Ruhazwe JR
JF-Expert Member
- Jan 31, 2011
- 3,402
- 944

Ilikuwa hivi;
Ilikuwa leo majira ya saa moja na nusu jioni,Nimetoka kwenye mihangaiko nimefika Ubungo ili nipande Daladala nyingine kuelekea Nyumbani,Daladala niliyopanda nikafanikiwa kupata siti ya dirishani ili nipunge upepo.
Tukiwa bado tuko kwenye mataa ninauchovu wa mwili na roho,ikanibidi nitoe simu yangu aina ya Nokia N97,nikaweka Headphone ili nisikilize radio kujua yaliyojiri duniani.Nikiwa bado natafuta masafa ya Radio,ghafla nikaona bonge la mkono kutokea nje likamata simu yangu na mtu kukimbia nayo.Nikajua tayari nimesha fanyiwa kamchezo si kazuri,haraka sana nikapita dilishani kumfata mwizi,nyuma ya daladala niliyokuwa nimepanda kulikuwa na gari kubwa la mizigo ambapo kwenye gari lile kulikuwa na vijana wa ziada,walipoona nimeshuka haraka nao wakashuka kunisaidia tukamfukuzia mwizi umbali kazaa lakini hatukufanikiwa.
Maskini simu yangu NOKIA N97,ikawa imeniacha kimwili.
Wana JF nawaombeni mchukue tahadhari msije mkajikuta mmeingia kwenye hii janga kama lilonikuta leo.
RIP SIMU YANGU