Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Afadhali basi usanii wake angeufanyia hapa hapa nyumbani. Huko kwenye anga za kimataifa hakika anatuaibisha kwa kiwango cha kutisha.

Lakini tulimchagua wenyewe, kwa ujuha wetu wapiga kura, na pia shinikizo/ushawishi wa nguvu za mafisadi/mafia wa kibongo.
 
Huyu msanii ´kazi yake kula tu hela ya watanzania bila mpango. Kuonegzeka kwa ukusanyaji nadhani sio kipimo sahihi kuwa amepambana na Rushwa. Nadhani tunatakiwa kufahamu kiwango cha uwekezaji kilichopo na baada ya hapo ndio tufahamu kuwa mapato yatokanayo ni kiasi gani.

Wakati Mkapa anachukua nchi Dola moja ya kimarekani ilikuwa karibia Tsh 500, sasa ni 1200. Inamaana kama wakati ule tulikusanya Tsh 100,000, na leo tukikusanya Th 240,000 bado hakuna ongezeko. Kuna secta nyingi zimeuzwa: Hizi nazo zinaongeza wigo wa mapato lakini sio kuwa zinaonyesha kupungua kwa rushwa kwa zitakuwa tu chanzo cha mapato.

Nadhani kikwete angetuambia kuwa: Nimewezesha kukubali ufisadi unaofanyika tanzania japo kujulikana kidogo, lakini ameshindwa kupambana na mafisadi makubwa kwa kuwa yanamzidi kimo na anahofu kuwa huenda wakamwangusha 2010, kwa kuwa wao ndio waliompa urais na wala sio Watanzania.

Rais wa ajabu, sijui ana nini na marekani. Atuambie asindelee kutudanganya hata kama kama kuna bi.mdogo basi tujue!

Hapo ndipo kwenye point...Yeye anamaanisha mapato yameongezeka kwasababu anataka tuamini kuwa rushwa iko kwenye ukwepaji kodi pekee.

Hataki kusema kuwa ufisadi ndio umekomaa ndani ya utawala wake badala yake anazungumzia ongezeko la mapato ya ukusanyaji kodi peke yake na kudai kuwa eti ndio kigezo na kipimo chenye ku reflect kupungua kwa rushwa...Wapi bana....EPA na nchi wameuza wanadai eti ni chumvi?

DOLA BILIONI SABA NDANI YA MIAKA CHINI YA SABA ILIYOPITA NI ONGEZEKO LA CHUMVI?

KWANINI TUENDELEE KUFANYWA WATUMWA KWASABABU YA UOZA HUU WA UONGOZI WA WAAFRIKA?

Anapodai kuwa rushwa imeongezewa chumvi na kushangiliwa, then nina mashaka na hao waliohudhuria...Kama kipimo cha umasikini kinapimwa kwa kulinganishwa na rushwa...then rushwa si kwamba imeongezewa chumvi...Bali ni kwamba rushwa ndio maisha na hata Mh Rais mwenyewe(Alipata ushindi wa tsunami kwa rushwa za wanamtandao) hawezi kuona hilo na kwasababu hiyo Tatizo limekuwa kubwa zaidi na kwa ukweli tunahitaji mabadiliko ya hali ya juu.

Hao viongozi waliokutana na kuzungumza huko kwenye hicho kikao na kushangiliana wanakuwa na fikra gani wakishatoka nchini mwao?

Unajuwa ni muhimu sana tuwe tunawapima akili viongozi wetu...Maana hii sasa ni too much.

Wakisahfika huko kwa wazungu na kufanya vikao basi wanawageuka wananchi na kudai ni wajinga na hawastahili haki kwani wanaongezea chumvi kwenye makosa yao ya kuwauzia nchi kina SIN CLEARER...
 
This is incredible eti kweli alisema maneno hayo au? Anyways jana nilipata bahati ya kumuona cha kusema kimenishinda so far bado ninatafakari kwanza kabla ya kumwaga!
 
This is incredible eti kweli alisema maneno hayo au? Anyways jana nilipata bahati ya kumuona cha ksuema kimenishinda so far bado ninatafakari kwanza kabla ya kumwaga!

