Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2022
1,689
3,265
Njia ya hakika ya kuwa na dola za kutosha ni kuwa na trade surplus. Yaani uuze kuliko unavyonunua. Lakini hili halipo karibu kwa nchi zote za Afrika. Sasa mbinu iliyobaki ni kukabiliana/kumanage uhaba wa dola. Nchi hufanyaje hivyo?
 
Ongozeni mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi; punguzeni imports kwa bidhaa au huduma ambazo nchi inaweza kuzalisha.

Wizara ya fedha, viwanda na biashara, kilimo, mifugo na uwekezaji wanatakiwa waje na real working model ili haya yawezekane.

Mfano, kila mwaka mnajua matumizi ya sukari ni zaidi ya tani laki 6, uwezo wa ndani kuzalisha ni tani laki 3; nchi inshindwaje kuja na parament solution?
Kila mwaka nchi inaagiza agro-inputs (ikiwemo mbolea) zaidi ya tani laki 8;
Kwanini tusiwe na industrial production ya agro-inputs kwa soko ambalo lipo?

Nyerere kwa old technology aliweza kuwa crude petroleum refinery na bi-products ya petroleum ni mbolea na lami; leo mna-import kila kitu, msitegemee miujiza.

Lazima balance of trade and balance of payments iwe na surplus.
Hapo tutatoboa.

Jumatatu njema!
 
Nadhani tupunguze matumizi yasio ya lazima,Kuna miradi ya kisiasa inayofirisi nchi sababu malipo mengi yanafanyika Kwa dola huku vyanzo vikibaki vile vile.

Katazo na onyo kali litolewe kuzuia several transactions kufanywa Kwa dola (Rent,Tozo,etc)..

Strategic bilateral agreements zifanywe dhidi ya nchi ambazo tunanunua zaidi commodities (Vyakula,Raw materials,Spares,etc) ili settlement Za malipo yafanyike Kwa kutumia local currency.

Tuvufungue Milango zaidi kuruhusu FDI Kwa kupunguza masharti yasio na tija..Wawekezaji walete mitaji Kwa wingi.

Watanzania walioiba fedha kuoitia utumishi wa umma na Rushwa wapewe amnesty ili kuzirudisha nyumbani na kwenye mzunguko (Mabilioni ya dola yamefichwa kwenye visiwa -Safe heavens na waliokuwa viongozi,viongozi).

Tupige marufuku wageni kuja na kufanya biashara ya export tokea kwenye roots..Watoe kazi Kwa wazawa kuepuka mapato mengi ya exports kuondoka nchini.

Mashamba makubwa 500 yaanzishwe kimkakati yenye ukubwa kati ya ekari 2000 mpaka 5000 Kwa mkulima mmoja..mikopo ya fedha na mitambo isio na riba Itolewe kuchochea kilimo ktk mazao makuu 7 (Ngano,Mahindi,kahawa,Alizeti,Mpunga,Korosso,Kunde,Ufuta,Miwa,Chai,Maharagwe..etc,Wahitimu wa kilimo ewalazimishwe kufanya kazi za uzalishaji vijijini Kwa kupewa ruzuku na vifaa na mitambo ya kilimo .

Ujenzi wa viwanda 200 kupitia EPZA.Wazawa wawezeshwe kupanua na kujenga viwanda kupitia EPZA ili kuboost export ktk kupitia export demands zilizopo na uongezaji thamani’mfano.Nguo,ngozi,Maziwa,Chakula,etc
 
Njia ya hakika ya kuwa na dola za kutosha ni kuwa na trade surplus. Yaani uuze kuliko unavyonunua. Lakini hili halipo karibu kwa nchi zote za Afrika. Sasa mbinu iliyobaki ni kukabiliana/kumanage uhaba wa dola. Nchi hufanyaje hivyo?
Wale walalamikaji kwenye mikutano ya Bashite wangemuuliza hili.
 
Ongozeni mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi; punguzeni imports kwa bidhaa au huduma ambazo nchi inaweza kuzalisha.

Wizara ya fedha, viwanda na biashara, kilimo, mifugo na uwekezaji wanatakiwa waje na real working model ili haya yawezekane.

Mfano, kila mwaka mnajua matumizi ya sukari ni zaidi ya tani laki 6, uwezo wa ndani kuzalisha ni tani laki 3; nchi inshindwaje kuja na parament solution?
Kila mwaka nchi inaagiza agro-inputs (ikiwemo mbolea) zaidi ya tani laki 8;
Kwanini tusiwe na industrial production ya agro-inputs kwa soko ambalo lipo?

Nyerere kwa old technology aliweza kuwa crude petroleum refinery na bi-products ya petroleum ni mbolea na lami; leo mna-import kila kitu, msitegemee miujiza.

Lazima balance of trade and balance of payments iwe na surplus.
Hapo tutatoboa.

Jumatatu njema!
Mama amefungua nchi!
 
Back
Top Bottom