana unahitaji mimba ya polepole.
Polepole anaweza kubadili wakati vikao havija kaa, kwa nguvu gani aliyonayo mtu huyo?
 
Back
Top Bottom