Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

ionjo vya Arsis 5 -4

nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.

maji yakunywa yakaletwa, bahati yule alietumwa ka;eta chupa sita kwenye plasiti zake.

Mzee; Fungua basi hilo fungashio, wape watu maji na mie nipe chupa moja.

Tukapewa maji wote akasema.

Mzee Ali; Dokta kunywa basi nusu hio moja nataka hayo yako ya kunywa niyatie dawa, tumaliza kazi ya leo.
Dokta: hata siwezi kuyanwa haraka haraka.

Mzee Ali; yapunguze humo kwenye ndoo ya maji.

Mke wa Mzee; Ngoja, nyie watoto leteni gilasi safi, usiyamwage bure Dokta.

Mara yule binti walikua wamekaa nje ya mlango kwa uani, akaleta gilasi.

Mzee Ali akasema hayq lete hio gilasi hapa akaiweka mbele wake akatoa kama unga unga una vijani vijani hivi vimekauka akatia kwenye gilasi kama robo gilasi akmwambia haya lete hio chupa yako uliokwisha fungua. Akaichukua akaijaza yale maji, lile vumbi la maji na vile vijani kama vingine vikapanda juu vingine vikaenea kwenye gilasi.

Mzee Ali; Dokta kunywa kidogo kidogo kwa spidi yako, ukinywa kidogo ongeza maji, hii noiliokutilia kipimo chake maji chupa moja utaiona nzito lakini usiiogope haina ladha yoyote utaona harufu ya majani tu. Dokta akaanza kuinywa kidogo anaongeza maji aksma..

Haya maji si tunaweza kuchanganya kwenye hii chupa maana naona nzito sana.
Mzee Ali: unaweza Dokta, tia humo ongeza maji mengine kwenye gilasi mpka aitapofikia, kunywa kwa raha zako, nradi umalize hayo maji ya lita moja.

Dokta akawa anakunywa taratibu sana, mimi naona Dah hii lita moja huyu Dokta itamchukua saa nzima kuimaliza.

Mimi: Naomba nikasikilize simu kidogo nje, Mzee naomba funguo za gari.
Mzee Ali, anamaliza sasa hivi huyu.
Mimi; Sikawii kabisa.

Nikachukua funguo za gari nikaenda kwenye gari kutazama kweli kuna simu zilipigwa. Nikapiga nisioijua namba. Kupokelewa kwanza ile sauti naijua, lakini kichwa kinanambia haiwezekani.
Mimi: Nani mwenzangu?
Jini1: Wewe kila siku tunaongea leo umesahau sauti yangu?
Mimi: Huu utani au vipi, toka lini tukaongea na simu?
Jini1; Sasa si nimekuhitaji mkuu na wewe uko kwenye vilinge vya uganga, ningekujaje hapo bila idhini yako?
Mimi: Hii kali hii?
Jini 1: Sasa mkuu, ikiw naweza kuja tunakua pamoja, nishindwe kuongea na simu. Tena na simu mpya hata wewe hauna hio. Nimeletewa zawadi na rafiki yako wa Kiarabu tuliekea nae Unguja.
Mimi; Acha utani, sema unataka nini ntaka kurudi ndani.
Jini 1; Arsis anakwambia hata saa ngapi ukirudi uende kule mnakokutana, anataka kuongea na wewe kule.
Mimi; Poa.
Jini 1: Na mimi nitakuja ofiusini kwako kabla hujaenda kwa Arsis, kuna vitu kanambia nimalize mimi tu kukuelezea.
Mimi; Poa, huku nikawa narudi ndani, kweli nikakuta Dokta ndio anamalizia malizia maji yake ya dawa Sijakaa sana akayamaliza.

Mzee Ali; Sasa nenda na huyo mwenzaki uani huko, ukisikia kutapika utatapika kwenye hio ndoo tupu, huyo anajua cha kufanya atakuelekeza.

Wakatoka Dokta na mkewe.

Mzee Ali; Mmeona jamani kazi zetu, hizi ndio zimenitoa kwetu Kojani kunileta mjini huku, matatizo ya majini ni mengi sana.

baba yeye kakaa kimya tu, hua hapoendi kuongelea vitu asivyoivijua au akiwa na mtazamao tofauti, yaani kwa ufupi haendi kubishana kabisa. Mimi nikawa naguna kuashiria kumsikiliza.

Mzee Ali; Sasa hiviu yyule ataanza kutapika uchawi aliomezeshwa. mimi sifahamu kitatoka nini, watu wengine wanatoka mpoka vyura tumboni.

Mimi: dah, hatari.

Mzee Ali: Si ndogo, si umeina mijini ilivyokua inakuja ile, kama sina kinga za kikwetu saa hizi patashika nguo kuchanika, ndio maana siku hizi tunawalisha zile skin taiti wakija kina mama. Bila vile kuna sinema hapa si mchezo. Nyie mmekuta huyu Dokta hivyo vojini vyake vya siku nyingi ndio maana hakua na piroka ypoypote, lakini kuna wale wa kusukumiwa halafu wanajua wanataka kutolewa, inakua earangati humu si la kawaida, wengi tunaita vijana wenye nguvu zao wawafunge kamba.

Mimi; Sasa mnajuaje kama huyo atakua na fujo na huyu hana?
Mzee Ali; uzoefu wa kazi kijana, mimi hii kazi ya ukoo na nimefundishwa na wazee wangu na majini wenyewe wanaonisaidia hizi kazi. Mika mingi sasa, toka mimi mdogo ndio mambo nayoyaona haya.

Haijapita muda yule mkewe wakarudi na ndoo zote mbili ile yenye maji kwanza ilikua imebaki kama nusu na ile tupiu ikawa na maji kiasi hivi.

Mkewe: Nimemwabia Dokta akakoge atulizane, maana anaonesha kachoka sana.
Mzee Ali; haya akimaliza aje kuona mwenyewe kinachoendelea, kazi iliobaki ndogo, huvixhma tu hayo mauchawi aliyatoa. Umelete basi.
Mkewe akatoka kaacha zile ndoo hapo pembeni.
Mzee Ali tazameni tu muone kuna nini?

Mie nikanyuka nikatazama mzee akasema inatosha nikiona mimi tu, yeye hakunyanyuka.
Mimi: naona kama kuna megu mbegu sijui za nini hizi? Na naona kama kiuna hirizi tatu, mboili nyeusi moja nyekundu.

Mzee Ali: hakuna vichupa humo? Au karatasi za tarasimu?
Mimi hakuna ziko hizo tena sijui kama ni herizi hizi au nini?

mzee akanyanyuka akatazama ndani ya ndoo.

Mzee Ali ; hizi sio herizi za kibinadamu, hizi herizi za kijini, itambaa tu hivi vimepigwa fundo, kila tangi hapo na jini wake, itakua majini yanamgoimbani ahuyu, kila mmoja awe ndio kiti chake yeye hapo.
Mara wakarudi, hapoi ndio nikamuona Dokta vizuri, maana alikua amevua lile dira na skin taiti, alikua amevaa abaya zile za ghali inaonesha, na kishakoga yupo fresh. Uong mbaya alikua bomba haswa na ana mzuto fulani na ile rangi yake, Mie moyo paa. Nikamlaani shetani pale.

Mzee Ali; Dokta tazama madude yaliotoka hayo ywambiw unaytajua?
Dokta; siiyajui.
Mzee Ali: sasa hapo tumetoa vifungo vua kijini, bila hivyo kutoka jini haondoki. haimaanishi kama majini wametoka , hawapo kwa saas lakini wanaweza kuingi an kutoka musa wowote mpaka tuwatoe kabisa. Hao kazi ya kuwatoa atakwambia Sheikh... ka leo tumemaliza iliobaki kazi yangu nitaifanyia mwenyewe hapo uani ya kutekeza hivi vifungo.
Dokta; Na hizi mbegu za nini? nazi nimeitapika mimi?
Mzee Ali; Vyote hivyo ndio vifungo vyenyewe, unaweza kukta jiniwa mbegu mwingine, jini wa hizo mwingine, lakini mimi najua hivyo vifundo vyeusi na vyekundu majini ya Kingazja hayo ya koo tpofauti, hayao yanashindana. Yalikua yanakiushndania, sasa inawezekana hizo mbegu vimbomu vyao wanavyopigania au vofungo, lakini nitapata habari zake nitakujulisha kesho kwa simu. Haya Dokta tumealiza kwa leo. Jamani tumemaliza, hio kazi ya leo imeishia hapo, kama mna swali lolote naagana na Dokta nje hapo.

Na mimi na mzee tukatoka, tukakawacha wenyewe waongee kwa mbali huko walipomaliza tukaagana na Mzee Ali tukabadilishan namba. Tukaelekea kwenye gari yetu, tukakutana na dokta na yeye kile kigari kweli kilikua chake.

Mimi: Dokta nimefurahi kukujua.
Dokta: Jinsi nilivyokua taabani hata hii gari naona tabu kuendesha. Nyie mnaendea wapi?
Mimi: Sisi sipo mbali hapa Ilala tu.
Dokta: Mimi nakaa Upanga, hivi hapo Ilala siwezi kupata chakula maana sijala kiti kabisa leo, aliponambia kuna kutapishana sikula kuanzia asubuhi.
Baba: Yupo Barafaa Ilala, chpsi kuku, pzuri kama huwezi kuendesha wacha Simba aendeshe mpaka hapo mimi tutakutana hapo, hata mimi mmenitamanisha kuku wa barafaa. Haya nneda simba kamuwndeshe Dokta. Nikacheka.

Nikashuka Dokta akshuka akakaa kwa abiria, nikaanz akundesha, mimi kimya.
Dokta; Nyinyi mnakaa Ilala na nyinyi mmekuja kwa shida zenu kw Mzzee Ali?
Mimi: Hapana, mimi najuana na Sheikh...wa Unguja ndio kanambia nije kumjua Mzee Ali na nione kazi anazofanya, imekua na wewe ndio upo hapo.

Tukafika kwa Barafaa, ile kuweka gari, barafaa kuniona.
Barfaa; Simba kama kawaida yako, nikamwabia hapan aleo nimekuletea mgeni, Dokta unachukua au unakula hapahapa?
Dokta: Bora nile hapahapa kama utanisubiria nile.
Mimi;l Poa haya twende tukakae palee, naona Mzee kishaingia itabidi anisubiri.

Nikaenda kwenye gari ya mzee nikamwambia akasema sisi tuchukulie nyumbani huyo Dokta akikataa kuendesha mxhukulie teksi wewe noo na gari yake nyumbani titampa mtu ampelekee. Mimi ukija nyumnai nichukulie iule order yetu ya kawaida. Akamuaga Dokta kwa mabli, akaondoka zake.

Mimi: Barafaa ile kawaida yangu ya kuchukua nifungie na pale tupe nusu mbili na chpsi na juisi kwa wingi, jagi moja na glasi.

Barafaa: Poa Simba, umeongeza mke? Au uko njiani?
Mimi; IshaaAllah iwe dua ya heri.

Tukala pale na dokta nikam zee alivyosema, dokta akasema hajisikii vizuri, labda kwa yale maji madawa aliopewa, lakini amaekula vizuri atapata nguvu na juisi ile akaipenda ya Barafaa, akatiliwa kwenye chupoa za takeaway, nikamchukulia taxi tukabadilishana namba nikamwabia sasa hivi kuna kijana atamepelekea gari yake, atampigia amuelkeze wapi. Dokta akasema hakuna shida akaondoka na mimi nikaondoka nazigo nikulitegemea. Nikakuta mzee kishawambia kuna kuku chipsi nakuja nazo, nikakuta nyumbani wanazingoja kwa hamu. Nikawawachia pale nikaenda na mimi kukoga kubadili kujipumzisha kidogo niende kwa arsis. Nikakumbiuka Jini1 alisema anata aongee na mimi.

Nikaingia ofisini kwangu ili niongee nae.
Simba.

...5.5
Nilipoingia, nimeingia na kahawa yangu. Sijakaa sana Jini 1 kagonga mlango akaingia. Tukasalimiana, baada ya kiusalimiana tu.
Jini 1; Ona hii.

Kutazama kanipa simu. Mpya ya kisasa kwa siku hizo, motorola ndondogo sana na kikoba chake cha ngozi.

Mimi: Hongera, ulikua unasema nini?
Jini1; nimekuja kukuonesha simu yangu mpya, lakini mama yuko hapa, yeye ndio alikua kule mlikokwenda leo, mimi nilikua nachezea skmu yangu mpya. huku anacheka.
Mimi: mwache aje, maana mimi nataka niende kwa Arsis, si amenambia tuonane nae?
Jini1; Arsois anasema sio muhimu aliotaka kukuelezeza yote tukueleze sisi, ndi ohahyohayo anasema usihangaikelabda uwe na yako mengine.
Mimi: Mwambie ahsate sana, sina yangu leo, nikiwa nayo itakwenda. Wacha mamako aje, nimechoka sana leo.

Maramlango ukagongwa, nikajua aina ya ule mgongo ni mamake Jini 1. Nikasema, ingia. Akafungua mlango akaingia, tukasalimiana pale.
Jini2; Simba, umeona mambo leo?
Mimi; Hata sielewi nini kinaendelea.
Jini2; Yule Dokta ana matatizo kweli, ule Mzee Ali na yeye anamatagtizo makubwa sana kuliko Dokta, yule anahigtaji kusaidiwa lakini hajijui. Dokta anahitaji msaada lakini mimi binafsi siwezi kuingilia wala kufanya kazi yake, hio ni Arsis tu. Mimi Nilikua pale kwa ajili a kuangalia kama nyinyi nione kama kuna mambo na majini ya kichawi.
Mimi; Ukayaona?
Jini2: Huyo Ali majaini hyake yote yua kichawi, mchawi mkubwa yule asiejijua. Dokta ana majini ya Kikwao aina mbili, yanayoitwa Kibuki na Yanyoitwa ndammulaki, haohao vibuki wote lkini wa koo mbili, moja ya babake na moja ya mamake, wanashinda nani zaidi.
Mimi; Mambo yenu hayo mimi yananihusu nini?
Jini 2; haykuhusu lakini nimeongea na Arsis kasema tukueleze kila kitu, subiri nimalizie nilioyaona huko kwa mtazamo wangu, ukiwa na maswali mengi utamuuliza Arsis.
Mimi; haya sema.
Jini 2: kwanza salaam zako kwa kwa bakora, anasema hakuna dawa zozote pale alizopewa, kapewa majani ya kutapisha yale yamechanganywa na majivu yakatiwa kwenye maji, ndio akatapika. Sema yule Dokta ana akili sana alipojua anakuja kutapishwa hakiula kitu chochote chochote leo alikua anakunywa maji tu, ndio maana hana nguvu, lakini sasa hivi yuko poa, chakula mlichokula kwa Barafaa ni dawa kuliko majivu alionyweshwa huko. Mzee SAli muhuni sana. Unajua vile vifundo kaviingiza yeye na vile vimbegu kaviingiza yeye kama mchezo wa kitoto tu wa mazingaombwe, mngekua mnatazama vizuri mngeona lakini mlikua hamtazami. Hakuna chochote pale makororo yake tu.

