Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
17,741
Reaction score
42,173
Ilikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?

Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii

Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini

Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja

Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine

Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa

Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii

Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine

Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe

Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅

Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti

Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti

Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi

Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe

Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?

ShesRise_1 🖐
 
Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe.
GIF by The Bachelor.gif

Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?

ShesRise_1 🖐
Nilijifunza toka udogoni ila iliniingia kikweli kweli in my 20's baada ya maisha na kazi kunifanya nichangamane na watu wa aina mbalimbali. Sasa hivi sibugudhiwi kabisa na mawazo na mitazamo ya watu, hata kama sikubaliani nayo.
 
Kuna binti nilimpenda kisawasawa wakati huo nilikua sina mbele wala nyuma napiga kibarua kiwanda fulani ...tulielewana sana baadae napata fursa maisha yanabadilika ...nikamtafutia kazi sehemu kafanya siku mbili kaacha ......then analazimisha mipango ya mahusiano na ndoa ilihali mipango yangu kwake anaivuruga...mahusiano yalifika tamati nikakubali hata kama miminaliona njia nuri ya kumsaidia kwake haikuwa nzuri tuliachana
 
View attachment 3593224

Nilijifunza toka udogoni ila iliniingia kikweli kweli in my 20's baada ya maisha na kazi kunifanya nichangamane na watu wa aina mbalimbali. Sasa hivi sibugudhiwi kabisa na mawazo na mitazamo ya watu, hata kama sikubaliani nayo.
Hongera dear 😍

Mimi udogoni nilikua na hako ka ubinafsi kuamini mawazo yangu pekee hata nikikosolewa nilikua naona napingwa na sipendwi lakini taratibu nikaanza kubadili mtazamo na kuelewa kua ninavyotaka haiwezekani
 
Mimi Abigail Bado
Itanichukiaua muda sana kuamini wanasisiemu ni watu wenye akili timamu na kuheshimu mitazamo Yao.

Kama wasivyoheshimu yangu,na mie siheshimu Yao.
Hii ni tofauti dear mitazamo ya CCM ni ya kuliangamiza taifa watu wote wastarabu hawakubaliana nao na wanapinga kwa nguvu zote sela za CCM kwa sababu zinaumiza

Ila hapa tunaongelea ile mitazamo ambayo hata mtu akiwa nayo haidhuru
 
Ilikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?

Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii

Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini

Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja

Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine

Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa

Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii

Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine

Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe

Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅

Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti

Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti

Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi

Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe

Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?

ShesRise_1 🖐
Hivi unajua utanifanya nikupende,haya ndio mambo yangu
 
Kuna binti nilimpenda kisawasawa wakati huo nilikua sina mbele wala nyuma napiga kibarua kiwanda fulani ...tulielewana sana baadae napata fursa maisha yanabadilika ...nikamtafutia kazi sehemu kafanya siku mbili kaacha ......then analazimisha mipango ya mahusiano na ndoa ilihali mipango yangu kwake anaivuruga...mahusiano yalifika tamati nikakubali hata kama miminaliona njia nuri ya kumsaidia kwake haikuwa nzuri tuliachana
Mlipishana mitazamo na vipaumbele aliwaza ndoa zaidi na wewe uliwaza ustawi before ndoa

Ni bora zaidi mliachana kuishi na mtu msielewana ni kazi
 
Binadamu duniani wamegawanyika makundi makubwa mawili, Conservatives na Liberals.

Liberals kwa kiasi kikubwa wanatambua na kuheshimu uhuru wa watu wengine katika mitazamo na machaguo yao binafsi, Conservatives wao wanaamini binadamu wote wanatakiwa kuwa na mawazo ya aina moja na hawana uvumilivu kabisa na mawazo tofauti.
 
Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅

Hapa ulijikuta wewe ni nabii au mtume hahah
 
Binadamu duniani wamegawanyika makundi makubwa mawili, Conservatives na Liberals.

Liberals kwa kiasi kikubwa wanatambua na kuheshimu uhuru wa watu wengine katika mitazamo na machaguo yao binafsi, Conservatives wao wanaamini binadamu wote wanatakiwa kuwa na mawazo ya aina moja na wako hawana uvumilivu kabisa na mawazo tofauti.
Asante kwa ufafanuzi kaka
Wewe upo kundi gani hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom