beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,325
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imebaini kuwa Shirika la Ndege (ATCL) lilipata hasara ya Sh60.24 bilioni kwa mwaka wa fedha 2019 /2020.

Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka ameyasema hayo leo Alhamis Februari 17, 2022 wakati akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Februari 2022.

Amesema katika uchambuzi wa kamati katika taarifa ya CAG kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2020 ulibaini kuwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ilikuwa na mtaji hasi Sh246.66 bilioni.

Amesema pamoja na changamoto za mtaji, ATCL imekuwa na ongezeko la deni la Sh152. 16 bilioni ambapo deni hilo linahusisha Sh70.94 bilioni (asilimia 47 ya deni lote), deni ambalo ATCL wanadaiwa na Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

Amesema kamati imefanya uchambuzi wa kina katika hesabu zilizokaguliwa za ATCL na kubaini kuwa ATCL ilipata hasara ya kiasi cha Sh60.24 bilioni kwa mwaka wa fedha 2019 /2020 hivyo kufanya hasara jumuifu tangu mwaka 2015/2016 kufikia Sh152.96 bilioni.

“Uwepo wa madeni ya muda mrefu ni kihatarishi cha uendelevu wa kampuni kwa siku zijazo. Kwa msingi huo, kihatarishi hicho kimesisitizwa kwa kina katika hati ya ukaguzi iliyotolewa na CAG katika hesabu za ATCL kwa mwaka wa fedha 2019/2020,”amesema.

Amesema CAG alitoa hati safi ya ukaguzi yenye masuala ya msisitizo (Unqualified audit opinion with emphasis of matter).

Kaboyoka amesema suala la msisitizo katika hati hiyo ya ukaguzi ni hoja ya mtaji na madeni ya ATCL hali ambayo inaweza kusababisha kampuni kushindwa kujiendesha kwa siku zijazo.

Amesema hoja nyingine ambazo zinachangia ATCL kutokuwa na ufanisi wa kutosha kifedha hadi sasa na uwepo wa madeni makubwa ya siku za nyuma ambayo hayajalipwa.

Aidha, kuna deni la kiasi cha Sh87.25 bilioni (Asilimia 59 ya deni lote) ambalo ni deni la Kampuni ya Wallis Trading Inc. iliyokuwa imeikodishia ATCL Ndege miaka ya nyuma.

Pia walibaini kutofikiwa kwa malengo ya kifedha ya kampuni kwa kiwango cha asilimia ambapo mwaka 2019/2020 ATCL ilipanga kupata mapato kiasi cha Sh661.64 bilioni.

Hata hivyo, walifanikiwa kupata mapato Sh157.60 bilioni hivyo kuathiri ufanisi wa kampuni.

Amesema wamebaini uwepo wa vifungu kadhaa vya kimkataba ambavyo vinasababisha ATCL kuongeza deni ikiwemo shirika hilo kuingia mkataba wa gharama za ukodishaji wa ndege Sh15.46 bilioni kati yake na TGFA kutokuwa na kipengele cha vihatarishi visivyotabirika.

Amesema gharama hiyo ilitokana na ukodishaji wa ndege ambazo hazikufanya kazi wakati wa kipindi cha janga la uviko - 19 kati ya Machi 15 na Juni 30, 2020.

Amesema endapo kipengele hicho kingekuwepo kwenye mkataba, ATCL wasingetozwa gharama hizo.

Pia amesema ATCL iliingia gharama mara mbili ya Sh16.97 bilioni kama gharama za matengenezo ya ndege kutokana na dosari za kimkataba kati yake na TGFA.

“Masuala hayo matatu kwa kiasi kikubwa ndiyo yaliyochangia kutofikiwa malengo na ufanisi wa ATCL kwa mwaka wa fedha 2019/2020,”amesema.

Chanzo: Mwananchi

Pia, soma:

 
Ndo maana nawashangaa wa machinga wanaomsifu Magufuli.
Yeye ndo kaongeza lundo la vijana wasio na ajira rasmi. Lakini hela akazipeleka kwingine kabisa kusipowakwamua.
Akajifanya ni mtetezi wao kwa kuwaweka juani.
Hela za ndege zingeweza kuwainua watu wangapi kiuchumi?
Tangu 2015 ni watu wangapi unaowajua wameinuka kiuchumi?
 
Mambo Sasa hadharani, yale mashirika yaliyokuwa yanatangazwa kutoa gawio kumbe yalikuwa yanapata hasara, awamu ya tano ilijiendesha kwa uwongo mkubwa sana na Siasa za kitapeli
IMG-20220217-WA0048.jpg
 
ATCL haiwez kupata faida in terms of cash . Tanzania ni nchi kubwa Sana kijiografia ni vema serikali ikakubali shirika litoe huduma Kama huduma Kwa Safar zote za ndani ili kuwezekana kuwa na nauli affordable Kwa Watanzania wengi. Mambo ya kusafir masaa 24 Kwa bus kutoka Bukoba mpaka Mbeya yanachosha Sana.
 
ATCL haiwez kupata faida in terms of cash . Tanzania ni nchi kubwa Sana kijiografia ni vema serikali ikakubali shirika litoe huduma Kama huduma Kwa Safar zote za ndani ili kuwezekana kuwa na nauli affordable Kwa Watanzania wengi. Mambo ya kusafir masaa 24 Kwa bus kutoka Bukoba mpaka Mbeya yanachosha Sana.

