BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
Taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma

Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Tundu Lissu, akiwa pamoja na Mgombea wa Kiti cha Makamu wa Rais, Mhe. Salum Mwalim Juma Mwalim, muda huu wanaelekea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Uchaguzi House) jijini Dodoma kuwasilisha fomu zake za mapingamizi dhidi ya wagombea wengine katika nafasi ya Urais wa JMT, baada ya hapo atazungumza na Waandishi wa Habari Ofisi za Chadema, Kanda ya Kati, jijini Dodoma.

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Agosti 26, 2020

====

Tundu Lissu amewawekea Pingamizi Wagombea Wawili wa Urais. Amewawekea pingamizi Ibrahim Lipumba wa chama cha CUF na Dr. John Magufuli wa chama cha CCM.

Hadi muda unaisha, hakuna aliyemuwekea Pingamizi Tundu Lissu. Hivyo kaondoka na kuelekea Ofisi za CHADEMA za Kanda kuongea na Wanahabari.

Majibu ya Tume, soma: Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Zaidi, soma:
Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mgombea wa Urais

Uchaguzi 2020 - NEC imemteua Dkt. John Pombe Magufuli kugombea Urais na Mama Samia Suluhu Umakamu wa Rais kupitia CCM

Uchaguzi 2020 - Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA
IMG-20200826-WA0023.jpg
2498045_IMG_20200826_154344.jpg
 
Wawe waangalifu wasije kutekwa kabla hawajafika.

Hata huo mkutano wake na waandishi unaweza kuzuiwa ili kumfichia mtu fulani aibu.

Swali la kujiuliza hapa ni je, iwapo Magufuli, kama mgombea, atakuwa ni mmoja wa aliewekewa pingamiza, atajitetea kama mgombea au atajitetea kwa mwamvuli wa Ofisi ya Uraisi?

Binafsi naamini sheria itamtaka ajitetetee kama wagombea wengine.

Tusubiri.
 
Back
Top Bottom