Mimi kuna mfanyakazi wa nmb ametoa taarifa zangu za miamala ya fedha kwenye akaunt yangu kwa watu.

Nimemshitaki kwa meneja ila bado sijaridhika maana sina uhakika atachukuliwa hatua gani. Kama nmb imefikia mahali pa kuajiri watu wasio na uwezo hadi wanatoa siri za wateja wao hadharani kwa watu wengine, naiweka benki kwenye mabano.
 
hii ni financial insititution,humu ni mambo yanayohusiana na wateja moja kwa moja. sio lazima wajibie humu,naamini wanasoma na wanafanyia kazi. kama unataka mrejesho naona waneweka anuani zao hapo ama unaweza tembelea tawi lao ama hq,maadamu hupeleki fitina.

Mi nishawahi kuzinguliwa na afisa mmoja kuhusu kadi yangu kuletewa wanaicheleweshaa fu ananijibu hovyo,nilimwona meneja na huyo mhusika aliitwa mbele yangu na kuelekezwa. thanks a week later nilipata kadi.
 
Mi naomba mashine za kuhesabia pesa Na Sisi Wateja tuekewe maaana
Niliwahi kwenda kutoa million mbili tawi la Mtaa wa congo jamaa kanipiga laki Moja, kufika nlipo kusudia nahesabu pesa imepungu laki Moja , najua kwamba Natakiwa kuhesabia kabla ya kuondoka lakini kutokana Na foleni kubwA sikufanya hivyo, nkapiga Huduma kwa Wateja kuwashauri watuwekee mashine wakasema saws lkn Bado, naomba mtuwekee hizo mashine ile laki inaniuma sana.
 
NMB tafadhari tungependa kujua nafasi za tellers northern zone mlizotangaza toka mwezi wa tisa mpaka leo mbona kimnya au ndo ilikua njia ya kujitangaza tu huku hamna nafasi? Tafadharini saaana
 
Huu uzi labda kaweka mtu tu, sbb km wangeweka kwa nia ya kupata mrejesho wangekua wanajibu hoja hizi.
 
Nimefungua akaunti ya mtoto tangu 2013 mpaka leo sijapata atm card kwa nini,kila siku bado,bado,mpaka leo,
 
nyie NMB nyie sina hamu na nyie kabisa nlifungua account chap chap baada ya kuambiwa account ya mwanzo imefungiwa sasa namba yangu simu hamjaifuta toka mwezi wa saba mpaka sasa hivi haijafanyiwa chochote na yale mabarua mlionisumbua kuandika
 
NMb sijawaelewa kabisa nilienda mwezi wa sita kukooa nikawaonyesha salary slip inamakato wakakataa kunikopesha mpaka nimalize deni nikajitahidi nimalize deni nichukue mkopo niende, shamba ile nafika tu wanadai eti hatukopeshi tumepewa barua na serikali mpaka hapo baadae
 
Kuna wateja wa NMB wameomba mikopo kutoka taasisi nyingine, mikopo imepitishwa yapata wiki mbili hamjawaingizia pesa, tatizo ni nini ? Kwani malipo kutoka taasisi hizo yameshafanyika, ila mmebaki nyinyi kuwaingizia pesa hao Wateja.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Naomba kuuliza nilijiunga NMB mobile lkn line yangu ikapotea halafu nikarenew tena je hiyo nmb mobile itaendelea kufanya kazi?
 
NMB mbona card za visa zinasumbua Sana, shida ni nini? Kwa mfano jana wa kadi za njano walikuwa wanatoa pesa lakini viza na master card, zilikuwa zinagoma, hebu mtueleze shida ni nini?
 
Back
Top Bottom