Uhaba wa Dola ndio chanzo cha upungufu wa mafuta

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,821
Tukifikia hatua hii ya sekta nyeti kukumbwa na uhaba wa Dola basi yajayo ni Changamoto zaidi.

Ushauri Kwa Serikali izuie Moja kwa Moja Uagizaji wa bidhaa zisizo za lazima zilizojaza maduka yetu Ili vitu vya msingi visikosekane.eg furnitures,urembo,Baadhi ya nguo na vitu vinginevyo kama hivyo.

Kwa nini Hadi Leo Bado mafuta ya kula kutoka Nje yanaingia ndani wakati wakulima Wetu wamelima vya kutosha? Saruji ya Nje ya Nchi unaingia ndani kufanya nini?

Mwisho hii ndio hasara ya kuwa net importer badala ya kuwa exporter,hapa tuanze mikakati ya kuishi kimkakati Kwa kuchagua bidhaa ambazo hatuna ushindani mkubwa hasa za Kilimo,mifugo na uvuvi tuzipe uwekezaji wa kutosha ndani ya mda Fulani Ili tuwe net exporters.Hii tabia ya kwenda jumla jumla bila malengo yanayopimika imeligharimu Taifa Kwa miaka Mingi sana,Tume ya Mipango Lisaidieni Taifa.

My Take
Mwenzako akinyolewa zako tia maji,tulimcheka jirani kumbe na sisi tuko kwenye Hali hiyo hiyo.

Bidhaa Kumi zilizogharimu fedha nyingi zaidi kuagiza nje ya nchi (2022):
1.Mafuta-Trilioni 8
2.Mitambo- Trilioni 5.9
3.Chuma- Trilioni 2.5
4.Vipuri- Trilioni 2.2
5.Plastiki- Trilioni 1.78
6.Mbolea- Trilioni 1.1
7.Madawa- Bilioni 789
8.Ngano- Bilioni 696
9.Magari- Bilioni 668
10.Vyakula na Vinywaji -Bilioni 419
 
Makamba alisema Bungeni wame strack Dili la mafuta ya bei nafuu kutoka Arabuni mbona haleti mrejesho? Mafuta Yako wapi?

Pili tuliambiwa tunapanua miundombinu ya kuhifadhi mbona hatuambiwi utekelezwaji wake?

Serikali pungeni program zisizo na Tija Kwa Sasa Ili pesa ikafanye mambo ya msingi eg Samia legal foundation,Samia Scholarship,kusaidia pesa viongozi wa bodaboda na vishimo vya dizaini hiyo.
 
Tukiacha kununua nguo tutavaa nini?
Acha kukurupuka,wapi nimesema muache kuvaa nguo? By the way Serikali ipunguze uingizaji wa nguo za Nje kwenye maduka zimejaa.

Enzi za Mwalimu mlivaa viraka na mkamsifia Mzalendo hata Sasa mnaweza vaa viraka
 
Makamba ni tapeli mkubwa wa nchi hii hakuna namna
 
Unataka kututoa kwenye mchakato wetu wa kufungua nchi. Sie tumefungua nchi bwana.
Kufungua Nchi na uhaba wa Dola wapi na wapi? In fact tungeifungua vizuri na kupata wawekezaji wengi tusingekumbwa na hiyo shida
 
... itumike Rubble au RMB kuagiza bidhaa! Dola tupa kuleee! Alisikika mwehu akifoka kwa hasira baada ya kukosa makombo jalalani.
 
Ushauri Kwa Serikali izuie Moja kwa Moja Uagizaji wa bidhaa zisizo za lazima zilizojaza maduka yetu Ili vitu vya msingi visikosekane.eg furnitures,urembo,Baadhi ya nguo na vitu vinginevyo kama hivyo.

Kwa nini Hadi Leo Bado mafuta ya kula kutoka Nje yanaingia ndani wakati wakulima Wetu wamelima vya kutosha? Saruji ya Nje ya Nchi unaingia ndani kufanya nini?

Kwenye Urembo,Furnitures,nguo means utaua mnyororo mkubwa wa watu ,K/kko ,Karume /Manzese itanyong'onyea.

Bora kuzuia Uagizaji wa mafuta ya kupikia ,sukari ,saruji etc ambavyo vinapatikana kwa wingi hapa kwetu.
 
Acha kukurupuka,wapi nimesema muache kuvaa nguo? By the way Serikali ipunguze uingizaji wa nguo za Nje kwenye maduka zimejaa.

Enzi za Mwalimu mlivaa viraka na mkamsifia Mzalendo hata Sasa mnaweza vaa viraka
Nguo kila siku zina agizwa lakini pia zinatoka mpya labda kama u ataka tusieende na wakati?
 
Kwenye Urembo,Furnitures,nguo means utaua mnyororo mkubwa wa watu ,K/kko ,Karume /Manzese itanyong'onyea.

Bora kuzuia Uagizaji wa mafuta ya kupikia ,sukari ,saruji etc ambavyo vinapatikana kwa wingi hapa kwetu.
Kwenye furnitures hapo wazuie kabisa hakuna cha mnyoro Wala nini,wauzie za ndani ya Nchi

Kwenye urembo tunaweza punguza hasa Vito vya thamani, saa, mapambo ya Nje nk havina maana yeyote watu wa ndani wanaweza zalisha, watu walete malighafi tuu.
 
Akili yako ukizuia imports ndio tutapata solution ya ukosefu wa dollar, hakuna short cut au siasa kwenye haya mambo, na ukizuia imports ujue exports zako nazo zitapigwa break, solution ongeza uzalishaji uza soko la limataifa upate dollar, nchi imejaa machinga tuu na wakulima wa nyanya unategemea nini, dhahabu na utalii ni rushwa tupu na hakuna pesa inaenda hazina
 
Makamba alisema Bungeni wame strack Dili la mafuta ya bei nafuu kutoka Arabuni mbona haleti mrejesho? Mafuta Yako wapi?

Pili tuliambiwa tunapanua miundombinu ya kuhifadhi mbona hatuambiwi utekelezwaji wake?

Serikali pungeni program zisizo na Tija Kwa Sasa Ili pesa ikafanye mambo ya msingi eg Samia legal foundation,Samia Scholarship,kusaidia pesa viongozi wa bodaboda na vishimo vya dizaini hiyo.
Wewe na wanufaika wenzio wa ufisadi Serikalini ndo mnaoamini maneno ya Makamba maana hayatoi bila mrejesho wa Wapambe. Kila anachofanya Makamba ni deal kwake na mgao Kwa Wapambe kama wewe.
 
Back
Top Bottom