Mara nyingi sana, halafu jini bakora hakunipa tena, nilikua nafanya uhuni ujanani. Mwenyezi Mungu anisamehe sana. Kuujaribu huo nishaingia mpaka chooni kukoga na wanawake.
Sasa kuna mzizi huo anaujua babu yangu, sasa hivi anaujua yule shangazi yangu wa shamba. ni mti gani. Jini bakora anaujua lakini hanipi, anasema ikitokea kazi yake ndio atauleta, hanipi kukaa nao kabisa.
Huo ukimtia nao mtu mdomoni hata awe kapandisha wazimu au majini, sekunde hiohio anaishiwa nguvu anakua shwari kabisa na analala fofofo.
Shangazi yangu anasema ule ndio wanatumia wachawi na wanga kulaza watu wafanye kazi zao usiku. Shangazi anasema ule wakijua unao wattakuua ili waupate, kupewa kwake mpaka ule viapo..
Ule wa kua huonekani, hata leo nikiutaka wananipa, ule sokosi kua nao. KUna sehemu haufanyi kazi una sehemu zake.