Nimeibiwa leo; jifunze na wewe usiibiwe kama mimi

Nimeibiwa leo; jifunze na wewe usiibiwe kama mimi

Du, pole sana mkuu kwa yaliyokukuta!
Usi ipe RIP kwani bado inaenda kutumika, iombee maisha mema siku moja ukutane nayo tena,,,
 
nimekuelea muheshimiwa Mwizi
naomba basi unirudishie japo laini tu!
Nani bado anaweka simu exposed dirishani kwenye daladala?

Sema wewe ndio umejifunza, usituambie unatufundisha kitu ambacho hujui kama sisi hatukijui already.

Na ungeweza kugeuziwa kibao ukapigwa wewe mwizi trying to chase a kibaka down vichochoro roads.
Una mengi ya kujifunza, usijaribu kutufunza sisi.

 
View attachment 117202
Ilikuwa hivi;
Ilikuwa leo majira ya saa moja na nusu jioni,Nimetoka kwenye mihangaiko nimefika Ubungo ili nipande Daladala nyingine kuelekea Nyumbani,Daladala niliyopanda nikafanikiwa kupata siti ya dirishani ili nipunge upepo.

Tukiwa bado tuko kwenye mataa ninauchovu wa mwili na roho,ikanibidi nitoe simu yangu aina ya Nokia N97,nikaweka Headphone ili nisikilize radio kujua yaliyojiri duniani.Nikiwa bado natafuta masafa ya Radio,ghafla nikaona bonge la mkono kutokea nje likamata simu yangu na mtu kukimbia nayo.Nikajua tayari nimesha fanyiwa kamchezo si kazuri,haraka sana nikapita dilishani kumfata mwizi,nyuma ya daladala niliyokuwa nimepanda kulikuwa na gari kubwa la mizigo ambapo kwenye gari lile kulikuwa na vijana wa ziada,walipoona nimeshuka haraka nao wakashuka kunisaidia tukamfukuzia mwizi umbali kazaa lakini hatukufanikiwa.

Maskini simu yangu NOKIA N97,ikawa imeniacha kimwili.

Wana JF nawaombeni mchukue tahadhari msije mkajikuta mmeingia kwenye hii janga kama lilonikuta leo.

RIP SIMU YANGU

Asante kwa taarifa mkuu... Ulipotea sana! Karibu tena!
 
Na angekamatwa huyo
angejuta kuzaliwa;

Siku ukiwa na nafasi kula doria maeneo ya
ubungo uone wezi wanavyowaibia watu
then unaweza maliza hasira yako kwa kuwapa
kipigo kile kile cha kuleeee!.

Pole sana lakini.
 
Nakumbuka 2010 pale ESSO - ARUSHA tupo kwenye daladala majira kama ya saa 2 hv jioni, me nilikaa siti ya kwanza kabisa dirishani kule back beacher pembeni akiwa amekaa mama wa makamo na katoto kake huku kakichezea toy yake ya simu la kuwakawaka flani hv. Ghafla nikaona limkono lirefu kama shetani tokea nje ya dirisha kwenda kwa yule mama na kumnyang'anya mtoto toy yake..!
Nilibaki nimeduwaa na kushangaa jinsi yule kibaka alivyotoa mbio na lile toy.!
Yaani ni hatari sana.
 
View attachment 117202
ilikuwa hivi;
ilikuwa leo majira ya saa moja na nusu jioni,nimetoka kwenye mihangaiko nimefika ubungo ili nipande daladala nyingine kuelekea nyumbani,daladala niliyopanda nikafanikiwa kupata siti ya dirishani ili nipunge upepo.

Tukiwa bado tuko kwenye mataa ninauchovu wa mwili na roho,ikanibidi nitoe simu yangu aina ya nokia n97,nikaweka headphone ili nisikilize radio kujua yaliyojiri duniani.nikiwa bado natafuta masafa ya radio,ghafla nikaona bonge la mkono kutokea nje likamata simu yangu na mtu kukimbia nayo.nikajua tayari nimesha fanyiwa kamchezo si kazuri,haraka sana nikapita dilishani kumfata mwizi,nyuma ya daladala niliyokuwa nimepanda kulikuwa na gari kubwa la mizigo ambapo kwenye gari lile kulikuwa na vijana wa ziada,walipoona nimeshuka haraka nao wakashuka kunisaidia tukamfukuzia mwizi umbali kazaa lakini hatukufanikiwa.

Maskini simu yangu nokia n97,ikawa imeniacha kimwili.

Wana jf nawaombeni mchukue tahadhari msije mkajikuta mmeingia kwenye hii janga kama lilonikuta leo.

Rip simu yangu

pole mkuu.utapata nyingine tu
 
ahaa kumbe!....najua sijafunga ndoa na ushamba iposiku utaishaa tu mkuu polepole ndio mwendo

usimsikilize huyu ,
kuibiwa ni bahati mbaya, yoyote anaweza kuibiwa ni timing tu anayoitumia mwizi. wanaibiwa mabaunsa sembuse wewe uliyekuwa umejisahau na kuchoshwa kwa usafiri wa daladala na kazi za siku nzima.
 
Pole ila usirudie tena kuruka dirishani na kumkikmbiza mwizi ni hatari sana,ungepitiwa na bodaboda ama gari kabisa..kwani simu sh ngap bhana..mgerest in peace we na simu bure..
 
Nakumbuka 2010 pale ESSO - ARUSHA tupo kwenye daladala majira kama ya saa 2 hv jioni, me nilikaa siti ya kwanza kabisa dirishani kule back beacher pembeni akiwa amekaa mama wa makamo na katoto kake huku kakichezea toy yake ya simu la kuwakawaka flani hv. Ghafla nikaona limkono lirefu kama shetani tokea nje ya dirisha kwenda kwa yule mama na kumnyang'anya mtoto toy yake..!
Nilibaki nimeduwaa na kushangaa jinsi yule kibaka alivyotoa mbio na lile toy.!
Yaani ni hatari sana.
Hahahaa..umenichekesha sana mkuu hasa hapo kwenye red..umenikumbusha pia pale ubungo kuna jamaa lilikwapua Bible ndogo ya mmama wa watu akienda kanisani..jamaa lilidhani ni pochi afu likajirusha darajani..kidogo likufe
 
mkuu,
si kila wakati ni hivyo ulivyosema wakati mwingine mateso yanazidi mwanzo mwisho na hakuna wokovu kabisa

Nilikua namkumbusha signature yake, nimeyaona hayo maneno ndio maana nikayaweka....Ni kweli kabisa, haya mambo hayana kanuni!
 
pole sana. kuna wizi mwingine nilishuhudia kwa macho yangu wiki hii hii, nikiwa nje napunga upepo nyumbani, kuna mama alipita karibu na nyumbani kwangu akasimama akawa anaongea na simu, maongezi yake inaonekana yalikuwa marefu kidogo. ghafla, niliona vijana wawili wamepanda pikipiki wakaendesha pikipiki polepole kupita nyuma yake maana alikua pembeni na barabara, yule aliyepakiwa aliikwapua ile simu, na yule dereva alipasha moto pikipiki sijawahiona. ile mama kugeuka anayechukua simu nani tayari pikipiki ilikuwa inaondoka, akawa kama amepigwa na butwaa fulani, ile kuja kuanza kuita mwiziiiiii jamaa walikuwa wanapasha pikipiki inaenda mbio na mlio mkubwaaaaa, walitokomea na kelele za wizi zikipigwa na hawakukamatika. hawa vijana wa pikipiki aisee wanaiba kwa kupokonya, ukiwa unaongea na simu usijekujisahau mtu anaweza kuipitia na pikipiki kama mwewe.
 
Mkuu nahisi utakuwa hujazoea kupanda daladala, maana kwa sisi wazoefu kuna nyakati na maeneo ya kuweka simu hadharani na nyakati na maeneo ya kuisweka mbali sana.

Pole sana!!
 
hahahahahahahahahah..........mkuu huwezi amini jamaa kaingiza mkono ndani kama nusu mita,can you imagine kiasi gani jamaa alivyo professional kwenye fani
Mimi jamaa alichukua simu yangu bila hata kunigusa,yaani sijui mafunzo wanachukulia wapi!
 
Pole sana. Ndo maana nikiona wanavalishwa tairi na kuchomwa siwahurumii.
Arusha hiyo ni kazi maalum inafanyika eneo la tengeru,mabasi hata ya mikoani yakifika pale abiria wanatangaziwa wafiche simu maana pale lazima ulizwe.

Dah tengeru ni noma dereva huwa anatangaza kabisa kila abiria kuficha simu mana hutaona hata alipotokea mwiz
 
Simu ununue wewe,
Risiti unayo wewe,
Kutumia atumie mwingine
Kaka mbona MAJANGA...!!!!!!!!!

KARIBU TENGERU NA UNGA LTD (KIDDING)
 
Back
Top Bottom