MJADALA: Nini kifanyike kuondoa Uhaba wa Sukari kuendelea kujirudia kila mwaka Tanzania?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
1709731028391.jpeg
Uhaba wa sukari nchini Tanzania ni tatizo linaloathiri sana wananchi na uchumi kwa ujumla. Hali hii inaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na:
  1. Uzalishaji duni: Uzalishaji wa miwa, malighafi ya sukari, unaweza kuathiriwa na mambo kama hali mbaya ya hewa, magonjwa, au mbinu duni za kilimo. Hii inaweza kusababisha upungufu wa sukari katika soko la ndani.
  2. Usafirishaji na ugavi: Matatizo katika usafirishaji na ugavi wa sukari kutoka viwandani kwenda kwenye masoko yanaweza kusababisha uhaba. Miundombinu duni ya usafirishaji inaweza kusababisha usambazaji usio wa kutosha wa bidhaa.
  3. Upungufu wa fedha za kigeni: Kutokana na uhaba wa fedha za kigeni, nchi inaweza kukabiliwa na ugumu katika kuagiza sukari kutoka nje, ambayo inaweza kusababisha upungufu katika soko la ndani.
  4. Udhibiti wa bei: Udhibiti wa bei na sera za kifedha zinaweza kusababisha wazalishaji kushindwa kutosheleza mahitaji ya soko au kusababisha upungufu wa bidhaa.
Kukabiliana na uhaba wa sukari, serikali inaweza kuchukua hatua za kuongeza uzalishaji wa sukari, kuhimiza uwekezaji katika sekta ya kilimo, kusaidia wakulima na viwanda vya sukari, na kusimamia vizuri usambazaji na bei ya sukari. Pia, kuweka mifumo imara ya usimamizi wa ugavi na kuhakikisha uwazi katika biashara ya sukari ni muhimu ili kuzuia upungufu wa bidhaa.

Nini kifanyike kukabiliana na tatizo hilo Tanzania?

Kwanza kabisa, serikali inaweza kuchukua hatua za haraka ili kupunguza uhaba wa sukari na kupunguza athari zake kwa wananchi. Hapa kuna baadhi ya hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa:
  1. Kuongeza uzalishaji wa sukari: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuhamasisha wakulima wa miwa kuongeza uzalishaji, kuboresha mbinu za kilimo, na kuhakikisha kuwa viwanda vya sukari vinafanya kazi kwa ufanisi ili kutosheleza mahitaji ya soko.
  2. Kuagiza sukari: Serikali inaweza kuagiza sukari kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya soko wakati ambapo uzalishaji wa ndani hautoshi. Hata hivyo, hatua hii inaweza kuwa ni suluhisho la muda mfupi na inaweza kuathiri sekta ya kilimo ya ndani.
  3. Kudhibiti bei: Serikali inaweza kuchukua hatua za kudhibiti bei ili kuzuia kupanda kwa bei kwa viwango visivyokuwa vya kawaida. Hii inaweza kujumuisha kudhibiti bei ya rejareja na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hawatumii hali hii kama fursa ya kuongeza faida kubwa.
  4. Kuhimiza ushindani: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuhimiza ushindani kati ya wazalishaji na wafanyabiashara ili kuhakikisha kuwa kuna chaguo zaidi kwa wananchi na hivyo kudhibiti bei.
  5. Kuongeza uelewa wa umma: Serikali inaweza kufanya kampeni za elimu kuhusu matumizi sahihi ya sukari na njia mbadala za lishe ili kupunguza matumizi ya sukari na kuhimiza lishe bora.
Kwa ufanisi, hatua hizi zinaweza kusaidia kupunguza uhaba wa sukari na kupunguza athari zake kwa wananchi wa Tanzania.

