Vionjo vya Arsis 5 - 1
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
Baada ya kurudi kisa cha Unguja mengi sna yaliendelea lakini kw aufupi nilirudi kwenye maisha yangu kawaida ya kwenda kutengeza magarei na kushughulika na kiduka changa kidogo, kwa siku hizo, cha spare za umeme wa magari.
Tulipoondoka unguja, yule binti na mamake walikuja Dar na mamangu, ilifanywa siri kubwa kuondoka kwao na wakaja kwa ndege ya kukodisha na ndugu wengine ili waweze kujifich kuondoka kwao, kuepusha kujulikana kwani Unguja minong'ono ya kisa ilikua mingi.
Kwa ufupi yule mama nilikuata nae Dar na binti yake lakini hawajakaa sana Dar wakaondoka nchi za nje, walikua hawana kabisa hamu na Tanzania, bara wa Unguja. Mambo yaliwakumba si madogo.
Katika kua nao Dar, yule mama akanihadithia kua mwanamke aliemstua, alikua ni mke wa yule DSheikh wa Unguja tulikua nae siku ya kikao na wahalifu. Akanambia yule Shehe ndio tuna w))wasiliana na kamuomba namba zangiu za simu, nikampa. Tukawa na mimi tuna mawasiliano ya hapa na pale na yule Sheikh.
Siku moja akanambia kwenye simu, Simba, nafahamu ulikua kimya sana kwenye kikao cha siku ile ya hukumu pale nyumbani lakini mimi naelewa wewe ndio ulikua kiongozi wa yote yale ingawa u kijana mdogo sana. Nafahamu kwa pete yako ulioivaa, hio pete sio ya kawaida kabisa na wenyewe waliokipa hio pete wana nguvu kubwa sana. Natamani niwaelewe. Nimeshindwa mbinu zangu zote kuwafahamu.
Mimi; Unafikiria tu hivyo.
Sheikh, mimi nafahamu babu yako na namfahamu yule Sheikh wa Tanga mlikja nae tulikutana nae kwa babu yako tanga miaka si mingi sana nyuma. babu yako ndio mwenye hio pete, naona kakuachia mikoba.
Mimi; hapana, ana yake.
Sheikh: mimi nimeongea na babu yako juzi, kuna tatizo jingine kabisa limetukabili, akanambia niongee na wewe. Toka siku zile mnaondoka mimi nawasiliana na babu yako. Nilifikiri kakujulisha kua tunafahamiana.
Mimi: Nafahamu mnafahamiana, toka nilipokua Unguja.
Sheikh; Sikiliza Simba, kuna dada mmoja niDaktari wa binadam, huyu dada ni mgazija, na yupo huko huko Dar. lakini ana matatizo makubwa sana ya mambo yao ya majini ya Kingazija sijui ya hapa Unguja, maana huyo ameshaolewa mara mbili, zote na madaktari hukohuko dar, lakini zote kaachika, mmoja kazaa nae, mmoja hajawahi kuzaa nae.
Wazee wake walinifata hapa Unguja, ni watu maarufu sana, wakamleta hapa Unguja, tukamshugulikia sna, lakini hayo majini yanatulia anafanya mambo yake vizuri sema ayataki kabisa awe na mahusina na mwnamme. Binti wa Kiislam ana kisomo chake cha juu, ana mtoto wa kike mmoja anakua tena, lakini kawa mlevi, hatoki ma-klabu ya starehe huko na hata akija hapa. Wazee na ndugu zake sio watu wa hivyo kabisa, anawaibisha sana. Simba tunamsaidia vipi huyu ndugu yetu?
Mimi; Kwa jinsi unavyonieleza, huyu mkamate koo babu. Mimi siyajui kabisa mambo haya jamani. Mimi ni kama bendera, nasukumwa na upepo tu, unakovuma ndio huko huko.
Sheikh: sasa huo upepo umevumia kwa huyo binti Daktari, wacha ukupeleke utakavyo. babu yako kasema tuongee na wewe, anakijua hiki kisa chote.
Mimi: Sheikh mimi nakushauri huyo mchukueni tu mumpeleke kwa babu, mkimfikisha pale babu hachomoi, itabidi amshughulikie tu. Lakini mimi binafsi siyajui yote hayo.
Sheikh; Nimekuelewa sana Simba, wacha tuone tunafanya nini maana huyo binti ukimuona wala huwezi kujua mambo yake, anaishi vizuri tu anapoata kazi nzuri nzauri tu, lakini atishi maisha ya kihuni mpaka lini? Aliekua mumewe ni Daktari mkubwa sana na mwenye heshima sana Tanzania. Yeye mwenyewe anafahamiu tatizo lakini anashindwa kujizuia hio hali. Anajishangaa.
