Nini hasa kilijiri mpaka Luteni Jenerali Imran Kombe akauliwa na Askari Polisi?

Suala jingine linaloniacha na maswali mengi ni hivi inakuaje Mkuu wa Usalama wa taifa hata kama amestaafu kutopewa ulinzi na Idara japo walau walinzi walau watatu?

Mazingira ya kazi yenyewe na ukiongezea kuwa alikuwa mkuu wa U"spy" , inakuwaje Idara isimpe ulinzi?
.
Vipi angetekwa na kwenda kuvujishwa siri za nchi? Ukizingatia Uzee halafu yuko peke yake?!!
 
Suala jingine linaloniacha na maswali mengi ni hivi inakuaje Mkuu wa Usalama wa taifa hata kama amestaafu kutopewa ulinzi na Idara japo walau walinzi walau watatu?

Mazingira ya kazi yenyewe na ukiongezea kuwa alikuwa mkuu wa U"spy" , inakuwaje Idara isimpe ulinzi?
.
Vipi angetekwa na kwenda kuvujishwa siri za nchi? Ukizingatia Uzee halafu yuko peke yake?!!
Maswali ya ki-spy
 
Hizo ndo Blunders zenyewe mkuu, mtu ambae ni jasusi tena cover ya ujasusi hana na alikuwa mkuu wa ujasusi idara haijampa ulinzi!

Uta juaje hiyo ndio njia sahihi ya kumfanya akae kimya Sababu anajua wakimtaka na hana Ulinzi inakuwa Simple !!?.

Kwa kifupi hizi Kazi sio kabisa ,kila unapo ota Mabawa ndio unajiweka kwenye target Muda wowote.
 
Mambo kama "Corridors of Power" au KITENGO na kadhalika ni masuala mazito sana.

Uzito huja baada ya mtu kukiuka misingi ya kuwepo masuala hayo mawili.

Kwenye viambaza vya utawala yaani "Corridors of power" kuna mambo mengi sana yanatendeka na sio tu yanahusu wanasiasa.

Mambo haya yanahusu uwezo ulo juu ya masuala kama maisha binafsi, familia na hata ushirikiano baina ya nchi jirani.

Maeneo hayo mawili yaani viambaza vya utawala na sehemu ya Kitengo vinashiba chakula kinachotoka kwenye taarifa kama za ujasusi ndani ya dini, hadhara na hata duru za Freemason.

Ujasusi barani Afrika umebobea sana kwenye hayo maeneo matatu na kila code inatumika hapo.

Nafikiri serikali ililipa fidia ya 600 milioni ambayo mahakama kuu chini ya jaji Mchome iliamuru.zilipwe na mjane wa marehemu Roseline na mwanae Sheila sasa wanaishi kwa amani ingawa wamemkosa mzee Kombe.

Mwenyezi Mungu airehemu roho ya Marehemu Luteni Jenerali Imrani Kombe shujaa wa vita vya Kagera vya kumng'oa nduli Amin.
Oooh sheila kombe Wa Stanbic bank... kumbee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sija maanisha hivyo Mkuu,wapo Watu wanao ona ni sawa kufanya Kazi flani na wapo wanao ona Kazi flani haiwafai kwa Sababu zao.Mimi nime tahadharisha kwa wale wanao fuata Mkumbo ,wahakikishe wame ziandaa Nyonga zao kabla ya kuruka Mto.
Kweli mkuu Cha muhimu mtu ajue majukumu yake na maadili ya kazi yake ili maisha yaende au vp mkuu??
 
Back
Top Bottom