Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

tanzania.jpg

Vyama vya upinzani bado sana..

Kunyoosha kidole au kukosoa si kazi kubwa kama kuendesha nchi. Baada ya kusema hivyo, napenda kusema ya kwamba, hizi zote ni kazi zinazoitaji kwenda sambamba. CCM pamoja na yote yanayotokea hivi sasa, bado ni chama madhubuti zaidi kuongoza nchi yetu kwa sasa. Tusijidanganye na mapenzi yetu ya vyama vya siasa, upizani (Chadema ,CUF nk..) hawako tayari kuchukua madaraka ya nchi kwa sasa. Ukweli ni kwamba vyama vya upinzani viko katika hali nzuri zaidi kujijenga na kuleta changamoto zaidi kwenye bunge letu katika hiki kipindi na kipindi kijacho.

Kukosolewa na kujirekebisha kwa chama ndiko kuna imarisha chama, kwa hiyo wale wana JF ambao hawataki kusikia vyama vyao vinakosolewa wanavidhoofisha vyama vyao.

Kuna mambo mengi tu tunayoweza kujivunia sisi watanzania, haya mambo yameletwa na wananchi chini ya uongozi wa CCM. Leo tunazungumzia ufisadi ambao ni pigo kubwa sana kwa jamii. Vyombo vya habari vimefanya kazi nzuri kuhamasisha wanachi kwa ujumla katika hili jambo. Sasa umefika wakati wa kuangalia mambo mengine muhimu pia. Wana JF na waandishi wa habari msijisahau mkawa kama nchi za magharibi na utangazaji wa habari mbaya tu(negative publicity) kuhusu Afrika au Tanzania (specifically). Au ni kwasababu ya kuishi au kusoma magharibi? Wana JF tuchambue mambo kwa uwazi zaidi kwa faida ya Jamii na sio vyama vya siasa.

Kuongoza nchi sio lelemama, nitatoa mfano mfupi tu wa HAMAS kule Palestine, hawa wamekua nguzo muhimu sana katika mapambano ya kivita zidi ya waisraeli, lakini walikua hawako tayari kutawala, sasa hivi,HAMAS wameshikilia GAZA na wanashindwa kuiendesha na kuendeleza mapambano vizuri kama zamani, wanapoteza wafuasi wao wengi (well this is another issue). Je ni kweli tuko tayari kumpa nchi jini huyu tusiyemjua??🙂


Let this stand on its own!!
 
Naona wamesha merge

RE:Vyama vya upinzani bado sana..

Imepoteza maana yake. Haya ndio niliyokua nikisema, Kwanini waiunganishe hii hapa? Inapoteza maana ya hii thread. Tunaanza kuwa na ukiritimba ata hapa? Nimeomba hii "Vyama vya upinzani bado sana.." Wengine hatuna chama, wala makundi...so I would rather stand on my own or not be involved!!

Acha vilio kama mtoto mchanga!

Nini kinakuzuia kuendelea kuchangia hapa?
 
Acha vilio kama mtoto mchanga!

Nini kinakuzuia kuendelea kuchangia hapa?

Joseph Mushi na mwenzako ambaye umeshazoea malumbano, kama hapo juu. Jamii inaitaji kupata fresh ideas, sio your narrow views kila siku. Kama huna cha kuchangia kaa kimpya..
 
Joseph Mushi na mwenzako ambaye umeshazoea malumbano, kama hapo juu. Jamii inaitaji kupata fresh ideas, sio your narrow views kila siku. Kama huna cha kuchangia kaa kimpya..

Unaanzisha thread halafu unashindwa mwenyewe cha kuchangia....
 
Lugha yako ni too commanding bana!
Hapo ndo shida!
 
Sisi chadema pamoja na matatizo hayo ya kutoka kwa Akwlimbe lakini hauyumbi,Akwilombe alikuwa mtu mdogo sana,pamoja na uzuri wake katika jukwaa,sie bado ni watu makini.


jaribu kuwa serious watu wanakata issue hapa ,kama huna la kusema unaweza kupita bila kusema lolote .Kuna hitajika mabadiliko ya makusudi kabisa na ya kuonekana .

Hivi hawa wanao lalamikia upinzani kila siku wao wamefanya nini ili kujaribu kuusaidia upinzani ?Kama wanaogopa kusakamwa na CCM je wapinzani si watu kama wao ?
 
Joseph Mushi na mwenzako ambaye umeshazoea malumbano, kama hapo juu. Jamii inaitaji kupata fresh ideas, sio your narrow views kila siku. Kama huna cha kuchangia kaa kimpya..

Sasa kwahiyo ulifikiri mimi nimeficha jina langu?
Ama unaona ufahari kutaja jina langu hapa JF kufikiri kwamba najificha?
Mi nakwambia niko serious...
Jk asipofanya something then tusionane wabaya!
 
Unaanzisha thread halafu unashindwa mwenyewe cha kuchangia....