Mimi: Duh! Sasa anatatizo gani yule Dokta?
Jini 2: Ssa ana matatizo ya majini aina nne yule, hao wa kwa babake na mamake, kuna huyo mtu anampenda sana Dokta tangu shule, huko kwao Unguja, jini la Forodhani hilo, limenganada toka shulle halitaki kumuachia, huyo ni mtu kabisa, unajua nyinyi hamjui majini ni nini. Atakufahamisha Arsis, mimi usiniulize.

Jini 2; Sasa mzee Ali kayaongeza mengine ya Kipemba ili wachume pes kwa mteja wao, Dokta pesa anazo akifanya mchezo wanamfilishi, analipwa viuzuri yule na masafari kila siku yanamuingizia pesa nyiungi tu kwa maisha yenu. Million mbili tatu kutumia kwake wala sio tatizo, mzee Ali kishajua hilo ndio hasemi ukweli, kajifanya chuma ulete mpoemnba yule.
Mimi; Hya unayonambia hata sijui kwanini? Si mmwambie mwenyewe?
Jini 2: Anajua kila kitu yule Daktari lakini hana nguvu, majini ya kwao huko yote ada yao ni kulewa tu, tena mapimbe yake ya Kizungu,m huyo kibuki wa babake, ndama mulaki, anataka kunywa, wakija hao wa mamazake nao wanataka kunywa na ufahari, wangazija wana mambo wale. Bira wale wa babake akiwatumia vizuri anawezaakutengeza pesa nyingi sana, hawa wa kwa mamake ni starehe tu wao. na huyo anaejidai mumewe, huyo mkorofi ndio hataki Dokta aolewe waka aanzishe mahusiano na mwnamme mwengine, huyo ni mtu tena Muislam safi, sema mapenzi tu yamemjaa, haoni hasikii. Huyo kumdhibiti shida sana maana sio mchawi hafanyi mambo yake kichawi, yeye yupuyupoi tu, hata majini ya baba zake na mama zake yameshindwa kumkimbiza pale huyo. Ynabidi yakubaliane nae tu.
mimi; Makubaliano gani?

Jini 2; hayo sasa muulize Arsis. Kuhusj majini ha mzee Ali toka ajuane nae ndio yanamchnganya aidi, hata haelewi nini kinamtokea.
Mimi; sasa majini yake hayawafukuzi?
Jini 2: hayakai, yanapigwa kila siku, yale yapo pale kuchuma habaro zak ynakuja kwambia mzee Ali, akiongea na Dokta aoenkane mganga hodari anajua kila kitu, kumbe utapeli tu. Maana hua anamwambia Dokta mpaka afari zake za kazini, kakutana na nani alikua wapi. Dokta hapo kishauingia mkenge, anaona ajabu, huyu zmee anajuaje mambo yangu.

Mimi: Dah, hatari sana, sasa kwanini wanyaacha?
Jini 2: hayo muulize Arsis, mimi sina ujuzi, hata mimi leo nilifanya kazi hizo za kijinga za kuchinguza watu tu nikuletee maelezo. Unataka kujua nini kingine?
Mimi; Sitaki kujua chochote zaidi, nikitaka nitamuuliza Arsis, sitaki kuchunguza watu tunakatazwa ndani ya Qur'an.
Jini 2 lakini wewe hukuchunguza, wewe umeambiwa uende ukajonee tu ya dunia, upo katika kupewa elimu na Arsis, soisi tunasaoidia tu kukufahamisha usije ukaona kuna maajabu pale, hakuna lolote, watu wanajipigia pesa tu. Unajua Dokta vile vilivyotoka aliamabiwa kila kinachotoka alipe shiliingi ngapi? Kila kifundo pale elfu 50 na mbegu zile elfu 50 na kaambiwa vitu havijaisha mwilini mwake, Mzee Ali kishajitengezea njia ya kupiga pesa zingine. Sasa kama hupendi dhuluma ndio uyazuie hayo.
Mimi: Niyazuie vipi, si zuieni nyie?
Jini 2: Hayo sasa ya Arsis sio yangu. Mie naondoka nimemaliza kukujulisha, ukitaka mengine huyo anaechezea simu kutwa kucha yupo hapa, mie wacha niende, anyajua yote ,mbea huyo.
Jini 1: kazi yako wewe mama, unisukumie mimi?
Mimi: Wala sina hajaa ya kujua mengine, wacheni nikapumzike.
Jini 1: umeahidi utampa mtu apeleke gari ya Dokta, usisahau.
Mimi Botra umenikumbusha wacha nimpigie simu mshikaji ajipatie pesa za usiuku usiku. Tukaagana na Jini 1, nikamwabia hongera kwa simu, namba yako dio ile ulionipigia? Aaah nimebadili laini, sasa hata nikik...5upia huoni namba yangu, ile ukipiga haionekani, wewe usinipigie, mimi nitakupia Simba, wewe si unaniita tu nakuja? Tena siku nyingi hutaki kuongea na sisi.
Mimi: kwa heri

Akaondoka.
Simba.
...5.5
 
Wana ukumbi,
Kabla sijaendelea kujibu hoja na kumalizia kionjo cha Arsis cha kojani na Comoro. Naomba mnisome ka umakini yafatayo;

1) Maswali na msaada kwa watu wanaokuja Private.
ka sasa sijibu mtu private, iwe kwa msaada au maswali mengine. Sababu kubwa ni mbili; ya kwanza, tunaweza kujibu swali au msaada kwa mmoja PM lakini ikawa ikawa ni ya wengi tukilijibu jukwaa la wai, kuna wengi hata kuitumia hio PM hawajui na kuuliza wanakua wagumu, wengine hawajajiunga kabisa wao wanasoma tu na kutamani kuuliza lakini hawawezi, ni kibinadamu tu.

La pili, ni kua kuna watu wameshanijaribu mara kwa mara kuniuliza maswali ya kimtego PM kutaka kujaribu kufahamu naishi wapi na tuonane au wanione vipi, sifahamu nia zao.

Cha ajabu na kushangaza, kuna watu wananiofa pesa, wengine wanani ofa asilimia za biashara zao. Wengine wameniofa mpaka penzi. Hawa ni zaidi ya mmoja, wa kutokea Tanga, Dar, Mwanza na Unguja. Waislam kwa wasio Waisla., sijapokea ombi kam hilo nje ya mikoa hio. Au wanasema kweli kuhusu mikoa au wanasema uongo, au wanasema kweli kuhusu dini na imani zao au wanasema uongo. Sipo kuchunguza mtu, lakini nawaambia sitoi majibu Private waka sitaki kujibizana na mtu Private.

Naomba wote muelewe, mimi sio mganga wa kienyeji, sio mchawi, sio kazi yangu kufanya tiba. Hata jukwaa la wazi ninaloweza kulifanya ni kushauri tu ninachokielewa, sina zaidi ya hapo. Kama mlidhani huu ni uzi wa mganga wa kienyeji au "Shehe" au mchawi, mmekosea sana. Huu ni zui wa kuongelea niliopitia na itafikia ninaopitia mpaka leo ili wengi tuielewe dunia.

Arsis yupo kweli, kama ni jini ni mtu na wasaidizi wake wapo kweli majini wawili wa kike, Jini bakora yupo kweli na ana hekima kubwa sana na anaijua miti shamba kuliko tunavyofikiria, tumieni fura ya kuuliza tiba zenu kwa miti, mizizi, matunda, na hata chakula kii ule vipi. Mtashanagaa uwezo wake. Yote nayajibu kupitia JF kwa idhini yao.

Majini na mizimu ya Kisimba ipo kweli na ni ya jadi ya kwetu ya pande zote za baba na mama lakini mimi binafsi nimeachana nayo kabisa, haina ugomzi na mimi kwa kua sikuachana nayo kwa vibaya, mke wangu nae kaachana nayo, mamaya gu kaachana nayoi kwa kiwango kikubwa lakini bado yupo huko kwa siri, Babagu nae bado yupo huko kwa dhahiri kabisa ingawa umri hamuungi mkono lakini hajaacha vituko vya usimba kila vinapomtokea. Nawaombea wazazi wangu usiku na mchana waachane na usimba wa kishenzi. Arsis amesema usiongee nao kuhusu hilo mpaka wa kuhusishe usianze kuwauliza au kuwiangilia, anasema yeye ana dili na hao masimba wenyewe, wote ni rafiki zake na wengi wao washakaa sawa, sielewi anamaanisha nini kwa hilo, hasemi zaidi.

kama una swali, maswali, tatizo au chochote kile uliza jukwaa la wazi iwe faida kwa wengi.
Simba.
 
Inatokea post namba 223.

Nimeona tuwekane wazi kidogo. Kisa kilichokwisha post namba 223 kimeelezea nilipokabidhiwa majini na babu yangu, yeye alikuita kufunguliwa macho. Kwa kiwango fulani kweli nilifunguliwa macho.

Kisa kilochofatia nikaonesha safari yangu ya kwanza baada ya kuoa, ilionipeleka Shinyanga na majini wakafanikiwa kumfanyia tiba mwanamke aliekua anasumbuliwa na majini. Ieleweke kua sijatibu mimi na wala sijui walitibu vipi zaidi ya mimi kumshika kichwa tu yule mwanamke na walichonielezea hao majini siku ile na baadae.

Kisa hicho ni cha miaka mingi sana nyuma, sasa hivi ni mtu mzima. Babu yangu alishatangulkia mbele ya haki. Shamba letu la ufukweni Duga, lipo mpaka leo, wanaokaa pale kwa sasa ni watoto na wajukuu wa babu walioamua kuishi pale. Watoto waliopo pale ni mmoja mkubwa kwa baba yangu wa kike. Na wakiume na mkewe na wanawe ni kwa mama mwingine na baba yangu, wanachangia baba tu.

Binafsi huwa nakwenda sana Duga shamba la babu, kwa sana namaanisha kila msiumu wa kamba huwa tunaenda mimi na mzee kuvuna kamba. Licha ya kamba, kwa babu kuna minzi mingi sana, kuna miembe mingi. Babu yangu alikua anapenda sana miti ya kudumu, kuna miembe ya aina )ofautoi isiopungua 500 na minazi zaidi ya 1000 aliyoiacha marehemu babu.

Bahati watoto zake wote wanajiweza, wanashughuli zao na mali zao, na wawili, mkubwa wa kike na miumewe na watoto zao na mkubwa wa kiume watumbo lingine ndio wanaoishi huko full time. Waliamua wenyewe waishi huko ili shamba lisikose mtu na lina utajiri wa kutosha. Mbali ya minazi na miembe alioicha babu, kuna miti mingi ya hapa na pale ya matunda, ambayo haipo kwa kiwangi cha biashara. Babu alipanda kila aina ya matunda kidogpo kidogo, shamba la babu ni kubwa sana, sio la kitotpo na nazi karibia kila siku zinangushwa, na pesa wanagawa kwa kila ndugu, Hakuna tatizo, wasimamizi ni wazuri sana na wacha Mungu.

mambo ya tiba na pango kuna wanafunzi wa babu lakini hawako kwa kiwango cha babu lakini mradi wapo tu. Umaar8fi wa kwenda kutibiwa watu kwa mzee Mabruyki uliisha alipoondoka mwenyewe. Mimi binafsi sijairithi kazi ya uganga ya babu, kabisa tena. Wapo majini alioniwachia babu, ikitokea, wao ndio wanatibu watu bila mimi kujua wanachokifanya zidi ya kunijulisha tu.

Arsis yupo, pete yake naivaa kila siku. Jini wa bakora yupo na bakora ya babu aliirithi binti yake ambae anakaa shamba kwa sasa, yeye ndio anaitumia kwa tiba watu wakienda. Anaelewa mwenye anatibu vipi, mimi simuingilii wala simuulizi. Ni shangazi yangu, yeye ananipenda sana na anawaambia kila mtu., mimi ndio mroithi wa babu kwenye uganga.

Visa vinavyofatia sana sana vitakua vya mahojiano kat yangu na Arsis, nitajitahidi kuvifanya vyepesi vieeweke ingawa mimi sio mwandishi.

Arsis mpaka leo ni rafiki yangu na anakuja kila nikimuita xile sehemu zake za kumuita. Mwenyewe anapenda sana kila nikija kwenye msimu wa kamba nimuite kila siku tuongee. Mpaka leo kwa Dar nikita kumuita nakwenda pale oshen road, [pia alinionesha na sehemu nyingine mtajijua wakati kisa kinaende;lea. Hii ipo nje ya mji kidogo.

Visa vijavyo vina elimu kubwa ssna ya Arsis, sio yangu. Mimi najifunza kwake.

Kuna watu wengi wanaongelea kuhusu majini waongo, wazuri, wabaya. Kwenye mahojiano na Arsis tutapata mwanga mkubwa sana kwa mujibu wa Arsis. Napend ieleweke, Arsis anasisitiza sananijifundishe kusoma uandishi ili niandike vizuri, ananambia yeye atanisaidi kumbukumbu kwa niliyoyasahau na atanisaidia kunielezea yale amabyo nitahisi yanahitaji aeleee zaidi.

Nawaahidi nitapitia post moja moja za nyuma na kurekebisha maandishi, kupunguza au kuzidisha na kurekebisha nilipokosea na kuyakusanya kwenye post moja ikiwezekana, yaani kufanyia editing. Ardis kanambia kuna makosa mengi sana, afahamu kua anusoma huu uzi, sifahamu kama ni member JF au hapana, nimemuuliza hilo akanambia " mimi nimekwambia nasoma tu, usiniulize zidi kuhusu hilo". Hiyo ni kawaida yake Arsis, mtajionea mbele huko namuuliza mpaka anakasirika.lakini ni mtummwema sana. Mwenyewe anashikilia nimwite mtu. Ingawa kiukweli sijui ni kiumbe wa aina gani. Mimi nachukulia ni mtu kama mimi lakini hataki aonekane. Isipokua anasema umeshaniona mara nyingi lakini hujui kama ni mimi. Anasisitiza anakuja kwa sura na muonekano tofauti bila mimi kufahamu.

Itaendelea.
Hivi Bujibuji Simba Nyamaume ni jini wa ukoo wenu wa Simba kama alivyo FaizaFixy ? Ambaye siku chache nyuma alikuwa akijiona ni fox kabla hujamshtua
 
Hapo juu ni tangazo la simba, hili chini la Arsis;

Salaam.

Mimi nitaendelea kufundisha kuhusu Adam na mengineyo kidogo kidogo, nikirudi nitauliza maswali kwa niliokwisha yafundisha, unaruhusiwa kutazamia majibu au kujibu ulivyoelewa wewe. Ni elimu kubwa sana ya Kiislam.

Nafahamu wengi sana humu ni mara ya kwanza kusikia hilo na hawaielewei Qur'an lakini wanajifanya wabishi kwa kutokuelewa kwao. Nawajulisha kua, Adam kumuongelea hakututoi kwenye akida kabisa. Wasiogope, kama hawajui akida ni nini katika Uislam waulizew Masheikh zao, itakua ngumu sana kuacha kubishana kijinga ikiwa hata akida ya Kiislam ni nini, wataanza kusema kila kitu ni kufuru.