Kama ni huduma kwa nini bei ilivuka ya fastjet
 
ATCL ilikuwa na madeni makubwa ya kurithi ndiyo yanatosababisha ionekane hasara. Lakini ilikuwa inatengeneza faida. Acheni upotoshaji.
 
“Uwepo wa madeni ya muda mrefu ni kihatarishi cha uendelevu wa kampuni kwa siku zijazo. Kwa msingi huo, kihatarishi hicho kimesisitizwa kwa kina katika hati ya ukaguzi iliyotolewa na CAG katika hesabu za ATCL kwa mwaka wa fedha 2019/2020,”amesema.
PAC imejaa CCM watupu na kwahiyo hapa wanajaribu kuonesha hasara hii inatokana sana na Madeni ya Muda Mrefu na kuiepusha serikali na lawama lakini kwa mujibu wa Ripoti ya CAG, hata Variable Costs/Operational Costs zinazidu Revenues:-

Sehemu ya ripoti hiyo inasema:-
Katika kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) nilibaini kuwa, ingawa mapato yanayotokana na kusafirisha abiria na mizigo kwa ndege yaliongezeka kwa asilimia 41 hadi kufikia shilingi bilioni 157.60 katika mwaka wa fedha 2019/20 kutoka shilingi bilioni 111.67 mwaka wa fedha uliopita, matumizi yaliyohusiana moja kwa moja na usafirishaji wa abiria na mizigo yaliongezeka kwa asilimia 45 hadi kufikia shilingi bilioni 193.44 katika mwaka wa fedha 2019/20 kutoka shilingi bilioni 133.64 mwaka wa fedha uliopita.
Yaani, ATCL ilitumia Sh 193.44 Billion ili kutengeneza mapato ya Sh 157.60 Billion!!

Hizo Sh 193.44 HAZI-INCLUDE madeni ya nyuma wala fixed costs !!

Kwa maana nyingine...

...Hata pasingekuwa na madeni ya miaka ya nyuma bado ATCL ingekuwa imepata hasara ya zaidi ya Sh 35 Billion

Hii maana yake ni kwamba...

...Hata kama ndege zote ZOTE zile tungekuwa tumepewa bure na hivyo gharama za ununuzi kutoziingiza kwenye vitabu vyetu, bado ATCL ingekuwa imepata hasara hiyo Sh 35 Billion

Hii maana yake ni kwamba...

...Ukichanganya na Cost of Depreciation ya ndege, hasara yake itakuwa kubwa zaidi!

residentura
 
Ni upumbavu kusema ATCL ilipata hasara wakati huo huo ilikuwa ikidaiwa kiasi cha hatua chache ifilisiwe na pengine ndege ya raisi ingelichukuliwa kutokana na deni lile?

Na hii nchi asingalikuwa JPM, leo hii Shirika la umeme Tz tanesco lingelifiliska kabisaa nalo lingegawanwa na wadeni


Ukiondoa hiyo ya kufanya biasha na kulipa malimbikizi ya madeni kwenye mashirika ya serikali, ni lini yalijiendesha na yakapata faida?
 
Si Aliyekuwa Makamu ndio Rais ?, Atoe Maelezo au alikuwa likizo ? , Alishindwa hata kuwa whistle blower under the Carpet ? (Ashirikiane na Kigogo)
 
Mambo Sasa hadharani, yale mashirika yaliyokuwa yanatangazwa kutoa gawio kumbe yalikuwa yanapata hasara, awamu ya tano ilijiendesha kwa uwongo mkubwa sana na Siasa za kitapeliView attachment 2122191
Weka habari yote sio nusu nusu kupotosha watu, km huwezi wacha tukufafanulie.

1. 59% ya deni la ATCL ni deni la kurithi kutoka Awamu ya Vasco...na alietutia hii Hasara ni Mteule wa Vasco, DG wa ATCL enzi hizo David Mataka ambae aliingia Mkataba wa kimchongo wa Kukodi ndege na kampuni ya Wallis Tradings Inc...ndege ambayo haikuwahi kuruka ht mruko mmoja ikaenda garage na haikuwahi kurudi huku ss tukibaki na deni.

2. Enzi za JPM David Mataka alifunguliwa Kesi ya uhujumu Uchumi na Matumizi mabaya ya madaraka ila Tarehe 20/08/2021 Miezi 5 baada ya JPM kufariki bwana huyu akaachiwa kwa faini ya 8m huku akituachia mzigo wa madeni yanayo endelea kukua(accumulative loss)...km ilivyokua kwa singa singa mnamuachia mtu kwa vijisenti kiduchu then yy ametuachia deni la himilivu....

3. 41% ya deni lililobakia ni deni la wakala wa Ndege za Serikali(TGFA) anaeidai ATCL maana ATCL haimiliki ndege bali imekodishiwa...na hapa deni ni la taasisi moja ya serikali kuidai taasisi nyingine ya serikali...

4. This country is fool of thieves, midiocres, As* kissing na Chawa walioathirika na utumwa mambo leo.

5. Hii inchi inakosa watu wenye maono, uadilifu, uthubutu na Uchungu wa inchi...imebarikiwa watu wenye kuweka mbele maslahi binafsi na ya rafiki zao mbele ya Maslahi ya Taifa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom