kelphin
JF-Expert Member
- Dec 24, 2019
- 9,120
- 14,492
Moja ya mambo ambayo yamekua changamoto kwa wadau wengi ni malalamiko juu ya umeme kuisha haraka pasipokujua nini sababu.
Leo kelphin ntakupa au ntakukumbusha jambo moja au zaidi ya kuzingatia. Ikiwa kuna mdau yupo anafahamu zaidi anaweza kuongezea pia.
Vifaa vyote vinavyotumia umeme hupimwa kwa watts. Watts nyingi maana yake kitatumia umeme mwingi kuzidi chenye watts chache.
Hatuongelei ukubwa wa muonekano wa kifaa tunaongelea watts zake..
Hivyo kinaweza kua kidogo kwa umbo ila kikawa kinatumia umeme mwingi kuzidi kile kikubwa kwa umbo.
Watu wengi husema”yaani sina fridge ila umeme wangu unaisha sana”
Wanasahau ya kua fridge za kisasa nyingi sasahivi vinamfumo wa kisasa wakufanya zitumie umeme mchache
Hivyo ununuapo vifaa vyako basi yakupasa sana uzingatie watts zake
Japo kua baadhi ya makampuni huandika uwongo juu ya vifaa vyao
Hivyo unashauriwa kununua vifaa kutoka kwenye makampuni yakuaminika zaidi
LAKINI pia watu wengi hupuuzia earthing ya nyumba zao
Na pengine sio mala moja kupita kwenye nyumba nyingi na kukuta earth wire imekatwa na watoto wala usizingatie.
Ila earth wire inapokatwa hushindwa kukusaidia kulinda vifaa vyako wakati wa mvua na radi bali ku balance utembeaji wa umeme wako pindi waya zako zinapopoteza ubora wake
Hivyo fuatilia earthing system yako
Hakikisha kile chuma kilichofukiwa aridhini kipo na hakijaliwa na kutu.
Kuna muda panya hutafuna waya kisha earth wire inagusana na live wire
Kitu kitakachopelekea earth kubeba umeme na kupeleka aridhini
(Hapa umeme hukimbia pasipo mfano).
Je, utajuaje kama earth yako inatumia umeme wako? Hapa panaitaji utaalamu kidogo. Itakubidi upime voltage kati ya live na earth na hakikisha unapata 220ACV kama upimavyo live na neutral.
Ukiona hupati hivyo Pima neutral na earth ukiona inasoma 220ACV basi jua earth yako inadaka umeme
Shughulikia hilo haraka iwezekanavyo.
Pia tumia njia hi: Zima kila kitu (usichomeke hata charge ya simu)…kisha angalia kama units zako zinapungua, kama ndio basi yawezekana umeme wako unavuja …hivyo ita fundi aangalie mfumo wako wa earth.
Lakini pia kumekua na changamoto kidogo juu ya utumiaji wa umeme juu ya mtu mmoja kwa mwingine kwenye nyumba za kupanga.
Jambo hili yaweza kua vigumu kidogo kulitolea majibu ya mojakwa moja kwakua huwezi jua matumizi ya mtu ndani kwake na suruhisho la jambo hili ni kila mtu kutumia mita yake.
Thus ukipita baadhi ya nyumba watu huvuta mita zao pekee(separation meter)
Ikumbukwe kua kazi ya meter ya Tanesco ni kupima matumizi yako ya umeme kulinganishwa na vifaa vyako
Hivyo vilevile unavyoongeza kuwasha vifaa vyako na kuvitumia kwa muda mrefu ndivyo unavyoongeza ulaji wako wa units zako.
Hivyo unashauriwa kuzima kabisa vifaa vyako pindi uonapo huvutumii(usiweke standby bali vizime kabisa)
Kwakua standby hupunguz tu ulaji na sio kukata 100%.
Lakini pia nkuongezee hili
Meter yako inauwezo wa kupima utumiaji wako wa umeme ..najua yaweza kua hujanielewa hapa.
Kadri unapowasha vitu vyako maana yake basi ndivyo unaruhusu mkondo wa umeme kutembea kwa wingi
Na meta inatambua, hivyo unaweza kuangalia mtililiko wa umeme kwa kuingiza code tu kulingana na meter yako.
Kama meter yako ni EDMI yaani inaanzia 430.. bonyeza 96 then ok
Itasoma current yako. Namba hizo zinakua kubwa kadri ya uwashavyo vifaa vyako na kua ndogo kadri ya uzimavyo vifaa vyako.
Hivyo basi ikiwa utazima kila kitu na kubonyeza 96 then oky na meter yako isiandike 000 basi yawezekana kuna shida kwenye wiring yako.
Nb code hizi hutofautiana kulingana na AINA ya meter yako.
Kwa wale wanaotumia meter za Inhemita yaani zenye 37… tutabonyeza 005 kisha ok
Karibu.