Nimeibiwa leo; jifunze na wewe usiibiwe kama mimi

Nimeibiwa leo; jifunze na wewe usiibiwe kama mimi

Pole kaka simu inauma kaka ukiibiwa mfano mim mwenyewe nliibiwa cm huku ikiwa ckioni naongea na mtu nkajtahd kumfuata nikakutana na bonge la bisbis nkagive up mtoto wa watu yaani walaaniwe kabisa hawa vjana wa kikwete

Ha ha ha ha sema alaaniwe jk.
 
Kanunue simu nyingine! na kiherehere cha kucheza na masimu kwenye madirisha ya madaladala mkome! nyie ndo wale mnaotupigia kelele za manyimbo ya kina diamond kwenye daladala! Ingia kwenye hiace,tulia ufike unakokwenda ndo uanze kucheza na masimu yako.
 
Pole ila unge wasaka hao mateja wahapo ukajifanya unataka simu ya kanyanka ungeuziwa ileile simu yako
 
mjini shule kaka
maeneo kama ubungo, buguruni,kinondoni manyanya pale sio sehemu ya kushika simu mkononi
pia maeneo kama posta mpya unapopanda daladala za kugombani kuwa makini
 
ina-sound kama ndo mara ya kwanza unaingia jijini. huu wizi wa kawaida kabisa. katiza pale Karume utaona mtu anazunguka kama anataka kutoa maelekezo kumbe anazengea cheni za madada kwenye daladala.
 
Du, pole sana kamanda wangu. Ni kweli siku hizi kuna wakwapuaji wengi tu hasa kwenye maeneo yenye traffic jams. Kuna siku nimeshuhudia mtu anaibiwa chain wakati gari likiwa kwenye foleni maeneo ya kariako. Kibaka alipita karibu na dirisha la gari, akakata chain ya dada aliyekuwa amekaa kwenye seat ya dirishani na kutokomea nayo taratibu bila wasiswasi. Dada wa watu akabaki tu anamsindikiza kwa macho. Abiria walishuhudia tukio lile lakini, kwa jinsi gari lilivyokuwa limeshona, hakuna aliyethubutu kushuka kumfuata kibaka yule. Ilikuwa kama sinema!

Kuweni makini wandugu. Wakwapuaji wa namana hiyo wapo sana na wana timing ya hatari hata zaidi ya kipanga anavyomtaimu kifaranga wa kuku. Mimi niliwahi kuibiwa simu usiku wakati natoka kazini. Nikiwa ndani ya gari na nikiwa nimeketi kwenye seat karibu na dirisha, nikawa nimeshika simu yangu na-browse internet. Tukafika mahali barabara sio nzuri hivyo dereva akawa anaendesha gari kwa mwendokasi mdogo. Ghafla bin vuu nikaona kono la kibaka linachomoza kwenye dirisha. Kutahamaki, simu yanagu imekwapuliwa---kibaka huyoooooo anatokomea gizani!!!!! Iliniuma sana kupoteza simu yangu na laini iliyokuwa na contacts kibao. Kwa kuwa laini ilikuwa na salio la kufa mtu, nikapiga simu customer care wakaifunga. Keshoye nikaenda kuswapu laini na kuingia gharama ya kununua simu mpya, achilia mbali kupoteza contacts muhimu.

Siku nikuwakuta wananchi wenye hasira wanamchapa kibaka yeyote, nitajitolea kununua lita 10 za mafuta ili tumalize mchezo mapema. Sina hamu na vibaka tena!
 
Mie bwana nilikuwa nimeshakuhurumia. But ulipoandika R.I.P simu yako nikajichekea.
 
Pole sana nadhani siku nyingine utakuwa makini.
 
pole sana mkuu,wizi wa namna hiyo upo sana maeneo ya mwenge,manzese na bunju b (mahakama ya simu)
 
pole lakini huo ni ushamba, umekuja lini mjini? hiyo mbona ni style ya siku nyingi iliyokata wasichana masikio yao kwa kukwapuliwa heleni zao madirishani? Kaa na liushamba lako
 
Pole mkuu. Kwa mafundisho niliyowahi kupata sehemu fulani hiyo inaitwa GIVING (kutoa). Mtu utatoa kwa njia yoyote hata kwa kuibiwa. Jenga mazoea ya kutoa bila kulazimishwa.
 
Back
Top Bottom