Afungwa Kifungo cha Maisha Baada ya Kulipiwa Umeme (Luku) kwa Simu ya Magaidi

Mdakuzi

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
3,460
4,231
Unakumbuka tukio la kigaidi lililotokea Kampala, Uganda wakati wa mechi ya fainali ya World Cup 2010, kati ya Spain na Holland?

Tukio lile lilimfanya mtangazaji wa Radio Salaam FM ya Mombasa, Habib Suleiman Njoroge kuingizwa kwenye kesi ya ugaidi wa tukio lile, na sasa anatumikia kifungo cha maisha.

- Unajua Ilikuwaje?

Mara tu baada ya lile tukio, vikosi vya upelelezi vya MI6 na FBI ni miongoni mwa vikosi vilivyoalikwa ili kufanya uchunguzi, kwa ajili ya kufanikisha kuwanasa wahusika wote.

Jambo la kwanza waligundua mabomu yote yaliyotumika katika tukio lile yaliundwa Mombasa nchini Kenya, na yakasafirishwa kwa basi hadi Malaba, mpakani mwa Kenya na Uganda.

Kisha, Mtanzania (Seleman Hijar Nyamandondo) aliyasafirisha hadi Kampala kwa gari aina ya Land Qruiser (Pickup) na kuyafikisha kwa aliyekuwa Msuka Mipango Mkuu, Issa Ahmed Luyima.

- Alivyoingizwa Mtangazaji!

Vikosi hivyo vya uchunguzi vilibaini, moja ya simu (device) zilizowasiliana na waliolipua mabomu yale, bado ilikuwa ikitumika huko maeneo ya Ukambani, nchini Kenya kwa namba tofauti na ya awali.

Kazi ya kuisaka simu hiyo ikaanza na ikanaswa ikiwa mikononi mwa mchuuzi wa sokoni, Mohamed Adan Abdow naye akiuziwa na Mtanzania, Husein Agade huku akiwa sokoni hapo.

Baada ya simu (device) hiyo kunaswa na kufanyiwa uchunguzi ikagundulika kwamba, iliwahi kufanya huduma ya kununua umeme (kama Luku), wa mita ya nyumba anayoishi mtangazaji huyo, Njoroge iliyopo Mombasa.

Hilo liliwatosha wachunguzi hao kuamini kwamba magaidi hao waliishi kwenye nyumba ya Njoroge wakati wakiunda mabomu hayo na ndiyo maana waliwajibika kulipa bili ya umeme.

- Funzo Kuu
Hiki kilichotokea kwa mtangazaji, Njoroge ni kama ambavyo mhalifu yeyote angelipia kisimbuzi chako au umeme wa mita yako kwa simu yake na moja kwa moja ukaingizwa mtegoni, endapo simu yake itachunguzwa.

Hivyo, si vema kupokea huduma za kulipiwa vifaa vyako vya nyumbani pasipo kumjua vizuri unayemwomba akulipie.

Ova
 
iNawezekana si yeye lakini aliwasaidia
 
Mzee kuna vitu zaidi walijua, sio rahisi et ufungwe kisa umenunulia mtu umeme kwa simu yako, mana hakuna sheria inayokataza, tena mbele ya M16 na CIA, huyo mtu alikuwa na deep connection na hao wahusika, bongo hapa yule ambae gereji yake ilitumika mbona aliachiwa? Hawakufungi kizembe hao jamaa, ukinaswa jua upo kweli
 
Story nzuri, uandishi mzuri.

Lakini natamani kufahamu zaidi, utetezi wake ulikuwaje? Aliongelea vipi suala hilo?

Japo nimewahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa hizi kazi kuwa kila mhalifu huacha alama, na hii ndio ilikuwa alama yenyewe.
 
Asante b... kwa pongezi. Kwangu ombi lako ni sawa na agizo. Nitafanyia kazi hilo ili kukidhi kiu yako.

Ova
 
Back
Top Bottom