Uislam hauna mipaka ya elimu, lakini elimu Kiislam ni lazima iwe na ushahidi, ushahidi wetu wa kwanza ni Qur'an na Qur'an haina ushahidi aina mbili tofauti, ama Adam ni mtu wa kwanza ama sio mtu wa kwanza. Ama Hawa yupo kwenye Qur'an ama hayupo Wawache kuongea hewa, hata alienza kumita Hawa, Hawa analijua hilo, kwanni amuite Hawa, nyie Waislam hamjui neno hewa kwa kiarabu linaitwaje? Kama mmejua, sasa katafuteni limetokea wapi.

Nawapa tanbihi Waislam ingienii kwa gea ya elimu, mwisho wa siku bisheni au pingeni mchoke, lakini tunzeni kauli zenu. Mboa Waislam wakubwa wakubwa wa kuanzia zamani wamehitilafiana, hata madhehebu yenu milopachika majina ya watu wote wamehitilafiana au hamjui hilo?

Tuhitilafiane kielimu, sio kijinga jinga.

Mimi sina dhehebu pia wa imani zote lakini naifata Qur'an.

Waislam hamjui watu waloitwa kwanza Wakristo huko Syria ni Wafuasi wa Yesu ambae mnasema ni Muislam, mapagani waliwashngaa misimamo yao, kuwaita Wakristo ni kama leo Muislam uitwe Muhammdan. Kuitwa mkristo a Muhammadan ni kupondwa pondwa na mapagani, kua Muhammadan au kua Mristo sio sifa nzuri kabisa.

Bora hata mabaniani wanasema wao ni Brahmim tena walewa tabaka ya juu kabisa, wanaheshimiwa sana na mabaniani wote. Brahmim maana yake ni wa Ibrahim.
Arsis.
 
Nilipoingia, nimeingia na kahawa yangu. Sijakaa sana Jini 1 kagonga mlango akaingia. Tukasalimiana, baada ya kiusalimiana tu.
Jini 1; Ona hii.

Kutazama kanipa simu. Mpya ya kisasa kwa siku hizo, motorola ndondogo sana na kikoba chake cha ngozi.

Mimi: Hongera, ulikua unasema nini?
Jini1; nimekuja kukuonesha simu yangu mpya, lakini mama yuko hapa, yeye ndio alikua kule mlikokwenda leo, mimi nilikua nachezea skmu yangu mpya. huku anacheka.
Mimi: mwache aje, maana mimi nataka niende kwa Arsis, si amenambia tuonane nae?
Jini1; Arsois anasema sio muhimu aliotaka kukuelezeza yote tukueleze sisi, ndi ohahyohayo anasema usihangaikelabda uwe na yako mengine.
Mimi: Mwambie ahsate sana, sina yangu leo, nikiwa nayo itakwenda. Wacha mamako aje, nimechoka sana leo.

Maramlango ukagongwa, nikajua aina ya ule mgongo ni mamake Jini 1. Nikasema, ingia. Akafungua mlango akaingia, tukasalimiana pale.
Jini2; Simba, umeona mambo leo?
Mimi; Hata sielewi nini kinaendelea.
Jini2; Yule Dokta ana matatizo kweli, ule Mzee Ali na yeye anamatagtizo makubwa sana kuliko Dokta, yule anahigtaji kusaidiwa lakini hajijui. Dokta anahitaji msaada lakini mimi binafsi siwezi kuingilia wala kufanya kazi yake, hio ni Arsis tu. Mimi Nilikua pale kwa ajili a kuangalia kama nyinyi nione kama kuna mambo na majini ya kichawi.
Mimi; Ukayaona?
Jini2: Huyo Ali majaini hyake yote yua kichawi, mchawi mkubwa yule asiejijua. Dokta ana majini ya Kikwao aina mbili, yanayoitwa Kibuki na Yanyoitwa ndammulaki, haohao vibuki wote lkini wa koo mbili, moja ya babake na moja ya mamake, wanashinda nani zaidi.
Mimi; Mambo yenu hayo mimi yananihusu nini?
Jini 2; haykuhusu lakini nimeongea na Arsis kasema tukueleze kila kitu, subiri nimalizie nilioyaona huko kwa mtazamo wangu, ukiwa na maswali mengi utamuuliza Arsis.
Mimi; haya sema.
Jini 2: kwanza salaam zako kwa kwa bakora, anasema hakuna dawa zozote pale alizopewa, kapewa majani ya kutapisha yale yamechanganywa na majivu yakatiwa kwenye maji, ndio akatapika. Sema yule Dokta ana akili sana alipojua anakuja kutapishwa hakiula kitu chochote chochote leo alikua anakunywa maji tu, ndio maana hana nguvu, lakini sasa hivi yuko poa, chakula mlichokula kwa Barafaa ni dawa kuliko majivu alionyweshwa huko. Mzee SAli muhuni sana. Unajua vile vifundo kaviingiza yeye na vile vimbegu kaviingiza yeye kama mchezo wa kitoto tu wa mazingaombwe, mngekua mnatazama vizuri mngeona lakini mlikua hamtazami. Hakuna chochote pale makororo yake tu.

Mimi: Duh! Sasa anatatizo gani yule Dokta?
Jini 2: Ssa ana matatizo ya majini aina nne yule, hao wa kwa babake na mamake, kuna huyo mtu anampenda sana Dokta tangu shule, huko kwao Unguja, jini la Forodhani hilo, limenganada toka shulle halitaki kumuachia, huyo ni mtu kabisa, unajua nyinyi hamjui majini ni nini. Atakufahamisha Arsis, mimi usiniulize.

Jini 2; Sasa mzee Ali kayaongeza mengine ya Kipemba ili wachume pes kwa mteja wao, Dokta pesa anazo akifanya mchezo wanamfilishi, analipwa viuzuri yule na masafari kila siku yanamuingizia pesa nyiungi tu kwa maisha yenu. Million mbili tatu kutumia kwake wala sio tatizo, mzee Ali kishajua hilo ndio hasemi ukweli, kajifanya chuma ulete mpoemnba yule.
Mimi; Hya unayonambia hata sijui kwanini? Si mmwambie mwenyewe?
Jini 2: Anajua kila kitu yule Daktari lakini hana nguvu, majini ya kwao huko yote ada yao ni kulewa tu, tena mapimbe yake ya Kizungu,m huyo kibuki wa babake, ndama mulaki, anataka kunywa, wakija hao wa mamazake nao wanataka kunywa na ufahari, wangazija wana mambo wale. Bira wale wa babake akiwatumia vizuri anawezaakutengeza pesa nyingi sana, hawa wa kwa mamake ni starehe tu wao. na huyo anaejidai mumewe, huyo mkorofi ndio hataki Dokta aolewe waka aanzishe mahusiano na mwnamme mwengine, huyo ni mtu tena Muislam safi, sema mapenzi tu yamemjaa, haoni hasikii. Huyo kumdhibiti shida sana maana sio mchawi hafanyi mambo yake kichawi, yeye yupuyupoi tu, hata majini ya baba zake na mama zake yameshindwa kumkimbiza pale huyo. Ynabidi yakubaliane nae tu.
mimi; Makubaliano gani?

Jini 2; hayo sasa muulize Arsis. Kuhusj majini ha mzee Ali toka ajuane nae ndio yanamchnganya aidi, hata haelewi nini kinamtokea.
Mimi; sasa majini yake hayawafukuzi?
Jini 2: hayakai, yanapigwa kila siku, yale yapo pale kuchuma habaro zak ynakuja kwambia mzee Ali, akiongea na Dokta aoenkane mganga hodari anajua kila kitu, kumbe utapeli tu. Maana hua anamwambia Dokta mpaka afari zake za kazini, kakutana na nani alikua wapi. Dokta hapo kishauingia mkenge, anaona ajabu, huyu zmee anajuaje mambo yangu.

Mimi: Dah, hatari sana, sasa kwanini wanyaacha?
Jini 2: hayo muulize Arsis, mimi sina ujuzi, hata mimi leo nilifanya kazi hizo za kijinga za kuchinguza watu tu nikuletee maelezo. Unataka kujua nini kingine?
Mimi; Sitaki kujua chochote zaidi, nikitaka nitamuuliza Arsis, sitaki kuchunguza watu tunakatazwa ndani ya Qur'an.
Jini 2 lakini wewe hukuchunguza, wewe umeambiwa uende ukajonee tu ya dunia, upo katika kupewa elimu na Arsis, soisi tunasaoidia tu kukufahamisha usije ukaona kuna maajabu pale, hakuna lolote, watu wanajipigia pesa tu. Unajua Dokta vile vilivyotoka aliamabiwa kila kinachotoka alipe shiliingi ngapi? Kila kifundo pale elfu 50 na mbegu zile elfu 50 na kaambiwa vitu havijaisha mwilini mwake, Mzee Ali kishajitengezea njia ya kupiga pesa zingine. Sasa kama hupendi dhuluma ndio uyazuie hayo.
Mimi: Niyazuie vipi, si zuieni nyie?
Jini 2: Hayo sasa ya Arsis sio yangu. Mie naondoka nimemaliza kukujulisha, ukitaka mengine huyo anaechezea simu kutwa kucha yupo hapa, mie wacha niende, anyajua yote ,mbea huyo.
Jini 1: kazi yako wewe mama, unisukumie mimi?
Mimi: Wala sina hajaa ya kujua mengine, wacheni nikapumzike.
Jini 1: umeahidi utampa mtu apeleke gari ya Dokta, usisahau.
Mimi Botra umenikumbusha wacha nimpigie simu mshikaji ajipatie pesa za usiuku usiku. Tukaagana na Jini 1, nikamwabia hongera kwa simu, namba yako dio ile ulionipigia? Aaah nimebadili laini, sasa hata nikik...5upia huoni namba yangu, ile ukipiga haionekani, wewe usinipigie, mimi nitakupia Simba, wewe si unaniita tu nakuja? Tena siku nyingi hutaki kuongea na sisi.
Mimi: kwa heri

Akaondoka.
Simba.
...5.5
Vionjo vya Arsis 5-5

nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.

Alipoondoka Jini 1 nikakaa nikajifikiria niende au nisiende kwa Arsis, nikaamua niende, linalowezekana leo lisingoje kesho.

Nikampigia kijana mshikaji nikampa dili ya kupeleka gari Upanga nikamwambia ukiningoja sehemu nitakupitia turiudi wote, aua ukirudi mwenyewe sawa. Nikamwambia akimaliza huko anipigie anicheki niko wapi, niakua mitaa sio mbali na Upanga.

Nikatoka nikaitoa gari ya Dokta nje, kijana akaja nikamkabidhi aipeleke, nikampigia Dokta, nikahisi kama alikua usingizini, nikamueleza, akanishukuru akasema alikua anafikiria asubuhi atakwendaje kwenye kazi zako. Nikamwabia usijali, akikufikishia huyo kijana nipigie hata saa ngai unijulishe, na alichelewa ikipita lisaa limoja kuaniza sasa nijulishe. Akasema sawa.

Mimi nikaondoka kuelekea kwa Arsis. Kufika langni oshen roodi, kama kawaida nikaita akaja kwa sauti tu.

Arsis: Vipi hali, Simba?
Mimi: Sio poa.
Arsis; Huku anacheka, nimeona babu yako kakupatia mchumba mpya. Unasemaje.
Mimi: Arsis sipo hapa kwa kufanyiana utani, nimekuja hapa nikuulize vitu.
Arsis: Unafikiri natania, hio ndio fikira za babu yako. haya uliza.

Mimi: Arsis, majini wako wamenielezea mengi kuhusu huyo Dokta na mazee Ali lakini kuna mengine wamenambia nikuulize wewe.
Arsis; Nafahamu, kuna vitu hawajui, uliza tu Sumba.
Mimi; Nani huyu Dokta?
Arsis: huyo ni Dokta kweli ytena Daktari bungwa amesoma Urusi, Japan, Australia na ameishi sana Uingereza, kweli ameolewa na madakatari wawili zamni, mmoja ndio mume wake wa kwanza na ni dokta mkubwa sana Tanzania. Huyo wa pili aliolewa kama hasira tu alipoachika na mumewe wa kwanza, Huyo wa pili mtu wa kwenu anga, walikutana walikua wanafanya kazi pamoja. lakini wameachana pia. Ngumu sana huyo kukaa na mume. Ana mengi sana.
Mimi ; Hilo ndio swali langu, kwanini hakai na mume?

Arsis: Huyoi ana mtu alimpoenda sana lakini huyo mtu sio kiwiliwili ni nafsi tu. Ni binadam alaieuliwa lakini nafsi yake haijaingia kwenye umauti.
Mimi: hapo unanichanganya Arsis.
Arsis: naahamu, kwa kua hauna elimu ya majini. Majini wengi sana ni nafsi za watu. Huyo kija n wa Kiarabu ni katika waliouliwa wakati wa mapinduzi Unguja, alidhulumiwa maisha yake, nafsi ipo hai lakini mwilli umekufa na umezikwa kwenye mashimo ya halaiki, Ni kijana wazazi wake walikua kwenye baraza la Sultan lakini hawakua serikalini ni washauri tu. nafsi yake ikawa inatembea tembea sana mpaka leo, huko Unguja, hususan sehemu alipomuona mara ya kwanza Dokta, na maeneo ya nyumbani kwao huyo kijana, karibu ya forishani kwenye majumba ya matajiri siku hizo. Alipomuona Dokta, siku hizo mwanafunzi sekondari, akampenda ndio akawa hatoki kwa Dokta.
Mimi: hatoki vipi?
Arsis: Yupo nae karibu na akamuoa kivuli chake, kwa sababu hawezi kumuoa mwili wake, mpaka sasa anaamini ni mkwe na aana wivu sana hataki mwili wa Dokta uolewe au utembee na mwanamme wengine, akiokewa akitemnbea na wanaume wengine, huyo kijana anatuma rafiki zaake wa kijini wahuni wanamtesa sana Dokta, mpaka imefikia hapendi kabisa wanaume. Kwa bahati mbaya sana mpka akajatribu usagaji lakini hakuupenda akaachana nao kabisa. Alifanya lajini kwa muda tu, alikua na mwanamke wa kibindam mmoja Zanzibar, akaachaa nae kwa ajili ya huyo kijana, alimtesa sana huyoi mwanamke na marafiki zake, ytule mwanamke akaamkimbia Dokta. hataki hata kusikia sauti yake, anamuogopa kabisa.

Huyu wa pili wa hapa hapa Dar, huyu muhunimuhuni sana, huytu hatraki mapenzi ya kweli anatagfuta pesa tu, ni rafiki yake Dokta, lakini hata yeye sio masagaji wa kweli ni muhuni tu, ndio akapna huyu hana mume na mzuei hivi labda msagaji, akaanza kumjribu waksagana ndio wakaanza hivyo, yule anajua jua ni juhuni sana. Dokta nae alihjifunza funza kwa yule wa Unguja, sasa mara moja wakawa wakikuta wanasgana. Lakini haikuchukua muda, Dokta akawa anajichukia kufanya huo uchafu akaacha kabisa, miaka mingi sana sasa. Alikua anaogopa binti yake anakua halafu amuone vile mamake, analala chumba kimoja narafiki yake. Dokta akajifikiria sana akamuomba Mwenyezi Mungu akamuondoshe ahyo kabisa. Akasema boira hayo majini ya ndotoni kuliko huu ushenzi.

