Nataka kumfungulia mchepuko wangu duka la bidhaa za kike (urembo) na watoto. Nipeni ushauri kuhusu bajeti na mahala sahihi hapa dar

Ni biashara nzuri kwa mtazamo wangu, muhimu kuangalia location nzuri.

Ila waungwana humu tuache mtoa mada aionjoi kutumia hela zake kwa kumwazishia biashara mchepuko wake.

Huwezi jua anapewa nini na huyo Mchepuko wake

Sisi wajibu wetu itakuwa kumtia moyo siku akiumizwa naye, maana wakati anaenda kulala nyumba kubwa, Mchepuko naye analeta Kijana Dogo dogo wa kumkata Kiu

Hivyo tu 🤪
Naunga mkono hoja!
 
Mi nadhani kwa vile mara nyingi hizi pesa tunazohonga sio "hard earned money", ngoja tu wanawake wazifaidi. Hela ya jasho haiwezi kuhongeka hata siku moja, ila hii ya deals nk ngoja waitafune.
 
Habari wakuu

Niliwahi kuleta uzi humu kuhusu mke wangu niliempa mtaji akafanye biashara ya duka la kuuza urembo wa kike pamoja na saloon lakini akauwa ile biashara.

Yule alikua anafanya biashara kisa wenzake wanafanya lakini nina mchepuko wangu huwa ananipoza nikiwa dar, yeye kiukweli anajua hii biashara. Kuna muda anakuja kukaa hapa kwangu karibu wiki mbili na naona kabisa matumizi yake ya hela yapo vizuri na pia yupo sensitive na costs. Nimeamua kumsupport nimfungulie biashara yake sababu kwa sasa anafanya hio biashara ila anamfanyia mtu (mwanamke mwenzake) na wamekua hawapatani kwa muda sasa.

Naombeni ushauri kuhusu mahala pa yeye kuanzia ambapo hapatokuwa na kodi kubwa ila pawe na kiasi kizuri cha wateja, na vile vile jumla ya mtaji wa kuanzia ukiachana na kodi. Hayo maswali mnaweza sema nikamuulize yeye mwenyewe lakini yeye alikua ni mfanya kazi tu, hajui kuhusu details zaidi lakini ile kazi anajua kuifanya, kuna muda anaji-makeup mwenyewe ila ni kama kafanyiwa na professional makeup artist.


Niko hapa Nawasikiliza, ukiwa na details nzuri nzuri kabisa kama vile location hadi namna ya kupata wateja kwa location hio basi shuka hapa na wadau wakikubali idea yako mimi nitakupa zawadi (vijihela vya vocha, 10k, 20k hadi 30k), ila tu iwe very useful info, na kama ni sensitive basi njoo directly PM. Au kama unajua mtu ana duka la hayo mambo na anataka kuliuza basi njoo moja kwa moja PM
Sasa kwanini mlioa, aisee hii dynamic siielewi kabisa. Yaani umekubaliana kabisa na mtu kuwa tutakuwa sisi wawili tu halafu unaanza kuuvunja mkataba kifisadi. Sasa sibora utoe taraka, yote hayo ya nini. Halafu tunaita wake sio waaminifu ila sisi tunasigina sheria kinoma. Ungefunga ndoa isiyosema siyo sisi 2 ningekuona wa maana. Ila this is stupidity. Tuhurumieni dada zetu, nao ni binadamu.
 
Mwingine huyu hapa. Naona unamkaribisha shetani sebuleni. Jivuruge mkuu jiwashie moto. Kila la kheri.
 
Unashirikishaje watu Dhambi zako? Sisi tuna yetu na Muumba hatujayamaliza tafafhali na nnakuambia Acha UZINZI
 
Nimesoma kila neno mzinifu wewe...

Mkeo kuua biashara haina maana hana uzoefu
Eti jamani amejuaje kuwa mchepuko hataiua biashara? Biashara kufa hakuna sababu moja kwamba muhusika hana experience, ni sababu ila sio sababu pekee.

Comment yangu ni hiyo tu, hata hivyo naunga mkono hoja ya mchepuko kufunguliwa biashara, kwasababu kuna muda hawa watu ni wa muhimu sana, na tukisema kila mwanamke ajifungulie biashara mwenyewe, biashara zitakuwa za kuhesabika mjini hapa.
 
Hapana, nakupa ushauri tu namna ya kumfurahisha mchepuko wako, why should I be jelous kwa mtu ambae hata simjui, and by the way, I have my life na ninaheshimu sana waume za watu, na pia ninajiheshimu na kuiheshimu ndoa yangu

Point yangu hapa ni kwamba, jaribu kuwekeza kqenye familia yako, mchepuko unamuona bora leo kwa sababu kuna mitego ametega kwako na anajua udhaifu wako, akishapata anachokitaka atakuonyesha true color yake

Kama mkeo hawezi biashara, jaribu kuangalia ni kitu gani anaweza kufanya ikiwezekana mpeleke hata training au short course za ujasiriamali ili aweze kujisimamia, trust me, atakua msaada na mtapiga hatua maana mtasaidiana kwa vipato vyenu

Pengine hana ujuzi wa kutosha kusimamia biashara ambayo umemfungulia au ako na different intrest, jaribu kuangalia namna ya kumfanya aweze kujishughulisha kuliko kupoteza nguvu zako kwa mchepuko
Na pia biashara zote hizi anazoziona zimesimama mjini, alishawahi kujiuliza zimechoma mitaji mara ngapi mpaka kufikia break even?

Binafsi sipingi mchepuko kufunguliwa biashara sababu hatujui ni kwa namna gani anamfaa mkuu, napinga mama mjengo kukatiwa tamaa.
 
Jamaa mmoja aliingia cha city.. Alianzisha mahusiano nje ya ndoa na mchepuko ambaye hakuwa gongo la mboto mwisho wa lami
Baada ya muda mchepuko akaja na wazo la kupanga ili kupunguza gharama za gesti na pia kwa sababu za kiusalama.. Mwana kakolezwa kakolea
Akamwambia bidada atafute chumba.. Chumba kikapatikana akapewa hela akalipie miezi sita.. Akalipia akapewa na mkataba kwa jina lake mpangaji

Maisha yakaanza na godoro alilopewa pesa akanunue, akanunua sita kwa sita na risiti yake kabisa kwa jina lake.. Mdogo mdogo akawa ananunuliwa vitu vya ndani na hata wakienda wote risiti alikuwa anachukua yeye kwa jina lake

Mambo yakaendelea mpaka akafunguliwa biashara ya duka la vinywaji na bites.. Na ili akopesheke ikabidi awe na leseni ya bishara.. Mkataba wa pango, leseni friji na kila kitu vyote alikuwa anaandika majina yake japo pesa hatoi yeye

Baada ya mwaka bidada akaanza kusumbua anataka atambulike rasmi kama mke mdogo! Jamaa akaona huu mtihani sasa dini yake haimruhusu kuoa wake wawili
Bidada visa vikazidi jamaa akikataa kulala kwake anamtishia ataleta mwanaume mwingine.. Baadae ikawa ni ugomvi kila wakati

Jamaa akaona isiwe tabu akaamua kubwaga manyanga kunusuru ndoa yake..lakini akaamua achukue kila kitu alichomnunulia yule mchepuko

Siku ya siku kaja na canter achukue vyake binti kakimbilia kwa mjumbe kwamba anaibiwa.. Jamaa kuja kuulizwa anasema ni vitu vyake kaamua kuvichukua akaombwa ushahidi hana

Binti yeye katoa mikataba na rundo la risiti kwa kila alichokuwa ananunuliwa.. Risiti zote zilikuwa kwa majina yake kuanzia nyumbani mpaka kwenye biashara.. Jamaa kabaki katumbua macho
Kwa panic na hasira akawa anachimba mkwara wa kumfanyizia mchepuko wake.. Akaambiwa akithubutu ajue kila kitu kitafika kwa mkewe.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ni kumuuwa tuu huyo mchepuko basi
 
Back
Top Bottom