Kwenye biashara usiogope majina makubwa yaliyokutangulia; Hill water, mabasi ya Tilisho ni somo kubwa la kuingia sokoni ukiwa mpya

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Watu wengi tunaogopa kuanzisha biashara fulani kwa kuogopa kwamba ma giant wameshajaa hivyo hatutapata wateja.

Soko la maji ya kunywa lilikuwa limetawaliwa na kilimanjaro, kila sherehe ya harusi utakayoenda maji unakuta Kilimanjaro. Kila hotel kubwa ama bar kubwa maji unakuta kilimanjaro, leo hii kilimanjaro kakimbizwa sokoni.

Mitaani pia maji yalikuwa uhai, baadae akaja afya, ila hill water kaja mpya tu ila kawakimbiza sokoni.

Kwenye biashara ya ma bus. Nani aliwaza njia ya Moshi Arusha kuna bus zitakuja wazidi ma giant wa njia hiyo kwa miaka zaidi ya 20 yaani kilimanjaro express ama Dar express kwa wateja. TILISHO na yeye hakuogopa.. kaja sokoni mpya kwa mbinu ya wahudumu mabinti wapenda social media.. mwisho wa siku kaiteka njia bus zake kila siku zinajaa.

Hilo ndilo somo kubwa la biashara.

Usiogope waliokutangulia.
 
Kuna uchawi unaitwa "kata mbuga". Huu ukiupata hata urais unaweza kupata. Kwasabb unakufanya hata underground uonekane star na biashara mpya inaoneonekana kongwe.

Hill Water na Tiliisho Bus walikuja nikawapatia huo uchawi..

Kama unauhitaji uchawi huu nicheki inbox
 
Watu wengi tunaogopa kuanzisha biashara fulani kwa kuogopa kwamba ma giant wameshajaa hivyo hatutapata wateja.

Soko la maji ya kunywa lilikuwa limetawaliwa na kilimanjaro , kila sherehe ya harusi utakayoenda maji unakuta kilimanjaro. Kila hotel kubwa ama bar kubwa maji unakuta kilimanjaro.. leo hii kilimanjaro kakimbizwa sokoni

Mitaani pia maji yalikuwa uhai, baadae akaja afya.. ila hill water kaja mpya tu ila kawakimbiza sokoni.


Kwenye biashara ya ma bus. Nani aliwaza njia ya moshi arusha kuna bus zitakuja wazidi ma giant wa njia hiyo kwa miaka zaidi ya 20 yaani kilimanjaro express ama dar express kwa wateja. TILISHO na yeye hakuogopa.. kaja sokoni mpya kwa mbinu ya wahudumu mabinti wapenda social media.. mwisho wa siku kaiteka njia bus zake kila siku zinajaa


Hilo ndilo somo kubwa la biashara.

Usiogope waliokutangulia
Mtu alie kaa sokoni kwa muda mrefu kumpiku ufanye kazi ya ziada labda afanye uzembe kama Mengi alivyo fanya uzembe kwenye maji lakini kama angejua kwenda na wakati hata sasa angekuwa bado yuko sokoni.

Kwanza maji yake yalikuwa mazuri, maji yakulinganisha na maji ya Kilimanjaro ni afiya na odizungwa tu mengine ya kina mo jamo na wengine chumvi tupu
 
Juzi nimetoa 1000Tsh dukani wanipe maji
Nikashangaa napewa kilimanjaro 1 litre na chenji 300

Kutoka buku 2 hadi 700!!
Kilicho muumiza mengi alijisahau wenzake wakatumia mwanya huo lakini maji ya Kilimanjaro mpaka sasa bado ni bora zaidi pamoja na maji ya afya maji mengi yana chumvi akijipanga akashusha bei mbona bado jina analo tu mtu akikaa sokoni kwa muda mrefu kumshusha iko kazi labda afanye uzembe
 
Unaweza ukadhani ni mgeni kwenye biashara kumbe mdau ana miaka ya kutosha kwenye game alikuwa anausoma mchezo na kupata uzoefu.

Biashara haina kutoka ghafla. Ukiona mtu kapiga bingo kwenye biashara na bado yupo sokoni jua sio jambo la ghafla. Alijipanga kweli kweli.
 
Back
Top Bottom