Maana yule kijana anakuja kuingiliana nae kwa kivuli, hio ndio inakua ndoto tu. Umeelewa?

Mimi: Inaingia akailini lakini sijaelewa vizuri.
Arsis" Sio lazima uelewe kila kitu mara moja, utaelewa tru kidogo kidogo. Dunia iina siri nyingi sana.

Mimi: sasa hao majini wa kwao hawajauia hio hali ya kuingiwa na jini wa Unguja na hawa wanawake wasagaji?
Arsis: Majini ya kibuki ya ukoo wale hayaingilii kabisa mambi yake binafsi, wenyewe hao vibuki wapo wasagaji wapo mashoiga, hawaingiliaa maisha ya mtu binafsi, wao yao ni starehem kuvaa vizuri, kula vizurui, kua na pesa na kujionesha tu. Wanapenda sa harusi na misiba. Ni majini wasio na akli labda wale waliojaaliwa kutoka kizani. Wana mila za ajabu sana haoi Simba.

Hao hua wanaalikana kulewa tu ili kumkaribisha binadamu mwenye kibuki. Bila pombe hapo yule boinadam hakubaliwi. Na ukiwakubalki hao ukiwapa mapombe wanajuana wenyewe kama ile jini yenu ya Simba. Kila kitu utaona inakwenda vizuri.

Mimi: sasa yeye kwanini wanamtesa?
rsis: Wale kibuki wanaubaguzi sana, wapo ukoo wa baba yake na wapo ukoo wa mama yake, kila mmoja anataka kujionesha nani zaidi. Halafu wote koo hizo wanakubaliana kitu kimoja, kua huyu ni wa kwao halafu mpaka leo hajaolewa kwa ada yao ya harusi.

Mimi ; Ndio nini hiyo?

Arsis: Muoe wewe utajua ndio nini hiyo.
Mimi: Arsis sitaki utani, mi simtaki kumuoa kabisa.

Arsis: usikasirike ni mwanamke mzuri na ataemuoa akifanya ada yao ya Kingazija, atafaidi sana na yule nafsi ya jini haitamsumbua tena si uliambiwa wana mikataba yao?

Mimi; Siiji, hio ndio nilitaka kukuuliza.

Arsis; Nafsi wamekubaliana na hawa kibuki wasiingiliane na hiyo nafsi haiwei kumuoa huyu ibaki hukohuko imeoana na kivuli la sivyo ikimuingilia sana huyiu mwanamke maboi yake ya kibdamu inakua hio nafsi inawatia matatani hao binadam wengine. inaoatuma kupitia majini washenzi. Nfasi hizo zinaonana Arsis, kama wewe unavyonana na miili ya wengine. Hmuingilini mmbo yenu. Ni hivyo hivyo kwa nafasi na zinawea kua na mahusianoi kama nyinyi mlio na miili, hakuna togfauti.
Mimi: sasa wewe Arsis unamsaidia vipi?
Arsis: kana tunataka kuingia makubaliano na majini wakubwa wa vile viujini vya Mzee Ali viondoke x)visimfatefate kabisa. Ndio tunataka wewe umsindikiz Kojani, ipo safari karibu sana.
Mimi: kwani mimi")?

Arsis: kwa sababu wewe ukiwepo huko na yeye anakua kaona mtu mwingine anemfahamu anaiukua hana wasiwasi sana. Hawa(ezi kwenda peke yake, na mambo yaliomtokea kwa marafiki zake, sasa hivi anaogopa hata kua na rafiki wa karibu mwanamme au mwanamke, kapitia mengi sana huyo Dokta, kama isingekua majini hya kwao kumlinda na wachawi, sasa hivi huyo wehu au matrehemu.
Mimi; kwanini?
Arsis: huyo mumewe wa pili alikua na mke, huyo mwanamke akaanza kumrpga kwa kila aina ya waganga na wachawi lakini amtokeo yake huyu Dokta hajadhurika kashurika mumewe na yeye, lakini walishaacha yule mwanamke akamini iau amemshinda huyu kwa aganga wake. Hajijui masiki ya Mungu. N huyu Dokta alikua anota ota anafanyiwwa uchawi lakini alikua anaona ndoto tu hizo. Ni mamboi mengi lakini cha muhimu, sasa anahitaji aolewe, ndio njia ya kumsaidia na arudishe furaha na amani yake asiogope tena binadam wenzie. Na hio ni rahisi sana. Kwanza waondoke vijini vya Mzee Ali, muongo tu tapeli yule. Mimi nashauri kabla hujaenda Pemba nenda Unguja ukaonane na mkubwa wa vibuki vya upoanda wa babake, ukiend tu pale watajua umefata nini na hawatamvumbua tena, sisi tutakua tayari tunfanya mikataba nao. Lakini mimi nataka uende ukaione dunia, siku mbili tu inakutosha. Ukaone na sherehe yao ya pombe, lakini huyu atakua ytauari hataki hio sherehe, akiifanya huko basi kataka mwenyewe tu sio vibuki. Fanyta uende huko.

Mim: msiniinginze kwenye mamboi yenu, sitaki vita na majini.
Arsis; hakuna jini duniani anaeweza kufanya vita na wewe, akiona hio ete tu wanakimbia mbali sana na wanakuheshimu sana, Madini ya hio pete sio ya kawaida hata Mafalme wa kijini wanayatak hawayapati. Wafalme akijini wakiipayta hio peyte ulioivaa wapo tayari kukyufanya tajiri mkubwa duniani, wao wanachotaka ni hicho kito na hio chuma iliochnganywa hapo, waiyeyusha hio hawajali muhuri uliopo hapo, watan)vunja nia za mwasiliano tulizoiwekea, itakua saa watafanya mawasilano na watu wanaotaka wao, na sana ni watu hatari na wenye nguvu duniani. Simba kwa sasa inatisha, lazima uende Unguja, vipi mimi sijui, mimi nakushairi tu nenda ili urudishea maisha ya mtu huyu muhimu sanakwenye hadhi yake.
Mimi; Ana umuhimu gani?
Atsis: huyo dakatariamesoma sana na ana ubunifu sana kwenye kazi yake, ndio maana hata Wazungu wanamtaka duniani huko, huyo sasa hivu yupo Tanzania lakini amaeajiriwa na chuo kikubwa cha Wamarekani, unafikri watamuajiri mtu hovyo hovyo? Sasa kanini asiajiriwe na Srerikali ya tanzania ikawa fanida kwa Watanzania? Fikiri hilo, isiache hizo safari mbi na ya tatu itakua ngazija, ukaone ada ya harusi za wangazzija labada itakujia hamu ya kuoia mngazija.
Mimi: Arsis; kwaheri.
Arsis; kwaheri huku anacheka.

mimi nikaondoka pel kufika kwenye gari nikatazama zi,mu yangu nikakuta yule dokta alinipigia muda si mrefu kama dakika kumi nyuma na yile kijana kama nusu saa nyuma. Nikaanza na Dokta, nikampigia hata haikuita mata)ra mbili aka[pokea.
Dokta: Hello, Simba? Nilikupigia kukujulisha tari imeletwa, Ahgsante sana. Sasa hivi nipo fresh kabisa, imekua viuri nilichukua wale kuku pale hivi nawala sasa hivi, nimeipenda juisi yao.
Mimi: Okay poa, hakuna shida, si umeshapajua pale?
Dokta; Napajua pale siku nyingi lakini ndio mpaka niende na wenzangu. Lakini nilikua sijawahi kunywa hii jiuisi yake, nilikua naagiza soda tu.
Mimi: Nikahisi kama anahamu ya kuongea zaidi, nikamkatiz; Sawa Dokta, mradi gari imefika salama na wewe upo salama tuombeane dua tu.
Dokta; Kuna kitu nilitaka kukuuliza kuhusu Mzee Ali.
Mimi: Dokta naendesha sasa hivi nimesimama kuona miss call yako, tu tuongee kesho, samahani.
Dokta: Bila samahani, nitakupigia kesho, niasmehe sana.
Mimi; No problrm ahsante.

Tukaagana pale nikampigia mshikaji aliepeleka gari.

Mshikaji: Hoyaa Simba, mimi nishaondoka s)muda mregfu nimempa gari yule dada, nilitamani anikaribishe ndani, yupo bomba kishenzi. Nitum tana kwake.
Mimi; Ushafika ilala?
Mshikaji: bado natumiampesa alionipa, yule dada ana poesa ndefu sio njaa njaa kama wewe.
Mimi: Unatumia peke yako? Nambi uko wapi na mimi nije.
Mshikaji: Wewe hupawezi hapa tunapotumia sisi nipo kariakoo, wewe nenda tu tutaonana mitaani.
Mimi: kariakoo sehemu gani mimi ndio nakaribia mitaa ya Kariakoo.
Mshikaji: Unapjua Pajero bar? ndio nipoa hapa na mipashkuna ya Kariakoo inaimba taarabu.
Mimi: Mshikaji mpaka unajimwaga hivyo, itakua mshiko mrefu basi?
Mshikaji: Bia za kuzugia ninazo leo lakini za ofa ndio sina au utapiata uniachie kitu?
Mimi; Sipajui wala sipiti kwenye ma bar.
Mshgikaji: Wewe usiingie, piata nje mimi nitatoka?
Mimi: Ipo wapi kwnai, akanielekeza.
Mimi; Pole, sana hapo umeumizwa, napajua sasa. Sipiti njia hio, mimi nipo Mtaa wa Lindi sasa naelekea nyumbani. Tuwasilane kesho unipe michapo ya Pajero, kuna moja hilo halitoki hapo linaitwa Nusura, jeupe kama toto kla kigiriki.
Mshikaji; Yupo hapa na mabwana zake anawachuna na mashoga zake kibao. Sijui kapata shamba gani la kutokea wapi sijui limaitwa haruna, linatumia hilo kama halina akili vizuri, sijui jambazi hili. Tushapigwa raundi tatu bar nzima hii na hilo jamaa.
Mimi: kwaheri utanipa michapo kesho.
Mshkaji: Hakuna noma, nitume kwa yule Dada saa yoyote hata nimpelekee ndizi za sokoni kwa pesa zangu, sitaki usafiri wala unilipe kitu, ile ndio mi dada ya kujuana nayo si hii ya Pajero, inanuka mibia.
Mimi; kwaheri, nikakata simu, nikajua huyo kishalewa, hanyamazi.
Simba.
...5.6
 
Usiseme wanaukumbi.
Sema ndugu zangu Waislamu,
Tujadili mambo yetu ya dini yetu.
لَا أَعْبُدُ مَا تَعْبُدُونَ

[ AL - KAFIRUN - 2 ]
Siabudu mnacho kiabudu;
Njoo ufundishe dini yako inasemaje kuhusu mapepo.
Simba.
 
I just wanted to know...
Since it came in my dreams once as I saw women in a room telling me I have inherited "nguvu za Simba" from my Dad
 
sio lazima kuhatibu mada ya mtu kama hujaipenda kaa kimya hujalazimishwa kuchangia
Usijali Sheikh Che mittoga haharibu, anazidisha elimu, mjibuni hoja zake.

Kwanini anaharibu mada na yeye anachangia mada?
Simba.
 
kama kuna mtu kauliza swali hajajibiwa aseme lipo oost namba ngapi?
Simba.
 
I just wanted to know...
Since it came in my dreams once as I saw women in a room telling me I have inherited "nguvu za Simba" from my Dad
So you have. She will come again and again until you know yourself.
Simba.
 
Kwa hiyo kwa maelezo yako wakristo wanadharaulika? Sababu ni kumfuasa Yesu mwana wa Mungu? Tunajua huna historia nzuri na Mungu. Tunajua ulifungiwa kwenye chupa. Mtu mwema hawezi kufungwa. Ni Mungu alikufungua? Ni binadamu? Ni maandishi ya Qur'an? Ni majini wakubwa zaidi?
Na ni kwa nini unauchukia ukristo?
Hapo juu ni tangazo la simba, hili chini la Arsis;

Salaam.

Mimi nitaendelea kufundisha kuhusu Adam na mengineyo kidogo kidogo, nikirudi nitauliza maswali kwa niliokwisha yafundisha, unaruhusiwa kutazamia majibu au kujibu ulivyoelewa wewe. Ni elimu kubwa sana ya Kiislam.

Nafahamu wengi sana humu ni mara ya kwanza kusikia hilo na hawaielewei Qur'an lakini wanajifanya wabishi kwa kutokuelewa kwao. Nawajulisha kua, Adam kumuongelea hakututoi kwenye akida kabisa. Wasiogope, kama hawajui akida ni nini katika Uislam waulizew Masheikh zao, itakua ngumu sana kuacha kubishana kijinga ikiwa hata akida ya Kiislam ni nini, wataanza kusema kila kitu ni kufuru.

Uislam hauna mipaka ya elimu, lakini elimu Kiislam ni lazima iwe na ushahidi, ushahidi wetu wa kwanza ni Qur'an na Qur'an haina ushahidi aina mbili tofauti, ama Adam ni mtu wa kwanza ama sio mtu wa kwanza. Ama Hawa yupo kwenye Qur'an ama hayupo Wawache kuongea hewa, hata alienza kumita Hawa, Hawa analijua hilo, kwanni amuite Hawa, nyie Waislam hamjui neno hewa kwa kiarabu linaitwaje? Kama mmejua, sasa katafuteni limetokea wapi.

Nawapa tanbihi Waislam ingienii kwa gea ya elimu, mwisho wa siku bisheni au pingeni mchoke, lakini tunzeni kauli zenu. Mboa Waislam wakubwa wakubwa wa kuanzia zamani wamehitilafiana, hata madhehebu yenu milopachika majina ya watu wote wamehitilafiana au hamjui hilo?

Tuhitilafiane kielimu, sio kijinga jinga.

Mimi sina dhehebu pia wa imani zote lakini naifata Qur'an.

Waislam hamjui watu waloitwa kwanza Wakristo huko Syria ni Wafuasi wa Yesu ambae mnasema ni Muislam, mapagani waliwashngaa misimamo yao, kuwaita Wakristo ni kama leo Muislam uitwe Muhammdan. Kuitwa mkristo a Muhammadan ni kupondwa pondwa na mapagani, kua Muhammadan au kua Mristo sio sifa nzuri kabisa.

Bora hata mabaniani wanasema wao ni Brahmim tena walewa tabaka ya juu kabisa, wanaheshimiwa sana na mabaniani wote. Brahmim maana yake ni wa Ibrahim.
Arsis.
 
Se cannot identify anyone, its against JF rules.

If JF does not identify us how can we identify others?
Simb
I don't know, If you don't know whom you've dream t about how can I know? Am not a charlatan.
Simba.
Okay...
So am I one of the so called "ukoo wa Simba" and suppose I ask..if I tell you my clan name...are you be able to tell?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom