Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

Je, kuna watu wanaoweza kusoma mawazo ya wengine? 🧠

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
19,317
Reaction score
45,590
KARIBU KWENYE MADA WANA GREAT THINKERS 🧠 ☕️

Unaweza vipi kusoma mawazo ya mtu mwingine au kujua kinachoendelea kwenye akili yake?

Unaamini kama kuna watu wanaoweza kusoma akili au mawazo ya watu wengine?

Unadhani ni nini huwa kinatokea pale mtu anapoona maandishi ya mtu au akiwa kwenye mazungumzo na mtu mwingine, halafu akagundua kwamba huyu mtu anawaza kitu fulani?

Na ajabu, unakuta baadae yule mtu anafanya kitendo au vitendo vinavyothibitisha kwamba yale aliyogundua mwanzo yalikuwa sahihi


Kisayansi hali hii inaelewekaje?

Hawa watu tunaweza kuwaita watambuzi.watu wenye intuition kubwa wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua watu, au ni geniuses?

Na wewe binafsi unaamini unaweza kusoma akili ya mtu?

Kama ndiyo unafanya hivyo kwa namna gani?

Maoni yangu 👇

Kikawaida kabisa, naamini kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kutambua mambo hata bila mtu kuyaeleza moja kwa moja

Sio kwamba wanatumia akili ya ajabu au wanaingia kwenye akili ya mtu mwingine bali kuna wakati mtu akiwa makini sana anaweza kuona signals ndogo ndogo ambazo watu wengine hawazioni

Hata kama mtu anajaribu kufake au kuficha mawazo yake kwa kuongea au kuandika kitu tofauti na anachohisi, ukiwa makini sana unaweza kugundua kuna kitu hakipo sawa

Ni sawa na mtu ambaye anaweza kukuonyesha kwamba amefurahi sana kwa sababu umepata kazi

Anaweza kucheka kukusifia na kukuambia:

Hongera sana ShesRise_1 nimefurahi kwa ajili yako umepata kazi

Lakini wakati huo huo kuna signals nyingine unaweza kuziona

Labda kwenye facial expression yake namna anavyocheka tone la sauti macho, movements za mikono, posture yake au hata namna anavyoendelea na mazungumzo
Unaona kabisa yeye wa ndani
Na yeye wa njee ni kama mifumo haisomani

Na kama wewe ni mtu ambaye una observation nzuri na ubongo wako unafanya kazi shap utagundua haraka sana

Huyu mtu kwa ndani hafurahii kama anavyosema

So patterns ukiziona unagundua huyu anawaza kwa namna nyingine kabisa tofauti na anachokionesha

Na kinachofanya jambo hili liwe interesting zaidi ni pale unapokuja kugundua kwamba baadae yule mtu anafanya kitu kinachothibitisha kile ulichohisi mwanzo

Swali la mjadala?👇

Hua najiuliza nimeisoma akili yake, au nilikuwa nimeisoma signals zake vizuri na kwa haraka?

Na kama kweli kuna watu wenye uwezo huu mkubwa wa kutambua kile ambacho wengine wanajaribu kuficha...

Uwezo huu unatokana na nini?

Ni intuition?
Ni experience?

Au kuna kitu kingine ambacho bado Labda wengi wetu hatujakifahamu kwa undani
Na kama kipo je ni kitu gani?

Nataka kusikia mawazo yenu🧠

Cc: Marcostilone

ShesRise_1 ✋️
 
Hata Mimi uwezo wa kumsoma mtu ninao japo sio kwa kiasi kikubwa sana. Na huu uwezo umetokana na kukutana na watu mbalimbali, mazingira mbalimbali na hua ni msikililizaji sana na mtulivu pale ambapo mtu huongea au anapofanya vitendo.

Huwa sibandui macho yangu usoni kwake pale anapofanya kitendo chochote au pale anapozungumza.
 
Hata Mimi uwezo wa kumsoma mtu ninao japo sio kwa kiasi kikubwa sana. Na huu uwezo umetokana na kukutana na watu mbalimbali, mazingira mbalimbali na hua ni msikililizaji sana na mtulivu pale ambapo mtu huongea au anapofanya vitendo.

Huwa sibandui macho yangu usoni kwake pale anapofanya kitendo chochote au pale anapozungumza.
Hubandui jicho sio
Unamkazia mtu sasa si utaogopwa jamani
 
Rafiki kakunja uso anatupa mikono na kusonya juu 😅😅

Yalikupata kaka?
Sema huyu Rafiki alishindwa kuficha kabisa yeye alinuna live 😢
😂😂😂
Nakumbuka kuna tukio lilitokea, yaani nilikuwa na mshikaji wangu mahali fulani nikamwambia '' Oyaa Mwanangu " kuna gari itanifuata hapa nilipo. Jamaa akasema hakuna kitu kama hicho. Baada ya muda within 20 minutes ikaja gari fulani yaani jamaa alinionyesha kisirani waziwazi

Halafu watu wakisema uchawi upo hamuamini 😀😀😀
 
😂😂😂
Nakumbuka kuna tukio lilitokea, yaani nilikuwa na mshikaji wangu mahali fulani nikamwambia '' Oyaa Mwanangu " kuna gari itanifuata hapa nilipo. Jamaa akasema hakuna kitu kama hicho. Baada ya muda within 20 minutes ikaja gari fulani yaani jamaa alinionyesha kisirani waziwazi

Halafu watu wakisema uchawi upo hamuamini 😀😀😀
So uligundua ana wivu kupitia ishara?
Mi nataka kujua je mtu anaweza kusoma mawazo ya mwingine

Au ni ishara ndio zinatafsiri kile mtu anachokiwaza ?
 
Hiyo ni taaluma kama zilivyo taaluma nyinginezo, kuna wanaosomea hapo utakutana na CID ama wale ndugu zetu wa Intelligency na kuna ambao wamezaliwa nayo hiyo taaluma hapo utakutana na manabii uchwara...ndio maana nchi zilizo endelea huwa wanajinasibu sana kwenye tarehe ya mtu ya kuzaliwa kupitia hiyo humpatia mtu kazi na kumchagulia pa kwenda tokea akiwa mdogo...ni kamada karefu kidogo ila yeyote anaweza kuiamsha power with-in akipenda...ebu jaribu kupitia mada za Pascal Mayalla zitakupa ufunuo kidogo​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom