Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ipo very clear hio aya. Mkitaka ufafanuzi wake zaidi, wacha nimalize kumpigia type Arsis na kisa chake cha Adam , kaahidi atakuja kutoa somo la majini kutokana na Qur'an na uelewa wake. Anasema ni somo zuri sana kwa watu wote bila kujali dini zao. Ni kinyume kabisa na watu wanavyofikiria.

Nakumbusha tu, msikirie Jini ni kiumbe wa ajabu, sijui mafunzo hayo Waislam wanayatoa wapi, mbona mara nyingi tunasema majini kilugha ya Kiarabu na ilivyotumika sehemu zingine za Qur'an ni sisi watu. Arsis atakuja kuchambua, mtaalamu wa somo hilo.

Mimi nimejibu swali aliloulizwa mwengine kwa kua ni jukwaa la wazi na nikaona a;ieulizwa anapiga piga chenga n ahio aya ipo wazi. Kuwaabbudu haifai kabisa.
Simba.
Asante mkuu tunaisubiri elimu kwa hamu
 
😂imebidi nicheke hujasikia jini anaitwa John kwani uliishi wapi na watu went majini ukawajua majina yao,wapo majini wa kiislamu kikirsto wahindu mpaka na infidel wasio na dini na rafiki alikuwa na jinn mzungu anaongea kizungu alisema anaitwa Moureen halafu nakuambia yote yanini wewe amini vyovyote vile.
Kuna jini wa kiafrika?
 
ASILI YA MAJINI -- 1
Katika mada hii tutaanza kuangalia asili ya hawa viumbe kwa mujibu wa Quran na hadithi.
Majini ni Viumbe walioumbwa na ALLAH, Viumbe hivyo vimeumbwa kwa mwale wa moto kama quran inavyosema katika Sura Al-Hijr (15:27)

وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ - "And the jinn we created before from smokeless fire"
Tafsiri '' Na majini tuliwaumba kabla kutokana na moto''
Aya hii inaonesha kuwa majini wameumbwa kutokana na moto na hapa nikuelezee kidogo ikiwa majini wameumbwa kutokana na moto na tunajua kuwa moto unatoa joto ambalo ni form of energy ukirudi katika sayansi utaona kuwa Energy can be transform from one form to another kama ilivyo katika law of conversation of energy ilivyo elezwa na Robert mayor mwaka 1842 hivyo basi ikiwa jini kaumbwa na moto na moto unatupa form of energy ambayo ni Thermal energy na energy hii inaweza kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine ndio maana Majini wanaweza kubadilika katika namna tofauti.
Lakini pia aya hii inatupa jibu kuwa ndio maana hatuwezi kuwaona majini katika umbo lao kwani wakiwa katika umbo lao wanakuwa kama form of energy ambao huwezi kuwagusa au kuwaona bali unaweza kuhisi uwepo wao kama vile ambavyo huwezi kuligusa joto ila unaweza kujua hapa kuna joto kupitia ngozi yako either utaungua au jasho litakutoka au mfano mwingine huwezi kugusa mwanga ambao tunasema ni light energy ila unaweza kuhisi mwanga kwa giza kuondoka au mwangaza kuongezeka.
Sasa swali linakuja ikiwa hatuwezi kuwagusa au kuwaona vipi baadhi ya watu wanasema mameona majini au wametokew na majini? Hapa jibu ni kuwa wamewaona katika umbo ambalo sio asili yao yaani jini amekuja katika form ya mwanadamu au mnyama au akajidhihisha kwa sauti tu.
Tuje katika hadithi Je hadithi za bwana mtume zinasemaje juu ya asili ya viumbe hivi. Nitarudi kuhusu hadithi za mtume
Nakuelewa vyema sana, endelea na darasa mkuu.
 
