Inatokea post namba 1384
Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 G.
ilishangaa sana. Kilichhonishangsza ni Jini Bakora. Kwa mara ya kwanza nikajua kumbe anakuja sehemu kama mtu kabisa na hatujui kua ni jini. Siku ile nikafikiri huyu huyu ndio Arsis nini anacheza na akili yangiu? Siku nyingine kabisa nikataka kumuuliza Arsis katika maongezi yetu pale oshen rod, akanijibu kabla sijuliza. Arsis aliua ana ajabu moja ya kunijibu kabla sijauliza. Hua anaanza kama kunipa elimu hya kitu fiulani, huku ananijibuj nilichpotaka kuuliza. Mfano siku hio alikua ananielekeza.aina za majini na majina yao Kiarabu, Kingereza, kiindoneshia.Akanielekeza majini wanaoweza kujibadili na wasioweza, akachomeka na "na jini Bakora" anaweza kujibadili tena jini mkubwa sana. Akija hapa hata jini mwenzake asie na ujuzi anakua hamjui kama huyu jini, atajua huyu binadam mwenye kuoza majini. Nakumbuka siku hio nikataka kumuuliza kwanini ananitajia majina ya majini "kiindonesia", akasema bila kumuuliza. Mke wa mzee Ali ana rouhan ya kiindonesia, ana elimu sana lakini hajibadili kabisa ingawa anaweza. Nikamuuliza, kwanini Arsis. Akacheka, akasema, ameshika sana dini hataki kutumia elimu yake vibaya.
Hayo ya siku ingine jamani. nisiharibu kis, ngoja nimalizie hatraka haraka.
Yule kijana akapelekwa kubvaa, kweli walijua kumchagulia nguo, wakaambiwa wasimtie mafuta mazuri, wkati anavaa wakapewa majani wafukize chumbani kwake, yalikua makjani na mizizi mikavu ilipotiwa kwenye moto, moshi una harufu kama bangi sema huu mzito na unalaia, koo na macho yanawasha washa.Kutoka kapendeza sana na katoka kipara hajulikani kama huyu ndio alikua kama zimwi. Alikua kashika cap yake mpya mtoto wa babu mkononi, nikajua ni mtoto wa babu kampa, maana mtoto wa babu anapenda kweli cap, mwenyeqe anaziita base ball cap, lakini babu alimkataza kuvaa za mtumba. Babu yangu alikua wote anatukataza kabisa kuvaa nguo za mitumba, anasema kama hauna nguo vaa hata kaniki moja au shuka, usivae kafa ulaya. Ukimuuliza kwanini anakwambia nuksi tupu.
Wakaja tukaka nao, lakini ndio haongei, haoneshi kasoro yoyote ile, anasikia, anaguna, anacheka, antabasamu, anajua watu wote. Kuna vijiti kama saizi ya kidole hivi alipewa na jini bakora awe anaweka mdomoni, anatafuna tafuna. kikiisha aweke kingine. Nilijua baadae sana kazi yake ni nini.
kwenye mabasi huko kila mtu anahamu ya kurudi ndani, maana hawajui nini kinaendelea lakini wamepata fununu kijana yupo ndani.
Babu yake akasema muiteni mama'ke, mama'ke akaletwa, akaanza kulia, akamkimbilia mwanae na yeye yule kijana akawa anatabasamu tu, akasimama wakakumbatiana na mamake kama vile anasema sikuachi tena, mama vilio hapo na mtoto vilio na wengine wenye roho ndogo kama Mzee Ali na yeye akaanza kutokwa na machozi na mafua membamba yanamdondoka.
babu: kawaitewni wote na wale wachawi waaje hapa tuagane.
Wakaitwa watu wakajazana kila. anaeingia analia, anakwenda kumkumbatia, wanamsemesha wanawatazama tu kama hawaamini wanachokiona, yeye anatabasamu tu. Anajua kila mtu, kuongea ndio hawezi na kakaa kama zuzu fulani hivi walipokwisha kuwepo wote. babu akasema kwana ztusome Qur'an hgalafu kila mtu aseme lake kisha tuagane. Wakaitwa vijana wa kusoma Qur'an wakasoma, wakamsalia mtume mara mia moja. Walipomaliza.
Babu: jamani mimi naitwa Maruki, sijui kwanini, msiniulize, Huku anacheka. Mimi sio uweo wangu huu kua na ni mtu wa tiba, na yaliotokea yote sio uwezo wangu. Ni Allah katukutanisha na kutujaalia kuokoa wengi sana. Sio huyu tu. waapo huko vijana wengine sita, wengine wadogo sana kuliko huyu. Wapo kama mazimwi kwa hatua tofauti tofauti bila makosa yoyote. Mkitaka kujua ulizeni hawa mbwa, watawaambia sababu zao. Ni sababu zaa kijinga kabisa. Sana sana gtamaa ya utajiri. Haya nyinyi semeni, utajiri unawasaidia nini?
Lakini AlhamduliLlah qote qale na wengine wapo Mwnaza na Tabora, wengi zaidi, walioweza kuokolewa wameokolewa, ambao hali zao mbaya sana, wamekufa na wao, lakini kidogo sana. Hawa mbwa wakiona huwezi kufanya kazi zao vizuri wanakuwacha ufe tu, wanakulisha uchafu maisha yako yote, hao wanakupeka sijui wapi huko, mbwa hawa, mtawauliza wenyewe, mimi naweza kuwaua sasa hivi, lakini itakua hakuna faida. Bado wengine, hawa mbwa , huyu wanawafanyisha kazi bar na kujiuza miili yao. sasa watakua vizuri na hawa mbwa watalipia gharama zao zote. Huyu mshenzi na wenzake wana mali nyingi sana Tanzania nzima, msimuone hivi huyu ni wakala wa shetani wa kichawi. Huyu kunywa damu kwake ni kama wewe na mimi tiunavyokunywa juisi a machungwa. Hatoki kwake asubuhi bila kunywa damu, na yule mbwa wake malaya kishaanza na yeye kunywa damu kama mamake.. Leo umekunywa nini wewe mbwa? Sema,tusikie.
babu ndio nikajua kumbe kuna siku anakua mkali. Alimuuliza kwa kwa ukali kabsa, sauti ikawa inatoka ananguruma, kimoyomoyo nikajisema huyu sasa hivi ni simba. ataua sasa hiuvi, simwingilii kabisa. Yule mama akaendelea, imemwagwa yote ikachomwa moto. kumgtazama babu alivyomkazia macho, nikajiua leo babu kakasirika, hata sura ilikua inaonesha, nikajisemea leo ukimchokoza, simba anakuumiza kama sio kukuua.
Babu: Huyu kapagtikana siku kumi nyuma, tukaanza kazi dakika hio hio, huyu ni mjukuu wangu. wanza tushukuru Mwenyezi Mungu, huyu kijana wetu kupatikana salama. Mimi sisemi zaidi, ni mengi na waliyafanya haya ili huyu mbwa mkubwa wao awe kiongozi mkubwa, kumbe hawajui kila mwizi qna siku arubaini. Mbwa hawa. Maneno aseme mwenyewe.. Haya sema...
Mama Yule; Akaanza kuwaambia ndugu wote kilichotokea mwanzo mpaka mwisho, waliokua wanalia, waliokua wanasema huyu hatufai kwenye ukoo.
babu: Kila mwenye swali lake amuulize huyu na mbwa na hawa wengine. Aliepotolewa na mwanae, mume, mke, dada amuulize huyu mbwa. Huyu kila wiki anaua huyu. Maisha ya mtu kwao hawa ni kama panya tu. Nyie mnaopoteza watoto wachanga, hawa ndio wakuwashika. Mbwa hawa wengine wapo hai waroro lakini hawafai kabisa, wanawapelekea matajiri wakichawi wawaingilie, We mbwa mnaanza kuwaingilia watoto wa umri gani, akmuuliza yule mzee mchawi. Akajibu kuanzia wachanga wa mwaka mmoja tunajaribu, tunawamwagia usoni wankula yote ile na wenzao wanakuja kuwasafisha kwa kuilamba, ndio furaha yao. Mzee yule akanyanyka akmpiga kofi yule jamaa mpaka akaemnda chini, babu akamwabia mwache mbwa huyu. Mtawauliza we nyewe huko, mimi nilitaka mjue uaalimu wao. hayua fanyeni haraka kila mtu aende kwao.
Maswali yakawa kibao, mwengine anauliza umejifunza vipi ,anajibu. Umeanza lini? anajibu, wanagapi ushawafanya hivi ?Akajibu hawana idadi ni wengi sana hatuweki hesabu, ni mwiko kuweka hesabu. Huuyu binti yako kaanza lini hii kazi yako? KUanzia mdogo, huyu ndio kashika kazi zangu zote, mimi sana sifanyi tena nafundisha tu. Mmoja akauliza, kwanini tusikuue? Akasema nimemrishwa kwanza mimi na qenzangu hawa na wengine hamuwajui, turudishe mali zote kwenu na kwa watu tuliowazulumu. Za huyu binti yangu na za huyu na huyu. Baada ya hapo niueni. Sina sababu ya kuishi tena.
Babu: hakuna atakae kuua, na nyinyi na wale mbwa wengine ambao hajauliwa muishi kama mlivyotesa wenzenu. mwengine akasema mimi nipeni huyo binti awemtumishi wangu, mali hio.
EWote tukacheka. Wahuni whawakosekani sehemu.
Watu wakaanza kuuliza wana mali ngapi? yule mama aksema nyingi sana. Akataja nyumba ake zaidi ya kumi na sita, Mwanza huko, mpaka capri pint ana majumba kakodisha, magorogfa Dar. Ana bar kibao zimejaa misukule. Tanzania nzima mpaka nchi za jirani. Mzee Ali akuliza Dubai na Ulaya hamna mali? Wakasema wanazo lakoini huko zina masharti makubwa kuna wakubwa wengine huko, lazima wao wapate aidi, Hatupendi sana huko,
Akataja nyumbani ana masanduku ya noti, kama ishirini na biti yake anayo mengi zaidi, yeye anapenda sana kuweka pesa. Hata godoro lake ni la noitti tupu na mito yake ni maiti za watoto wachanga. Watu wakaanza kunong'ona. wakauliza ziote zao au za wanaushirika wengine ? akajibu zikifika kwako ni zako peke yako, hazina ushirika. Wanapeana faida wakiwa kwenye ushirika na wale wapya tu. Akasema wale wapya lazima wawe na sisi wa zamani ndio biashara zao zipate wateja ziingize mali. wale wanaume wawili mmoja kamuingiza yeye kwenye uchawi, yule kijana ni mtoto wa dadake, mamake alikuwepo pale akasema sio mwanangu kuanzia leo, naahidi mbele ya watu. Yule mwanammme mtu mzima ni shemeji yake ambae mkewe alishakufa siku nyingi, kumbe ni yeye alimuua kichawi, huyo hakufanywa msukule walimtoa kfara ya damu kwa ajili alikua na mdomo sana. Kwa mujibu wake.
ykongewa we.
Babu akasema sasa uamuzi ni wenu ndugu. Huyu kijna atabaki na mimi, nitaondoaka nae kesho aendelee na dawa mpaka akae sawa. Mtaalamu wa damwa hapa kasema huyu wiki tu ataongea.
Mama Yle: hatukumuharibu kwa sababu tulitaka kivuli chake kiwe kiima kisiwe na athari yoyote, kusema andesema kwa sauti ya mwengine, Na aliekua apewe kivuli ni yule kija alaiekwenda kumnunulia nguo. Yaani wote ni ndugu kwenye ukoo.
babu; nani mnamuamini kwene ukoo wenu, wote wakasema yule mzee.
Babu, sasa tunakupa wewe majukumu mazito, mali zao zote hawa watakwend kuwagaia, na kila aliedhulumiwa ndugu au mtoto na hawa au washirika wao, mali zao ziwalipa. Na kabisa walipe gharama zenu nyote mpaka kufikia hapa. Msiwe na wasiwasi hawa ni matajiri wakubwa woe, nyinyi hamjui, mimi nafahamu siri zao zote. Hapa hawa wote wapo chini ya ulinzi wakibwa zao wameuliwa na wengne wamedhibitiwa majeshi mengi na mkubwa yapo kazini. bqabu akaendelea; Huyu kototo, mtoto, mamake na kijana yoyote wa kike na kiume wa kwenye ukoo wa baki nae kwa jili ya tiba. Mama yao akawachagua, hawa ndio wanapatana sana. Wale vikjaja wakakubali kubaki.
Babu: leo hii wakachukue vigtu vyao kama vipo hoteli waje hapa haraka sana, Nyinyi wengine kama mtasafiri hata leo, Hawa wagtakua chini ya mzee wenu, hawafanyi chochote boila yeye.
Mzee: Mimi sitaki hata kuwaona sutra zao.
Babu; Iabidi ustahamili mpoaka mpate haki zenu, mkiziwacha ndio zinachululiwa na wachawi wengine au zinapote hivihivi, hawa hawawe zitena kufanya lolote bila amri yako kuanzia leo, hata kazi yoyote hawawezi kufanya. Yaani hawa ni afadhali mgtu awe msukule kuliko wTvyiku Hawa, mimi nakushauri kila mmoja mpe mtu mmoja awe nae maana hawa hata kuoga hawaendi bila kumarodhwa na mtu utakae wapa. Kila mmoja akaanza kuguna.
Babu akasema haya mtajua wenyewe ndugu, Mzee Ali na wewe baki,wacha waende jawa, na mkitoka hapa asirudi mtu mkifika ndio mtanijulisha safari yrnu, msiogope nyote wapo chini ya ulinzi maisha yo yote hawa mpka kufa kwao.
Wakaondoka kurudi hoteli, mimi namzee ali tukaenda na wale vijana walioambiwa wabaki kuwasaidia kumlea yule kijana na mamake. wamedhukua tu vutu vyao na b)vya yule mama wakrudi, Babu hakukaa tena alikua mwenyewe kishafanya mipango yake akaondoka nao usiku ule bila sisi kujua kwa gari lake na mwane akamapeleka. Siku ya pili anatupigia kisha fika kwake. aksma na nyinyi kipenda kuja njooni mkipenda kwenda nendeni tutawasiliana zaidi kuanzia kesho.
Kwa ufupi yulle kijana na mamake wakaa miezi miwili shmaba kwa babu mpaka akawa mzima kabisa anaongea na anafanya kazi zote, akawa hataki kuridi Mwanza, wakahamia Dar., wanaishi hapo mpaka leo.
Walipata mali nyingi sana kwa wale washenzi, wale walichwa wakawa ndio kam mental, mata)ra ya mwisho ukoo ukawatawanya, wakishia hospitali za vichaa hakuna aliekua anawataka hata kuwaona.
babu alitumiwa million kumi na yule mzee wao. Ni bossa kibwa sana Mwaza, sitaki kumtaja jina ni mtu maarufu sana na mwenye pesa zake. Zilikua ni pesa nyingi sana kwa zamani, mimi akaniwekea tanoi zangu Mzee Ali sijui.
kkazi zote za upande usioonekana zilifanywa chini ya usimamizi wa Arsis.
Kuna kisa kingine cha kukoaa msukule hii ilikua Zanzibar ni tofauti kabisa hiki. Tutakileta siku za usoni.
Tutaendelea.