Kushiriki Mjadala bonyeza Link hii https://jamii.app/UhabaWaSukari
UPDATES
- PROFESA KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Msimu uliopita hali ya uzalishaji wa Sukari ilifikia rekodi ya juu kabisa 460,000 Nchini, wakati huo mahitaji yalikuwa 490,000 kulikuwa na upungufu wa Tan 30,000

Mwaka huu (2024) uzalishaji mpaka sasa ni 370,000, kwa namna yoyote hatuwezi kufikia lengo tulilojiwekea la kufikisha Tani 550,000 kutokana na Mazingira ya Mvua

Ndani ya kipindi cha Miaka 10 tumefika katika kiwango cha juu cha uzalishaji wa Sukari, tulikotoka Mwaka 2001 tulikuwa tunazalisha Sukari chini ya Tani 200,000

Mwaka huu (2024) kuna pengo kubwa na hivyo upungufu utakuwa mkubwa kuliko ulivyokuwa Mwaka 2023

- DAVID MULOKOZI, Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Super Brands LTD - Manyara
Sisi tunahusika na utengenezaji wa vinywaji vikali na vinywaji vingine ambavyo utengenezwaji wake unahusisha Sukari

Hali ya Sukari sio nzuri Nchini, hii haikuanza siku moja, sukari ilianza kupotea taratibu hali ambayo ilisababisha sisi tuliopo Mikoani tukaanza kwenda maeneo mengine kuitafuta, hiyo ikasababisha mazingira ya kupandisha bei ya bidhaa kutokana na changamoto ya uzalishaji

Ndani ya Mwezi mmoja kuna viwanda kadhaa vya utengenezaji wa vinywaji vikali vimefungwa kutokana na uhaba wa Sukari, ukichanganya na uhaba wa Dola kumekuwa na ugumu wa kuendelezea uzalishaji

Uhaba wa Sukari umesababisha kuwe na changamoto katika uzalishaji wa mambo mengi

- PROF. KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Mvua kubwa zimesababisha uvunaji wa miwa kuwa mgumu, miundombinu ikaharibika ikawa ngumu kuendeleza uzalishaji, sio kwamba hatuna miwa, changamoto ni hizo nilizozitaja

Pia, uagizaji wa Sukari siyo jambo la wiki moja, inaweza kuchukua hadi miezi miwili hadi mitatu, mfano Sukari inaweza kutolewa India, Brazil au Thailand ambapo nako kuna mabadiliko ya utoaji Sukari kutoka kwenye Nchi zao

Baada ya UVIKO-19 bei ya Sukari ilipanda zaidi ya mara tatu kote Duniani kutokana na mabadiliko ya Soko la Sukari yaliyotokea katika Nchi nyingi

- BERNARD KIHIYO, Mkurugenzi wa Chama cha Walaji Tanzania
Kumekuwa na ahadi nyingi nzuri kuhusu Sukari, tukiambiwa hili litaisha au itakuwa hivi lakini baada ya muda jambo halimaliziki

Sisi tuna Mtandao wa Walaji Mikoa yote, tunapata ripoti kuhusu uhaba wa Sukari pamoja na bei kuwa juu, sio jambo jema

- PROFESA KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Sababu kubwa iliyosababisha bei ya Sukari kupanda sio Tozo, ni upungufu au uhaba wa SukariHiyo ikasababisha Wafanyabiashara ambao sio Waaminifu kuanza kupandisha bei

Sukari inayozalishwa ndani haina Tozo, Tozo ni kwa ajili ya Sukari inayoagizwa kutoka nje. Mfano Serikali imefuta Ushuru wa Forodha lakini bado bei zikawa zinapandishwa, hapo ni suala la uadilifu

Tulivyokuwa kwenye UVIKO-19, Nchi ambazo ni wauzaji wakubwa wa Sukari walikuwa kwenye ‘lock down’, hiyo ilisababisha upatikanaji wa Sukari kwenye Soko la Dunia ukashuka, sasa hivi ndio tumeanza kupata nafuu

- AHOBOKILE MWAITENDA, Mshauri wa Fedha na Kodi
Unaweza kukuta mzalishaji mmoja wa Sukari anatengeneza Sukari Mkoani Kagera, baada ya kuzalishwa inapelekwa kwenye kituo nje ya mkoa huo kwa ajili ya kuanza kusambazwa kisha ndio inarejeshwa kwenye kituo husika kama sehemu ya usambazaji

Hiyo ni moja ya changamoto inayoweza kusababisha kukosekana kwa usambazaji mzuri wa Sukari

- PROF. KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Miaka mitatu ya nyuma, Fedha ya Zambia haikuwa na mlinganisho mzuri na Fedha yetu, kwa sasa hilo tatizo halipo

Sukari inayoingia kutoka nje lazima iwe na vibali vyote muhimu, ikitokea imeingia bila kufuata utaratibu ndipo utaona inaanza kuuzwa kwa bei ya chini, ndivyo ilivyokuwa ikitokea Sukari iliyoingia kinyume cha Sheria kutoka Zambia

- DAVID MULOKOZI, Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Super Brands LTD ya Manyara
Sukari ya nyumbani ikiwekwa sokoni hiyo hiyo ndiyo inunuliwe na makampuni yanayohusika na uzalishaji wa bidhaa kwa kutumia sukari ni rahisi kusababisha changamoto ya uhaba kwa kuwa Viwanda vinatumia Sukari nyingi zaidi

- PROF. KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Hakuna upungufu wa Sukari kwa ajili ya matumizi ya ViwandaNitoe wito kuwa Wazalishaji wa viwanda ambao wanatumia Sukari katika uzalishaji wao waje Bodi ya Sukari tuzungumze tutawezesha wapate Sukari badala ya kutegemea ile inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani

- SEIF MAALIM SELASSIE, Mgombea Urais 2020 kupitia AAFP
Ingetokea nimechaguliwa na kushinda Urais wakati nagombea wala tusingekuwa na mjadala huu wa Sukari kwa sasa, kwani ningekuwa nimeshughulikia changamoto hiyo mapema

- PROFESA KENNETH BENGESI, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania
Wanaokamatwa kwa kuuza Sukari kwa gharama ya juu ambayo si bei elekezi, sio Wafanyabiashara wadogo tu hata wakubwa. Tunachoangalia ni kwa mfano wanaouza Sukari Kilo moja Tsh. 6000. Kama kuna wanaoendeleza kuuza kwa bei kubwa Mwananchi atoe ushirikiano kwa Bodi tutawawajibisha wanaofanya hivyo

Kuna watu wasipopata Sukari kipato kinakuwa hakina uhakika, ndio maana Serikali ilifuta Tozo mbili ya Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT na ile ya Ushuru wa Forodha Isingekuwa hivyo Wananchi wa kipato cha chini wangeweza kuuziwa Sukari hata Tsh. 10,000, tulipoona bei hazishuki ndipo tukaweka bei elekezi
 
Serikali kujua kutenganisha mahitaji muhimu ya kibinadamu na siasa.

Ukiachana na sukari ni mambo mengi sana yemeharibika nchini Tanzania.serikali haijali tena wananchi wake🥺wanachi wanapewa umuhimu kipindi cha uchaguzi tu,uchaguzi ukiisha basi mwananchi ni takataka.

Kwa hali ilivyo sasa nilitegemea Mkuu wetu/Rais wetu aseme neno au tendo lolote la faraja lakini kimya🥹ukiwa umetawala,vicheko ni kwa watu wachache sana.ni huzuni.
 
Serikali iruhusu biashara huria ili kuongeza ushindani kwa wazalishaji na pia wauzaji wa hiyo sukari. Kitendo cha serikali kuzuia sukari kutoka nje kuuzwa nchini, ndiyo chanzo cha haya yote.

Serikali ipunguze pia kodi zisizo na ulazima kwa wazalishaji wa ndani ili kupunguza bei ya bidhaa muhimu kama sukari.
 
Hakuna njia zaidi ya kuongeza uzalishaji. Kama ambavyo JPM alivyompatia Bakhresa bonde alime miwa ndivyo serikali inatakiwa kufungua na kuwapa wazawa mabonde mengine zaidi na zaidi. Kuagiza nje kihuria hakutaweza kutatua tatizo maana kuna siku dola za kuagizia zitakosekana. Na kuruhusu makampuni ya nje kuzalisha nalo ni tatizo maana watataka wakiuza waondoke na dola.
 
Sukari ipo ya kutosha nakuhakikishia, ila tatizo ni kuruhusu wafanyabiashara wakubwa kuitikisa serikali. Kuna godown moja lipo Nyerere road ukiwa unaelekea airport kabla ya kampuni ya sigara ukitokea Kariakoo, Kila siku usiku zinaingia tani za sukari za kutosha na serikali inajua. Ni hivi, wafanyabiashara wakubwa mfano wa Mo, wanaenda Mtibwa Sugar, Kilombero na Kagera sugar, wanalipia CASH sukari itakayozalishwa May 2023 hadi October 2023 kabla ya kipindi Cha mvua. Kwahiyo %kubwa ya sukari inaenda kwao, wenyewe ndo wana control bei ya sukari. Tatizo ni kubwa mno, sio rahisi kulimaliza.
 
Uhaba wa sukari nchini Tanzania ni tatizo linaloathiri sana wananchi na uchumi kwa ujumla. Hali hii inaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na:
  1. Uzalishaji duni: Uzalishaji wa miwa, malighafi ya sukari, unaweza kuathiriwa na mambo kama hali mbaya ya hewa, magonjwa, au mbinu duni za kilimo. Hii inaweza kusababisha upungufu wa sukari katika soko la ndani.
  2. Usafirishaji na ugavi: Matatizo katika usafirishaji na ugavi wa sukari kutoka viwandani kwenda kwenye masoko yanaweza kusababisha uhaba. Miundombinu duni ya usafirishaji inaweza kusababisha usambazaji usio wa kutosha wa bidhaa.
  3. Upungufu wa fedha za kigeni: Kutokana na uhaba wa fedha za kigeni, nchi inaweza kukabiliwa na ugumu katika kuagiza sukari kutoka nje, ambayo inaweza kusababisha upungufu katika soko la ndani.
  4. Udhibiti wa bei: Udhibiti wa bei na sera za kifedha zinaweza kusababisha wazalishaji kushindwa kutosheleza mahitaji ya soko au kusababisha upungufu wa bidhaa.
Kukabiliana na uhaba wa sukari, serikali inaweza kuchukua hatua za kuongeza uzalishaji wa sukari, kuhimiza uwekezaji katika sekta ya kilimo, kusaidia wakulima na viwanda vya sukari, na kusimamia vizuri usambazaji na bei ya sukari. Pia, kuweka mifumo imara ya usimamizi wa ugavi na kuhakikisha uwazi katika biashara ya sukari ni muhimu ili kuzuia upungufu wa bidhaa.

Nini kifanyike kukabiliana na tatizo hilo Tanzania?

Kwanza kabisa, serikali inaweza kuchukua hatua za haraka ili kupunguza uhaba wa sukari na kupunguza athari zake kwa wananchi. Hapa kuna baadhi ya hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa:
  1. Kuongeza uzalishaji wa sukari: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuhamasisha wakulima wa miwa kuongeza uzalishaji, kuboresha mbinu za kilimo, na kuhakikisha kuwa viwanda vya sukari vinafanya kazi kwa ufanisi ili kutosheleza mahitaji ya soko.
  2. Kuagiza sukari: Serikali inaweza kuagiza sukari kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya soko wakati ambapo uzalishaji wa ndani hautoshi. Hata hivyo, hatua hii inaweza kuwa ni suluhisho la muda mfupi na inaweza kuathiri sekta ya kilimo ya ndani.
  3. Kudhibiti bei: Serikali inaweza kuchukua hatua za kudhibiti bei ili kuzuia kupanda kwa bei kwa viwango visivyokuwa vya kawaida. Hii inaweza kujumuisha kudhibiti bei ya rejareja na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara hawatumii hali hii kama fursa ya kuongeza faida kubwa.
  4. Kuhimiza ushindani: Serikali inaweza kuchukua hatua za kuhimiza ushindani kati ya wazalishaji na wafanyabiashara ili kuhakikisha kuwa kuna chaguo zaidi kwa wananchi na hivyo kudhibiti bei.
  5. Kuongeza uelewa wa umma: Serikali inaweza kufanya kampeni za elimu kuhusu matumizi sahihi ya sukari na njia mbadala za lishe ili kupunguza matumizi ya sukari na kuhimiza lishe bora.
Kwa ufanisi, hatua hizi zinaweza kusaidia kupunguza uhaba wa sukari na kupunguza athari zake kwa wananchi wa Tanzania.

Kushiriki Mjadala bonyeza Link hii https://jamii.app/UhabaWaSukari
Hivi kweli unadhani uzalishaji haupo!
TPC yenyewe nimekuwa pale muda hii kiwanda unakoboa sukari sio kawaida ni 24hrs sana sana mweI April kuna utengenezaji machine hivyo wanafunga ila bohari kunakuwa kumejaa sukari ya miezi hata 3 na bado wanasafiriasha nje.

Ni kwa nini Serikali isikae na wamiliki wa hizi viwanda wakakubaliana kuuza ndani kiasi fulani kwa miezi 3 na mingine 3 watoe nje.
Na hii kwa kupokezana viwanda tulivyo navyo. Hivyo tutakuwa na sukari tosha ndani ya kila mwaka.
Tuache uhuni swrikali mnafanya usanii na maisha ya waTanzania.

Mbona ninyi mnaendesha magari kubwa, mikutano kila siku, safari kibao, punguzeni hizi vitu .
 
Sukari ipo ya kutosha nakuhakikishia, ila tatizo ni kuruhusu wafanyabiashara wakubwa kuitikisa serikali. Kuna godown moja lipo Nyerere road ukiwa unaelekea airport kabla ya kampuni ya sigara ukitokea Kariakoo, Kila siku usiku zinaingia tani za sukari za kutosha na serikali inajua. Ni hivi, wafanyabiashara wakubwa mfano wa Mo, wanaenda Mtibwa Sugar, Kilombero na Kagera sugar, wanalipia CASH sukari itakayozalishwa May 2023 hadi October 2023 kabla ya kipindi Cha mvua. Kwahiyo %kubwa ya sukari inaenda kwao, wenyewe ndo wana control bei ya sukari. Tatizo ni kubwa mno, sio rahisi kulimaliza.
Hii nilikua siijui hii kumbe ndio IPO hivi?
 
ushaur wang apewe BAKHRESA azalishe yeye atulishe kila ktu kitakaa sawa. haya makampun yanasaidian na wafanya biashara kutuhujumu wananch
 
Hii nilikua siijui hii kumbe ndio IPO hivi?
Mkuu siongei story za kusikia vijiweni, nimeshuhudia mwenyewe. Muulize mtu yeyote anayefanya kazi kiwanda cha sukari chochote hapa nchini kama kuna uhaba wa sukari, majibu yake hutaamini. Sukari ipo sema imeshikiliwa.
 
Wewe unafanya kazi kiwanda kipi cha Sukari?
 
Susieni kununua sukari
Au punguzeni matumizi ya sukari

Ova
 
Ain't that obvious ?, Ushasema uhaba..., sasa kuondoa uhaba unafanya nini zaidi ya kuongeza uzalishaji au supply ? Unless unaamini make believe stories kwamba kuna watu wanaficha
 
Tatizo sio Uhaba wa Sukari

Tatizo ni hujuma dhidi ya upatikanaji wa sukari?

Iweje sukari iadimike Tanzania tu lakin Nchi zote za jirani hata wasiolima Miwa wala kuwa na Viwanda vya sukari hawana uhaba

1) Wamiliki wa Viwanda kuwa ndio wenye vibali vya kuagiza sukari ndio kosa la kwanza la kimkakati

2) Serikali imetoa vibali karibia vya tani laki 4 lakini wahusika wakaleta tani pungufu ya laki mbili kwa sababu gani? jibu no rahisi tu wanataka ku maintain scarcity ili kulinda bei zisiporomoke

3) Wakati wanatoa hivyo vibali walitumia vigezo gani ?

Wakati wetu uliwahi kutokea uhaba wa bidhaa fulani adimu, kabla ya kumpa kibali kwa Muagizaji tunamfanyia due diligence kujua uwezo wake then tunamtaka alete Bank guarantee ikimaanisha kwa mfano unatakiwa ulete tani laki 2 na wewe ukaleta pungufu Serikali inachukua ile dhamana ya performance guarantee

lakini kwny sukari wanajua wakileta kwa kiwango kikichokubaliwa bei itashuka wakati wao wanetengeneza uhaba wa makusudi kabisa

Haya mambo ya kulinda Viwanda vya ndani wakati havina capacity ya kulisha soko la ndani ndio yalimgharinu sana Mwl Nyerere hadi Nchi ikaingia kwny msuko suko mkubwa wa kiuchumi n kijamii
 
Hao waliopewa vibali wanahitaji fedha za kigeni yaani $ ili waagize hiyo sukari. Benki kuu haitoi dollar, hapo ndio tatizo.
Suluhisho ni kuimarisha na kupanua kilimo cha miwa. Tanzania ina ardhi na mazingira safi kwa kilimo cha miwa
 
Ninamjua mtu aliyenyimwa kibali cha kuingiza sukari nchini kutoka Brazil kwa Tani zote zinazotakiwa kukidhi soko la ndani na Bei ya bidhaa hiyo itashuka sana hata chini ya bei elekezi ya Serikali (Bashe).
 
Back
Top Bottom