Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu. Magufuli na Lipumba ni wagombea halali

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,792


Mkurugenzi wa Uchaguzi: Tume ya uchaguzi baada ya kupokea pingamizi dhidi ya wagombea hao, imewataarifu wawekewa pingamizi mapema iwezekanavyo na wahusika wamewasilisha utetezi wao.

Pingamizi dhidi ya mgombea wa CUF kwamba hakurudisha fomu kwa mujibu wa masharti yaliwekwa na sheria, tume baada ya kupitia sababu za pingamizi pamoja na utetezi uliotolewa imejiridhisha, Professa Ibrahim Haruna Lipumba amerejesha fomu zake kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi hivyo tume ya taifa ya uchaguzi imejiridhisha pingamizi halina msingi na imelitupilia mbali. Professa Ibrahim Lipumba anaendelea kuwa mgombea halali wa kiti cha Rais kupitia chama cha CUF.

Pingamizi dhidi ya mgombea wa CCM

  1. Mleta pingamizi anadai kwamba, mgombea Urais kwa tiketi ya CCM hakuambatanisha picha kwenye fomu ya uteuzi.
  2. Hakurudisha fomu ya uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria
Tume baada ya kupitia sababu za pingamizi zote mbili kwa pamoja na utetezi uliotolewa imejiridhisha kuwa, Dr. John Magufuli, Mgombea wa kiti cha Rais kupitia chama cha mapinduzi amerejesha fomu zake ambazo zimeambatanishwa pamoja na picha kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya tume ya Taifa ya uchaguzi, hivyo tume ya Taifa ya uchaguzi imejiridhisha kwamba pingamizi hizo hazina msingi wa kisheria na imezitupilia mbali kwa maana hiyo, Dr. Magufuli anaendelea kuwa mgombea halali wa kiti cha Rais kupitia chama cha Mapinduzi CCM.

Kwa mujibu wa kanuni ya 39 kanuni ndogo sita ya kanuni za uchaguzi wa Rais na wabunge za mwaka 2020, sababu za uamuzi huu wa tume watapewa kwa maandishi, aliyeweka na aliyewekewa pingamizi, kwa msingi wa uamuzi huu, vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu wa kiti cha Rais na makamu wa Rais vinabaki kuwa 15.

Imetolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi

Pia soma; Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba(CUF)


425AD27B-1B92-42DB-AE3D-A2643F469C64.jpeg

DBB35E5F-5258-4C19-94A9-619FD0D99D00.jpeg
 
Wanazidi kutushangaza!Tungekuwa na Tume Huru, huenda Magu asingekuwa mgombea leo.

Kwa mujibu wa Lissu, Tume ndio iitoa maelezo yanayopingana na sheria, na mgombea uraisi Magufuli, akafuata maelekezo hayo yanayopingana na sheria, maelezo ambayo Lissu yeye alikataa kuyafuata na fomu zake akataka zikahakikiwa na NEC kama sheria inavyoelekeza(alisoma kifungu husika kwa wanahabari).

Swali:Kama Lissu alikuwa wrong,mbona NEC hao hao walikubali kukagua form zake na kuzihakiki kwa maana ya kuhakiki wadhamini wake tofauti na mgombea Magufuli na Lipumba ambao form zao zilihakikiwa huko mikoani na wasimamizi wa majimbo na wakazigonga mihuru badala ya fomu hizo kuhakikiwa na NEC?

Hoja nyingine ya Lissu ni kuhusu siku ya kurudisha fomu ambayo ilikuwa ni jana, na ndio siku ambayo,kwa mujibu wa sheria, ilikuwa ni siku ya uteuzi. Sasa hao wagombea wengine licha ya fomu zao kuhakikiwa na watu wasiostahili kisheria,lakini bado ziliwasilishwa katika siku ambayo haikuwa siku ya uteuzi(kwa maelezo ya Lissu) na hilo,kwa mujibu wa Lissu, pia ni kukiuka sheria ya uchaguzi.

Lissu pia kaweka wazi kuwa kwa mujibu wa sheria,Tume wanaweza kutoa maelekezo, ila sheria hiyo hiyo inatamka kuwa maelezo hayo hayapaswi kuwa kinyume na sheria yenyewe.

All in all,wahusika wamepata funzo tena bila shaka ni funzo kubwa tu hasa kuhusu hizi sheria zetu..

Cha ajabu,wao katika kujibu, hawatufafanulii zaidi ya kusema tu wametupilia mbali na kwamba majibu yatatolewa kwa muweka pingamizi kwa maandishi.
 
Back
Top Bottom