Chanzo cha uhaba wa dollars bara la Afrika na njia za kuondokana

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
11,193
19,141
Nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Kenya, Misri, Zimbabwe, Nigeria, Ghana, Tanzania na Zambia kwa sasa zinakabiliwa na uhaba wa dola za Marekani. Dola ndiyo sarafu inayotawala katika shughuli za kimataifa. Nchi hizi zinategemea sarafu ya Marekani kulipia madeni ya nje, bidhaa muhimu na pembejeo za viwanda.

SABABU
Sababu ya haraka ya uhaba wa dola ni

1. Kuzorota kwa urari wa malipo ya nchi (balance of payment), ikimaanisha miamala ya kifedha ya nchi na ulimwengu wote. Hii inaweza kuwa kutokana na tukio lisilotarajiwa kama janga la asili ambalo linaharibu sekta ya utalii ya nchi inayoingiza dola.

2. Kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa muhimu kutoka nje kama vile chakula na madawa.

3.Kuongezeka kwa malipo ya huduma ya deni (debt repayment) ambayo inadaiwa na 4. Kushuka kwa malipo kutoka kwa wafanyikazi nje ya nchi (doaspora remittances

4. Kuteremka kwa thamani ya bidhaa ambazo nchi inasafirisha nje (export) ikilinganishwa na kile inachoagiza (import).

5. Madhira mnalimbali mwanzoni mwa muongo wa 2020 ilifunguliwa na mfululizo wa mishtuko ambayo imechangia uhaba wa dola:-
(a)Kusimama kwa shughuli za uchumi kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa COVID-19
(b) Mdororo wa kiuchumi wa dunia uliopelekea kupungua bei za bidhaa nyingi muhimu za Afrika.
(c) Kusimama kwa shughuli za Utalii - chanzo muhimu cha mapato ya dola
(d) Kuibuka tena kwa mfumuko wa bei duniani na matokeo ya sera ya fedha ya kubana viwango vya juu vya riba kumeongeza bei za bidhaa
(e) Vita vyavUrusibna Ukraine. Bei za mafuta, vyakula na mbolea zilipanda wakati Urusi ilipovamia Ukraine. Kupanda kwa bei ya mafuta kunapunguza uhaba wa dola kwa nchi

NINI KIFANYIKE?
Kuchukua hatua za kisera kushughulikia uhaba wa dola.

1. Kupunguza matumizi ya umma. Hiyo itapunguza mahitaji ya bidhaa kutoka nje. Ni ngumu kisiasa.
2. Kuhimiza uzalishaji wa mauzo ya nje na bidhaa mbadala kutoka nje.
3. Kushirikiana na mashirika ya ukopeshaji ya kimataifa kama Word Bank na IMF katika kuweka ratiba nzuri ya ulipaji madeni ya muda mrefu
 
Mimi ningeongezea hivi,

Kupunguza matumizi ya dola kwa household ni kuzalisha na kuzalisha na zalisha tena

Uwe na maziwa yako, nyama ya kuku yako, mihogo na mahindi yako, mafuta ya alizeti yako, mapapai, karanga, maparachichi ndizi mchele maharage uliyolima mwenyewe

Fuga kuku wako mbuzi kondoo bata samaki njiwa bata mzinga simbilisi zako n.k

Hakikisha unatumia biogas yako kama nishati ya kupikia na kuwasha taa nyumbani

Utakuta badala ya kuhitaji dola inakuwa kinyume chake dola inaanza kukuhitaji wewe
 
Na kwann Dola, wakati Wenye akili Kwa Sasa wanaikimbia hiyo Dola ?.

Zimbabwe hapo tu Sasa wanaikimbia Dola, Dola Ukoloni.
 
Hakuna watu wakubali pesa za madafu au rubu kwenye biashara za kimataifa.
BRICS Sasa wanaikataa Dola.

Biashara inafanyika Kwa Ruble ya kirusi na Yuan ya Uchina na Local Currencies .

Mataifa mengi yenye mlengo wa Kimashariki( Uchina) na Kaskazin( Urusi) Kwa Sasa Transactions zao zinafanyika under Local currencies.

Ukiidekeza Dola, matokeo yake ni hayo ni kuzalilishwa!!.