Mwaga tu we all know ni senior kilaza wewe sema tu .Jamaa ni mnafiki na mpenda masifa nadhani anasikilizia Tarime iko vipi ajipange kuonyesha kwamba analea demokrasia wakati Tossi anawatosa wana Tarime
 
Moja ya dalili za Serikali inayokula rushwa ni kushuka kwa mapato ya Serikali au Serikali kushindwa kukusanya mapato. Mapato yetu (Tanzania) yamekuwa yakiongezeka kila mwaka tokea tulipoingia madarakani," alisema Rais Kikwete na kushangiliwa.
...

Kikwete kweli anazidi kuchemsha..
duh si kasomea uchumi huyu rais au...
Rushwa inayozungumziwa na wananchi sio ongezeko la hesabu ya fedha zinavyokusanywa bali jinsi fedha hizo zinavyotumika, jinsi mikataba mipya inavyosainiwa, jinsi wananchi wanavyo lazimika kuhonga ili kupata vibali, nyaraka na hata sheria ambayo ni haki yao..

Besides, makusudio ya ukusanyaji kodi haulingani mwaka hadi mwaka... kila mwaka kuna miradi mipya inafunguliwa na haiwezekani kabisa Tanzania ya mwaka juzi iwe sawa na hii ya leo... hata mtoto hukua kwa umri na mfuko wa tumbo lake hukua kila siku..huwezi kupima afya yake kwa kutazama tofauti ya kiwango cha chakula anachokula mwaka hadi mwaka..Noo mkuu unachoambiwa mtoto huyu ana utapia mlo!...mpeleke hospital..
He is not getting it!...
 
Mficha uchi hazai na mdharau mwiba mguu huota tende. Sasa EPA, Richmond, na vinavyofanana na hivyo ni uchi na mwiba.

Tusubiri wakianza kuota tende tutawajua zaidi halafu tutarudi kwenye archieve kuhusu ufisadi tuone walisema nini na waliamua nini. Sidhani kama mtu mwenye busara ataizuia chafya.

Hata kama ufisadi haupo kwa kiasi kinachosemwa sii busara kusemea nchi za mbali wakati wenye nchi ni wananchi na sii wagaibuni. Huu ni usanii. Sawa na msanii awapo tour or something!

Oh ALLAH/Messiah come today!
 
Unajua katika hii safari ninaona mambo mengi sana, ninaona kundi kubwa maofisa wa bongo, wakisafiri back and forth wanachanja mapesa ya taifa hili kama vile wiki ijayo ni mwisho wa dunia, so pathetic kwamba Secret Service mmoja mweusi aliniita pembeni na kuniuliza, how rich is your counrty bro?

Ni ka mwambia I wish I could tell you the truth, aliponiangalia usoni tu alijua kuwa sikufurahishwa na lile swali, akaniuliza kuwa yeye na mkewe the night before wamekuwa wakijiuliza sana kuhusu mtizamo wetu wa wa-Afrika na political standing ya Jaluo, nikamwambia kuwa wengi tunamuunga mkono sana, lakini tusingependa kuwaonyesha wazungu wa US kwa sababu wasije wakakosa kumpigia kura, ila siku Jaluo atakapopata urais ndio wataziona our true colors! Mkulu alifurahi sana,

Now backo to the point, hivi hii serikali exactly wanachofanya ni nini? State Department wamepiga kelele mpaka wamechoka na kuhusu kuja na makundi makubwa ya wajumbe wa msafara wa rais, yaani watu ni wengi mpaka hotel haitoshi! Mpaka nafasi za ndege hazitoshi, imebidi wakulu wengine wasafiri kwa treni, wiki tatu zilizopita rais alikuwa DC, leo anarudi tena kutafuta nini?

Wakuu humu mote ni hela za walipa kodi zinachomwa kama makaratasi, for what hasa? Jana nimeona mabasi mengi sana New York yamepambwa na ads kuhusu Tanzania na utalii, swali la kujiuliza ni who is paying for?

Yaani Mungu Atunusuru tu na mabalaa hili Taifa!
 
Hii inaonyesha wazi kwamba Kikwete hana nia kabisa ya kupambana na rushwa kwa vile ana 'downplay severity' ya tatizo lenyewe.Pili anatuambia yeye kwamba ukusanyanyaji wa kodi ni mkubwa.Sawa,lakini inawezekana pasingekuwa na rushwa tungepata 'three times more',kama Sh.bill.900 kwa mwezi hivi.Mimi naamini kwamba hii figure ya 'around bill.300' tunayopewa sasa ni 'inflated' ili jamaa waweze kula!
 
eacart150908.jpg

Do I need to say more? 🙁
JMK you know that Tanzanians are not stupid.
 
Bubu ataka kusema,

Unajua hicho kikatuni kinazidi kuonyesha maana zaidi hasa ukizingatia kwamba viongozi wa nyuma toka Nyerere hadi Mkapa waliyafanya waliyoyafanya waki face corruption uso kwa uso lakini JK mkuu wetu kaupa kisogo hivyo hawezi kujua kilichombeba isipokuwa anajiona hewani akipaa!..
 
Nadhani watu waliomshangilia JK wakati akijibu hilo swali ndio vichaa zaidi. Mapato ya serikali yakiongezeka, si ndio rushwa inashamiri ili kuzila hizo hela nyingi vizuri?? Au??

Mkuu yeye angeongelea serikali inawafaidisha vipi wananchi na hela inazopata pamoja na misaada, sio kusema pesa ni nyingi??

Baada ya hela nyingi kukusanywa haya ni baadhi ya matumizi"""

Safari overseas :::: open budget yaani any cost powa tu
Magari ya viongozi :::: luxuru cars za kila aina
Masurufu::::: Rais kukaa nje ya kituo 90% ya time, hapo ni matumizi ya kufa mtu
Richmond check, Songas check, Dowans check ++ sababu wanarudi hawa kwa tetesi
Tanroads hapo ndio baba wa matumizi haramu bongo
Mikutano, warsha, seminars sijui blah blah hapo ndio usizungumze

Kwahiyo Mkuu JK tunataka value ya pesa yetu inavyotumika ndio kipimo cha rushwa mkuu.
 
"Moja ya dalili za Serikali inayokula rushwa ni kushuka kwa mapato ya Serikali au Serikali kushindwa kukusanya mapato. Mapato yetu (Tanzania) yamekuwa yakiongezeka kila mwaka tokea tulipoingia madarakani," alisema Rais Kikwete na kushangiliwa.

Ni nani hao waliomshangilia?

Anaposema mapato yameongezeka je matumizi? je Mtanzania kanufaika vipi kwa Serikali kuongezeka kwa mapato zaidi ya Mafisadi na Viongozi kujiongezea neema?

Kama ni mafanikio ya mapato, basi tunayaona kwenye safari zake za nje kila siku, maana nyakati zile Marais wetu walijifunga mkanda na kuachana na misafara nje ya nchi na kuwekeza nguvu zao kuzunguka ndani ya nchi kuleta maendeleo, mwenzetu Mkwere kajijengea sifa ya kuzunguka dunia mara nyingi kuliko kiongozi yeyote wa Afrika katika mudahuu mfupi aliopo madarakani.

Infact kama sitakuwa nimekosea, Kikwete kasafiri mara nyingi nje ya nchi hata kuliko Gordon Brown wa Uingereza!
 
Hapo ndipo kwenye point...Yeye anamaanisha mapato yameongezeka kwasababu anataka tuamini kuwa rushwa iko kwenye ukwepaji kodi pekee.

Hataki kusema kuwa ufisadi ndio umekomaa ndani ya utawala wake badala yake anazungumzia ongezeko la mapato ya ukusanyaji kodi peke yake na kudai kuwa eti ndio kigezo na kipimo chenye ku reflect kupungua kwa rushwa...Wapi bana....EPA na nchi wameuza wanadai eti ni chumvi?

DOLA BILIONI SABA NDANI YA MIAKA CHINI YA SABA ILIYOPITA NI ONGEZEKO LA CHUMVI?

KWANINI TUENDELEE KUFANYWA WATUMWA KWASABABU YA UOZA HUU WA UONGOZI WA WAAFRIKA?

Anapodai kuwa rushwa imeongezewa chumvi na kushangiliwa, then nina mashaka na hao waliohudhuria...Kama kipimo cha umasikini kinapimwa kwa kulinganishwa na rushwa...then rushwa si kwamba imeongezewa chumvi...Bali ni kwamba rushwa ndio maisha na hata Mh Rais mwenyewe(Alipata ushindi wa tsunami kwa rushwa za wanamtandao) hawezi kuona hilo na kwasababu hiyo Tatizo limekuwa kubwa zaidi na kwa ukweli tunahitaji mabadiliko ya hali ya juu.

Hao viongozi waliokutana na kuzungumza huko kwenye hicho kikao na kushangiliana wanakuwa na fikra gani wakishatoka nchini mwao?

Unajuwa ni muhimu sana tuwe tunawapima akili viongozi wetu...Maana hii sasa ni too much.

Wakisahfika huko kwa wazungu na kufanya vikao basi wanawageuka wananchi na kudai ni wajinga na hawastahili haki kwani wanaongezea chumvi kwenye makosa yao ya kuwauzia nchi kina SIN CLEARER...

King Kiki aliimba kitoto chaanza kutambaa, mimi nasema Kijana amekuwa na tumpe nyumba (mke, nyumba na gari)

JMushi, this is brilliant! good job young fella! sasa yale makonzi ya Mchungaji yamefanya kazi😉
 
Unajua katika hii safari ninaona mambo mengi sana, ninaona kundi kubwa maofisa wa bongo, wakisafiri back and forth wanachanja mapesa ya taifa hili kama vile wiki ijayo ni mwisho wa dunia, so pathetic kwamba Secret Service mmoja mweusi aliniita pembeni na kuniuliza, how rich is your counrty bro?

Ni ka mwambia I wish I could tell you the truth, aliponiangalia usoni tu alijua kuwa sikufurahishwa na lile swali, akaniuliza kuwa yeye na mkewe the night before wamekuwa wakijiuliza sana kuhusu mtizamo wetu wa wa-Afrika na political standing ya Jaluo, nikamwambia kuwa wengi tunamuunga mkono sana, lakini tusingependa kuwaonyesha wazungu wa US kwa sababu wasije wakakosa kumpigia kura, ila siku Jaluo atakapopata urais ndio wataziona our true colors! Mkulu alifurahi sana,

Now backo to the point, hivi hii serikali exactly wanachofanya ni nini? State Department wamepiga kelele mpaka wamechoka na kuhusu kuja na makundi makubwa ya wajumbe wa msafara wa rais, yaani watu ni wengi mpaka hotel haitoshi! Mpaka nafasi za ndege hazitoshi, imebidi wakulu wengine wasafiri kwa treni, wiki tatu zilizopita rais alikuwa DC, leo anarudi tena kutafuta nini?

Wakuu humu mote ni hela za walipa kodi zinachomwa kama makaratasi, for what hasa? Jana nimeona mabasi mengi sana New York yamepambwa na ads kuhusu Tanzania na utalii, swali la kujiuliza ni who is paying for?

Yaani Mungu Atunusuru tu na mabalaa hili Taifa!

Amerudi DC kuja kumalizia shopping ya Idd na Xmas. Halafu kama kawaida ya fisadi hatakutana na Watanzania. Si ajabu wamechaguliwa Watanzania wachache wanaojali sana kupiga picha na JMK kuliko yale yanayoendelea Tanzania halafu picha itatolewa na maelezo kwamba JMK alikutana na Watanzania alipokuwa US.
 
Quote: Mwawado

1. Mheshimiwa Rais atafunga mwaka 2008 kwa ziara ya kikazi huko America ya kusini.

2. Ziara ambayo itajumuisha Nchi za Brazil,Venezuela na Cuba,ziara hiyo itafanyika katikati ya Mwezi wa Novemba.

3. Atakapokuwa anarejea Nyumbani atapitia USA kwa ziara ya siku mbili.

4. Jana asubuhi 27/09/08 (Jumamosi) Rais amerejea New York akitokea Washington DC,baada ya kumaliza Ziara ya kikazi,Anatarajiwa kuondoka USA Jumapili jioni.
 
Yani huyu kiumbe JK ni wa ajabu mno..........kuongezeka kwa figures hakuonyeshi uhalisia wa kipato .......ange calculate kupata real increase kwa kuangalia inflation rate na currency value pamoja na kuangalia population ilivyo ongezeka halafu ndo atuambie tumeongeza kiasi gani!!!!!!oopps nilisahau na kutoa gharama za ukusanyaji!watoe maposho na moshahara pamoja na gharama za kuendesha mashangingi ya maofisa wa TRA then ndo apanue domo inginevyo ni USANII tu KAMA KAWA........
 
Quote: Mwawado

1. Mheshimiwa Rais atafunga mwaka 2008 kwa ziara ya kikazi huko America ya kusini.

2. Ziara ambayo itajumuisha Nchi za Brazil,Venezuela na Cuba,ziara hiyo itafanyika katikati ya Mwezi wa Novemba.

3. Atakapokuwa anarejea Nyumbani atapitia USA kwa ziara ya siku mbili.

4. Jana asubuhi 27/09/08 (Jumamosi) Rais amerejea New York akitokea Washington DC,baada ya kumaliza Ziara ya kikazi,Anatarajiwa kuondoka USA Jumapili jioni.

shein pia alifanya official visit cuba na nchi baadhi za north america muda haujapita mrefu...sasa hata hatujafanya evaluation ya mafanikio ya ziara ya makamu wa rais huko ...na yeye tena anaenda kufanya nini....???

huu sasa ni ujinga.....nywele zimenisimama mkuu kusikia tena bado mkuu ataenda tena marekani mwaka huu..kufanya nini!!!???......ana nini ..??

ingekuwa nigeria asingekuwa anafanya namna hii kwa sababu wanaume wangempindua...!!

well nchi yetu ni ya amani...kama akiendelea hivi itabidi section ya chama chake imuombe ajiuzulu.....!!!...at least akijua kuwa kuna mpango unasukwa wa kumuondoa kistaarabu ..atatulia nyumbani..na kuchapa kazi!!!
 
Quote: Mwawado

1. Mheshimiwa Rais atafunga mwaka 2008 kwa ziara ya kikazi huko America ya kusini.

QUOTE]

hivi na sisi majirani zetu kwenye mchaka mchaka wanaweza kuwa wanatuimba wimbo kama huu???

mchaka..mchaka ..chinjaa * 2

amini ...ahaa..ahaa..

amini ..ameolewa !

wapi?

ahaaaaaaa ahaaaa wapi?

huko ulaya!!

na nanii? ahaaaa ahaaaaaaaaa na nanii??

na mwingereza ...

wivu...ahaaaaaaaa ahaaaaaaaaa wivu..

wamkereketa..shingoni..ahaaaaaaaa ahaaa

heeeeeee ahhhhhhhhhhaa haha!!
 
Jamani wazee wa kijiwe. Naomba tukumbushane kuwa Kikwete aliingia madarakani kutokana na uzoefu wake kama waziri wa mambo ya nje, wizara aliyoongoza kwa zaidi ya miaka kumi. Kama waziri wa nje, ufanisi wa kazi yake ulitokana zaidi na yeye kukutana na viongozi wa nje hivyo alikuwa akisafiri nje sana. Kwa bahati mbaya ameshindwa kugundua kuwa rais wa nchi siyo sawa na waziri wa mambo ya nje. Kwa maana nyingine, ni kuwa hajui majukumu yake kama rais.

Baada ya kuongea hilo la safari za nje ambazo kwa kweli zimekithiri sana kwa kiongozi wa nchi maskini kama Tanzania, ngoja niende kenye mada yenyewe kuhusu ufanisi wake katika kupigana na rushwa. Nadhani amefanya kosa sana kuainisha kuwa anapiga vita rushwa kuliko Nyerere na Mwinyi; ni afadhali angesema kuwa amemzidi Mkapa. Wakati wa Nyerere tunafahamu kabisa kuwa kuna mawaziri wengi waliopoteza madaraka yao kutokana na wizara zao kuhusika na rushwa hata kama hawakuwa wao wenyewe. Wakati wa Mwinyi, Professor Malima aliula wa chuya kutokana na rushwa. Katika vipindi vyote vya Nyerere na Mwinyi, hatukuwa na rushwa za kiwango kikubwa kama zinazoendelea hivi sasa.

Wakati wa Mkapa ambapo ndipo viwango vya rushwa vilipopanda kwa kasi sana, na hakuna waziri aliyewajibishwa kutokana na rushwa. Professor Mbilinyi alitemeshwa uwaziri kutokana na presha ya bunge iliyoongozwa na Wassira wakati akiwa NCCR-Mageuzi.

Tangu Kikwete aingie madarakani, kiwango cha rushwa hakijatelemka kiasi cha kujivunia na wala hakuna kiongozi yeyote aliyekwisha wajibishwa kwa hilo. Lowasa, Karamagi na Msabaha waliwajibishwa kwa presha ya bunge na wala siyo raisi mwenyewe. Je inakuwaje leo atambe kuwa yeye anapigana vita dhidi ya rushwa kuliko waliomtangulia bila kutoa metrics zozote?
 
Back
Top Bottom