EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,356
Dah R.I.P simu yetu..........
Anatuyeyusha huyo nilikuwepo eneo la tukio na issue nzima ilikuwa hivi.
Dah R.I.P simu yetu..........
Pole ndugu pole sana jamaa wanatiming mbaya ni aina ya wizi flani wakijinga sana hasa ukiibiwa!
Kuibiwa ni ushamba
Anatuyeyusha huyo nilikuwepo eneo la tukio na issue nzima ilikuwa hivi.
![]()
Wewe ni Mtanzania kweli? Maana nachoamini watanzania tunaibiwa sana hasa rasilimali zetu sasa sijui wewe uko kwenye kundi la wezi au wanaoibiwa?
Kama ulikuwa unatafuta masafa kwa kusogeza simu dirishani ulidhani upo angani?
Pole sana mkuu,hiyo simu ulikuwa unatumia mpaka unatupa,mie ninayo E71 toka 2008 hadi kesho. N-series,E-series ni kiboko.
Wewe ni Mtanzania kweli? Maana nachoamini watanzania tunaibiwa sana hasa rasilimali zetu sasa sijui wewe uko kwenye kundi la wezi au wanaoibiwa?
we badala ya kumpa pole mwenzio unamzidishia machungu hahahaaa, mie najiuliza tu nokia n7 sijui ina redio kumbe kama vitochi nilikuwa sijui.
Hongera
View attachment 117202
Ilikuwa hivi;
Ilikuwa leo majira ya saa moja na nusu jioni,Nimetoka kwenye mihangaiko nimefika Ubungo ili nipande Daladala nyingine kuelekea Nyumbani,Daladala niliyopanda nikafanikiwa kupata siti ya dirishani ili nipunge upepo.
Tukiwa bado tuko kwenye mataa ninauchovu wa mwili na roho,ikanibidi nitoe simu yangu aina ya Nokia N97,nikaweka Headphone ili nisikilize radio kujua yaliyojiri duniani.Nikiwa bado natafuta masafa ya Radio,ghafla nikaona bonge la mkono kutokea nje likamata simu yangu na mtu kukimbia nayo.Nikajua tayari nimesha fanyiwa kamchezo si kazuri,haraka sana nikapita dilishani kumfata mwizi,nyuma ya daladala niliyokuwa nimepanda kulikuwa na gari kubwa la mizigo ambapo kwenye gari lile kulikuwa na vijana wa ziada,walipoona nimeshuka haraka nao wakashuka kunisaidia tukamfukuzia mwizi umbali kazaa lakini hatukufanikiwa.
Maskini simu yangu NOKIA N97,ikawa imeniacha kimwili.
Wana JF nawaombeni mchukue tahadhari msije mkajikuta mmeingia kwenye hii janga kama lilonikuta leo.
RIP SIMU YANGU
pole ila hzo mbinu mbona za k long au uljsahau m2 wangu?
sasa JF umeingia kwa kutumia nini mkuu?Pc?
Dah! nilikuwa nikiwa na N97 najihisi kama laptop yani....R.I.P simu yangu