Ninaposema kiini namaanisha yeye aanze kutoa hoja mbadala mfano anasema adamu sio binadamu wa kwanza, Hoja mbadala hapa zinaweza kuwa adamu sio wa kwanza wa kwanza ni nani ? katajwa wapi? kwa ushahidi upi ? Adamu sio wa kwanza ni wa ngapi? Imetajwa wapi ? Adamu haijatumika kuonyesha binadamu bali cheo kwa ushahidi upi ? umeandikwa wapi? Hicho Ndio hicho kiini ninachosubiri kutoka kwa Arsis.
Tuje kwenye swala la Adamu katolewa wapi, Nadhani hapa kuna hoja mfu bwana simba anailazimisha ionekane ni hoja ya maana lakini kitaalamu sio hoja yenye nguvu, Hoja yenyewe ni ''wapi adamu katajwa kwenye quran kama binadamu wa kwanza?''
Hilo alishajibiwa mbona, Ngoja nirudie maelezo yangu nilimwambia hakuna aya ya moja kwa moja iliyotaja Adamu ni binadamu wa kwanza aya iyo haipo ila kuna aya ambazo zimebeba dondoo zinazoonyesha kuwa Adamu ni binadamu wa kwanza na nikamuwekea dondoo hizo, Kama vile ambavyo hakuna aya inayosema Adamu sio binadamu wa kwanza ama ipo? kama kuna ya inasema ''adamu sio binadamu wa kwanza naomba niwekewe'', Hivyo anachokifanya bwana Arsis ni kutoa aya ambazo zinatupa dondoo kuonyesha kuwa adamu sio binamu wa kwanza, Nadhani nimeeleweka.
Nimalize kwa kusema kuwa sisi waislamu tumeachiwa na Bwana Mtume Muhammad Quran na Sunnah kama Muongozo, Katika Sunnah ndio tunakuta hadithi mbalimbali ambayo ikiwa mambo yanatifautiana katika hadithi basi tutaangalia ijtimai yamaulamaaa inasemaje, Sasa katika fani ya Tarekhe wanazuoni wakubwa wamefasiri kuwa binadamu wa kwanza ni Adamu, Miongoni mwa wasomi wakubwa waliofasiri quran katika Uislamu ambao wameandika kuhusu Adamu kama binadamu wa kwanza ni Ibn Kathir, al-Tabari, na al-Qurtubi. Vivyo hivyo alishawekewa hadi hadithi humu kuonyesha Adamu ndio Baba wa wanadamu wote zaidi ya hapo ikletwa hoja hapa kwamba ikiwa atakataa hadithi hizi na maelezo ya wanazuoni ni vipi bwana simba anamswalia maiti aliyakuwa quran haijfundisha namna ya kumswalia maiti? Kwakuwa yote haya kayapinga basi ndio nasubiri yeye atakuja na hoja gani juu ya Adamu na kwakuwa mpaka sasa sijona kwenye utangulizi wake majibu ya hayo maswali basi tusubiri aendelee au wewe umeona kwenye utangulizi kuna majibu ya haya maswali niliyouliza?
Hapo umekiri kua kwenye Qur'an hakuna,, hapooi hapo unajichanganya unataja walitafsiri, sasa walitafsiri hewa? Wameyatoa wapi hayo waliotafsiri?

Kama ni aya si unaonesha aya hii, fulani kaitafsiri hi, halafu tunaichambua kuona kama ni wa kweli au walipiga porojo tu.

Unajua historia ya wanaoiita tafsiri?
Simba.
 
Sorry, Uislamu wote kwangu sio dini sahihi, ni ushirikina mtupu, mmejiunganisha sana na majini kwenye mambo yenu mpaka nashindwa kuiona nguvu ya Mungu na uwezo wake kwenye kutatua shida zenu.

Matatizo yenu mengi mnatatuliwa na majini, huku jina la Mungu mkilitaja juu juu tu ili ionekane mnamuamini, nashangaa nikimsoma huyu mleta story kuna mahali mpaka inaonekana Quran inashindwa kuondoa majini kwa wagonjwa, ila jini la mgonjwa linaondolewa na jini lingine {refer. mwanamke aliyetolewa jini na jini la mleta story Shinyanga}, sasa nyie msaada wenu mnaupata kwa Mungu au majini?!

Hii story nawaambia ukweli, imekuja kuivua nguo kabisa dini yenu, na kitabu chenu, na ndio maana nikimsoma faiza foxy kwenye hii story anaonekana kuipotezea, kama kukipuuza kile mleta mada anachoandika, ni kwasababu ameshaona dini yake anayoipigania humu kila siku, ina muunganiko wa moja kwa moja na majini, anaona aibu anajaribu kuificha, lakini haifichiki!.

Pesa za jamii ya waarabu wengi ni kwa msaada wa majini, sio Mungu, kufanikiwa kwenye mambo mengine kama safarini ni kwa ulinzi wa majini, sio Mungu, wengine wenu mnayafuga majini ndani, mimi nitashangaa sana kama siku ikifika nikamuona muislamu yeyote wa hii dunia ameurithi ufalme wa Mungu, unless muwe na hiyo pepo yenu wenyewe ya mabikra 72!, lakini sio yule Mungu wa rohoni ninae mwabudu mimi na kumtumikia, kwa jina la Yesu Kristu wa Nazareth.
Anzisha uzi wako ukihubiri neno la mungu wako unaemuamini.
 
ASILI YA MAJINI -- 1
Katika mada hii tutaanza kuangalia asili ya hawa viumbe kwa mujibu wa Quran na hadithi.
Majini ni Viumbe walioumbwa na ALLAH, Viumbe hivyo vimeumbwa kwa mwale wa moto kama quran inavyosema katika Sura Al-Hijr (15:27)

وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ - "And the jinn we created before from smokeless fire"
Tafsiri '' Na majini tuliwaumba kabla kutokana na moto''
Aya hii inaonesha kuwa majini wameumbwa kutokana na moto na hapa nikuelezee kidogo ikiwa majini wameumbwa kutokana na moto na tunajua kuwa moto unatoa joto ambalo ni form of energy ukirudi katika sayansi utaona kuwa Energy can be transform from one form to another kama ilivyo katika law of conversation of energy ilivyo elezwa na Robert mayor mwaka 1842 hivyo basi ikiwa jini kaumbwa na moto na moto unatupa form of energy ambayo ni Thermal energy na energy hii inaweza kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine ndio maana Majini wanaweza kubadilika katika namna tofauti.
Lakini pia aya hii inatupa jibu kuwa ndio maana hatuwezi kuwaona majini katika umbo lao kwani wakiwa katika umbo lao wanakuwa kama form of energy ambao huwezi kuwagusa au kuwaona bali unaweza kuhisi uwepo wao kama vile ambavyo huwezi kuligusa joto ila unaweza kujua hapa kuna joto kupitia ngozi yako either utaungua au jasho litakutoka au mfano mwingine huwezi kugusa mwanga ambao tunasema ni light energy ila unaweza kuhisi mwanga kwa giza kuondoka au mwangaza kuongezeka.
Sasa swali linakuja ikiwa hatuwezi kuwagusa au kuwaona vipi baadhi ya watu wanasema mameona majini au wametokew na majini? Hapa jibu ni kuwa wamewaona katika umbo ambalo sio asili yao yaani jini amekuja katika form ya mwanadamu au mnyama au akajidhihisha kwa sauti tu.
Tuje katika hadithi Je hadithi za bwana mtume zinasemaje juu ya asili ya viumbe hivi. Nitarudi kuhusu hadithi za mtume
Hio kopi na pesti yako inakuja kusambaratishwa na Arsis akipata wasaa, anasema hawa wanataka kunitoa katika kuwasomesha adam ni nini.

Mradi Arsis kanipa ujumbe huo, tukae mkao wa kielimu. Anasema anapenda sana hizi 'challenge" ndio zinazidisha elimu.
Simba.
 
Toka jana nausoma huu uzi na kila post kwa kina kila nipatapo wasaa.
. Hapa nitatowa maoni, ushauri na nasaha kwa wote.
. 1) nimegunduwa, kutokana na majibu ya Simba na Arsis kuwa ni vitu viwili tofauti kabisa.

2) Nimegunduwa kuwa Arsis ana level ya hali ya juu ya elimu nyingi kuliko Simba na wengi wetu. Pia anajaribu kumwachia Simba aendeshe mjadala lakini inabidi aje mara moja moja kutowa majibu au maelekezo. Yote katika kumuelimisha Simba iki atuelishe na wengine.

3) Nashauri Arsis aje kutuelimisha zaidi kuhusu Adam. Binafsi nimemuelewa sana Arsis kuhusu Adam, kwani hii mada siyo kwanza kujadiliwa hapa JF, duniani huko ni mjadala wa kielimu hasa. Arsis aanze kuelisha siyo kubishana. Amwachie Simba abishane na watu wa JF.

4) Simba ajikite kwenye vionjo vya Arsis, anavichelesha sana.

5) Wachangiaji na wapingaji wa hoja za Arsis mjipange kisomi, Arsis ni level nyingine kabisa.

Naogopa kutia yangu mpaka Arsis atakapoanza kuelezea Adam ni nani kama alivyo ahidi.
Mshangazi umeukubali mziki wa Arsis mimi ni nani nipinge?
 
Corazon Espinado.

Siyo utani. Kisa chako ni kizuri sana. Siyo kwa huo usimba ushuzi wako.

Kuna mengi yanaingia akilini. Ushauri wangu kwako, usiwe na haraka ya kupost ulichoandika. Andika post yako, tulizana, isome mara mbili tatu, rekebisha makosa ya kiuandishi kadri ya uwezo wako, kisha ndiyo post.

La pili ni ombi, naona kuna masuala ya dini yamejitokeza, natamani uniruhusu niyajibu ninavyoelewa mimi.

Mambo yako na majinni wako sikuingilii, nikiwa na swali huko ntauliza.

Ombi langu la mwisho kwako, tafadhali sana wachana na u foxy wangu na usimba wako. Tumekutana kwenye mtandao yaishie kwenye mtandao na mada zilizopo. Mjmi sikujuwi kabisa. Nikisema nakujuwa ni kwa kukutania tu. Ispokuwa, umemtaja mtu wa Shinyanga ambae nafahamiana nae toka utotoni, wamekuwa pamoja na mume wangu kwa ukaribu kabisa. Nawahamu ukoo wake wote. Ulichoelezea kijuujuu kuhusu huyo mtu wa Shinyanga ni ukweli mtupu.

Tafadhali nielewe, maana naona uzi umeshaingia watu wa jazba, wewe "remain cool" utupe kisa au visa vyako. Narudia, nimekipenda kisa chako, wachana na vile visa vyako vya usimba ushuzi.
Kweli usipomsikiliza utamuelewa vp.
 
Mshangazi umeukubali mziki wa Arsis mimi ni nani nipinge?
Sio huyo tu, kuna kibinti kinajiita "sweet candy" kinatamani kionane na Arsis leo hii. Hujakisoma humu?

Arsis ana mvuto wa ajabu. Wanaompiga wote wanakuja kua hawataki wakose japo kumsoma.
Nafahamu kwanini.
Simba.
 
Cha haraka kabisa kujua ni macho yake, jini hata afanane vipi na binadam macho yake lazima yacheze kwa haraka kulia na kushoto.

Na viashiria vingine vingi tu. Ukishawazoea, uwepo wao tu hata kama hujawaona unajua hapa yupo jini au wapo majini wangapi na wa aaina gani, kabla hata hujaaona.
Simba.




Simba: Ya binadamu hayachezi kama yao, labda albinoi kwa kiwango fulani, wengineo.

Masokoni na madukani, wapo wanaofanya biashara wapo wanunuzi, wapo wauzaji, wapo wanautumwa, wapo wachawi, wapo wema.

Ni kama binadamu, masokoni na madukani walivyo, sema majini wametuzidi idadi. Mgfano mzuri ni hapa JF, verified users ambao hao ndio sio majini, wapo wachache sana. Na wengine kinasisi yusiojulikana na kuonana na wsala hatutaki tujulikane, ndio majini wenyewe, na wewe ukiwemo, hata jina lako linaashiria hivyo.
Simba.
Hahaha Du basi hata humu yamo ukiwa mmoja wao.Bana nina swali lingine hivi mtu anaweza kuliona jini asipokuwa na madawa au ndio hivyo anaweza kuliona ila asijue kama ni jini
 
Sijakiona cha kuelewa mimi au kutokuelewa, kwani wapoi niliandika au kusema kila ninalolifanya limetoka kwenye Qur'an?

Mimi nasema sijaona alipoandikwa kua ni binadamu wa kwanza. Nyie mmelitoa wapi hilo, kama kwenye Qur'an si mlifundishe tulione? Jukwaa la wazi na huru hili.

Mimi nafahamu lipo kwenyue boiblia, lakini kwenye Qur'an sijaliona.

Somo la adam ni nini au nani linaendelezwa na Arsis.
Simba.
ukianza tu kuandika majini, hiyo koran
 
Hio kopi na pesti yako inakuja kusambaratishwa na Arsis akipata wasaa, anasema hawa wanataka kunitoa katika kuwasomesha adam ni nini.

Mradi Arsis kanipa ujumbe huo, tukae mkao wa kielimu. Anasema anapenda sana hizi 'challenge" ndio zinazidisha elimu.
Simba.
Yeye aendelee na kisa cha Adamu hamna anayetaka kumtoa mbona kila muda nasisitiza hapa aendelee kivipi nitake kumtoa?
Mimi nimeamua kuelezea kwa jinsi ninavyofahamu na rejea yangu ni quran na hadithi za mtume. Nimeamua kuelezea kwakuwa kuna member aliniuliza jee yafaa kushirikiana na majini? Ndio nimeanza kumuelezea asili ya majini, nitakuja kueleza wanakula nini, lengo lao, je wanaoana, uwezo wao, majini wabaya ni wapi na wazuri ni wapi, utajuaje huyu ni mbaya au mzuri, Je kwanini wanaingia watu, wana maumbo gani ? N.k na yote haya nitawaelezea kwa mujibu wa quran na hadithi, kama kuna kitu mtu hajaelezwa aulize mimi nitamjibu kwa mujibu wa quran na hadithi tu na kama kuna mambo biblia imeelezea nitaweka pia
 
Yap nililiona mapema sana ukimsoma btn the lines namfananisha na mwalimu anayefundisha kwa mfumo wa kuulizia maswali

Hilo mbon nimelijibu kiwepesi kabisa, nani au wapi niliwahi kusema kila ninalolifanya lipo kwenye Qur'an. Nilioyafanya mimi wewe huwezi hata ya kuyafikiria, lakini kuanza kufundishwa Qur'an kwa kina na Arsis, nashukuru nimeyaacha maovu yanayoikatazwa na Qur'an.

Mwambie @Biurhan akupe visa vyangu vya usimba, ndio utajua Mwenyezi Mungu mkubwa.

Hiyo pint unayotaka kucheza nayo kukimbia bado ipo pale pale.

Qur'an hajasema kua Adam ni mtu wa kwanza kuumbwa , umeyatoa wapi?
Hawa mmetoa wapi Waislam?

Elimu kubwa hio Waislam, msiifanyie mchezo na msitake kubishana kijinga. Wasomi wanasema "empty your cup", mamiati huo, katafuteni maana yake.
Simba.
Jibu maswali
 
Yeye aendelee na kisa cha Adamu hamna anayetaka kumtoa mbona kila muda nasisitiza hapa aendelee kivipi nitake kumtoa?
Mimi nimeamua kuelezea kwa jinsi ninavyofahamu na rejea yangu ni quran na hadithi za mtume. Nimeamua kuelezea kwakuwa kuna member aliniuliza jee yafaa kushirikiana na majini? Ndio nimeanza kumuelezea asili ya majini, nitakuja kueleza wanakula nini, lengo lao, je wanaoana, uwezo wao, majini wabaya ni wapi na wazuri ni wapi, utajuaje huyu ni mbaya au mzuri, Je kwanini wanaingia watu, wana maumbo gani ? N.k na yote haya nitawaelezea kwa mujibu wa quran na hadithi, kama kuna kitu mtu hajaelezwa aulize mimi nitamjibu kwa mujibu wa quran na hadithi tu na kama kuna mambo biblia imeelezea nitaweka pi
Sawa, endelea. Jibu maswali, wengine tuelimike.
Simba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom