Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

YEAH SASA TOKEA HAPO HATA JAMBO LOLOTE KWA MTU YEYOTE NAKUBALI MITAZAMO HAIFANANI japo ukisema fact hata mtu apinge baadae litakuja kuonekana ilikuwa ni fact tu ......dogo nlikua nikimwambia fanya kazi 6 month nikupeleke shule upate fani...ujuaji leo after 8 month anarejea pale pale kwenye kwenda shule.....funzo kubali kutokukubaliana mpe mtu room agundue mbivu na mbiche mwenyewe in a hard way
Kutoa ushauri ni jambo moja
Mtu kuufanyia kazi ushauri wako ni jambo lingine tena la hiari

Wewe ulifanya kwa uwezo wako kazi alihitimisha yeye kwa kukataa kitu ambacho sio kosa lako
 
Ilikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?

Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii

Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini

Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja

Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine

Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa

Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii

Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine

Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe

Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅

Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti

Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti

Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi

Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe

Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?

ShesRise_1 🖐
After marriage
 
Wewe mpka saivi hujaelewa mada kuna tofauti ya mtifuano na kuweka hoja mezani na kuzijadili

Bila mmoja kuvuka mipaka na kuanza kumtoa akili mwingine
Huko kwenye kuzijadili lazima watu waumie. Misimamo ya watu ni utambulisho wao.

Utaelewa tu siku moja.
 
Ni jambo zuri ila urahisi wake ni hapa mtandaoni ila uso kwa uso inakuhitaji uwe na emotionali intelligence kuweza kuhimili mtu anayekupinga kitu ambacho unahisi uko sawa .
Urahisi ni hapa mtandaoni na physically ni rahisi pia

Usilazimishe watu wasiokuelewa wakuelewe
hiyo kutaka watu wahisi uko sawa kilazima ndio kosa linaponzia
Chukua wale wanokuelewa nenda nao hao wengine ambao mitazamo haifungamani na yako achana nao
 
Urahisi ni hapa mtandaoni na physically ni rahisi pia

Usilazimishe watu wasiokuelewa wakuelewe
hiyo kutaka watu wahisi uko sawa kilazima ndio kosa linaponzia
Chukua wale wanokuelewa nenda nao hao wengine ambao mitazamo haifungamani na yako achana nao
Mkuu wangu ShesRise_1 sikatai ila inataka moyo sana mshikaji wangu japo mimi naweza sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom