Nakubaliana na Serikali kuanzisha Kodi kwenye matangazo ya biashara mitandaoni. Wataanzani wanaharibu dhana nzima ya "digital marketing"

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Leo nimesikia kitu kilichonifurahisha sana kutoka wa waziri wa fedha wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 nalo ni kuja na mpango wa kuanza kukusanya Kodi kwenye matangazo ya biashara mitandaoni.

Sijajua kwa upande wa Serikali ukiachana na kukusanya Kodi kwenye matangazo hayo ni upi lakini kwangu mimi ni Jambo nililokuwa natamani kwa muda mrefu lije kwa sababu nina kisa cha mtu aliyenusurika kutapeliwa simu kupitia tangazo aliloliona mtandaoni.

Pia soma
Serikali kuanzisha mfumo wa kidigitali kukusanya kodi kwenye matangazo ya mitandao ya kijamii

Kisa chenyewe ni hiki : Kuna jamaa alikuwa anataka kununua simu.Akaona aingie kwenye mtandao wa Facebook ajaribu kutafuta wauzaji wa simu. Katika kutafuta tafuta akafanikiwa kupata muuzaji ambaye kwa aina ya simu aliyokuwa anahitaji alikuwa anauza kwa Bei nafuu. Muuzaji akamwambia tutakutumia mzigo ukilipia, jamaa akasema nataka nije mlipo nifanye malipo hapo na nikague mzigo. Wakakubaliana kwenda kuona mzigo ili anunue lakini alichoenda kukikuta kule ni kitu tofauti kabisa na kilichotangazwa, mzigo ulitangazwa 'new' lakini akaoneshwa 'used' na umechoka mbaya. Kuwauliza juu ya Jambo hilo walikuwa wanajichekesha tu.

Huo ni mfano mdogo wa matangazo yasiyojali thamani ya Bei, ubora na huduma yanavyovunja Imani ya watanzania kwa matumizi ya teknolojia katika suala zima la digital marketing

Hebu tufikirie mbali zaidi kwa huyu jamaa Kama angekubali kufanyiwa 'delivery' halafu analetewa kitu used tena kimechoka vibaya maumivu ambayo angesikia ,naamini ni makali sana.

Kwa wanaoagiza vitu China kupitia Alibaba au AliExpress watakuwa ni mashahidi wa ubora wa huduma na bidhaa na Kama kuna kasoro basi tunaweza kusema ni digital marketing. Leo hii ni rahisi kuamini ubora wa bidhaa kutoka China ambapo ni mbali sana kuliko kuamini ubora wa bidhaa kutoka Kariakoo. Kwa nini?

Kwa sababu 'digital marketing' ina mapungufu mengi sana kwenye nchi yetu na hii inatokana na udhibiti mdogo uliopo hivyo serikali kuja na mpango kwenye Jambo hili naliunga mkono asilimia zote. Kwa sababu:

Wafanyabiashara wa mikoani wengine wanaona Kariakoo ni Kama Guangzhou yao na wanapoona tangazo la biashara la mtu wa Kariakoo anafurahi kama wengine wanapoona matangazo Alibaba na kwingine hivyo Jambo hili litawasaidia kupata bidhaa bora.

Uwekezaji mpya wa bandari utakaofanywa na DP WORLD utasaidia kulikuza sana eneo la Kariakoo na kufanya Kariakoo kuwa kitovu cha biashara Afrika mashariki na Kati na biashara zikawa zinafanyika online kama zinavyofanyika sasa kutoka China. Matangazo ya hovyo ya biashara yatapunguza imani katika kuelekea huko.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni hakika kwenye Jambo hilo Rais Samia na Waziri Nchembe wapewe maua yao na mimi nawapa yakiwa bado mabichi kabisa.
 
Kwahio uwalipe instagram na TRA uwalipe pia? Sasa kuna maana gani ya teknolojia kukua? 🤣
Pengine hata haelewi anachozungumza, wakiambiwa walipe kodi, watapandisha bei.. ambapo badala ya mtu kutumia 30k kwa influencer wa Twitter au Insta anawalipa tu Insta au Twitter moja kwa moja... na tangazo linawafikia watu wengi kwa muda mfupi bila gharama za ziada.
 
Kwahio uwalipe instagram na TRA uwalipe pia? Sasa kuna maana gani ya teknolojia kukua? 🤣
Toka nje ya box utafakari upya. Uwekezaji kwenye bandari unakwenda kufungua nchi kwa kiwango kikubwa sana na Tanzania kuwa lango la biashara Afrika mashariki na Kati. Kama ambavyo tunaweka' order' Alibaba na mzigo unaletewa mpaka mlangoni bila kufika China ndio itakavyokua eneo Kama Kariakoo kwa baadae. Kwa matangazo ya ovyo yasiyojali thamani ya ubora, Bei au bidhaa yanayowekwa mitandaoni inawezekana tukachelewa sana. Kodi ni muhimu katika kudhibiti ' digital marketing'.
 
Kwahio uwalipe instagram na TRA uwalipe pia? Sasa kuna maana gani ya teknolojia kukua? 🤣
Toka nje ya box utafakari upya. Uwekezaji kwenye bandari unakwenda kufungua nchi kwa kiwango kikubwa sana na Tanzania kuwa lango la biashara Afrika mashariki na Kati. Kama ambavyo tunaweka' order' Alibaba na mzigo unaletewa mpaka mlangoni bila kufika China ndio itakavyokua eneo Kama Kariakoo kwa baadae. Kwa matangazo ya ovyo yasiyojali thamani ya ubora, Bei au bidhaa yanayowekwa mitandaoni inawezekana tukachelewa sana. Kodi ni muhimu katika kudhibiti ' digital marketing'.
 
Leo nimesikia kitu kilichonifurahisha sana kutoka wa waziri wa fedha wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 nalo ni kuja na mpango wa kuanza kukusanya Kodi kwenye matangazo ya biashara mitandaoni.

Sijajua kwa upande wa serikali ukiachana na kukusanya Kodi kwenye matangazo hayo ni upi lakini kwangu mimi ni Jambo nililokuwa natamani kwa muda mrefu lije kwa sababu nina kisa cha mtu aliyenusurika kutapeliwa simu kupitia tangazo aliloliona mtandaoni.

Kisa chenyewe ni hiki : Kuna jamaa alikuwa anataka kununua simu.Akaona aingie kwenye mtandao wa Facebook ajaribu kutafuta wauzaji wa simu. Katika kutafuta tafuta akafanikiwa kupata muuzaji ambaye kwa aina ya simu aliyokuwa anahitaji alikuwa anauza kwa Bei nafuu. Muuzaji akamwambia tutakutumia mzigo ukilipia, jamaa akasema nataka nije mlipo nifanye malipo hapo na nikague mzigo. Wakakubaliana kwenda kuona mzigo ili anunue lakini alichoenda kukikuta kule ni kitu tofauti kabisa na kilichotangazwa, mzigo ulitangazwa 'new' lakini akaoneshwa 'used' na umechoka mbaya. Kuwauliza juu ya Jambo hilo walikuwa wanajichekesha tu.

Huo ni mfano mdogo wa matangazo yasiyojali thamani ya Bei, ubora na huduma yanavyovunja Imani ya watanzania kwa matumizi ya teknolojia katika suala zima la digital marketing

Hebu tufikirie mbali zaidi kwa huyu jamaa Kama angekubali kufanyiwa 'delivery' halafu analetewa kitu used tena kimechoka vibaya maumivu ambayo angesikia ,naamini ni makali sana.

Kwa wanaoagiza vitu China kupitia Alibaba au AliExpress watakuwa ni mashahidi wa ubora wa huduma na bidhaa na Kama kuna kasoro basi tunaweza kusema ni digital marketing. Leo hii ni rahisi kuamini ubora wa bidhaa kutoka China ambapo ni mbali sana kuliko kuamini ubora wa bidhaa kutoka Kariakoo. Kwa nini?

Kwa sababu 'digital marketing' ina mapungufu mengi sana kwenye nchi yetu na hii inatokana na udhibiti mdogo uliopo hivyo serikali kuja na mpango kwenye Jambo hili naliunga mkono asilimia zote. Kwa sababu:

Wafanyabiashara wa mikoani wengine wanaona Kariakoo ni Kama Guangzhou yao na wanapoona tangazo la biashara la mtu wa Kariakoo anafurahi kama wengine wanapoona matangazo Alibaba na kwingine hivyo Jambo hili litawasaidia kupata bidhaa bora.

Uwekezaji mpya wa bandari utakaofanywa na DP WORLD utasaidia kulikuza sana eneo la Kariakoo na kufanya Kariakoo kuwa kitovu cha biashara Afrika mashariki na Kati na biashara zikawa zinafanyika online kama zinavyofanyika sasa kutoka China. Matangazo ya hovyo ya biashara yatapunguza imani katika kuelekea huko.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni hakika kwenye Jambo hilo Rais Samia na Waziri Nchembe wapewe maua yao na mimi nawapa yakiwa bado mabichi kabisa.
Kwa ww Mzee wa tawire sikushangai kwakweli...
 
Toka nje ya box utafakari upya. Uwekezaji kwenye bandari unakwenda kufungua nchi kwa kiwango kikubwa sana na Tanzania kuwa lango la biashara Afrika mashariki na Kati. Kama ambavyo tunaweka' order' Alibaba na mzigo unaletewa mpaka mlangoni bila kufika China ndio itakavyokua eneo Kama Kariakoo kwa baadae. Kwa matangazo ya ovyo yasiyojali thamani ya ubora, Bei au bidhaa yanayowekwa mitandaoni inawezekana tukachelewa sana. Kodi ni muhimu katika kudhibiti ' digital marketing'.
Kodi italipwa ofisini sio kwenye simu za watu. Watuache bana
 
Hivi kwanini tusibinafsishe bunge tu.. 😂🤣
Bunge tuwape DP world huenda tukapata matokeo afadhali kidogo🤣🤩
 
Nimesoma paragraph ya kwanza nikahamasika kuendelea kusoma nikakuta pumba kuanzia paragraph ya pili. Kwa akili zako zote umeona Wizara ya Fedha kupitia TRA watadhibiti utapeli kisa wanatoza kodi matangazo ya mitandaoni? TCRA na polisi kazi yao nini kama ni hivyo? Huoni kutoza kodi hadi matangazo ya mtandaoni ni kuzidi kumbinya mtanzania? Kumbuka kuna tozo ya Tsh 100 kwenye kila lita ya mafuta ya magari inakuja. Pia huu uzi ni kuhusu hiyo kodi au ni kuhusu DP World? Kiukweli hueleweki.
 
nchi ngumu hii kila siku wanakaa chini wanakuja na mbinu mpya ya kutumaliza watu wa chini.
 
Mwigulu aisee mimi sijawahi kumuelewa kabisa sijui kama ntakuja kumuelewa...anadumaza maendeleo ya Nchi wazi wazi kwa kodi zake za hovyo hovyo...
 
Back
Top Bottom