Tutaongea tena Simba ikiwezekana, wacha niendelee kumrai na kumsihi babu yako atusaidie. Kumwendea ghafla itakua si vizuri, na hatujui hata kama huyo binti atakubali kwenda, babu yako kasema Dar hawezi kuja kwa sasa, tuongee na wewe.
Mimi; Ongeeni nae tu, babu mtaalamu, mimi sina nilijualo.
Tukaagana kwenye simu. Siku kama tatu kupita babu yangu akanipigia siimu. Tukasalimiana, kama kawaida yetu tukataniana kidogo, mtu na wajina wake. Akalianzisha...
Babu; Simba, vipi unakataa kusaidia watu?
Mimi; Vipi tena babu? (Ingawa nilijua anamaanisha nini).
Babu; Sheikh... wa Unguja kanipigia simu, kanambia aameongea na wewe, lakini anachokwambia unamsukumia kwangu, usifanye hivyo Simba, huyo binti yupo Dar, itakua wepesi sana wewe kumuona, tena Sheikh anasema kuna bwana mmoja wa Kipemba yupo hapo Buguruni si mbali na kwenu, anajaribu kumsaidia huyo binti kimatibabu, lakini Sheikh anasema, hata huyo binti atakata tamaa maana muda unazidi kwenda, haioni ile tija anaoitarajia.
Mimi; Buguruni ya wapi hio, babu usifikiri kila buguruni ni karibu na kwetu, buguruni kubwa.
Babu: Cha msingi sio hicho Simba, hata iwe mbali vipi, nyie mna magari huko, hamtembei kwa miguu, halafu buguruni si ndio njia ya kwenda na kurudi kazini kwako Tabata?
Mimi; Babu, ukitaka lako unajidai profesa. Niache nipambane na magari huku, wewe pambana na binadamu. Hizo kazi zako zinatisha, kasheshe la Unguja halikua dogo.
Babu; Simba, kwani wewe unafanya nini zaidi, wewe wawachie wenye kazi zao, mimi nataka wewe ujifunze ya dunia, ujionee mwenyewe ndio kuna siku utaona ni heri usaidie watu kuliko kusaidia magari.
Babu; Wewe arrange siku tu na huyo Sheikh wa Buguruni ukamjue, ni vizuri, utajionea wanavyofanya tiba zao, ni elimu hio. hakikisha tu siku unayokwenda na huyo Dada awepo anashughulikiwa, wewe uwepo kama mtazamaji tu, tuanzie hapo Simba.
Mimi; babu mbona unanipa kazi ngumu?
Babu: nenda, unaweza kukuta toto la Kingazija jisomi hilo, limenona, ukajipaytia mke wa Kunguja. Muhimu wewe nenda, yule Shjheikh hatojua umeenda kufanya nini, mimi nimemwabia huyu Sheikh wa Unguja rafiki yake, asimwambia kabisa unaenda kufanya nini, yeye amwambie, wewe unaenda kwa mabo yakohuyoi Sheikh, lakini yeye mwenyewe Sheikh atanuelea, hatomueleza chochote kuhusu kazi zetu, maana hawa waganga wengi waoo wachawi tu, hatopenda kuingiliwa himaya yake.
Mimi: babu mimi sitaki, kwanza umeshanitisha hapo, yamalizeni wenyewe.
Babu; Usiwe hivyo, usikatae mwito kataa uliloitiwa.
Mimi: Si nimeshajua ninaloitiwa babu?
Babu; Simba wacha niende, tutaongea kesho, naona leo hatuelewani lugha.
Nikacheka, babu na yeye akacheka, akanichomekea, huyo mtoto ukimuona na sifa zake nilizopewa natamani nije huko Dar, toto, toto kweli, si mchezo. Unamuogopa sana mkeo?
Mimi; Njoo wewe babu.
Babu; Natamani kuja, lakini umri ushakimbia tena.
Mimi: babu kawahi kusali, wacha na mimi nikawahi. Kwa heri
Tukaagana pale. Nikaendelea na mambo yangu.
Simba.
... 5.2
Vionjo vya Arsis 5 - 2
nilivyokutanishwa na majini ya Kingazija (Comoros) na Kipemba Kojani.
Babu yangu alikua akitaka lake liwe basi hakatishwiu tamaa na "challenges", mwenyewe alikua akiita "viunzi", alikua mara kwa mara anakumbusha, h"akuna jema lisilokua na viunzi lazima ujue kuviruka, ukiona kimekushinda kukiruka, rudi nyma kitazame vizuri unaweza kuuona upenyo ambao kwanza haukuuona, au ongeza kasi ukiruke juu zaidi, utapita tu. Hakuna kiunzi kikaishinda nia jema". kwa hio akitaka lake liwe haliachi mpaka liwe. Babu alikua na misemo mingi sana ya kumhamasisha mtu asikate tamaa na awe kwenye ubora.
Siku hya pili asubuhi kabla sijaondoka nyumbani, nilikua naishi nymba ya pili ya wazazi wangu, mlango wangu na wao wa uani ni mmoja. Mzee akanipigia simu asubuhi mapema...
Baba: Simba, leo sichukui gari langu kwenda kazini, twende pamoja, usiache. joo tunywe kahawa.
Mimi; Poa nakuja kama dakika 15.
Nikajitayarisha, kibaraza chake cha kahawa ya asubuhi ni uani kwake, in fact ni kibaraza chetu cha kahawa na kukutana kama famoily kupiga story.
Nikapita uani nikamkuta anapiuga kahawa, yupo tayri kwenda kazini. Tukasalimiana pale nikamkuta na mother na mukuu wake, mwanangu wa pili tena huyo ndio kawa partner wake toka kazaliwa, hata mamake hamuiti mama, anamwita mamangu mama na babangu ndsio babake. Yule wa kwanza kwa mamake, mke wangu, ndio chanda na pete, huyu na bibi yake.
Tukawa tunapoiga kahawa, pale, mzee kimya.
Mimi: Vipi gari yako mbovu?
Baba: hapana kuna kazi kidogo ya babu yako kama itakuepo tugtatoka pamoja, haina haja kuchukua gari nzuri.
Mimi: kazi gani tena?
Baba: Babu yako kasema alishaongea na wewe lakini unaogopa kwenda kuliona daktari la kiunguja, babu yako igtakua kakutafutia mke.
Mimi: Nikacheka, sikumjibu kitu, huku moyoni najisemea, yule babu mkorofi sana, kajua hapa kwa mzee sichomoi.
Baba; Kama upo tayari, twende kazini tusichelewe.
Mimi; Kama dakika kumi hivi nikawajulishe huko kua naondoka, maana wao wanajua nipo hapa kwenye kahawa.
Baba; Hakuna nenoi hata nusu saa tutakusubiri.
Niliporudi nikapiga kikombe kiungine cha kahawa tukaondoka, kimya kimya kwenye gari. Mzee alikua akitoka nyumbani ana dua zake na nyirfadi zake anzisoma kimya kimya, saa nyingine hata ukimsemesha hakujibu. Tunaoisha nae tumemzowea.
Tukapiga kazi kama kawaida, jioni saa 11 akanambia wajulishe yumbani kwako tutachelewa, maana huko nimeambiwa niende baada ya kusali magaharibi, ndio mchumba wa babu yako atakuwepo.
Mimi; Mchumba wa babu tena?
Baba; Babu yakjianavyomsifu huyo, si mchezo.
Mimi; Si uende wewe, mimi sina sababu kwenda.
Baba; Bau yako ansema, imi na wewe tukakae tutazame tu kinachoendelea, tujuane na huyo Sheikh wa Kipemba wa Buguruni, basi. Hatuendi kufanya wala kufanyiwa uganga. Na babu yako akisema hivyo ujue ana maana yake.
Mimi; Babako ananiingiza kwenye uganga wake, mimi staki.
Baba; Babu yako hawezi kukuingiza kitu ambacho kitakua taklifa kwako. Ukiona anakulazimisha sana huko kuna kitu cha maana. Mbona mimi hajanilazimisha kumroithi uganga wake?
Mimi; Ndio nashangaa japo, warithi si watoto au wajukuu?
Baba; Kweli ni watoto, sasa wewe hurothishwi, wewe unapewa. Kama kurithi si mpaka afe? Nani ajuae nani ataondoka kwanza? Hayo mengine muulize babu yako, mimi siyajui, mimi kanambaia twende na wewe huko ukamuone Daktari wa Kiunguja, na mimi nimepata hamu ya kumuona anasema ten ni daktari bingwa wa maradhi ya ngono. Huyoi anafaa kujuana nae.
Mimi: kajuane nae wewe? Ukimjua wewe inatosha.
Baba: kasema twende woite, babu yako ana mambo kuna mabo ambayo hawezi kuongea na mimi, lakini wewe rafiki yako mnajuana. msiniingize mambo yenu. Mjadala uishe. Baada ya magharibi tunaenda. Wacha nifanye kazi zangu. Si unaona simu inaita nimeitoa sauti tu.
Mzee akapokea simu yake akaanza kuongea mambo yake, mimi nikatoka nikaenda gereji kufanya kazi zangu huku nawaza.
...5.3
Simba.