Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

Ni muhimu Kuheshimu mawazo ya wengine bila chuki!

Ila umeandika bandiko zuri sana,migongano mingi na mifarakano katika jamii zetu inasababishwa na kutokubaliana na baadhi ya mambo mbali mbali,wakati mwingine sio ishu kubwa ila ni ego zetu huwa zinatusumbua.

Kwamba huyu ataniambia nini? Au nikikubali wazo lake nitaonekana mimi ni mzaifu au sina msimamo,kumbe wakati mwingine ni swala kuikandamiza ego yako na utayaona mambo katika uhalisia wake
 
Hii ni tofauti dear mitazamo ya CCM ni ya kuliangamiza taifa watu wote wastarabu hawakubaliana nao na wanapinga kwa nguvu zote sela za CCM kwa sababu zinaumiza

Ila hapa tunaongelea ile mitazamo ambayo hata mtu akiwa nayo haidhuru
Ni kweli
Lakini mi naona kwangu ni sahihi

Ni kama mtu anaeamini Mungu anaponya,Kisha mwingine anadiss hakuna.
Vilevile mtu ataesimama upande usio wa haki alisema ndio Kuna haki.na mie ntasimama upande mwingine nkiamini huko ndio Kunatenda haki.
Katika hili nitakuwa kinyume nao siku zote mpaka wataposimamia haki

So anaeamini kijani wako sahihi nitapingana na mtazamo wake.
 
Ilikuwaje mpaka ukakubali kwamba watu tuna mitazamo tofauti, na kwamba hata iweje hatuwezi kufanana mawazo?

Hapa naongelea kujifunza kuheshimu mitazamo ya watu wengine, hasa ile yenye upande chanya na isiyoleta madhara kwa jamii

Kwa mfano, kuna mtu anaamini Mungu yupo, na mwingine anaamini hayupo
Huo ni mtazamo wake binafsi
Kuamini kwake hakupunguzii kitu wewe unayeamini, wala hakumuongezei kitu asiyeamini

Vivyo hivyo kwa mtu anayesema yeye ni team kataa ndoa
Huo pia ni mtazamo wake binafsi
Aoe au asiolewe, hilo haliathiri maisha yako moja kwa moja

Hii naweza kuiita mitazamo chanya, kwa sababu haina madhara kwa watu wengine

Lakini pia kuna mitazamo hasi ambayo watu wengi waliostaarabika wanaweza kuipinga kwa sababu inaweza kuharibu jamii Kuna baadhi ya mawazo ambayo, hata kama watu wamekubaliana wenyewe, bado yanaweza kuleta madhara kwa jamii ikiwa hayatakemewa

Mitazamo ya aina hiyo ndiyo mara nyingi huzua mjadala mkubwa kwa sababu athari zake zinaonekana zaidi kwenye maadili na malezi ya jamii

Leo nazungumzia zaidi ile mitazamo ambayo, hata mtu akiwa nayo, haimdhuru mwingine

Kwa hiyo hakuna haja ya kuchukiana au kulalamika sana kwa sababu tu mtu ameamua kuamini au kuishi tofauti na wewe

Mimi zamani, sijui ilikuwa ni utoto au uelewa mdogo nilikuwa naamini kwamba kila ninachoamini mimi basi na wengine wanapaswa kuamini hivyo hivyo😅

Kama sipendi kitu fulani nilitaka hata mtu niliye karibu naye asikipende
Lakini baadaye niligundua kwamba hilo haliwezekani
Kwenye maisha tunakutana na watu waliokulia mazingira tofauti, tamaduni tofauti, na malezi tofauti

Kwa hiyo ni kawaida kabisa watu kuwa na mitazamo tofauti

Baada ya muda nikajifunza kwamba sina uwezo wa kubadilisha kila mtu ili awe kama mimi
Badala yake, ni bora kutafuta watu ambao tunaendana kitabia na kimawazo kuliko kutumia nguvu nyingi kuwalazimisha watu wabadilike wawe kama mimi

Maana mwisho wake unaweza kujikuta unaishi kwa hasira, chuki, na maumivu kwa sababu watu hawajawa vile ulivyotaka wawe

Je, wewe ilikuchukua muda gani kujifunza kuheshimu mawazo na mitazamo ya watu wengine, bila kuwaona hawana akili, bali kwa kutambua tu kwamba binadamu hatufanani?

ShesRise_1 🖐
Tukiwa watoto huwa tunaamini kila kitu unachotaka ni sahii.... Ila umri unavyoenda ndio unapata experience.

Binafsi sikumbuki ni lini ila kwa sasa kadri ya umri naelewa zaidi kuwa kutofautiana ni kawaida. Kuna mambo hata mwaka mmoja uliopita nilikua naona si sahii ila leo naona ni sahii...

So kuweka sawa. Hakuna nyakati sahii za kusema nilianza kuelewa kutofautiana, binadamu tunajifunza kila mara na kuna jambo jipya kila mara linatokea.....
Experience ina matter zaidi...
 
Mjukuu wangu.
Ustaarabu ni kuheshimu mawazo ya watu wengine hata kama huyakubali mawazo hayo.

Ustarabu mwingine ni kushughulika na hoja ya mtu bila kumshambulia yeye binafsi.

Kila mtu anatazama mambo kwa "angle" yake;
 
Fact​

Lau wote tungekuwa kama unavyosema basi hata mijadala huku jf ingekuwa na faida sana,lakini upuuzi umetujaa
 
Hapana bhna mtu akisema hataki ndoa wewe unapata madhara gani?
Labda nitaona ni shoga aliyekosa maadili, au ni gumba/tasa asiyeweza kuzalisha, au ni mtu mzembe mwenye uoga wa maisha.

Haiwezekani tukakubaliana kila kitu. Hatuna uzoefu sawa wa kimaisha.

Na mimi binafsi naamini, ili mijadala inoge lazima kuwe na mtifuano.
 
Ila umeandika bandiko zuri sana,migongano mingi na mifarakano katika jamii zetu inasababishwa na kutokubaliana na baadhi ya mambo mbali mbali,wakati mwingine sio ishu kubwa ila ni ego zetu huwa zinatusumbua.

Kwamba huyu ataniambia nini? Au nikikubali wazo lake nitaonekana mimi ni mzaifu au sina msimamo,kumbe wakati mwingine ni swala kuikandamiza ego yako na utayaona mambo katika uhalisia wake
Umeongea vizuri kijana🔥
 
Mlipishana mitazamo na vipaumbele aliwaza ndoa zaidi na wewe uliwaza ustawi before ndoa

Ni bora zaidi mliachana kuishi na mtu msielewana ni kazi
YEAH SASA TOKEA HAPO HATA JAMBO LOLOTE KWA MTU YEYOTE NAKUBALI MITAZAMO HAIFANANI japo ukisema fact hata mtu apinge baadae litakuja kuonekana ilikuwa ni fact tu ......dogo nlikua nikimwambia fanya kazi 6 month nikupeleke shule upate fani...ujuaji leo after 8 month anarejea pale pale kwenye kwenda shule.....funzo kubali kutokukubaliana mpe mtu room agundue mbivu na mbiche mwenyewe in a hard way
 
Sio rahisi hivyo kabisa. Unachokiona hakina madhara kuna wengi wanaona kinacho.

Lazima tugombane, ni sehemu ya maisha.
Ukitumia sayansi na logic kuna mambo mengi yanaonekana yana madhara ila kiuhalisia hayana madhara. Conservatives wengi hawatumii Sayansi au logic kujenga msingi wa hoja zao bali wanatumia hisia/ biases/ personal experiences zaidi, wengi pia ni wajinga.

Dini pia zina mchango mkubwa sana wa kuwafunga watu kuwafanya kutokuwa objective katika mitazamo yao.
 
Ni kweli
Lakini mi naona kwangu ni sahihi

Ni kama mtu anaeamini Mungu anaponya,Kisha mwingine anadiss hakuna.
Vilevile mtu ataesimama upande usio wa haki alisema ndio Kuna haki.na mie ntasimama upande mwingine nkiamini huko ndio Kunatenda haki.
Katika hili nitakuwa kinyume nao siku zote mpaka wataposimamia haki

So anaeamini kijani wako sahihi nitapingana na mtazamo wake.
Sawa mamaa
 
Hembu nipimie Niko spectrum gani kwa kuzingatia haya;
Sipendi dini kutumika ku control watu au jamii, sijali wanawake wanavyovyaa, sijali mtu akiwa au asipokuwa shoga, sipendi mtu akijenga hoja kwa mambo ya nchi nzima kwa kusema hizi ni "mila na tamaduni zetu"
Wewe ni Liberals
Ila hapo kwenye ushoga🤔
 
Tukiwa watoto huwa tunaamini kila kitu unachotaka ni sahii.... Ila umri unavyoenda ndio unapata experience.

Binafsi sikumbuki ni lini ila kwa sasa kadri ya umri naelewa zaidi kuwa kutofautiana ni kawaida. Kuna mambo hata mwaka mmoja uliopita nilikua naona si sahii ila leo naona ni sahii...

So kuweka sawa. Hakuna nyakati sahii za kusema nilianza kuelewa kutofautiana, binadamu tunajifunza kila mara na kuna jambo jipya kila mara linatokea.....
Experience ina matter zaidi...
Upo sahihi kadri mda unavyoenda ukomavu unaongezeka
 
Labda nitaona ni shoga aliyekosa maadili, au ni gumba/tasa asiyeweza kuzalisha, au ni mtu mzembe mwenye uoga wa maisha.

Haiwezekani tukakubaliana kila kitu. Hatuna uzoefu sawa wa kimaisha.

Na mimi binafsi naamini, ili mijadala inoge lazima kuwe na mtifuano.
Wewe mpka saivi hujaelewa mada kuna tofauti ya mtifuano na kuweka hoja mezani na kuzijadili

Bila mmoja kuvuka mipaka na kuanza kumtoa akili mwingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom