ionjo vya Arsis 5 -3
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
Nikapigapiga zangu, lakini nikawa naona muda hauendi, mimi nimezowea ikiisha alasiri nakua nimeshamaliza kazi zangu naondoka zangu nyumbani.
Baafda ya magharibi tukaondoka na Mzee mpaka Buguruni, tukaingia pale wanapouza mbao, ule mtaa wa mwhiso kabla hujaenda ule wa relini, tukaingia ndani huko, kufika aehemu akakuta kyna kijana kasimama barabarani, njia yenyewe ilikua nyembamba tu, anatusimamisha.
Kijana: Mnaenda kwsa mzee ali?
Baba; Ndio.
Kijana, kwake hapa, akatuonesha nyumba, lakini njoo hapa muegeshe gari, kama nyumba ya tatu kulia hivi kulikua kiwanja kitupu lakini kina uzio, hakijajegwa, akafungua geti tukaingiza gari ndani.
Kijana; wekeni tu hapa, kulikua kuna gari nyingine mule, moja tu. Vile vi pajero vidogo. Moyoni nikajisemea ndio ya hiuyo dokta nini. Tukashuka tukapelekwa ndani kwa mzee Ali.
Hilo ni jina la kweli la Mzee Ali, sio la kubuni, watu wanaokaa mitaa hio watamfahamu, ni zee wa kipemba mfupi hivi ana mwili kidogo, ukimtazama yupo kama King Majuto, na yeye ana vituko vituko lakini naona kwa kua nilijenga picha ya Majuto nilipomuona.
Tukasalimiana pale akasema...
Mzee Ali, nimeambiwa mnakuja mtu na mwanae, lakini mbona naona ni mtu na kakake? Karibuni huku kwanza halafu tutaenda hapo uani.
Akatuingiza kama sitting room.
Mzee Ali, Wewe bwana ndio utakua... na huyu atakua .... Nimeambiwa niwapokee na Sgeikh wa unguja, tunafahamiana miaka mingi sana yule bwana, na hapa kuna binti mmoja alikua anamshughulikia hiuko Unguja lakini akamjulisha kwetu hapa, mndio tunamshughulikia, akanisisitiza siku anakuja na nyie muwepo mjonee wenyewe haya mambo maana kasema watu wa kisasa nyinyi hua mnapinga kila kitu. Sasa ngojeni niende nikamjulishe kuna wageni, anajua lakini si vizuri tukamvamia woite watatu, atakuja kijana kuwaita tukiwa ytyari, sasa hivi kama dakika tano tu, sianzi chochote mpaka muepo, ndio maagizo ya Sheoikh....Yulew bwana akisema kitu najua kuna mshindoi mkubwa. Nisubrini kidogo.
Jinsi anavyoongea nikahisi kaona kaletewa wateja wengine kama Dokta. Kukaa kidogo tukaja kuitwa, tukkaingia, tukakuta wanawake wawili.
Mzee Ali; Huyu binti ni Dokta... atawajulisha zaidi yeye mwenyewe. Na huyu ni mke wangu, maana kazi hizi kama ni mwanamke lazima awepo mkeo au dadako au mamamko, huwezi kubaki na mteja tu. Mashetani wana hatari, akacheka.
Mzee Ali, Dokta, huyu ni... na huyu ni mwanae, au mdohgo wake bwana? SAkacheka.
Baba: Vyovyote tu sawa, lakini zaidi sio vyote hivyo, ni rafiki yangu.
Wote tukacheka pamoja na Dokta.
Baba; Dokta wa wapi?
Dokta: Kwa sasa mimi nipo na NGO moja ya Kimarekani inatwa Columbia inafanya tafiti hapa tanzania na nchi nyingine za Afrika.
Baba: tafiti za kutibu?
Dokta: sio hivyo, sisi tunafanya tafiti ya UKIMWI, tunachukua data hospitali zote, kujua mambo mengi tu, ni kazi kubwa, tunaifanya Tanzania nzima na nchoi nyingi za jirani.
Bava: Sawa nimekuelewa.
Mzee Ali; Dokta hawa wamejulishwa kwangu na Sheikh...kama wewe, lakini hawa sio Waunguja, au waunguja jamani, akacheka.
Baba: haoana sisi ni wa hapahapa Dar lakini tulihamia tu, kwetu ni tanga.
Mzee Ali; Alinambia Sheikh kitu kama hivyo. Katribu ni sana. Sasa tusichelewe muda ukapita wa kazi zetu, kazi zetu zinaenda kwa muda wake, watu wengi hawaelewi hilo.
Akanyanyua sauti kama kuita nje ya mlango wake pale. haya leteni hiuvyo vitu nilivyowakabisdhi hapo nje. Binti mmoja mkubwa tu, akaingia na kiteo kina moto na ubani ule kwenye mfuko akampa Mzee Ali.
Mzee Ali na ile ndoo tupu leteni na ndoo moja ya maji. Na lile fuko langu la dawa.
Wakaleta pale, ikawekwa pmbeni huko ile ndoo tupu na ya maji, na lile fuko. Mzee Ali akasema...
Mee Ali; Dokta soigea hapo elekea huko, jamani huyu Dokta leo yupo kwa dokta wa madokta hapa, leo lilikua zoezi la kumtapisha uchawi aliolishwa. Imekua vizuri na nyie mpo mtajionea wenyewe.
Mzee Ali akatia ubani kwenye moto, kwa wingi tu, moshi ukazagaa maana chumba chenyewe kilikua cha kiasi tu sio kidogo sana wala sio kikuba, hakina kitu ndni isipokua kina zilia zuri tu na saisi tumekaa chini pembeni, tunatazama show.
Aksemasema maneno yake kama Kiarabu hivi, lakini nikajua sio Qur'an hio, kwa siejiua atafikiri inasomwa Qur'a. matra kidogo yule dokta akaanza kama kutingisha kichwa hivi akaanza kunyoosha kidole, ka mee halafu kwangu...
Dokta huku kakaza macho yamekua ya ukali kweli. hawa wanakuja kufanya nini hapa, sio watu wazuri kabisa, mimi kwa unaniita wakati hawa wapo? Ka ukali kabisa.
Mzee Ali: Sisis hatukukuitra wala hatuna haja ya kukuita wewe leo, shughuli yako bado, umejileta mwenyewe. Ondoka zako tu, siku yako ikifika utakuja tu ukipenda usipende.
Dokta: Wewe mdogo sana, huniwezi mimi, wach nende zangu ubki na migeni yako hio
kama akajirusha akalala chini kama nusu dakika akakaa, ni vizuri alikua amevaa skin tight na juu kama dira hivi. Na yule mkewe mzee Ali kavaa hivyo hivyo. Mzee Ali akaendelea na maneno yake.ytule dikta akaanza kuongea, lakini kwa sauti nyingine kabisa sio ya ukali.
Dokta; Unataka nini umeniita?
Mzee Ali: Sema wewe nani?
Dokta: Akataja jina sina haja ya kulitaja.
Mzee Ali umetokea wapi?
Dokta; Mimi natokea njuani> Unapajua njuani wewe?
Mzee Ali: Mko wangapi?
Dokta; Akacheka kwa sauti nzuri tu ya kike, tupo wengi tu, unataka nini?
Mzee Ali' Siku yenu ikifika mtanoma wote, mimi nataka wote mkae pembeni leo tuna kai yetu, msitake tuanze vita isiokua na maana.
Dokta; nani anataka kukaa hapa leo?
Mara kama akajitingisha hivi akaanza y)tena kuongea, kwa sauti ya kiume.
Dokta: Wewe huwezi kitu, huyu sisi tumeshasema zamani bila ada yetu hatutulizani, sisi tunamlinda huyu, hatuna ubaya nae wowote, lakini mbisi kama nini.
Mzee Ali; Mbona mimi nawaita siku zote hamjaja, wanakuja wale walioondoka tu?
Dokta: Tumekuja kwa heshima ya hawa wageni tukwambie wewe na wao wanasikia, sisi hatuna ubaya na huyu na yeye anajua ada yetu, sasa hatupi ada yetu, tunamfanya atupe kwa nguvu akipenda asipende atatupa. Mbaya wenu nyinyi mnaemtafuta huyu hapa tukiondoka anakuja yeye. Kwaherini wacha niondoke.
Mzee Ali; Ngoja kwanza, sema wewe nani? Akataja jina, kwaheti, huyo akachomoka, akaingia mwengine anaongea kwa upole tu lakini kume.
Dokta: Mimi msingenina kuja leo lakini imabidi tu nije.
Mzee Ali: Wewe nani?
Mimi: Sina ubaya na huyu, mimi mtu tu kama wewe.
Mzee Ali; Ndio uongo wa majini huo, mengine yanssingizia wao watu. Unataka nini uko nani?
Dokta" Nipo peke yangu, sihitaji kua na mtu yeyote, haiwahusu niliofata kwa huyu.
Mzee Ali: umefata nini?
Dokta: Wacha niondoke atakwambia mwenyewe huyu anajua, muulize yeye, ananijua sana mimi.
Huyo akachomoka bila kwa heri wala kuaga. Nikahisi sasa Dokta hana jini lililompanda.
Mzee Ali; mmeona kazi hio, huyu Dokta mwili wake upo wazi majini kila namna yanamuingoia, ynagombana yenyewe kwa yenyewe, kutaka kua karibu yake. Hio shida kubwa lakini ina bidi tufanye lililotuleta leo. Leo tuntaka tumtapishe uchawi aliolishwa huyu, na yoyote yule.
Mzea Ali; Dokta hujambo mama?
Dokta; Sijambo.
Mzee Ali: leo nakupa ile ddawa unywe kama nilivyokwambia, ukimnywa ukisikia kichedfu kichefu tapika hapa kwnye hii ndoo tupu, ngoja niisogezew poambeni hii ndoo ya maji, haya ndio yatabatilisha uchawi wpwpte utakaomutapika. Akachukua fuko lake la madawa akaiata pale mlangoni nje, hebu nileteeni chupa za maji safi hap dukani nje.
Simba.
...5.4
ionjo vya Arsis 5 -4
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
maji yakunywa yakaletwa, bahati yule alietumwa ka;eta chupa sita kwenye plasiti zake.
Mzee; Fungua basi hilo fungashio, wape watu maji na mie nipe chupa moja.
Tukapewa maji wote akasema.
Mzee Ali; Dokta kunywa basi nusu hio moja nataka hayo yako ya kunywa niyatie dawa, tumaliza kazi ya leo.
Dokta: hata siwezi kuyanwa haraka haraka.
Mzee Ali; yapunguze humo kwenye ndoo ya maji.
Mke wa Mzee; Ngoja, nyie watoto leteni gilasi safi, usiyamwage bure Dokta.
Mara yule binti walikua wamekaa nje ya mlango kwa uani, akaleta gilasi.
Mzee Ali akasema hayq lete hio gilasi hapa akaiweka mbele wake akatoa kama unga unga una vijani vijani hivi vimekauka akatia kwenye gilasi kama robo gilasi akmwambia haya lete hio chupa yako uliokwisha fungua. Akaichukua akaijaza yale maji, lile vumbi la maji na vile vijani kama vingine vikapanda juu vingine vikaenea kwenye gilasi.
Mzee Ali; Dokta kunywa kidogo kidogo kwa spidi yako, ukinywa kidogo ongeza maji, hii noiliokutilia kipimo chake maji chupa moja utaiona nzito lakini usiiogope haina ladha yoyote utaona harufu ya majani tu. Dokta akaanza kuinywa kidogo anaongeza maji aksma..
Haya maji si tunaweza kuchanganya kwenye hii chupa maana naona nzito sana.
Mzee Ali: unaweza Dokta, tia humo ongeza maji mengine kwenye gilasi mpka aitapofikia, kunywa kwa raha zako, nradi umalize hayo maji ya lita moja.
Dokta akawa anakunywa taratibu sana, mimi naona Dah hii lita moja huyu Dokta itamchukua saa nzima kuimaliza.
Mimi: Naomba nikasikilize simu kidogo nje, Mzee naomba funguo za gari.
Mzee Ali, anamaliza sasa hivi huyu.
Mimi; Sikawii kabisa.
Nikachukua funguo za gari nikaenda kwenye gari kutazama kweli kuna simu zilipigwa. Nikapiga nisioijua namba. Kupokelewa kwanza ile sauti naijua, lakini kichwa kinanambia haiwezekani.
Mimi: Nani mwenzangu?
Jini1: Wewe kila siku tunaongea leo umesahau sauti yangu?
Mimi: Huu utani au vipi, toka lini tukaongea na simu?
Jini1; Sasa si nimekuhitaji mkuu na wewe uko kwenye vilinge vya uganga, ningekujaje hapo bila idhini yako?
Mimi: Hii kali hii?
Jini 1: Sasa mkuu, ikiw naweza kuja tunakua pamoja, nishindwe kuongea na simu. Tena na simu mpya hata wewe hauna hio. Nimeletewa zawadi na rafiki yako wa Kiarabu tuliekea nae Unguja.
Mimi; Acha utani, sema unataka nini ntaka kurudi ndani.
Jini 1; Arsis anakwambia hata saa ngapi ukirudi uende kule mnakokutana, anataka kuongea na wewe kule.
Mimi; Poa.
Jini 1: Na mimi nitakuja ofiusini kwako kabla hujaenda kwa Arsis, kuna vitu kanambia nimalize mimi tu kukuelezea.
Mimi; Poa, huku nikawa narudi ndani, kweli nikakuta Dokta ndio anamalizia malizia maji yake ya dawa Sijakaa sana akayamaliza.
Mzee Ali; Sasa nenda na huyo mwenzaki uani huko, ukisikia kutapika utatapika kwenye hio ndoo tupu, huyo anajua cha kufanya atakuelekeza.
Wakatoka Dokta na mkewe.
Mzee Ali; Mmeona jamani kazi zetu, hizi ndio zimenitoa kwetu Kojani kunileta mjini huku, matatizo ya majini ni mengi sana.
baba yeye kakaa kimya tu, hua hapoendi kuongelea vitu asivyoivijua au akiwa na mtazamao tofauti, yaani kwa ufupi haendi kubishana kabisa. Mimi nikawa naguna kuashiria kumsikiliza.
Mzee Ali; Sasa hiviu yyule ataanza kutapika uchawi aliomezeshwa. mimi sifahamu kitatoka nini, watu wengine wanatoka mpoka vyura tumboni.
Mimi: dah, hatari.
Mzee Ali: Si ndogo, si umeina mijini ilivyokua inakuja ile, kama sina kinga za kikwetu saa hizi patashika nguo kuchanika, ndio maana siku hizi tunawalisha zile skin taiti wakija kina mama. Bila vile kuna sinema hapa si mchezo. Nyie mmekuta huyu Dokta hivyo vojini vyake vya siku nyingi ndio maana hakua na piroka ypoypote, lakini kuna wale wa kusukumiwa halafu wanajua wanataka kutolewa, inakua earangati humu si la kawaida, wengi tunaita vijana wenye nguvu zao wawafunge kamba.
Mimi; Sasa mnajuaje kama huyo atakua na fujo na huyu hana?
Mzee Ali; uzoefu wa kazi kijana, mimi hii kazi ya ukoo na nimefundishwa na wazee wangu na majini wenyewe wanaonisaidia hizi kazi. Mika mingi sasa, toka mimi mdogo ndio mambo nayoyaona haya.
Haijapita muda yule mkewe wakarudi na ndoo zote mbili ile yenye maji kwanza ilikua imebaki kama nusu na ile tupiu ikawa na maji kiasi hivi.
Mkewe: Nimemwabia Dokta akakoge atulizane, maana anaonesha kachoka sana.
Mzee Ali; haya akimaliza aje kuona mwenyewe kinachoendelea, kazi iliobaki ndogo, huvixhma tu hayo mauchawi aliyatoa. Umelete basi.
Mkewe akatoka kaacha zile ndoo hapo pembeni.
Mzee Ali tazameni tu muone kuna nini?
Mie nikanyuka nikatazama mzee akasema inatosha nikiona mimi tu, yeye hakunyanyuka.
Mimi: naona kama kuna megu mbegu sijui za nini hizi? Na naona kama kiuna hirizi tatu, mboili nyeusi moja nyekundu.
Mzee Ali: hakuna vichupa humo? Au karatasi za tarasimu?
Mimi hakuna ziko hizo tena sijui kama ni herizi hizi au nini?
mzee akanyanyuka akatazama ndani ya ndoo.
Mzee Ali ; hizi sio herizi za kibinadamu, hizi herizi za kijini, itambaa tu hivi vimepigwa fundo, kila tangi hapo na jini wake, itakua majini yanamgoimbani ahuyu, kila mmoja awe ndio kiti chake yeye hapo.
Mara wakarudi, hapoi ndio nikamuona Dokta vizuri, maana alikua amevua lile dira na skin taiti, alikua amevaa abaya zile za ghali inaonesha, na kishakoga yupo fresh. Uong mbaya alikua bomba haswa na ana mzuto fulani na ile rangi yake, Mie moyo paa. Nikamlaani shetani pale.
Mzee Ali; Dokta tazama madude yaliotoka hayo ywambiw unaytajua?
Dokta; siiyajui.
Mzee Ali: sasa hapo tumetoa vifungo vua kijini, bila hivyo kutoka jini haondoki. haimaanishi kama majini wametoka , hawapo kwa saas lakini wanaweza kuingi an kutoka musa wowote mpaka tuwatoe kabisa. Hao kazi ya kuwatoa atakwambia Sheikh... ka leo tumemaliza iliobaki kazi yangu nitaifanyia mwenyewe hapo uani ya kutekeza hivi vifungo.
Dokta; Na hizi mbegu za nini? nazi nimeitapika mimi?
Mzee Ali; Vyote hivyo ndio vifungo vyenyewe, unaweza kukta jiniwa mbegu mwingine, jini wa hizo mwingine, lakini mimi najua hivyo vifundo vyeusi na vyekundu majini ya Kingazja hayo ya koo tpofauti, hayao yanashindana. Yalikua yanakiushndania, sasa inawezekana hizo mbegu vimbomu vyao wanavyopigania au vofungo, lakini nitapata habari zake nitakujulisha kesho kwa simu. Haya Dokta tumealiza kwa leo. Jamani tumemaliza, hio kazi ya leo imeishia hapo, kama mna swali lolote naagana na Dokta nje hapo.
Na mimi na mzee tukatoka, tukakawacha wenyewe waongee kwa mbali huko walipomaliza tukaagana na Mzee Ali tukabadilishan namba. Tukaelekea kwenye gari yetu, tukakutana na dokta na yeye kile kigari kweli kilikua chake.
Mimi: Dokta nimefurahi kukujua.
Dokta: Jinsi nilivyokua taabani hata hii gari naona tabu kuendesha. Nyie mnaendea wapi?
Mimi: Sisi sipo mbali hapa Ilala tu.
Dokta: Mimi nakaa Upanga, hivi hapo Ilala siwezi kupata chakula maana sijala kiti kabisa leo, aliponambia kuna kutapishana sikula kuanzia asubuhi.
Baba: Yupo Barafaa Ilala, chpsi kuku, pzuri kama huwezi kuendesha wacha Simba aendeshe mpaka hapo mimi tutakutana hapo, hata mimi mmenitamanisha kuku wa barafaa. Haya nneda simba kamuwndeshe Dokta. Nikacheka.
Nikashuka Dokta akshuka akakaa kwa abiria, nikaanz akundesha, mimi kimya.
Dokta; Nyinyi mnakaa Ilala na nyinyi mmekuja kwa shida zenu kw Mzzee Ali?
Mimi: Hapana, mimi najuana na Sheikh...wa Unguja ndio kanambia nije kumjua Mzee Ali na nione kazi anazofanya, imekua na wewe ndio upo hapo.
Tukafika kwa Barafaa, ile kuweka gari, barafaa kuniona.
Barfaa; Simba kama kawaida yako, nikamwabia hapan aleo nimekuletea mgeni, Dokta unachukua au unakula hapahapa?
Dokta: Bora nile hapahapa kama utanisubiria nile.
Mimi;l Poa haya twende tukakae palee, naona Mzee kishaingia itabidi anisubiri.
Nikaenda kwenye gari ya mzee nikamwambia akasema sisi tuchukulie nyumbani huyo Dokta akikataa kuendesha mxhukulie teksi wewe noo na gari yake nyumbani titampa mtu ampelekee. Mimi ukija nyumnai nichukulie iule order yetu ya kawaida. Akamuaga Dokta kwa mabli, akaondoka zake.
Mimi: Barafaa ile kawaida yangu ya kuchukua nifungie na pale tupe nusu mbili na chpsi na juisi kwa wingi, jagi moja na glasi.
Barafaa: Poa Simba, umeongeza mke? Au uko njiani?
Mimi; IshaaAllah iwe dua ya heri.
Tukala pale na dokta nikam zee alivyosema, dokta akasema hajisikii vizuri, labda kwa yale maji madawa aliopewa, lakini amaekula vizuri atapata nguvu na juisi ile akaipenda ya Barafaa, akatiliwa kwenye chupoa za takeaway, nikamchukulia taxi tukabadilishana namba nikamwabia sasa hivi kuna kijana atamepelekea gari yake, atampigia amuelkeze wapi. Dokta akasema hakuna shida akaondoka na mimi nikaondoka nazigo nikulitegemea. Nikakuta mzee kishawambia kuna kuku chipsi nakuja nazo, nikakuta nyumbani wanazingoja kwa hamu. Nikawawachia pale nikaenda na mimi kukoga kubadili kujipumzisha kidogo niende kwa arsis. Nikakumbiuka Jini1 alisema anata aongee na mimi.
Nikaingia ofisini kwangu ili niongee nae.
Simba.
...5.5