DOKEZO Kwanini Shule mpya za Sekondari na hususan za Vijijini hazifundishi Masomo ya ECONOMICS, COMMERCE na BOOKKEEPING?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Shule nyingi mpya za serikali zinazoanzishwa na zile za vijijini hazifundishi masomo ya biashara hususan Commerce, Bookkeeping na Economics? .

Mfano hivi karibuni serikali ilifungua shule mpya katika wilaya ya Mbinga kama vile BENAYA, NGUZO, KIPAPA, KILIMANI KATI, LAMATA, KAGUGU, N.K lakini hakuna shule hata shule moja yenye mchepuo wa Biashara. Vilevile shule zote za wilaya ya MBINGA hususan za vijijini hakuna shule yenyee mchepuo wa Biashara isipokuwa MATIRI SEKONDARI pekee. Vilevile shule mpya za A- LEVEL zinazoanzishwa hazina michepuo ya EGM, HGE na ECA mfano ni shule hizi mpya za wasichana za kila mkoa za LINDI GIRLS', DKT. SAMIA SULUHU HASSAN - RUVUMA, DAR ES SALAAM GIRLS', DR. SAMIA S.H -SONGWE Zina michepuo ya arts na sayansi pekee.

Hii ndo hali halisi iliyopo shule za sekondari za mijini ambazo ni chache ndo zinapewa kipaumbele kwenye masomo ya BIASHARA na kuziacha zile za vijijini.

Rai yangu kwa serikali hususan OR- TAMISEMI iajiri walimu wa masomo ya BIASHARA ambao ni wachache sana ambao kwa mujibu wa takwimu hawawezi kufika 1000 nchi nzima ili kuongeza idadi ya shule zenye michepuo ya biashara.

Vilevile kuongeza tahasusi za ECA, EGM NA HGE kwenye shule za sekondari mpya na zile za zamani ili kupunguza wimbi kubwa la wanafunzi wanaodailiwa kwenye tahasusi za HGL,HGK na HKL. Kwa sababu takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa masomo ya BIASHARA na UCHUMI kwa asilimia yanafundishwa kwenye shule zile kongwe kama vile UMBWE, AZANIA, WERUWERU, KIBAHA, NDANDA, MINAKI, SONGEA BOYS AND GIRLS, MTWARA GIRLS, LOLEZA,, NGANZA,N.K
 
CCM imechoka... Usitarajie jipya..
Haina budi kupumzishwa.
 
Hali hii imepelekea hata walimu wa masomk ya biashara kusota sanaa mitaani maana ni shule chache zimekuwa zikifundisha masomo hayo hivyo walimu wa masomo ya biashara wanakuwa hawaitajiki
 
Kipaumbele cha nchi ni masomo ya dini, angalia kwenye micheluo inayopendekezwa.
Masomo ya kilimo, biashara, hawauziki, viongozi wa Elimu wanaogopa maeneo Yao kuwa na ufaulu duni.
 
.

Rai yangu kwa serikali hususan OR- TAMISEMI iajiri walimu wa masomo ya BIASHARA ambao ni wachache sana ambao kwa mujibu wa takwimu hawawezi kufika 1000 nchi nzima ili kuongeza idadi ya shule zenye michepuo ya biashara.
Rai yako tumeipokea
Wacha kusubiri ajira za ualimu, jiajiri kijana fursa zipo nyingi za kilimo, ufugaji pia tumia elimu yako ya uchumi kufanya biashara
 
Back
Top Bottom