Sijashindwa kuchangia, siku nyingine ukianzisha thread si lazima kuwa wewe ndio una majibu yote. Kukaa kimpya sio kuwa sijui, ninajifunza mengi nikisikiliza watu wengine sometimes..let other people express their opnion, hayo ndio matatizo ya madictator
 
Sasa kwahiyo ulifikiri mimi nimeficha jina langu?
Ama unaona ufahari kutaja jina langu hapa JF kufikiri kwamba najificha?
Mi nakwambia niko serious...
Jk asipofanya something then tusionane wabaya!

Najua hufichi jina lako (its a personal choice), kwa sababu ume mention facebook group (Good stuff!) uliyoanzisha hapa JF wewe mwenyewe.
 
Hala hala maisha ya watu yasiwe hatarini jamani!
Demokrasia iko wapi?
 
Kwasababu hata ndugu zangu wameshaanza kulalamika huko bongo wakinitaka niiondoe ile group niliyoianzisha huko facebook!
 
Ndugu zangu wasije wakaguswa!
Kwani issue itakuwa nyingine!
 
yooooooote 9, hongera kaka kwa post buku....aluta continua

Nashukuru Mkuu!
Ila seriously brother wangu uko bongo ananisihi sana nisiendelee na huu mpambano especially baada ya postings huko facebook!
Sasa inabidi nimpigie maana naona kama ame panic!
So yeye ana sisitiza kuwa mambo si mazuri huko bongo kuhusiana na issue hii nzima!
 
Kuna mchangiaji moja kwenye thread ingine anaitwa Kigarama. Yeye katoa maelezo mazuri sana kuhusu concept ya opposition ambayo nakubaliana nayo. Yeye anasema opposition ni dhana , na sio vyama vya siasa. Nafikiri tukilielewa hili kazi yetu inaweza ikawa rahisi kidogo.

Tatizo moja la Tanzania ni kufikiri kwamba kazi ya kuitoa CCM madarakani ni ya vyama vya upinzani pekee. Lakini uzoefu katika nchi zingine unaonyesha tofauti kabisa. Huko Zambia, Malawi, Kenya, Zimbabwe, na kwingineko ambako upinzani uliimarika na hata kushinda chama tawala tunaona kwamba forces nyingi zilishiriki zikiwemo, kwa uchache kabisa, jumuiya za kiraia (NGOs, Civil society organisations), Taasisi za dini, vyama vya wafanyakazi, wanafunzi, n.k. Kwetu tunafikiri kazi ya kuwakomboa wananchi kutoka kwenye makucha ya CCM ni ya vyama vya upinzani pekee. Binafsi sioni mwanga kabisa wa kuitoa CCM madarakani bila kuunganisha nguvu, sio tu za vyama vya upinzani, bali za kila mtu anayekerwa na mfumo uliopo tukiwemo sisi hapa katika JF. Siku tukigundua hili ni siku ambayo tutaacha kusema kwamba "upinzani bado kabisa" badala yake tunaweza kusema "sisi bado kabisa" kama tunafikiri bado CCM haijatuchosha vya kutosha!

Kwa hiyo ndugu Mapambano, usikwepe majukumu, kama CCM inakukera na unafikiri inafaa kutolewa madarakani, ujue kuwa kazi hii ni ya kwetu sote, na kama tumeishindwa usipate faraja kwamba walioshindwa ni wengine tu, wewe, mimi na wote wenye kukerwa na kuchoshwa na CCM ni mojawapo kabisa tulioshindwa kutekeleza wajibu huu! Tukielewa na kukubali hili tutakuwa tumepiga hatua moja mbele katika adhima yetu ya kumshinda adui CCM.
 
Nashangaa kwa huyu Bwana anaye msema vibaya Mbowe. Well pamoja na kwamba bado sijaamua kuwa mwanachama yeyote wa chama cha siasa lakini ninafurahia sera za Mbowe na Chadema yake. Nimeshangaa kwamba CCM katika manifesto yao ya 2005wameweka mambo mengi sana ambayo uchaguzi wa 1995 na 2000 waliyokuwa wanayapinga aliyokuwa anayanadi Bwana Mbowe.
Mimi nasubiri kuwa kiongozi huru pale bunge litakapopitisha sheria ya wagombea binafsi (maana nasikia jana mahakama imetupilia mbali rufani ya serikali kuhusiana na jambo hili)Nasubiri kuona muswada unapelekwa Bungeni soon.
Lakini pamoja na hayo sera za Chadema na Mbowe wake ni makini.
Shida ni kwamba hata siku moja msitegemee kusikia CCM wanazikubali waziwazi.
Nadhani ili tuwe na hakika nao tuwajaribu 2010 maana CCM tumewajaribu sana na tumeishia kuibiwa tu kila siku. Hatuwezi kuwahukumu watu ambao hatujawajaribu. 2008 tuwape Chadema uwanja, wakishindwa waondoke pia.
 
wapinzani:

Freeman Mbowe – failed in school, failed in business, failed in politics, and all this after being born in the royal family, the House of Mbowe. And he still has the audacity to vie for Presidency. In the current political state of play, he is irrelevant, and, as a HIPC (Heavily Indebted Party Chairman) he is finished as a politician


SOURCE hii hapa:
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=13378


ca31.jpg


j6.jpg
 
Back
Top Bottom