Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

Unaamini katika Mungu?
ili nijue nakujibu kwa muktadha upi
Usinijibu katika muktadha wa mungu kwa sababu hata mapenzi kabla ya ndoa ni kinyume na maandiko ya Ukristo na Uislamu ila boyfriend au girlfriend wanaofanya ngono ni mtindo wa kawaida wa maisha katika jamii nyakati hizi.

Huwa kuna maandamano ya kupinga ushoga.
Llini uliwahi kusikia kuna maandamano ya kupinga uasherati au zinaa? Lini uliwahi kusikia mwanasiasa wa Tanzania anatokea povu akizungumza dhidi ya uasherati, uzinzi au cheating?
 
Nimetafuta jibu litakalokutosha wee nimekosa aisee ila
Binafsi sivutiwi na mapenzi ya jinsia moja kwa sababu naona yako kinyume na natural kwangu

Si kitu kinachonivutia kuona au kuhisi et mwanaume anapelekewa moto😢

Naona hayalingani na namna natural ilivyo kwangu ndiyo maana hayanivutii binafsi
Usinijibu katika muktadha wa mungu kwa sababu hata mapenzi kabla ya ndoa ni kinyume na maandiko ya Ukristo na Uislamu ila boyfriend au girlfriend wanaofanya ngono ni mtindo wa kawaida wa maisha katika jamii nyakati hizi.
 
Ni kwe
Ilikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?

Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii

Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini

Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja

Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine

Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa

Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii

Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine

Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe

Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅

Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti

Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti

Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi

Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe

Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?

ShesRise_1 🖐
Ni kweli kuna mtu anaunga mkono ccm,huo ni mtazamo wake hakuna haja ya kumtukana na kumwita chawa,kuna mtu anaunga mkono chadema pia huo ni mtazamo wake hakuna haja ya kumchukia.Hivyo ndivyo dunia ilivyo
 
Binadamu duniani wamegawanyika makundi makubwa mawili, Conservatives na Liberals.

Liberals kwa kiasi kikubwa wanatambua na kuheshimu uhuru wa watu wengine katika mitazamo na machaguo yao binafsi, Conservatives wao wanaamini binadamu wote wanatakiwa kuwa na mawazo ya aina moja na hawana uvumilivu kabisa na mawazo tofauti.
Concervative hao ni kisanga
 
Nimetafuta jibu litakalokutosha wee nimekosa aisee ila
Binafsi sivutiwi na mapenzi ya jinsia moja kwa sababu naona yako kinyume na natural kwangu

Si kitu kinachonivutia kuona au kuhisi et mwanaume anapelekewa moto😢

Naona hayalingani na namna natural ilivyo kwangu ndiyo maana hayanivutii binafsi
Sina shida na wewe kuvutiwa au kutovutiwa na ushoga, hata mimi sivutiwi nao lakini sijali kwa sababu ni maisha yao waliyochagua. Mfano mimi pia sivutiwi na vazi la niqab au burqa lakini sijali, siwezi kutokwa na povu au kuandamana dhidi yake. Ishu ni kwa nini uanze kuhangaika na jambo ambalo alikuhusu au kukuathiri hadi utunge sheria za jinai, watu wafanye maandamano na iwe ajenda kubwa kila mahali?!
 
Ni kwe

Ni kweli kuna mtu anaunga mkono ccm,huo ni mtazamo wake hakuna haja ya kumtukana na kumwita chawa,kuna mtu anaunga mkono chadema pia huo ni mtazamo wake hakuna haja ya kumchukia.Hivyo ndivyo dunia ilivyo
Kwenye siasa za vyama vingi lugha zinazoonekana ni za kejeli, dhihaka na matusi ni vitu ambavyo haviwezi kukwepeka(kwa sababu pia ni subjective sana) na hivyo pia havipaswi kuwa jinai ila utekaji na mauaji ni vitu vinavyoweza kuepukika.
 
Mawazo yangu🤔🙇🏿‍♂🙆🏿‍♂
56d1fc7b-def3-4137-814e-7e0696b4bcc6.jpeg
2f341d8b-c3bc-44db-a77a-ba1d1dc20b26.jpeg
6d1b76ce-16b6-4f88-8f48-8d23867037b9.jpeg
5abc06f6-6dc5-4f81-b6c8-188e77c5819c.jpeg
 
Sina shida na wewe kuvutiwa au kutovutiwa na ushoga, hata mimi sivutii nao lakini sijali kwa sababu ni maisha yao waliyochagua, sivutiwii na vazi la niqab au burqa lakini sijali, siwezi kutokwa na povu au kuandamana dhidi yake. Ishu ni kwa nini uanze kuhangaika na jambo ambalo alikuhusu au kukuathiri utunge Sheria za criminal, watu wafanye maandamano na iwe ajenda kubwa kila mahali?!
Hapa nakosa cha kujibu mkuu
Ni hatari mambo mengine tuache tu kama yalivyo
 
Back
Top Bottom