Ni wajumbe gani wanaopiga kura kumchaguwa Askofu mkuu wa KKKT Tanzania kwa mujibu wa katiba yao?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,593
93,303
Igweeeeee,

Kama heading ya thread inavyojieleza naomba kufahamu kwa anayefahamu katiba ya kanisa la KKKT Tanzania ni kina nani ni wajumbe wa mkutano mkuu wa kumchaguwa Askofu mkuu?

Kwa upande wa Kanisa Katoliki nadhani iko wazi hakuna Askofu mkuu wa kanisa katoliki Tanzania, maaskofu wote ni wakuu kwenye majimbo yao na ndio wawakilishi wa Yesu Kristo kwenye majimbo yao na isitoshe maaskofu wote wa kanisa Katoliki duniani wanateuliwa na Vatican (Papas)

Kuna vitu vinaniumiza akili kusikia Askofu Malasusa ameshinda uchaguzi na kuwa Askofu mkuu wa KKKT Tanzania kwa Mara nyingine tena, hapa ndio pananipa shahuku ya kuwajuwa wapiga kura maana idadi ya kura ni kubwa kuliko idadi ya maaskofu na hapa ndio naweza kuteguliwa kitendawili kama kuna mjumbe siyo Askofu halafu anapiga kura ya kuchaguwa Askofu mkuu.

Karibuni katika mjadala maana hili linaweza kuharibu imani za kiroho.
 
Hilo kanisa la kkkt litaendelea kupasuka pasuka sana.

Kwa mwaka huu tu huko Mbeya kulikuwa na timbwili walipelekana hadi mahakamani na kanisa lilifungwa na polisi, walioshindwa kesi wamejimega wana kanisa lao tofauti.

Kkkt ni mali ya watu hio
 
Kwa Moravian wajumbe kama wenyeviti na makamu wa majimbo huusika na uchaguzi, kkkt hawapishani sana na wamoravian nipo tayari kusahihishwa
 
Kwa Moravian wajumbe kama wenyeviti na makamu wa majimbo huusika na uchaguzi, kkkt hawapishani sana na wamoravian nipo tayari kusahihishwa
Hawana Uaskofu wa mnyororo? Wamezidiwa akili na Waislamu Mufti akishachaguliwa ni mpaka kifo au ajiuzuru kwa hiyari kwa sababu za kueleweka?
 
ndo mwanzo wa kuuana ili mtu akaimu madaraka ya umufti
Mufti mwenyewe yuko vizuri ni Mganga wa kienyeji, na kwa imani ya kiislamu mtu wa shirki hapaswi kushinda wadhifa huo.

N:b, comment yangu siyo shambulio la kidini Bali ndio ukweli wenyewe, na kwa wanaomjuwa Mufti vizuri kabla hajawa Mufti wanalielewa hili vizuri, na hata waislamu safi wanajuwa vizuri dini inakataza shirki.
 
Unajamba Maputo tu, mbwiiiiii.
Tukana utakavyoweza,ila Askofu Dr.Malasusa ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani na Mkuu Mteule wa KKKT kwa sasa, akisimikwa kazini anakuwa Mkuu wa KKKT na siyo Askofu Mkuu.Kwa imani ya KKKT Askofu Mkuu ni Yesu Kristo.
 
Back
Top Bottom