Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Inatokea post namba 808

Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 D.

Tukapiga story kidogo na Halima pale akanipa visheti na kahawa kama kawaida. Sikukaa sana, kabla ya kuondoka nikapiga piga simu, nikaongea na babu akaniambia yupo Tanga mjini tayari, nisiende popote niende moja kwa moja kwake Usagara. Nikaanza safari yangu.


Kufika Tanga moja kwa moja kwa babu. Nyumba hii anakaa mkewe mdogo babu lakini kuna upande wa bibi yangu, huu ndio ilikua nyumba orijino ya babu, hakai mtu yoyote isipokua bibi mwenyewe akija Tanga labda atke mwenyewe, wanawe au wajukuu wakija Tanga, sehemu yake ndogo tu ukilinganisha na jengo jipya anapokaa bibi mdogo, ni pakubwa sana. lakini kule ofijino kulikua ni uwanja mkubwa mtupu ambao babu alikua amefanya gereji wake ya kutengeneza magari ya watu ya kizamin, enzi zake. Alipohamia shamba kauza ma skrepu yote akajenga jenga jipya kubwa, zuri la kisasa, marupurupu ya kustaafu na mshiko wa kamba wa shambani kwake ulikua umemkubali. Maana babu alianza kununua kule na kupaendeleza kidogo kidogo kab;la hajajenga hii nyumba mpya.

Nikitazama hali ilivyo sasa na zamani tukiwa wadogo naiona nyumba imekua ndogo sana, lakini sio ytena ile ya zamani, imejengwa kisasa kabisa. Hii walimjengea wanawe, hususan shangazi yangu huyo yupo serikalini huko, mama'ke mke wangu, ndie alisimama kidete kujenga anavyotaka yeye. lakini hajakaa kabisa yeye, labda akija tu Tanga tena mpaka bibi awepo, ana jiumla lake sijiui makorora sijui wapi huko, kalipangisha, mwenyewe anaishi Dar. Kwa ufupi yeye ni mwenyeji sana Tanga, anjulikana kuliko hata mzee wangu.

Kufika tukasalimiana, na babu bibi, wanawe, ndugu jamaa na marafiki nikamkabidhi bibi zawadi yake ya visheti vya Halima, nikamwambia zawadi yako nyingine baadae pekeetu sitaki huyu mzee aone wivu. Nilikua na perfume nataka nimpe. Babu akanambia Simba wewe bibi yako kasema tukufungulie kwake, mgeni wake.
Mimi; Bibi hajaja?
Babu: Hawezi kuja, kule tutamwachia nani? Yeye akija mimi nabaki kule. Haya twende kule tukaone kama kuna kitu utahitaji.

Tukaingia, nikakuta kila kitu fresh kabisa, pasafi hakuna vumbi, kila kitu safi kabisa. Nikaanza kumchokoza babu:
Mimi; babu huku vinaishi vijini vyako nini? Mbona pako fresh pananukia udi, akasema wanaishi watu, sio majini.
Babu: kwani mjukuu wa bibi yako peke yako? Nanihii na nanihii umewasahau?
Mimi; Si nimewaona kule kwa bibi mdogo sasa hivi?
Babu: Wale wanakaaa hapa miaka yote, kwani hujui hilo?
Mimi; Najua babu lakini kweli babu mimi najua wanakaa na bibi mdogo kule nyumba kubwa.
Babu; Hii ndio nyumba kubwa, kule wapo leo tu mpaka wewe uondoke, wao miaka yote qanaishi hapa kwa bibi yako, bibi yako hataki kabisa nyumba yake ikae bila watu.
Mimi"; Si ungewaacha tu wakae hapa babu kwanini wamekwenda kule?
Babu; Hapa kazi mlioianzisha huko ni kubwa, sitaki mtu atuingilie huku. kazi yote itafanyika huku na utaifanya wewe, mimi mgeni wako hapa, ukinihitaji. Sikai huku.
Mimi; Nikacheka, sema tu ume miss bibi na vijukuu umevipeleka huko vyote vikusinge. Poa babu. Simba hashindwi na kitu.

Babu: Sasa sikiliza kwa makini,yupo nanihii kule, atakupeleka ukaone sehemu ya kufikia wageni wako uwajulishe kama watapapenda mfanye booking ya kuanzia Jumapili, wakija wote wafikie kule.. Chakula cha mchana Jumatatu wote watakuja kula hapa, ndio hio siku ya kazi. Baada ya hapo wanaoondoka wataondoka wataobaki watabaki, kwa hio wewe ndio utajuwa watu wangapi na kama hoteli itawatosha.
Mimi: Poa babu.
Babu; Haya tewende kule kwa bibi yako, wametayarisha chakula kule.

Tukaenda na babu , bonge la msosi utafikiri mlaji sana mimi, watoto zake na wajukuu wakawa wanamcharua babu, mgeni njoo mwenyeji apone. leo mkeo kafanya mambo makubwa hapa, hataki urudi shamba na sisi hatuondoki hapa babu mpaka wewe uondoke.
Bibi 2: kwani siku zote hamli hapa?
Mjukuu; Leo habari nyingine kabisa, babu usiwe unakaa sana shamba, siku hizi kaa sana huku kama zamani, shamba uwe unakwenda mara moja moja tu.
Babu; Mimi siku hizi bendera inafata upepo. Hii habari nzito ya leo sio yangu, hamumuoni mwenyewe hapo?

Huku ananioneshea mimi, wakacheka.
Bibi 2: Kipya kinyemi, mwacheni msimsakame jamani mume wangu, handsome langu hilo.


Tukala, tukacheka tukafurahi, yule mtoto wa babu akanambia twende bwana mkubwa, tukatoka nae, yeye anaishi Tanga, mwenyeji sana, kila mtaa anajulikana, ni mdogo kuliko mimi kwa miaka miwili nadhani. Vijana wenzake wanamtania, leo kaka mkubwa kaja, mambo fresh kabisa, lazima tunukie leo.


Tukaiona hoteli ipo pale pale ngamiani, mimi nikaona poa tu, kurudi nikaenda kwangu, nikampoigia Mzee Ali, akasema mambo upande wake poa kabisa.
Mzee Ali; mambo huku mazuri, wote mama yule anasema wameitikia mwito, basi kubwa moja kutoka Mwanza, Coaster itandokea hapa Shinyanga na wengine wawili watatu wa Tabora watakuja hapa tutaondoka nao, mimi nakuja na gari yangu siji na basi lao, naondoka kesho na wife wangu. Sema kuna wageni wengine watakuja kivyao kutokea Dar na kwingine, watafikia hoteli wanazojua wao huko, wataanza kuingia kuanzia kesho, tutakutana nao Jumapili tukifika. Vipi huko poa?

Mimi: Kuna hoteli ya kufikia nimeenda kuitazama kubwa tu.
Mzee Ali; Usihjihangaishe kabisa kwa hilo, wao tayari wana mipango yao pakufikia, wao mradi wanajua Jumapili tutakutana hapo Tanga ndio wataelewa mengine yote. Wanasema tayari tusiwe na wasiwasi, wakataka na mimi niwe nao, lakini mimi nimewaambia kuna wenyeji wangu. Mwenteji wangu ni wewe, nitafutie hoteli safi nakuja na mke wangu.
Mimi; Njoo, kuna nyumba tupu ya peke yako hapo, nzuri kuliko hoteli.

Tukamalizana pale, siku ya pili usiku usiku nikampokea mzee Ali na wife wake, ilikua Jumamosi. Nikawa mimi mwenyeji wake pale kwa babu na wale wajukuu wa babu wa kike ndio wakawa na mkewe, mashoga tena. mambo swaafi kabisa. Jumapili asubuhi, yaani siku ya pili yake, tukakaa, mimi babu na Mzee Ali, rukajulishana pale, wakaongea sana.

Babu; Msijali, kwa hio hapa hleo hakuna kazi kubwa kazi kubwa ni Kesho tu mchana, wote waliokuja waje kula hapa, chakula tutapikisha, wao waje kula na kuondoka tu. Wanafika wangapi?
Mzee Ali; Usijitia gharama ya kula mzee. Hawa wanajiweza wenyewe. Jumla tutakua kama watu mia na ishirini.
babu: hapana, wageni wetu hao, wao wafanye yao yoote, kula lazima hapa mchana, wote, asibaki mtu kabisa.

Tukaelewana pale. ikawa hatuna zaidi cha kufanya mimi nikamwacha mzee Ali akapumzike na mimi nikaenda kupiga misele na mtoto wa babu. Njiani kuna sehemu wanauza juisi akaja Jini1. Akanambia usijali, hanioni mtu, baadae uwe peke yako tunataka kuongea na wewe,mimi na jini bakora. Nikamwambia, poa.


Itaendelea.
Safi
 
unaposema Quran ilichukua vitabu vya biblia.. je,ww ushawahi kuisoma Quran ukadhibitisha imecopy toka katika biblia yaani yaliyomo kwenye Quran na Biblia yana fanana? au ww ulidhibitisha vp ya ndani ya Quran yanafana na yaliyo ndani ya biblia.?
Jibu swali, Torati ipo kwenye quran haipo? Kama unakubali ipo basi ni copy n paste na hakuna cha kushushwa kutoka wapi sijui..
 
Jibu swali, Torati ipo kwenye quran haipo? Kama unakubali ipo basi ni copy n paste na hakuna cha kushushwa kutoka wapi sijui..
Torati haipo kwenye Qurani, wala Zaburi wala Injiri.
Kama ipo iwekwe hapa tuione.
Mzizi wa Torati ni Amri Kumi alizopewa Musa.
Kwenye Qurani hazipo.
 
Na hii hapa anaambiwa Musa ?
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ

(MUH'AMMAD - 19)
Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
.............
Leo hadi utaje dhambi za Muhammadi.
Ukichomoa na hii nakuwekea nyingine.

Mbona umerukia "kuchomoa"? Kwani nilichomeka wapi?

Mafundisho mema kabisa hayo, hapo tunafundishwa kuomba dua, ndio Waislam tukiomba dua na sisi wenyewe tunajiombea "rabbana 'ghfirlana..."

sasa umeona sura inaitwa Muhammad ukapachika reference juu hapo kupotosha watu? Upoyoyo huo. Huo ni ujumbe kwetu sote, hakuna jina la mtu hapo. Unakuhusu wewe pia huo ujumbe kijana, Qur'an ni kwa walimwengu wote siyo kwa watu fulani tu. Kumbuka hilo.
 
Torati haipo kwenye Qurani, wala Zaburi wala Injiri.
Kama ipo iwekwe hapa tuione.
Mzizi wa Torati ni Amri Kumi alizopewa Musa.
Kwenye Qurani hazipo.
Hizo hazipo popote isipokuwa zimetajwa kwenye Qur'an. Biblia haina chochote katika hivyo hata Injili ya Yesu hakuna. isipokuwa...

Qur'an haina tofauti na ujumbe waliopewa mitume wa kabla ya Muhammad, yaani hivyo vyote ulivyotaja havipingani kabisa na Qur'an. ndiyo tunasema vitabu vya mitume wote utavipata kwenye Qur'an, kwa ujumbe wake kijana. Qur'an ni kitabu cha kipekee ulimwenguni. Kumbuka hilo.

Au ulifikiri Allah atawapa kila mtume ujumbe unaokinzana na wa mwenzake kama ilivyo ndani ya biblia?
 
Kupitia uzi huu nimegundua mambo kadhaa
1. Asilimia kubwa ya waumini wa Kiislam wanaamini katika stori za kufikirika na ni wepesi sana kushikwa kiakili hasa mtu anapotunga hadithi na kuihusianisha na dini yao.
2. Watu wengi wana matatizo na wanaamini yanaweza kutatuliwa kiroho na si kwa juhudi binafsi na akili! Kupitia uzi huu wa kufikirika nimeshangaa kuona watu wanaandika maombi yao kwa mtunzi eti awafikishie kwa huyo jini! Huu ni zaidi ya wendawazimu.
3. Uislam na shirki ni ndugu wa damu.
Mengine ntaendelea kuandika...
 
Mbona umerukia "kuchomoa"? Kwani nilichomeka wapi?


Mafundisho mema kabisa hayo, hapo tunafundishwa kuomba dua, ndio Waislam tukiomba dua na sisi wenyewe tunajiombea "rabbana 'ghfirlana..."

sasa umeona sura inaitwa Muhammad uka[pachika reference juu hapo kupotosha watu? Upoyoyo huo. Huo ni ujumbe kwetu sote, hakuna jina la mtu hapo. Unakuhusu wewe pia huo ujumbe kijana, Qur'an ni kwa walimwengu wote siyo kwa watu fulani tu. Kumbuka hilo.
Wacha kuruka ruka.
Kama ujumbe wa watu wote Allah huwa anasema kama hapa.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
(AL - BAQARA - 172)
Enyi mlio amini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.
...
Hiyo 47:17 ana amrishwa mtu mmoja ambaye ni Muhammadi.
Kama hutaki kuielewa hebu tuambie hii Aya anaambiwa Nabii gani maana hakuna jina
قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
[ AL - AH'QAAF - 9 ]
Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi.

Leo hadi utaje dhambi za Muhammadi.
 
Kwa mujibu wa Arsis, hakuna hatari yoyote, "jicho la tatu" ni uelewa tu kua mpana zaidi. Unaweza kufanyia mazoezi hisia zako ambazo unazo tayari zikawa zinakufanyia mambo ya kawaida lakini yakaonekana ya jabu. Jito la tatu na sensi ya sita hayana tofauti sana.

Arsis kaenda mbali zaidi na kusema unaweza kuyaona ya nje ya nyumba na wewe upo ndani, sio uchawi ni mazoezi tu.
Simba.
mheshimiwa stori siioni msukule part 3.. naona watu wana debate tu.
anyways umesema ukifunguq jicho la tatu unaweza kuwa ndan ya nyumba na ukawa unaona nje. sijui ila
wakat wa zama za khalifa umar aliwahi kuwa yupo kwenye mimbar madina akawa anatoa maelekezo ya jeshi lipo mbali sana kitu kama nchi nyingine wakamulliza akasema alikua anaona kinachoendelea hivi Umar alikua ana matukio yake i think ni level za uchamungu tu.
 
Bwana Arsis huu uzi wako unafuatiliwa sana kila nikikatiza more than 15 people are here naamini kuna watu wengi wanafuatilia na wana elimu kubwa tu juu ya mambo ya kiroho ila hawa comment.
Comment ziongezeke jamani tujifunze simmesikia Arsis anapenda challenge ila nimegundua kuna vitu ata Arsis anaweza kujifunza kutoka kwetu na anawapenda binadamu
Kweli tupo tunafuatilia kwa makini lakini kwa tahadhari pia tunashangazwa na usahihi katika mambo ambayo tunajua wanadamu wengi hawajui yanasemwa hapa.
 
Mchawi hana sababu hata usifanye lolote wakiamua wakuharibue maisha wataharibu unadhani walo haribiwa maisha na wachawi waliingia rada zao??

Hakuna njia ya kukwepa mwanga mchawi Ila ucha Mungu jitakase na madhambi jenga urafiki na Mungu hakuna mchawi jinn atakusogelea.
Sahihi sana ila kuna maarifa ya ki Mungu ukikosa waweza kusumbuliwa sana na wachawi licha ya uchamungu wako. Hasa mambo yako yaweza kusakamwa kama hawawezi moja kwa moja kukugusa wewe watagusa vya kwako.
 
Kweli tupo tunafuatilia kwa makini lakini kwa tahadhari pia tunashangazwa na usahihi katika mambo ambayo tunajua wanadamu wengi hawajui yanasemwa hapa.
Mkuu unavyosema kwa tahadhari unamaanisha nini?
 
Mkuu unavyosema kwa tahadhari unamaanisha nini?
Viumbe hawa katika ulimwengu wa roho ni werevu sana na wanatafuta namna ya kukubalika na wanadamu. Wanaujua uwezo wa ajabu wa mwanadamu lakini pia wanajua mapungufu yake. Tupo kwenye ushindani wa falme na mamlaka, vita hii ni kubwa sana na inapiganwa kati ya wanadamu. Na kati ya silaha kubwa sana anazotumia adui wa wanadamu ni UWONGO. Ndio maana nasema tuwe na tahadhari kubwa.
 
Viumbe hawa katika ulimwengu wa roho ni werevu sana na wanatafuta namna ya kukubalika na wanadamu. Wanaujua uwezo wa ajabu wa mwanadamu lakini pia wanajua mapungufu yake. Tupo kwenye ushindani wa falme na mamlaka, vita hii ni kubwa sana na inapiganwa kati ya wanadamu. Na kati ya silaha kubwa sana anazotumia adui wa wanadamu ni UWONGO. Ndio maana nasema tuwe na tahadhari kubwa.
Asante mkuu, Kuna comment ulisema kama kuna mambo ya kiroho huyajui wachawi watakusumbua unaweza kutoa mfano wa mambo ambayo tunatakiwa kuyajua na kuyafanya ili kuishinda hii falme ya giza?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom