Hapo naona kuna mgombea moja anaingia mitini, anaogopa atakujaulizwa akina Beny na Azori wako wapi na ni nani aliyeamurisha mgombea mwingine auwawe na kisha azikwe ndani ya masaa matatu.

Naona wagombea wawili tu ndio wanajitokeza kwenye mdahalo.
 
Nashauri tu kuwa mwaka huu kabla ya kuanza kuzunguka kufanya Kampeni kuwepo mdahalo kwa wagombea wakuu watatu.

Dr. John Pombe Magufuli aelezee mambo makuu aliyowatendea watanzania na mipango yake ya mbeleni.na lengo lake la kutaka kupanua zaidi. Huyu ni mgombea ambaye anapenda kuongea ila hajui aongee nini.

Tundu Antipas Lissu aelezee wapi aliposhindwa Magufuli na nini yeye ana mpango wa kuwafanyia watanzania.huyu ni mgombea mwenye sifa ya kuwa machachari na wakati mwingine anakimbia hadi kupitiliza kwao.

Bernard Camilius Membe aeleze wapi aliposgindwa Magufuli na nini yeye ana mpango wa kuwafanyiwa watanzania. huyu ni mgombea ambaye ana sifa za kuwa jasusi.amekosa mvuto kisiasa pamoja na jaribio la kumpamba sana.kifupi amepoa kama mate /udenda wa mgonjwa wa asubuhi.

Wawekwe hapo masaa mawili Taifa liwasikilize baada ya hapo kipyenga kipulizwe tukutane nao mitaani.
Jiwe hata akiwa Peke yake hawezi Kujieleza Sembuse Mdahalo?
Huyu anachoweza ni Ukatiri na Unyama tu. Sasa Baasi!
 
Utasikia kabadili wabongo kwenye Siasa ni wachache sana wanajali ni matumbo tu
 
Attachments

  • FC648C8D-08C7-4338-B81C-B92CA8A3D934.jpeg
    FC648C8D-08C7-4338-B81C-B92CA8A3D934.jpeg
    27.4 KB · Views: 1

Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa hoja zao tuulize maswali yetu wakiwa pamoja kwenye ukumbi mmoja tupate mgombea ambaye ni cream ili wanachi tuchague Rais makini ambaye atatavusha kwenye umaskini tulionao na kuweka sera zinazotekelezeka kwa weledi na maarifa yaliyotukuka.

Nawasilisha.

View attachment 1527961

View attachment 1527962

View attachment 1527963
 
Leo nilipata fursa ya kuangalia mdahalo kati ya Joe Biden na Donald Trump nikafikiria ingekuwa ni vizuri na nchi nyingine zikafuta utaratibu huu.

Sisi watu wa kawaida tukienda kwenye interview ya kazi tunapimwa kwa kuulizwa maswali. Mdahalo wa wagombea urais pia unatoa fursa kwa wananchi kupima vitu vingi kutoka kwa wagombea kama uwezo wa kufikiri, busara zao, jinsi gani watatekeleza ahadi zao n.k.

Nafikiri bila mdahalo wa wagombea urais wanasiasa hawawatendei haki wapiga kura.
 
Wakuu habari za jioni poleni kwa kutafuta na mihangaiko ya kutwa nzima. Mimi sina mengi ila nina imani humu kuna watumishi wa tume ya uchaguzi basi wafikishe salamu hizi, tunaomba mdahalo wa wagombea wote watakaoteuliwa kugombe Urais kuanzia, CCM, CHADEMA , ACT - Wazalendo nk ili tuwapime kwa hoja zao tuulize maswali yetu wakiwa pamoja kwenye ukumbi mmoja tupate mgombea ambaye ni cream ili wanachi tuchague Rais makini ambaye atatavusha kwenye umaskini tulionao na kuweka sera zinazotekelezeka kwa weledi na maarifa yaliyotukuka.

Nawasilisha.

View attachment 1527961

View attachment 1527962

View attachment 1527963
JPM akijibu swali langu nampigia kura yangu kwanini Serekali ilijiondoa kwenye Mkataba wa kuendesha Mambo yake kwa uwazi?
 
Back
Top Bottom