Zimbabwe Sasa Wame introduce new Gold backed Currency ( ZiG ) japo walianza Kwa kuchechemea ila inazidi kupata nguvu

Sio tu Zimbabwe, Kuna Nchi za Afrika nazo zimeanza kushtuka.

Kwasasa Werevu wamestuka Duniani.
 
Endelea kulishwa matangopori kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Mimi ningeongezea hivi,

Kupunguza matumizi ya dola kwa household ni kuzalisha na kuzalisha na zalisha tena

Uwe na maziwa yako, nyama ya kuku yako, mihogo na mahindi yako, mafuta ya alizeti yako, mapapai, karanga, maparachichi ndizi mchele maharage uliyolima mwenyewe

Fuga kuku wako mbuzi kondoo bata samaki njiwa bata mzinga simbilisi zako n.k

Hakikisha unatumia biogas yako kama nishati ya kupikia na kuwasha taa nyumbani

Utakuta badala ya kuhitaji dola inakuwa kinyume chake dola inaanza kukuhitaji wewe
Umeliweka vizuri sana. Nchi za wenzetu kama India na South Africa hakuna mtu anataka dollars zaidi ya wale wanaotaka kusafiri au kufanya malipo ya nje
 
Kwa nini wasema matango pori? Mbona tayari BRICS members wana transact kwa currencies zao!!
86% ya biashara ya nje ya India inafanywa kwa $,
Hakuna hata sheria za kuwalazimisha wafanyabiashara katika hizo nchi za BRICS kufanya biashara kwa currencies za nchi zao. Wafanyabiashara walio machawa wa serikali na makampuni/mashirika ya serikali ndio labda watajipapatua kufanya biashara kwa sarafu zao ili kuwafurahisha watawala tu, wengine wanaendelea kutumia $ kama kawaida.
 
Vipi kuhusu biashara kati ya China na Russia? Je wanatumia RMB na Rubble? Au
 
1. Kiingereza kianze kutumika kuanzia primary. Baadhi ya shule chache za serikali wameanza ila ni chache inabidi iwe nchi nzima, hii itafungua fursa kupeleka vijana wengi wanaomaliza vyuo na collegea kwenye ajira ulaya, middle east na Australia kwakuwa watakuwa wanaweza kuwasiliana vyema na kupata fursa. Kiswahili ni kizuri ila hakina fursa nje ya nchi au hata hapa nchini tu hamna kazi ya maana utapata bila kiingereza, sasa sijui kwanini kinatumika bado mashuleni??? Kenya wanapata fursa nyingi za kiswahili japo Tanzania ndio tunakitumia na za kingereza pia sababu wanajua lugha zote. Viongozi wote na watu wanaojiweza wanapeleka watoto wao e glish medium, ila kupata universal business language, english.

Hii itaongeza pato la nchi linalotokana na diaspora remittance ambalo nimkubwa sana. Mfano Kenya wanaingiza trillion 10 kwa mwaka wakati tanznaia ni 800 bilioni tu kutoka disapora.

2. Piga marufuku au weka kodi kubwa sana kwa vitu visivyo lazima ku-import - mfano fenicha, pombe, na mali ghafi zinazopatikana nchini.

2. Asimia karibia 20% ya dola inatumika kuingiza mafuta, serikali ije na mkakati wa mda mrefu wa kukuza matumizi ya magari ya umeme, kuongeza vituo vya gesi asilia na kufuta ushuru wa magari yabayotumia gesi asilia. Kufanya biashara na nchi majirani kwa kutumia sarafu zetu.

3. Serikali iongeze tija na uwekezaji kwenye sekta zinazoleta dola mfano utalii, kilimo cha baishara kama parachichi, korosho, chai, kahawa. Pia kuwe na mkakati wa kitaifa wa sekta za kimkakati za kuketa pesa za kigeni, uzuri tuna madini, kilimo, ICT n.k.

Utalii sio mbugani tu, uwekezaji kwenye kumbi za kisasa za mikutano, festivals, mashindano ya magari n.k. Rwanda hana mbuga ila kuna kila aina ya watalii wanaenda kutembea kwenye mikutano n.k.
Pia fukwe kama za dar hamna utalii kabisa kwasbabu hapajawekwa sawa tofauti na Zanzibar au mombasa.

4. Uvuvi bahari kuu, miundombinu ya usafiri kama barabara za kisasa, umeme wa uhakika, kuongeza teknolojia. Vitu kama charger za simu, vitochi vifaa vya umeme viwe local made.

5. Kuboresha uwanda huru wa kiuchumi (EPZ) ili kuvutia uwekezaji mkubwa. Ethiopia, Rwanda na Morocco wamefanikiwa sana.
Morocco ndio wanaongoza kwa sekta ya uzalishaji magari afrika kwa sasa viwanda vingi vya ufaransa vimehamia morroco yote kupitia EPZA.
 
BRICS Sasa wanaikataa Dola.

Biashara inafanyika Kwa Ruble ya kirusi na Yuan ya Uchina na Local Currencies .

Mataifa mengi yenye mlengo wa Kimashariki( Uchina) na Kaskazin( Urusi) Kwa Sasa Transactions zao zinafanyika under Local currencies.

Ukiidekeza Dola, matokeo yake ni hayo ni kuzalilishwa!!.

Zimbabwe Sasa Wame introduce new Gold backed Currency ( ZiG ) japo walianza Kwa kuchechemea ila inazidi kupata nguvu

Sio tu Zimbabwe, Kuna Nchi za Afrika nazo zimeanza kushtuka.

Kwasasa Werevu wamestuka Duniani.
Screenshot_20240416-124043.png
 
1. Kiingereza kianze kutumika kuanzia primary. Baadhi ya shule chache za serikali wameanza ila ni chache inabidi iwe nchi nzima, hii itafungua fursa kupeleka vijana wengi wanaomaliza vyuo na collegea kwenye ajira ulaya, middle east na Australia kwakuwa watakuwa wanaweza kuwasiliana vyema na kupata fursa. Kiswahili ni kizuri ila hakina fursa nje ya nchi au hata hapa nchini tu hamna kazi ya maana utapata bila kiingereza, sasa sijui kwanini kinatumika bado mashuleni??? Kenya wanapata fursa nyingi za kiswahili japo Tanzania ndio tunakitumia na za kingereza pia sababu wanajua lugha zote. Viongozi wote na watu wanaojiweza wanapeleka watoto wao e glish medium, ila kupata universal business language, english.

Hii itaongeza pato la nchi linalotokana na diaspora remittance ambalo nimkubwa sana. Mfano Kenya wanaingiza trillion 10 kwa mwaka wakati tanznaia ni 800 bilioni tu kutoka disapora.

2. Piga marufuku au weka kodi kubwa sana kwa vitu visivyo lazima ku-import - mfano fenicha, pombe, na mali ghafi zinazopatikana nchini.

2. Asimia karibia 20% ya dola inatumika kuingiza mafuta, serikali ije na mkakati wa mda mrefu wa kukuza matumizi ya magari ya umeme, kuongeza vituo vya gesi asilia na kufuta ushuru wa magari yabayotumia gesi asilia. Kufanya biashara na nchi majirani kwa kutumia sarafu zetu.

3. Serikali iongeze tija na uwekezaji kwenye sekta zinazoleta dola mfano utalii, kilimo cha baishara kama parachichi, korosho, chai, kahawa. Pia kuwe na mkakati wa kitaifa wa sekta za kimkakati za kuketa pesa za kigeni, uzuri tuna madini, kilimo, ICT n.k.

Utalii sio mbugani tu, uwekezaji kwenye kumbi za kisasa za mikutano, festivals, mashindano ya magari n.k. Rwanda hana mbuga ila kuna kila aina ya watalii wanaenda kutembea kwenye mikutano n.k.
Pia fukwe kama za dar hamna utalii kabisa kwasbabu hapajawekwa sawa tofauti na Zanzibar au mombasa.

4. Uvuvi bahari kuu, miundombinu ya usafiri kama barabara za kisasa, umeme wa uhakika, kuongeza teknolojia. Vitu kama charger za simu, vitochi vifaa vya umeme viwe local made.

5. Kuboresha uwanda huru wa kiuchumi (EPZ) ili kuvutia uwekezaji mkubwa. Ethiopia, Rwanda na Morocco wamefanikiwa sana.
Morocco ndio wanaongoza kwa sekta ya uzalishaji magari afrika kwa sasa viwanda vingi vya ufaransa vimehamia morroco yote kupitia EPZA.
Haya ni mawazo chanya kabisa, kongole
 
Back
Top Bottom