Stories of Change - 2021 Competition

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
995
1,508
Umeme ni hitaji muhimu katika maendeleo ya kila taifa na mtu binafsi,kwa kuwa umeme huzalishwa kwa gharama kubwa na serikali hivyo serikali haina budi kuuza umeme kwa watumiaji kupitia shirika lake la umeme TANESCO.Kwa sasa Tanesco kwa asilimia kubwa ya wateja wake wananunua umeme kupitia mfumo wa LUKU,ambapo mtu anaweza kufanya manunuzi kupitia simu yake ya mkononi,na mifumo mingine,hii ni hatua nzuri sana,lakini bado kuna changamoto ndani yake ambazo nitaziainisha hapa,na kuweka mapendekezo ya Mabadiliko katika mfumo huo na maboresho yake.

1) MFUMO TUTUMIAO SASA

Nyumba nyingi kwa sasa,huduma mbalimbali na hata viwanda vimefungwa mita za "LUKU" ambazo huendesha matumizi ya umeme, mita hizi huja mbili kwa kila mteja ambazo ni mita kuu inayofungwa juu ukutani ndani au nje na huwa imefungwa kwa Siri ndani ya boksi na nyingine ndogo ya mkononi ambayo huitwa "REMOTE METER" changamoto kubwa katika mita hizi huanzia pale mita ndogo inapoharibika, huchukua kipindi cha mpaka mwezi mmoja kukamilisha marekebisho pale mita HII ndogo inapo haribika hivyo wateja kukosa huduma za umeme na kusitisha shughulii zao hasa katika maeneo ya biashara na pia hugharimu takribani 7,800/= kuipata nyingine.

1.1) CHANGAMOTO ZA MFUMO HUU

Mfumo huu unakumbwa na changamoto katika sehemu wa mbili;
a) Kuharibika kwa mita ndogo(remote meter) ambalo ni tatizo kwa wengi.
b) Mlolongo wa kufanya manunuzi ya umeme na kuingiza "token" kwenye mita

Mita ndogo kuharibika limekuwa tatizo linalojitokeza kwa wateja wengi na huchukua muda mrefu fanya marekebisho hivyo mteja kukosa huduma.Pia zoezi la kununua umeme mpaka kuweka limekuwa refu, mteja analazimika kununua umeme akipata "token" ni lazima akaingize kodi kwenye mita juu ya nyumba nje au kwa remote meter, wengine hulazimika kutoka nje usiku ili waweke umeme kitu ambacho ni hatari kwa wengi.

1.2) MAPENDEKEZO KUZIKABILI CHANGAMOTO

Namna pekee ya kukabiliana na mfumo huu,ni kwa TANESCO kuboresha mfumo wa malipo ambapo,kipengele cha kuweka token code kwenye mita kiondolewe,mfumo wa LUKU ubadirishwe ambapo mteja atanunuaa umeme kidigitali akisha kukamilisha malipo nakutumiwa token code,umeme unawaka pasipo kwenda kuingiza code kwenye mita,HII itapunguza kuwafuata Tanesco kumbadirishia mteja remote mita Mara kwa Mara,na kupunguza mlolongo katika zoezi Zima,pia itaondoa gharama za manunuzi ya remote mita kwa wateja na Tanesco wenyewe.Pia Tanesco itengeneze application maalumu ambapo mteja anayetumia simu janja ataweza kufanya manunuzi kupitia app hiyo,na iweze kufanya kazi online na offline.

2) MFUMO MPYA PENDEKEZWA WA LUKU

Screenshot 2021-07-18 at 13.21.05.png


Mfumo tutumiao sasa unahitaji mita maalumu ya LUKU ambayo huja mbili mbili,serikali kupitia Shirima lake la umeme inalazimika kutumia gharama kubwa kuagiza mita hizo kutoka nje ambayo gharama kwa kila mita haliwezi ulinganishwa na gharama ya mteja anayotumia kuingiza umeme.

Napendekeza mfumo mpya ambao hautahitaji mita ya LUKU badala yake kifaa takachoitwa "CONNECTOR"ama kwa jina lolote, katika hiki kifaa kuta kuwepo na matundu ya kuingizia umeme(kutoka kwenye nguzo) na kutolea umeme(kuingia ndani), kulia kwa kifaa hiki kuta kuwepo na tundu litakaloitwa "PORT" ambapo kutakuwa na kifaa kingine "Feedback chip" ambacho itachomekwa hapo,na ndicho kitakuwa kikikamilisha mawasiliano Kati ya mteja na mfumo wa Tanesco na kitakuwa kidogo Kama flash disc au wireless sensor ya mouse au keyboard ya compyuta, mfumo wa LUKU ndio utakao ongoza kila kitu, na mteja ataweza kununua umeme kupitia app katika simu janja yake online au offline,pia mtu ataweza kununua kupitia simu ya kawaida kwa mfumo wa simu pesa au benki,mtu yeyote ataweza kuwa na app hiyo ambapo akaunti itakuwa ya mmiliki wa nyumba au kiwanda n.k,

Feedback chip itakuwa na "code" itakayomtambulisha mteja na mteja ili akamilishe manunuzi popote ataingiza hiyo "code" akimaliza umeme unawaka Chapu hata Kama nyumba IPO Gambushi mnunuaji yupo Mbozi.

Mteja ataweza kuona kiasi cha unit alizo nazo kwa kupitia simu yake kwa namba maalumu au app yake ambayo ukiifungua tu ioneshe power unit zilizopo.

Mfumo huu utapunguza gharama za manunuzi ya mita za LUKU kwa serikali,itaondoa suala la mteja KUKOSA umeme kwa muda flani kisa mita,itapunguza mlolongo wa kurecharge umeme,mteja ataweza kununua umeme popote alipo na ukawaka nyumbani bila tabu,litaokoa muda.

Huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia, twende na Mabadiliko, tuwe wabunifu.
 
Huu mchezo wa kuwapandisha wateja ngazi ili kuingiza token za umeme ufike mwisho, kuna watu wameshaanguka na kuumia vibaya, kuna wengine hadi wamepata miscarriage lakini nyie mnaona sawa tu.

Hatua ya haraka na ya dharura tunayohitaji ni Meter zote za zamani ambazo ni lazima upande ili kuingiza token, ziunganishwe na vimashine vya mkononi ili mteja aweze kuingiza token akiwa sebuleni kwake bila kuhitaji ngazi.

Pili, ufanyike mchakato wa muda wa kati wa kubadilisha huo mfumo wa kukodi ili mtu anapolipia umeme popote pale, meter ijiwashe yenyewe bila kuhitaji kuingiza token, hata kama nipo Dar na Meter ipo Mwanza, iwake yenyewe automatically. Mbona ving’amuzi tunalipia na hatuingizi token?

Natoa miezi sita tu, baada ya hapo nitaanza kuiba umeme kwa kuunganisha direct ili mkose kabisa!
 
Back
Top Bottom