Nini dhumuni la Serikali kuanzisha tahasusi hii ya biashara ikiwa na somo la 'Islamic Knowledge'?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Serikali kupitia TAMISEMI imetangaza ongezeko la tahasusi mpya kadhaa ambazo vijana wetu watatakiwa kusoma, nimeona nyingi haziridhishi labda zimewekwa kimkakati.

Moja ya tahasusi, si kwa ubaya, ila nadhani wengi tungependa kufahamu kuhusu hii combination mpya ya Biashara inayojumuisha masomo ya Economics, Business Studies na Islamic Knowledge. Hapo somo la Islamic Knowledge linahusika vipi na masuala ya biashara?

Ni bahati mbaya au makusudi. Huenda nimeachwa na mambo ya kisasa lakini kwangu bado haileti maana yoyote.

20240320_210902.jpg
 
Serikali kupitia TAMISEMI imetangaza ongezeko la tahasusi mpya kadhaa ambazo vijana wetu watatakiwa kusoma, nimeona nyingi haziridhishi labda zimewekwa kimkakati...
Hii nchi tatizo mambo muhimu ya kufanywa na wataalamu wa Elimu wanaachiwa wanasiasa ndio maana wanakuja na mawazo ya hovyo hovyo tu!

Ona mtu anakuja na wazo la kuwafanyisha walimu mitihani...! Jee hii ndio italeta msaada gani kwenye wanafunzi wanaohitimu?
 
..nadhani imewalenga zaidi wazanzibari (si kwa ubaya) .. uchumi wa bluu na biashara zaidi na nchi zenye kufuata Islamic laws , kwa kukusaidia ...kwenye list hiyo hiyo kaangalie mwisho nambari 58 Hadi 65 ..Kuna 'combinations' zenye masomo ya dini.

Huo ni mtizamo wangu. Simlazimishi mtu kuukubali wala simzuii kuukataa .
 
Serikali kupitia TAMISEMI imetangaza ongezeko la tahasusi mpya kadhaa ambazo vijana wetu watatakiwa kusoma, nimeona nyingi haziridhishi labda zimewekwa kimkakati...
Shida yenu mnakua na chuki za ndani, sasa hivi kuna Islamic Banking moja ya dokta zinazokua kwa kasi Duniani, kwa Tanzania PBZ, CRDB, KCB NA AMANA ZOTE ZINA VITENGO VYA ISLAMIC BANKING,

PIA KWA WAISLAMU HIJJA NI.NGUZO MUHIMU NA SAFARI ZA KWENDA HIJJA ZINAWAINGIZIA WATU MAMILIONI YA SHILINGI, MTU MMOJA KWENDA HIJJA NI ZAIDI YA MILIONI KUMI ACHILIA MBALI SAFARI ZA UMRA,

SASA LAZIMA UFAHAMU DINI SIO TU IBADA BALI NI BIASHARA NA NDIO MFUMO WA MAISHA , HUWEZI KUTOFAUTISHA MAISHA NA DINI
 
Back
Top Bottom