Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,118
Tanzania hakuna uraia wa nchi mbili lakini naona kama wageni wanaomiliki Pasipoti za Tanzania na za mataifa mengine wamekuwa wengi Sana.

Sikukuu za mwisho wa mwaka nilikuwa South kwa mwaliko wa familia Kula bata kidogo, katika moja ya hafla mwenyeji wangu alinikutanisha na rafiki zake ambao walijitambulisha kuwa wanatoka mataifa mbalimbali; it was kind of family bush dancing fun end of 2022.

Moja ya Jambo ambalo nimelishuhudia ni wenzetu wa nchi jirani na mataifa ya Yemen, Falme za Kiarabu, Oman kutumia Pasipoti za Tanzania wao na watoto wao. At the same time Kwa Sababu zisizofahamika wao pia Wana Pasipoti za mataifa mengine.

Kwa udadisi wangu mdogo huu utaratibu wa kutoa Pasipoti ubalozini unavutia wageni kufanya majaribio na wengi wanafanikiwa. Jambo la pili hawa wenye Pasipoti wanatumia Watanzania wasio wazazi au ndugu zao kuomba Pasipoti na wanapata.

Mfano kuna dada mmoja nilikutana naye mpenzi wake ni Mganda ila anapasipoti ya Tanzania! Nilivyotongoza kujua mbinu zilizotumika, inaonekana Yule mwanamke Mtanzania alitumika kumwombea huyo mume wake Pasipoti Kwa nyaraka zakikanjanja.

Kama salamu za mwaka mpya na baada ya akaunti yangu kupotea napenda kutuma salamu Kwa Uhamiaji kwamba watu wamechungulia fursa.

Pamoja na huduma nzuri na za haraka mnazotoa please msiruhusu wageni kuwa Watanzania; tutapata shida kama ilivyo south Afrika Kwa sasa kwamba wageni wamewaelemea na wengi wamepata uraia kimakosa Kwa uzembe wa serikali.

Wekeni masharti magumu kwenye Pasipoti na ikiwezekana sheria imfunge miaka yakutosha mgeni anayechokoza tunu hii ya Taifa. Pasipoti ndiyo Utanzania wetu nje.

Kesho kutwa magaidi yanaweza kupenyeza na labda wameshapenya na kupata Pasipoti wao na watoto wao Bila Sisi kujua. Pasipoti Kwao ni maandalizi ya kuja kutulipua huko baadaye.

SASA hivi biashara ya madawa NI kubwa, tunaweza kuchafuliwa na wageni watakapokamatwa na Pasipoti zetu ikadhaniwa n Watanzania.

Lakini pia naambiwa hapo bongo kitambulisho cha NIDA unapata fasta sana japo nashangaa Mimi sina kitambulisho! Nina namba lakini wajuba huku wao wanakitambulisho kabisa.

Serikali ya mama Samia Suluhu Hasani nikuombe mama fanya ufanyavyo Ila Sheria Kali Kwa mgeni kujipatia Pasipoti, kitambulisho cha UTANZANIA ni muhimu Sana.

Huna Sababu yakutumbua watendaji Iia waelekeze wazilinde hizi tunu mbili "Pasipoti na NIDA cards,"sidhani kama hawa ninaowazungumzia wanakosa pesa kiasi chochote hivyo wafungwe wanaohonga kupata na wanaohongaw.

Tumsaidie Rais kulinda Royal Tour isiwe royal kwapua utanzania.

Tanzania Kwanza.
 
Wekeni masharti magumu kwenye Pasipoti
Sasa passport zipo tu wabongo hawapewi elimu ya passport hawapewi elimu juu ya umuhimu wa passport, hawapewi elimu juu ya faida za kua na passport, hawapewi Uhuru wa kupatiwa passport km haki yao ya kikatiba, inategemea nini km sio wajanja kutumia fursa hio sababu wenye nacho wamelala hawaelimishwi hawaelezwi chochote kuhusu umuhimu wa kua na passport, hawaambiwi kwamba ukiwa na passport unaweza kuomba mkopo bank na ukapewa unategemea nini nani ana tatizo uhamiaji au watu wenye nchi yao?

Mboni TRA wanajotahidi kutoa elimu ya kutoa na kulipa Kodi hawa uhamiaji hawana kitengo cha elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa passport?

Na passport zilitakiwa zitolewe bure km tinavyopewa vitambulisho vya kupiga kura au vitambulisho vya taifa Ila basi tu usimamizi mbovu ndio maana passport tunailipia almost 200k
 
Mkuu wa UHAMIAJI plz come forward and explain to JF

Mkuu wa NIDA come forward and explain.

Kwann PASSPORT/NIDA zinatoka kama NJUGU Kwa WAGENI?

Ila nilichogunduwa Mimi ni kwamba Kuna rushwa kubwa sana uhamiaji/NIDA.

Kuna watu Wana network na wahusika wa hizi Departments.

Wakitengewa pesa fulani wanatoa NIDA, passport...
 
Mkuu wa UHAMIAJI plz come forward and explain to JF Mkuu wa NIDA come forward and explain.

Kwann** passport/NIDA**zinatoka kama NJUGU Kwa WAGENI?

Ila nilichogunduwa Mimi ni kwamba Kuna rushwa kubwa sana UHAMIAJI/NIDA.

Kuna watu Wana network na wahusika wa hizi Departments.

Wakitengewa pesa fulani wanatoa NIDA,, passport...
 
Back
Top Bottom