NMB, Naomba mnipe ufafanuzi kuhusu huduma yenu nzuri ya salary advance. Mimi ni mtumiaji mkubwa wa hii huduma na nikiri kuwa inanisaidia.

Lakini tatizo ni kwamba ndani ya hii miezi mitatu naona kuna mabadiliko hasi kwangu, yaani mmenipunguzia kiwango wakati mshahara wangu umeongezeka kutoka 955,000/= hadi 1,255,000/= kwa mwezi. Hapo awali mlikuwa mnanipa mpaka 200,000/= lkn sasa imepungua hadi 165,000/= . Naomba kujua tatizo ni nini?
 
Hongera angalau mmewapunguza wale maofisa mikopo waliokuwa wanadai rushwa ndoyo watoe mikopo hasa matawi ya kkoo
 
NMB, Naomba mnipe ufafanuzi kuhusu huduma yenu nzuri ya salary advance. Mimi ni mtumiaji mkubwa wa hii huduma na nikiri kuwa inanisaidia. Lakini tatizo ni kwamba ndani ya hii miezi mitatu naona kuna mabadiliko hasi kwangu, yaani mmenipunguzia kiwango wakati mshahara wangu umeongezeka kutoka 955,000/= hadi 1,255,000/= kwa mwezi. Hapo awali mlikuwa mnanipa mpaka 200,000/= lkn sasa imepungua hadi 165,000/= . Naomba kujua tatizo ni nini?
Wafuate whatsaap no 0747 333 444
 
-CRDB riba ya mikopo ni 13% kwa mwaka na kwa watumishi wanaruhusiwa kukopa,na wakalipa kwa miaka tano au sita hivi.
-NMB wao bado wanatoza riba ya 16% kwa mwaka.
-Wajasilia mali wengi,wanakimbilia CRDB,
-NMB inabidi wajitafakari au Benki kuu,iwe inatoa miongozo na kufanya udhibiti wa riba za mikopo
 
-CRDB riba ya mikopo ni 13% kwa mwaka na kwa watumishi wanaruhusiwa kukopa,na wakalipa kwa miaka tano au sita hivi.
-NMB wao bado wanatoza riba ya 16% kwa mwaka.
-Wajasilia mali wengi,wanakimbilia CRDB,
-NMB inabidi wajitafakari au Benki kuu,iwe inatoa miongozo na kufanya udhibiti wa riba za mikopo
miaka minane unaweza kukopa sawa na miezi 96
 
Mikopo kwa Watumishi na Wastaafu
1). Hongera kwa NMB kwa kutoa mikopo kwa Watumishi almaarafu kama SWL(Salary workers Loan) na Mikopo ya Wastaafu

2). Mikopo ya watumishi na Wastaafu,Ni miongoni mwa huduma za mikopo(product) inayotolewa na NMB ambayo recovery rate yake ni asilimia 100 kwa maana benki inakata monthly installment moja kwa moja,kwa hiyo risk of default Ni ndogo ukilinganisha na products zingine
.
3). SWL na Mikopo kwa Wastaafu,dhamana yake ni mshahara au pensheni ya kila Mwezi, kinachotakiwa mwajiri kukata na kuwasilisha Makati NMB au mfuko wa pensheni kupitishia mshahara au pensheni kwenye benki ya NMB.

Hali ilivyo hivi sasa:
-Mtumishi anaweza kukopa fedha ili kutatua matatizo yake na anaruhusiwa, kufanya topping up muda wowote kama,anakopesheka .
-NMB wakati mwingine, wanaweza kununua mkopo wa mtumishi, kutoka benki nyingine,na kulipwa topping up amount
-Wastaafu wanaruhusiwa kufanya topping up ya mkopo,baada ya kufanya marejesho ya miezi 6

Ushauri

-NMB ifirikirie kufanya topping up amount kwa Wastaafu,kama wanakopesheka, miezi 2 au 3 baada ya kuchukua mkopo -kama deni la mkopo halizidi mwaka mmoja , mstaafu ametimiza vigezo vingine vya kupata mkopo,ninashauri wapewe,kwa maana Wastaafu wengi kimekuwa Ni kilio chao.
 
Kimsingi mimi nililazimika kufungua akaunti NMB kwa sababu taasisi niliyokuwa nafanyia kazi ilikuwa na akaunti NMB hivyo kupata malipo kwetu sisi tuliokuwa benki nyingine ilikuwa shida.

Nilipata uhamisho na kadi yangu ya ATM iliisha muda wake na ikatumwa kwa tawi nililofungulia. Imekuwa changamoto kuipata hadi kadi emeexpire. Nimetembelea Tawi la NMB huku nilikohamia kwa zaidi ya mara nne. Nilijaza form za kurequest Kadi. Niliporudi after a month nikaambiwa kuwa ilikuwa haijafika.

Staff mmoja akanishauri nijaze form nyingine ili nitengenezewe kadi nyingine. Nikajaza. After a month hakuna kitu. Nikakuta staff mwingine akaniambia huwezi kupewa Kadi nyingine wakati hii iliyopo ipo kwenye mzunguko. Ngoja tujaze form tuiombe. Nikajaza. Hakuna Kadi.

Jana naenda wananiambia imeexpire na unatakiwa ujaze form upate Kadi nyingine.

1. Niwashauri tu NMB ni vyema pale front desk wawe wanakaa competent staff ambao wanafahamu taratibu za benki.

2. Jifunzeni kwa CRDB ambako unaweza kuchukua Kadi Tawi lolote unlike huu utaratibu wenu wa kutengeneza Kadi na kuituma kule mteja alikofungulia akaunti.

3. Jitahidi kufanya recruitment vyema ili kupunguza inept personnel ambao wanazidi kuharibu image ya benki.
 
NMB…Nimejaza fomu ya kufany online transcations…tangu mwaka jana. Nmefuatili hadi nimechoka. Naomba mnipe mhusika atakaye nisaidia Songea branch.
 
NMB huduma mbovu,wizi hasa wa loan officers ni wa wazi wazi kabisa tofauti na mabenk mengine,kubwa zaidi hamtaki wateja wenu wauze/ kufuta mikopo kuondokokana na hizo kero.

Mfano, ukichukua loan balance ya mwaka jana na ukachukua nyingine after some months,kwa nini halipungui? Ikipungua basi ni kwa kiwango kidogo sana? Binafsi na ndugu yangu yeyote mwenye NMB nitawashawishi waachane na Bank yemu
 
Nataka niwaulize swali hivi ukiingia kwenye ile app ya NMB click ukauliza salio pia kuna makato? Nimefanya kama mara tatu hivi naona 5000 imeondoka
 
Back
Top Bottom